Wafuasi wa CUF kizimbani kampeni za Busanda

Watu watatu wanaodaiwa kuwa wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Geita mkoani Mwanza, kwa tuhuma za kutishia kuua kwenye kampeni za uchaguzi mdogo zinazoendelea jimboni Busanda.

Watu hao Idrisa Salim (49), Faraji Omari (35) na Fadhil Ali (20) wote wakazi wa kijiji cha Katoro makao makuu ya jimbo hilo, walifikishwa juzi katika mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkuu wa Wilaya, Zablon Kesase. Mbele ya Kesase ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Ramadhan Sarijo, kwamba watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Aprili 28 mwaka huu usiku ikiwa ni siku moja kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa kampeni za uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mwendesha Mashitaka, siku ya tukio watuhumiwa hao kwa pamoja walimtishia mwanamke, Agnes Misumbusi wa Katoro kwa kumwambia kwamba watamwaga damu yake baada ya kutokea kutoelewana naye kuhusu masuala ya kampeni. Watuhumiwa wote wako nje kwa dhamana ya mtu mmoja kwa ahadi ya Sh 300,000 na kesi yao itatajwa katika mahakama hiyo Mei 27 mwaka huu.

Hili ni tukio la pili kufikishwa katika mahakama hiyo kutokana na masuala ya kampeni ambapo tukio la kwanza lililofikishwa mahakamani hapo juzi lilikuwa ni la mwananchi anayedaiwa kuwa mfuasi wa Chadema aliyetuhumiwa kukutwa na manati na mawe mfukoni kwa ajili ya kuwapiga wafuasi wa CCM na viongozi wao. Mkazi huyo wa Katoro, Ramadhan Salum (26) alifikishwa mbele ya Hakimu Kesase na kusomewa mashitaka ya kupatikana na silaha za hatari kinyume cha sheria.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s