“Njama za SMZ kwa tarehe 7 Machi, 2009”

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 5 Machi, 2009

Wapendwa Wanahabari,

Vyanzo vyetu vya habari vimetuarifu kwamba, kutokana na mwenendo wa zoezi la kujiandikisha ulivyo kwenye jimbo la Magogoni, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), ikitumia masheha, imepanga kuandaa uhamisho wa ‘uongo’ kuingiza wapiga kura katika jimbo la Magogoni.

Tayari barua hizo zimeshakabidhiwa kwa masheha wa majimbo kadhaa ya Unguja na zimeanza kufanyiwa kazi kwa masheha wa shehia zote za Magogoni kuwapokea watu hao na siku ya tarehe 7 Machi, 2009 ndiyo watu wenye barua hizo watajitokeza vituoni kujiandikisha kama wapiga kura.

Huu ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi na, kwa hakika, hata sheria za nchi. Ni uhalifu wa kumsaidia mhalifu kufanya uhalifu wake, kwani kwa mujibu wa sheria kudanganya kwenye uchaguzi ni kosa la jinai.

Kwa taarifa hii, tunawataka wale wananchi wote waliopewa barua hizo za ‘uhamiaji’ hewa, waachane kabisa na wazo la kujishirikisha katika uchaguzi wa Magogoni. Huko ni kutumiliwa kisiasa kuvunja sheria za nchi. Sisi, Chama cha Wananchi (CUF), tutashirikiana na walinzi wa sheria za nchi kuwafichua watu hao na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Pia tunaliarifu Jeshi la Polisi, ambalo lina wajibu wa kuzuia uhalifu usitokee na sio kupambana nao baada ya kutokea, kwamba iingilie kati kuuvunja mpango huo wa masheha na SMZ.

Pamoja na salamu za Chama

Imetolewa na:

Salim Bimani
Mkurugenzi
Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi)
Makao Makuu – Zanzibar
Simu: +255 777 414 112
Weblog: https://hakinaumma.wordpress.com
Website: http://cuf.or.tz

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s