ZEC yakusudia kupandikiza wapiga kura 2000 Magogoni

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 13 Machi 2009

“NJAMA ZA ZEC KUONGEZA IDADI YA WAPIGA KURA, JIMBO LA MAGOGONI”

Wapendwa Wanahabari,

Leo ni tarehe 13 Machi 2009 – siku tano baada ya kumalizika uadikishaji wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Magogoni kwa nafasi ya uwakilishi na pia uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Licha ya siku hizo kupita, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imeshindwa kutoa hadharani takwimu za walioandikishwa na, hivyo, wanaotarajiwa kupiga kura katika uchaguzi huo wa jimbo moja tu.

Tayari sisi, Chama cha Wananchi (CUF), tumeshapokea taarifa za uhakika kwamba ZEC ina njama za kuandikisha wapiga kura wengine ili wafikie idadi ya watu 7,000 kwa makusudi ya kukinufaisha Chama cha Mapinduzi (CCM). Taarifa tulizonazo ni kwamba bado ZEC imekuwa ikiendelea kutoa vipande vya kupiga kura kwa watu wasiohusika hadi leo hii.

Ili kuweka rekodi sawa na kujenga tahadhari ya mapema kwa Wazanzibari, Watanzania na Walimwengu wote, sisi, CUF, tumeamua kuziweka hadharani takwimu hizo kama zilivyokusanywa na ZEC, mawakala wetu na wa vyama vingine vya siasa:

TUKIO KITUO TAREHE WALIOANDIKISHWA
Uandikishaji Mpya V/Vidogo 28 Feb. 2009 187
1 Machi 2009 157
2 Machi 2009 49
JUMLA NDOGO Ia 393
Sk/Kinuni 28 Feb. 2009 66
1 Machi 2009 74
2 Machi 2009 49
JUMLA NDOGO Ib 189
Hosp/Welezo 28 Feb. 2009 43
1 Machi 2009 28
2 Machi 2009 49
JUMLA NDOGO Ic 120
Sk/Welezo 28 Feb. 2009 202
1 Machi 2009 267
2 Machi 2009 174
JUMLA NDOGO Id 643

TUKIO KITUO TAREHE WALIOANDIKISHWA
Ubadilishaji Vipande V/Vidogo 3 Machi 2009 435
4 Machi 2009 437
5 Machi 2009 346
6 Machi 2009 158
JUMLA NDOGO IIa 1,376
Sk/Kinuni 3 Machi 2009 343
4 Machi 2009 270
5 Machi 2009 159
6 Machi 2009 43
JUMLA NDOGO IIb 815
Hos/Welezo 3 Machi 2009 40
4 Machi 2009 79
5 Machi 2009 29
6 Machi 2009 9
JUMLA NDOGO IIc 157
Sk/Welezo 3 Machi 2009 442
4 Machi 2009 367
5 Machi 2009 312
6 Machi 2009 200
JUMLA NDOGO IId 1,321

TUKIO KITUO TAREHE WALIOANDIKISHWA
Uhamisho V/Vidogo 7 Machi 2009 164
Sk/Kinuni 7 Machi 2009 62
Hos/Welezo 7 Machi 2009 11
Sk/Welezo 7 Machi 2009 125
JUMLA NDOGO III 362

TUKIO KITUO TAREHE WALIOANDIKISHWA
Waliopoteza V/Vidogo 8 Machi 2009 45
Sk/Kinuni 8 Machi 2009 25
Hos/Welezo 8 Machi 2009 6
Sk/Welezo 8 Machi 2009 52
JUMLA NDOGO IV 128

UFUPISHO I (kwa mujibu wa siku):
SIKU WALIOANDIKISHWA VITUO VYOTE VINNE
Siku ya Kwanza = 28/02/09 498
Siku ya Pili = 01/03/09 526
Siku ya Tatu = 02/03/09 321
Siku ya Nne = 03/03/09 1,260
Siku ya Tano = 04/03/09 1,153
Siku ya Sita = 05/03/09 846
Siku ya Saba = 06/03/09 410
Siku ya Nane = 07/03/09 362
Siku ya Tisa = 08/03/09 128
JUMLA KUU 5,504

UFUPISHO II (kwa mujibu wa kituo):
KITUO WALIOANDIKISHWA KWA SIKU ZOTE TISA
Viwanda Vidogo Vidogo 1,978
Skuli ya Kinuni 1,091
Hospitali ya Welezo 294
Skuli ya Welezo 2,141
JUMLA KUU 5,504

Wapendwa Wanahabari,

Kwa hivyo, takwimu halisi ya hadi saa 10.00 alasiri ya tarehe 8 Machi, 2009, vituo vya uandikishaji vilipofungwa katika jimbo la Magogoni, zinaonesha kuwa walioandikishwa kuwa wapiga kura ni watu 5,504 tu. Vile vile, ZEC ilitangaza majina ya watu wasiozidi 33, ambao mwanzoni walikuwa wamekataliwa kuandikishwa lakini baadaye rufaa zao zikapita, kwenda Ofisi yake ya wilaya kujiandikisha. Hii maana yake, nyongeza haitofikia watu 50 juu ya ile 5,504 iliyoandikishwa vituoni.

