Salim Bimani: “Baina ya viongozi wa CCM na CUF, nani walevi wa tende!?”

Kutoka mkutano wa nane wa Maombolezi ya Januari 2001, uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti, mjini Zanzibar, tarehe 31 Januari, 2009.

Kwanza, kwa kuziheshimu roho za wenzetu waliotutoka, wote waliosimama wakae kitako. Ni hapo ndio tutajua kama kweli tunawaheshimu wenzetu na tunawakumbuka kama wakaombozi wetu. Tunawaomba mkae kitako kwani mkutano wa leo ni tafauti na mikutano mingine yote.

Kazi yetu ni moja tu iliyotuleta hapa: kuwakumbuka wenzetu na kuweka msimamo wa kuwang’oa CCM madarakani 2010 wakitaka wasitake. Mengi yamesemwa katika Risala, mengi yamesemwa katika Utenzi na mengi tumeyaona kwa vitendo kwa watoto mayatima hawa waliopoteza wazazi wao. Hakuna asotokwa na machozi.

Viongozi wanakuja kueleza, lakini mimi nasema moja tu: Rais Kikwete, sisi si walevi wa tende. Walevi wa tende ni wale wal’owaua Wazanzibari kwa bunduki siku ya Januari 26 na 27, 2001. Na tunakushangaa sana, kwenda Pemba, ukaja Unguja katika mwezi huu wa huzuni, lakini ukashindwa hata kusema “Poleni” kwa wale waliofikwa na maafa haya. Umeshindwa kabisa kutamka hayo.

Badala yake anakuja kutwambia eti pana barabara ya mgongo wa ngisi! Ipo wapi hapa? Barabara za nchi hii zina mashimo na viraka kila mahala. Tena bila aibu anasema Zanzibar imepiga hatua za maendeleo kuliko Bara. Aibu! Aibu! Aibu kabisa kabisa. Kwani hatuoni kwenye TV Dar es Salaam ilivyo? Kama hatuoni, kwani hatwendi? Ati anatwambia Zanzibar ina maendeleo; maendeleo yapi yaliyokuwepo Zanzibar, wakati hata hapa mjini penyewe usiku hapana taa hata moja, ikifika usiku, kila mtu na kimurimuri chake!? Hata taa barabarani haiwaki. Maendeleo haya? Dar es Salaam iko kiza?

Lakini haya ndiyo yaliyosemwa katika Risala, kwamba viongozi wa CCM wa Bara wakija Zanzibar, kazi yao kutugawa. (Rais Mstaafu Benjamin) Mkapa alisema nini? Nchi hii hawatoshika madaraka vijukuu vya watoto wa Sultani, wakati anao nyuma hapa (kwenye shamiana). Anao nyuma, wakati anahutubia, mjukuu wa mtoto wa mfalme yuko pale. First Lady (Shadiya Karume, mke wa Amani Karume na mjukuu wa mwasisi wa Zanzibar Nationalism, Sheikh Mohammed Salum Jinja) na wenzake wanaotoka jamii za Kiarabu, yuko pale.

Na huyu (Kikwete) anakuja kusema yale yale. Sasa tunakuambia sisi: mara hii hatuandikii mate na wino upo. Atakavyobwagwa, ndivyo hivyo hivyo (atakavyochinjwa). Sawa? Tusije tukasaliti damu za wenzetu, enh!

Na kama sisi ni wlaevi wa tende, tuko tayari uongozi mzima wa chama cha CUF na uongozi mzima wa CCM tukapimwe hospitali, nani atakayeripuka. Tukapimwe tujue, nani mlevi wa tende, nani mlevi wa gongo. Sisi tunaamini, wakati pale anahutubia, wengine washalewa tende nyuma yake huku (kwenye shamiana).

Babu Duni karibu…

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s