“CUF yalaani SMZ kuwafukuza waandishi kwenye ajali ya meli”

Taarifa kwa Vyombo vya Habari 7 Juni 2009

Wapendwa Wanahabari,

Kurugenzi ya Uenezi na Mahusiano na Umma ya The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi) imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia Idara ya MAELEZO kuwazuia waandishi wa habari kuingia kwenye eneo la tukio la ajali ya meli ya MV Fatih bandarini Zanzibar, hapo jana.

Kurugenzi inalaani vikali kitendo hicho kilichotekelezwa na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa maagizo kutoka afisa wa MAELEZO, kwa kuwa haki ya kukusanya habari na kuzisambaza ni ya msingi sana kwa taifa linalojali misingi ya utawala wa sheria na uwajibikaji. Kuvumilia vitendo kama hivi ni kukubali kuizamisha Zanzibar katika enzi za giza na usiri usiokuwa na maana.

Vile vile, kitendo cha askari wa JWTZ kujishusha hadhi kiasi cha kupokea na kuyafanyia kazi maagizo kutoka kwa afisa tu wa MAELEZO, ni cha aibu kwa Jeshi letu, maana sio tu kwamba kinaonyesha ufinyu wa mawazo wa baadhi ya walinzi wetu, bali zaidi kinaonyesha utayarifu wa walinzi hao kupokea na kutekeleza maagizo yaliyo nje ya mtiririko wa amri za kikazi (chain of command). Mtiririko wa kikazi kwa wanajeshi wetu ni kupokea amri kutoka kwa wakuu wao wa Jeshi na sio afisa yeyote tu wa serikali anayejisikia kuamuru jambo fulani.

Lakini tukio hili limeakisi utendaji halisi wa vyombo vyetu vya dola, hasa kwa upande wa Zanzibar, ambapo mara nyingi hupokea maagizo kutoka hata maafisa wa ngazi za chini wa serikali na kuishia kuvunja haki za binaadamu au kuingilia uhuru wa watu binafsi. Kuvumilia aina hii ya utendaji kazi kwenye vyombo vya dola ni kuridhia kuwa na dola inayoongozwa kiholela, kitu ambacho ni hatari kwa haki, usalama na kwa heshima ya raia na taifa.

Mwisho, tunakumbusha tena wajibu wa serikali kulinda misingi ya haki, uhuru wa watu, na uhuru wa vyombo vya habari. Iache kabisa kuvichukulia vyombo vya habari kama adui, bali ifahamu kwamba vyombo hivi ndivyo daraja la kimawasiliano baina ya serikali na watu inaowaongoza na pia ndio njia ya kuupatia umma habari sahihi na kwa wakati sahihi.

Habari sahihi zinazotolewa kwa wakati sahihi hujenga mwamko na mwamko ndiyo huleta maendeleo ya watu. Tunaitaka SMZ isiwe kikwazo kwa maendeleo hayo.

Pamoja na salamu za Chama.

Imetolewa na

Dawati la Uchambuzi na Mahusiano na Vyombo vya Habari
Kurugenzi ya Uenezi na Mahusiano na Umma
The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi)
http://www.hakinaumma.wordpress.com
http://www.flickr.com/photos.hakinaumma/

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s