Wapendwa Wanahabari,

Taarifa ambazo tunazo ni kwamba ZEC imekusudia kuongeza wapiga kura 2,000 ili kufikia hisabu ya wapiga kura 7,000 ambao walipiga kura mwaka 2005. Kwa upande mmoja, hatua hiyo inakusudiwa kuziba aibu ya 2005 ambapo ZEC ilipandikiza wapiga kura zaidi katika jimbo la Magogoni. Mara hii, kutokana na umakini wa mawakala na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, ‘utatu usio mtakatifu’ wa ZEC, CCM na SMZ (kupitia masheha) ulishindwa kupandikiza idadi hiyo na sasa wanataka kuona kwamba aibu yao inasitirika kwenye takwimu.

Kwa upande wa pili, uongezaji huo wa wapiga kura unakusudiwa kuibeba CCM, kwani ZEC imepanga kutokubandika orodha ya wapiga kura kwa ajili ya pingamizi hadi siku za mwisho mwisho, ambapo orodha hiyo haitawekwa kwa mfumo wa alfabeti na wala kwenye vituo husika na, hivyo, kufanya iwe vigumu kwa watu kuwabaini ‘mapandikizi’ na kuwawekea pingamizi. Itakumbukwa kuwa mbinu kama hiyo ndiyo iliyotumiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika chaguzi ndogo za Tarime na Mbeya Vijijini.

MSIMAMO WA CUF

Wapendwa Wanahabari,

Kwa ufafanuzi huo hapo juu na kwa taarifa hii, sisi CUF – Chama cha Wananchi, tunatamka yafuatayo:

1. Kwa madhumuni ya uwajibikaji, tunaitaka ZEC ichapishe na itoe hadharani takwimu za uandikishaji wa Magogoni kama ilivyosikusanya kutoka vituoni haraka. Ni jambo la kushangaza kwamba hadi tunatoa taarifa hii, mtandao wa ZEC, http://www.zec.go.tz, haujapachikwa takwimu za siku mbili za mwisho za uandikishaji (7 – 8 Machi, 2009). Tunaweka wazi kwamba hatutakubaliana na idadi nyengine yoyote ya wapiga kura wa jimbo la Magogoni itakayokiuka takwimu hizi zilizokusanywa vituoni na nyongeza hiyo isiyofikia watu 100 baada ya rufaa kumaliza kusikilizwa na kupita.
2. Kwa madhumuni ya kujengeana imani, tunaitaka ZEC ikabidhishe haraka Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lenye picha kwa vyama vyote vya siasa kama ilivyokuwa imeahidi hapo kabla.
3. Tunaukumbusha ‘utatu usio mtakatifu’ wa CCM, ZEC na SMZ (kupitia masheha wao) kwamba Zanzibar na Tanzania ni zetu sote. Kwa hivyo, waache mara moja fitina zao za kisiasa ambazo zinahatarisha utangamano wa nchi. Ni wao ndio watakaondelea kubeba lawama ikiwa wataitumbukiza tena nchi hii katika maafa.
4. Kwa Wazanzibari na Watanzania wote, tunawatanabahisha tena kuwa hizi ndizo serikali za CCM na tume zake za uchaguzi na huu ndio mchezo wao wa kuchezea amani ya nchi kwa manufaa ya kitambo ya kisiasa. Zanzibar na Tanzania ni kubwa kuliko CCM, ZEC, SMZ, masheha wao na hata kuliko CUF. Tusaidiane kuijenga nchi yetu na sio kuibomoa.
5. Kwa ulimwengu, tunatoa indhari tena na tena kwamba taasisi zilizoaminiwa kusimamia chaguzi huru, za wazi na za haki nchini mwetu, ndizo hizo hizo zinazosimamia uchafuzi na ufisadi katika uchaguzi. Ulimwengu una jukumu la kusaidia demokrasia ichukuwe mkondo wake Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, maana demokrasia ndio msingi wa maendeleo. Bila ya demokrasia, misaada inayotolewa kwetu, itaendelea kuishia kwenye midomo ya viongozi wasiowajibika kwa wananchi kwa kuwa sio wanaokuwa wamewaweka madarakani.
6. Mwisho, tunaendelea kusisitiza imani yetu siasa za kistaarabu – za kushindana bila kupigana. Tunatarajia wenzetu wa CCM wanaacha utamaduni wao wa kutumia fujo kama njia ya kuendelea kusalia madarakani.

Imetolewa na:

Salim Bimani
Mkurugenzi Uenezi na Mahusiano na Umma
The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi)
S. L. P. 3637, Makao Makuu – Zanzibar
S. L. P. 10979, Ofisi Kuu – Dar es Salaam
Simu: +255 777 414 112,
E-mail: cufhabari@yahoo.com
Weblog: https://hakinaumma.wordpress.com
Website: http://www.cuf.or.tz

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s