Juma Duni Haji: “Wanaoua albino wauawe, walioua Wazanzibari je?”

Kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Mhe. Juma Duni Haji, katika Mkutano wa Nane wa Maombolezi ya Januari 2001, uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti, mjini Zanzibar, tarehe 31 Januari, 2009

Sina hakika, lakini juzi nilipokuwa natizama Bunge (vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano), alipoulizwa Mheshimiwa Pinda (Waziri Mkuu) kuhusu mauaji ya maalbino, nadhani ilikuwa tarehe 27 Januari, siku ambayo watu sisi pia waliuliwa, basi namna vile alivyokuwa na huzuni, vile alivyokuwa akilia masikini na mie nikawa ninalia. Lakini kilio cha Pinda na changu kidogo vilikuwa tafauti, maana Pinda alichoambiwa na Kiongozi wetu wa Upinzani Bungeni (Hamad Rashid Mohammed) haoni kuwa si vizuri yule anayedhaniwa kupiga au kuua albino, apelekewe mahkamani, maana (kabla ya hapo) kwa namna alivyoona uchungu, Pinda alikuwa amesema anayeuwa albino naye auliwe.

Nikasema lo, Mashallah! Anayeua albino anaye auliwe, aliyewaua Watanzania na Wazanzibari tarehe 27, afanywe nini? Maana kama ni mwanaadamu na ni uchungu wa roho, roho ya albino na roho ya Mzanzibari ni sawa sawa. Tafauti iliyopo ni kwamba yule aliyemuua albino hajapatikana, bado anasakwa, lakini walowaua Watanzania na Wazanzibari tarehe 27 wanajuilikanwa. Tena wengine, baada ya kuua, Mheshimiwa Mkapa kawatunza vyeo, ati wamefanya kazi nzuri kutuua.

Sasa, kufa ni kufa, roho ni roho. Kamisheni ya Mheshimiwa Hashim Mbita ilishathibitisha yaliyotokea wakati huo wa tarehe 27, basi tungelitegemea angalau wao wakafikishwa mahkamani; maana wanajuilikanwa. Lakini Mheshimiwa Pinda analia kwa uchungu, anasahau kuwa sisi pia tunalia kwa uchungu. Lakini sisi tulipouliwa watu walipewa vyeo. Wanapewa vyeo kwa kutuua? Ee, Mungu we! Hilo ndilo lililonisikitisha.

Sasa kama hilo halitoshi, nikasikitika zaidi kwa Mheshimiwa Kikwete unakuja Zanzibar, badala ya kutusahaulisha yaliyotokea, unatukumbusha? Mashallah, hivo wewe ndo rais kweli weye!?

Maalim karibu…

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s