CUF sasa watishia kususia uchaguzi serikali za mitaa

Na Salim Said

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema, hakitashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu kama makubaliano ya wadau hayatatumika kuendesha chaguzi hizo.

Uchaguzi huo ambao huendeshwa chini ya usimamizi wa serikali za mitaa umekuwa ukilalamikiwa kwa kutokuwa huru na haki.

Februari, mwaka huu ulifanyika mkutano wa wadau kujadili jinsi ya kuendesha chaguzi hizo katika mazingira mazuri na kupunguza malalamiko ya vyama shiriki.

Akifungua mkutano mkuu huo juzi, mwenyekiti wa CUF taifa, Profesa Ibrahim Lipumba aliisihi serikali kuhakikisha kuwa chaguzi za mwaka huu zinaendeshwa kwa mujibu wa makubaliano ya wadau.

“Ninaisihi serikali uchaguzi wa mwaka 2009 uzingatie makubaliano ya wadau vikiwemo vyama vya siasa, serikali na asasi za kiraia uliofanyika Morogoro Febuari 19, mwaka huu,” alisema profesa Lipumba na kuongeza:

“Wadau wote walikubaliana kuwa mambo mengine yasiwahusishe watendaji wa vijiji na kata (VEO na WEO) katika zoezi la kuandaa orodha ya wapiga kura.”

Alisema ni muhimu serikali iheshimu makubaliano hayo kama alivyoahidi Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Celina Kombani wakati akifunga mkutano huo.

Katika nasaha zake, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa alisema uchaguzi wa serikali za mitaa ni nafasi muhimu ya vyama kujipima kwa kuwa ndio taswira ya uchaguzi mkuu.

“Uchaguzi wa serikali za mitaa ni uchaguzi mdogo, lakini ni muhimu sana kwa kuwa ndio unaotoa taswira ya uchaguzi mkuu, hivyo ni kazi kwenu kufanya maandalizi ya kutosha,” alisema Tendwa.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s