Mrema awa kivutio katika uchaguzi Mbeya

Date::1/18/2009

Na Brandy Nelson, Mbeya

MWENYEKITI wa TLP, Augustino Lyatonga Mrema juzi alikuwa kivutio katika mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mbeya Vijijini kwa tiketi ya CUF, Daudi Mponzi uliofanyika kwenye kiwanja cha stendi ya mabasi cha Mbalizi alipodai kuwa wamejitakia maisha ya shida kwa kuichagua CCM.

Alikuwa akihutubiua kwenye mkutano uliofurika mamia ya watu na kuhudhuriwa na viongozi wa vyama vinne vya siasa vya TLP na PPT Maendeleo ambavyo vimeamua kuungana na CUF kumpigia kampeni mgombea wake ili anyakue jimbo hilo lililoachwa wazi baada ya Richard Nyaulawa (CCM) kufariki mwishoni mwa mwaka jana.

Wananchi hao walianza kuonyesha kuvutiwa na Mrema mara aliposimama jukwaani wakati alipomshangilia na kupiga kelele kuonyesha kumkubali na bila kuchelewa waziri huyo wa zamani wa mambo ya ndani alianza hotuba yake kwa kuwaambia wananchi kuwa shida na maisha magumu waliyonayo wamejitakia.

“Hizi shida mnajitakia wenyewe msimlaumu Mwenyezi Mungu kwani Mungu amefanya kazi ya kuwaumba, lakini nyie mmefanya kazi ya kuichagua CCM na ndiyo maana mnabaki na malalamiko ya kusema ‘Mungu nisaidie maisha ni magumu’. Naomba niwasisitizie kuwa hili si kosa la Mungu, ni kosa lenu kwa kuchagua chama ambacho kimejaa propaganda,” alisema.

Mrema aliendelea kuwavutia wananchi hao aliposema kuwa alipokuwa naibu waziri mkuu alifanya kazi zake vizuri, ikiwa ni pamoja na kukamata ndege iliyokuwa na dhahabu zenye thamani ya Sh175 milioni, lakini waziri mkuu wa wakati huo hakufanya lolote zaidi ya propaganda.

Alisema kuwa ameamua kuiunga mkono CUF kwa sababu watendaji wake ni majasiri na wana uwezo mkubwa na kwamba CUF ni chama cha ukombozi hivyo kinastahili kuungwa mkono na wananchi wote, ikiwa ni pamoja na wa Mbeya Vijijini ambao alisema wanatakiwa kumpa kura za Mponzi.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema kuwa wananchi wa Mbeya Vijijini wana nafasi ya kubadilika na kumchagua mgombea wa CUF kuwa mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini ili maisha yao yaweze kubadilika .

Chanzo: http://mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=9366

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s