Mrema ataka CUF kiungwe mkono uchaguzi wa Mbeya

2009-01-06 21:03:05

Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Mwenyekiti wa TLP, Bw. Augostine Mrema amevitaka vyama vingine vya upinzani kuweka kando tofauti zao na kumuunga mkono mgombea ubunge wa chama cha wananchi, CUF katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Mbeya Vijini ili hatimaye waweze kuepuka aibu ya kushindwa mbele ya CCM.

Akizungumza na Alasiri jana, Bw. Mrema amesema endapo wapinzani wataparaganyika na kuacha jimbo hilo liangukie kiulaini mikononi mwa CCM, aibu itakuwa ni kwa wapinzani wote.

Bw. Mrema amekiomba chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA kuacha kulipiza kisasi na badala yake kuunganisha nguvu ya upinzani ili waing\’oe CCM ndani ya jimbo hilo la Mbeya Vijijini.

“CCM ikishinda uchaguzi huo, aibu itakuwa kwetu wapinzani wote… nawaomba sana wapinzani wenzangu, wenye nia ya dhati ya kuiondoa CCM madarakani, waunganishe nguvu na kuwaunga mkono wenzetu wa CUF katika uchaguzi wa Mbeya Vijijini,“ akasema Bw. Mrema.

Hata hivyo, pamoja na kutaka wapinzani waunge mkono CUF, Bw. Mrema amekishukia chama hicho na kusema kuwa hakikupaswa kuwawekea pingamizi wenzao wa CHADEMA.

“Pingamizi la CCM tu lilitosha, CUF hawakuwa na sababu ya kuongeza kuweka pingamizi kwa CHADEMA, kwani hatua hiyo inadhoofisha ushirikiano wa vyama vya upinzani ambavyo vina nia moja ya kuikomboa nchi hii,“ akasema Bw. Mrema.

Bw. Mrema pia akatumia nafasi hiyo kuwaomba CHADEMA kutowahamasisha wafuasi wake kupiga kura za maruhani, kama walivyofanya CUF huko Pemba mwezi Mei 2003, katika uchaguzi wa marudio kwenye majimbo 16.

Katika uchaguzi huo chama cha NCCR kiliwawekea pingamizi wagombea wa CUF na TLP ambao walienguliwa na kusababisha wasalie wa CCM pekee.

Hata hivyo, licha ya kuenguliwa kwa wagombea wa vyama hivyo, CUF iliwahimiza wafuasi wake kutowapigia kura wagombea wa CCM na badala yake wapigie vivuli, kura ambayo ilijulikana kama `kura ya maruhani`.

Bw. Mrema ameonya kuwa CHADEMA wakiiga mfano huo, watasababisha CCM ishinde kiulaini uchaguzi huo, jambo ambalo litakuwa ni pigo kubwa.

“Ili tushinde Mbeya Vijijini, inatupasa wapinzani tuache chuki, kulipiziana visasi na badala yake tushikamane na kuungana mkono,“ akasema Bw. Mrema.

Uchaguzi wa Mbeya vijijini unatarajiwa kufanyika Januari 25 mwaka huu, ukishirikisha vyama vitatu vya CUF, CCM na SAU.

Mgombea wa CHADEMA, na yule wa DP walienguliwa na msimamizi wa uchaguzi huo, Bi. Juliana Malange, baada ya kubainika kuwa hawakula kiapo mahakamani kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985.

SOURCE: Alasiri

Advertisements

One thought on “Mrema ataka CUF kiungwe mkono uchaguzi wa Mbeya

  1. concept:

    wananchi ndio wanaopaswa kushirikiana na chama makini kuiondoa CCM madarakani na sio vyama kushirikiana kama inavyolazimishwa kuaminika hivyo.

    vyama visivyo na mtandao. vyama vilivyojaa mashushushu. vyama vya ukabila na ukoo. vyama visivyo vya kitaifa, vyama vya semina na makongomano. vyama vya DSM pekee. utashirikiana navyo vipi?

    wananchi watambue hilo na wao ndio wenye uwezo wa kuleta ‘CHANGE’

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s