CUF yaionya CCM Kagera

Na Audax Mutiganzi, Misenyi

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimewaonya baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwataka kuachana na mchezo mchafu kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Diwani wa Kata ya Kitobo, wilayani Misenyi, mkoani Kagera.

Viongozi wa CUF wamesema baadhi ya viongozi wa CCM, hasa mabalozi wa nyumba kumi kumi, wameanza mchezo mchafu wa kuwatishia maisha wananchi wanaojitokeza kusikiliza sera zinazotolewa na mgombea wa kiti cha udiwani wa Kata ya Kitobo kupitia CUF, Erasmus Novatus.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wa CUF wakati wa kumnadi Novatus, walisema CCM imeanza mchezo mchafu kwa nia ya kuvuruga uchaguzi, jambo linaloweza kuchangia uvunjifu wa amani.

Viongozi wa chama hicho ambao ni Mratibu wa Uchaguzi wa Mkoa wa Kagera CUF, Renatus Kilongozi “Ikengya”, Diwani wa Kata ya Hamgembe, Onesphory Akenyaya na Diwani wa Kata ya Rwamishenye, Dismas Rutagwerela, walisema CUF kamwe haitavumilia mchezo mchafu unaochezwa na baadhi ya viongozi wa CCM katika uchaguzi huo.

Mratibu wa Uchaguzi wa CUF wa Mkoa “Ikengya”, alimtaja mmoja wa viongozi wa CCM wanaocheza mchezo mchafu wenye lengo la kuvuruga uchaguzi hadharani (jina tunalihifadhi).

Alisema balozi huyo anawatishia kuwafukuza wananchi katika kijiji anachokiongoza, watakaojitokeza kusikiliza kampeni inayoandaliwa na CUF katika uchaguzi huo.

Kilongozi amesema CUF imejiandaa kukabiliana na lolote litakalojitokeza mbele yake, hivyo siasa za vitisho zimepitwa na wakati, hazina nafasi katika karne hii, kwani vyama vya siasa viko kisheria na vinatambulika.

Alisema kiongozi anayewatishia wananchi wasihudhurie mikutano ya kampeni inayoandaliwa na CUF wanavunja sheria za nchi, hivyo serikali haina budi kuwachukulia hatua za kisheria bila kuangalia nafasi zao katika jamii.

Alisema CUF haiko tayari kuanzisha vurugu za aina yoyote, ila itajihami endapo itachokozwa: “Chama cha CUF ni chama cha wastaarabu kisichopenda vurugu. Kazi ya Chama cha CUF ni kurekebisha mapungufu yanayojitokeza ndani ya serikali,” alisema.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Hamgembe, Onesphory Akenyaya, aliwataka wananchi wasipotoshwe na wanasiasa wanaopanda majukwaani na kutafsiri Chama cha CUF kwa mtizamo tofauti. Alisema wanaotasfiri Chama cha CUF kwanza wajitafsiri wenyewe.

Aliwataka wananchi wanaopanda majukwaani na kukitafsiri chama cha CUF kwamba ni Chama cha Udini, wafahamu kuwa CUF haina udini na wala haina ukabila: “Jamani kama mnataka kuangalia mambo ya udini angalia Kamati Kuu ya CCM… asilimia kubwa ni Waislamu. Je, na CCM ni chama cha udini?” alihoji Akenyaya.

Wagombea wengine wa kiti hicho cha udiwani katika Kata ya Kitobo ni pamoja na Edson Mutalemwa kupitia CCM na Dominic Rwehumbiza wa Chama cha NCCR–Mageuzi. Uchaguzi huo utafanyia Januari 24, mwaka huu.

Uchaguzi huo unafanywa baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Josiah Nyamwihula, kufariki dunia kutokana na ajali ya gari.

Chanzo: http://www.newhabari.com/mtanzania/habari.php?id=710&section=siasa

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s