”Karume aiambie Idara ya Vitambulisho iwape Wazanzibari ZAN ID”

Taarifa kwa Vyombo vya Habari 15 Julai, 2009

Sisi Chama cha Wananchi (CUF) tumepokea kwa tafakari kubwa kauli ya Mhe. Amani Karume ya kumtaka kila Mzanzibari mwenye sifa na haki ya kupatiwa kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi (ZAN ID) kwenda katika Ofisi za Idara ya Vitambulisho kupatiwa kitambulisho hicho. Kauli hiyo aliitoa juzi alipokuwa kwenye Bustani ya Victoria alipokuwa akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Utalii, Zanzibar, na kunukuliwa katika gazeti la Zanzibar Leo la leo.

Kwa upande mmoja tunataka tuamini kwamba Mhe. Karume alimaanisha hasa alichokuwa anakisema na kwamba ni haja yake kuona kwamba kila Mzanzibari mwenye haki na sifa anapata kitambulisho hicho. Kwa upande mwengine tunataka tuamini kwamba, anatoa kauli hiyo kufurahisha wahisani tu, ambao wameshajulishwa kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia mtandao wake usio mtakatifu (unity of the demons) unaowajumuisha masheha, Tume ya Uchaguzi (ZEC) na Idara yenyewe ya Vitambulisho, inafanya kila lililo kwenye uwezo wake kuhakikisha kuwa Wazanzibari wengi ambao inaamini kwamba hawaiungi mkono serikali na chama chake tawala hawapatiwi vitambulisho hivyo na hatimaye wanaenguliwa katika zoezi la uandikishaji kwa ajili ya kushiriki kwenye chaguzi.

Hoja ya Mhe. Karume kwamba SMZ imeamua kuvitumia vitambulisho hivyo kwenye uchaguzi ili kuzuia uwezekano wa watu wasiokuwa na haki kupiga kura na pia kuondosha malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara, haina mashiko hata kidogo. Ukweli ni kuwa utumiaji wa vitambulisho hivi kwa ajili ya uchaguzi ndio hasa unaochochea uchaguzi usio huru na wa haki, kwani tayari uzoefu wa uandikishaji katika Wilaya ya Micheweni Pemba unaonesha kwamba mtandao huo usio mtakatifu umeanza kutumia suala la vitambulisho hivyo kama kikwazo dhidi ya Wazanzibari kushiriki kwenye chaguzi.

Kwa mantiki hii, tunamtaka Mhe. Karume aongeze maana katika kauli yake, sio tu kwa kuwataka Wazanzibari wakachukuwe ZAN ID, bali pia – na zaidi – kuitaka Idara ya Vitambulisho na mtandao mzima tulioutaja utoe vitambulisho hivyo kwa Wazanzibari, maana watu hawataweza kwenda kuchukua kile kisichotolewa. Na ukweli ni kuwa mtandao huo unawazuia Wazanzibari kupata ZAN ID. Tunasema haya tukiwa na ushahidi wa zaidi ya wananchi 100 wa wilaya ya Micheweni ambao ingawa walipatiwa risiti za ZAN ID tangu mwaka 2006, hadi sasa hawajapewa vitambulisho vyao kwa kisingizio kwamba vitambulisho hivyo havijaletwa kutoka Ofisi Kuu Unguja. Vile vile tuna ushahidi wa maelfu ya wengine ambao wamenyimwa kabisa fursa ya kuandikishwa kuwa Wazanzibari licha ya kwamba wamefikia umri kwa sababu tu masheha wamekataa kuwapa barua za kuwathibitisha.

Kama kweli Mhe. Karume anamaanisha kauli yake hii, basi achukuwe hatua za makusudi kuisimamia na kuona kwamba inatekelezwa. Vile vile kwa watendaji walio chini yake, kama kweli wanaamini kuwa kauli ya bosi wao ni agizo kwao, basi waifuatilie na kuifanyia kazi. Vyenginevyo, hatuna sababu ya kutokuendelea kuwa na shaka kwamba SMZ na mtandao wake usio mtakatifu ina dhamira ya kuuchafua uchaguzi ujao wa Zanzibar kwa kutumia suala la vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.

Pamoja na salamu za Chama.

Imetolewa na:

Salim Bimani
Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma
The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi)
Simu: +255 777 414 112
E-mail: cufhabari@yahoo.co.uk
Weblog: https://hakinaumma.wordpress.com

Advertisements

One thought on “”Karume aiambie Idara ya Vitambulisho iwape Wazanzibari ZAN ID”

  1. Uhakika kwa sasa sio Karume,kwani Karume ndio anamalizia muda wake,na inawezekana kabisa akawa na kauli nzuri zinazovutia na kutia moyo. Ila kuna mgombea ambae atakuwa ameshajijua kuwa yeye atagombea nafasi hiyo hapo 2010 hivyo basi mgombea huyo inawezekana kabisa amepewa uhuru wa kuamrisha na kupanga atakavyo huku Karume yeye akimalizia muda wake kwa nyimbo nzuri.Mgombea ambae pengine ameshawashiwa taa ya kijani na kupewa mamlaka ya kutumia vyombo vya dola na tume ndie atakuwa anaeratibu mikakati yote ya kumfanya afanikiwe ,aidha bila ya yeye kujitokeza atakuwa ameunda timu ,timu ambazo zinapokezana vijiti bila ya kujua alieanza kupokeza kijiti ni nani ,ni ufahamu tu ndio utakaowafanya wapokee amri hizo na kuzitekeleza kwa kuamini zinatoka juu.
    Makelele yakizidi yatamtoa nyoka pangoni.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s