Viongozi TLP, PPT watinga Mbeya Vijijini kuisaidia CUF

Date::1/18/2009

Na Brandy Nelson – Mbeya

IKIWA imebaki wiki moja kufanyika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Mbeya Vijijini, wenyeviti wa taifa wa vyama vya CUF, Tanzana Labour (TLP) na PPT Maendeleo, wamewasili mkoani Mbeya kuongeza nguvu katika kampeni za mgombea wa CUF, Daud Mponzi.

Viongozi hao wa ngazi ya kitaifa waliowasili jana pamoja na Mweyekiti wa CUF Taifa, Prof Ibrahimu Lipumba ni Augustino Mrema wa TLP na Peter Mzirai PPT Maendeleo.

Akizungumza baada ya kuwasil katika ofisi za CUF, Wilaya ya Mbeya Wijijini, Prof Lipumba alisema wameenda kuongeza nguvu na kuhakikisha kuwa anapatikana mbunge anayeweza kuwatetea wananachi na wakulima wa jimbo la Mbeya vijijini maendeleo kwa kuwa wamechoka na ahadi za uongo za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Wananchi wamechoka na uongozi wa serikali ya CCM kutokana na kuwa na mipango ya kisanii iliyowasababisha wakulima wa Mbeya vijijini kuwa na maisha magumu,” alisema.

Alisema ili kuhakikisha kuwa siasa za CCM ni za kisanii, chama hicho kiliamu kumpeleka Makamu Mwenyekiti mstaafu, John Malecela kwenye kampeni hizo ambaye hayati Mwalimu Julias Nyerere alisema kuwa siyo kiongozi.

“Hawa CCM baada ya kuona na kubaini kuwa wananchi wamewachoka, wameamu kumleta John Malecela ambaye mimi na mwita tinga tinga, kwani ameishiwa na hana nguvu yoyote kwa Sasa, hivyo anatakiwa kutulia na kazi hiyo amuachie mke wake, Anna Kilango ambaye ana Msimamo dhabiti katika kupambana na mafisadi,” alidai Prof Lipumba.

Alisema awali walimpeleka Pius Msekwa kwa kazi hiyo, lakini wakaona hawezi kuwashawishi wananchi ndipo wakamgeukia Malecela ambaye pia hana uwezo huo.

Prof Lipumba alisema siasa za CCM ni za kukomoana kwani, serikali ya awamu ya nne iliutelekeza uwanja wa ndege wa Songwe kwa lengo la kumkomoa Prof Mark Mwandosya wakidhani atapata umaarufu, kumbe wanawakomoa wananachi amabao wangenufaika na uwanja huo.

“Serikali ya Mkapa ndiyo iliyoidhinisha fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa uwanja wa ndege wa Songwe, lakini serikali hii imeutelekeza kwa nia ya kumkomoa Prof Mwandosya, hawajui kama kufanya hivyo ni kuwakomoa wananchi wa Mbeya Vijijini na mikoa jirani ambao ndiyo wangenufaika na uwanja huu,”alisema.

Alisema wananchi wa Mbeya Vijijini shughuli zao ni kilimo, lakini wamechoka hawana uwezo wa kuendesha shughuli hizo kutokana na kukosa pembejeo na miundo mbinu mibovu ikiwamo ya barabara.

Kwa upande wake Mwenyekiti chama cha PPT Maendeleo, Mziray alikitaka ChamaDemokrasia na cha Maendeleo (Chadema) kutoa tamko la kuinga mkono CUF katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Mbeya vijijini mapema kabla ya uchaguzi huo kufanyika ili baadaye kisije kujuta.

Alisema Chadema walitakiwa kuona aibu kwa kitendo walichofanya na kwamba wasipotoa kauli ya kuinga mkono CUF kabla ya uchaguzi kufanyika watajuta baadaye.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s