CUF yalaani mashambulizi ya Israel dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Palestina

CUF inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati hali hiyo na kuzuia mauaji hayo ya kutisha na hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili wananchi wa Palestina walioko Gaza. CUF inazitaka nchi za Marekani na zile za Umoja wa Ulaya kuacha kuiunga mkono Israel na kutekeleza wajibu wao unaotokana na nguvu kubwa za kijeshi na kiuchumi walizo nazo kwa kuiambia Israel isitishe mara moja mauaji hayo na kuamuru majeshi yake yaliyoivamia Gaza yaondoke mara moja.

pm_gaza3_wideweb__470x3360

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama Cha Wananchi (CUF) kinalaani vikali na kwa nguvu zote mashambulizi ya kikatili na kinyama yanayofanywa na Israel dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Palestina walioko katika ukanda wa Gaza ambayo hadi sasa yamesababisha mauaji ya watu zaidi ya 500 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 2,800.

Chama Cha CUF kinayachukulia mashambulizi hayo kama ni muendelezo wa vitendo vya kinyama na kikatili vinavyoendelea kufanywa na Israel kwa miaka 41 sasa, tokea nchi hiyo ilipozivamia na kuzikalia kwa mabavu ardhi za Waarabu ikiwemo Palestina hapo mwaka 1967.

Hakuna kisingizio chochote kinachoweza kutolewa na taifa hilo vamizi kuhalalisha mauaji yake ya raia wasio na hatia. Nguvu kubwa inayotumiwa na Israel ambayo haiwiani na kile inachodai kutaka kukizuwia haiwezi kukubaliwa na wapenda haki ulimwenguni. Kudhihirisha uovu wake, Israel imechukua hatua hizi za mauaji baada ya kuwaweka wananchi wa Gaza katika kifungo kwa zaidi ya miezi 18 na kuwazuilia huduma zote muhimu zikiwemo zile za kibinadamu kama chakula na madawa.

Chama Cha CUF kinatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati hali hiyo na kuzuia mauaji hayo ya kutisha na hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili wananchi wa Palestina walioko Gaza. CUF inazitaka nchi za Marekani na zile za Umoja wa Ulaya kuacha kuiunga mkono Israel na kutekeleza wajibu wao unaotokana na nguvu kubwa za kijeshi na kiuchumi walizo nazo kwa kuiambia Israel isitishe mara moja mauaji hayo na kuamuru majeshi yake yaliyoivamia Gaza yaondoke mara moja.

Katika kutambua msimamo wa kihistoria wa Tanzania uliokuwa ukisimamiwa kwa dhati na Rais wa kwanza wa Taifa hili, Mwalimu Julius Nyerere, wa kuunga mkono harakati za Wapalestina kujikomboa na kupinga Uzayuni, Chama Cha CUF kinamtaka Rais Jakaya Kikwete na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walaani vikali uvamizi wa Israel na mauaji ya Wapalestina katika ukanda wa Gaza na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa ilinde haki za binadamu za Wapalestina ikiwemo haki yao ya kujitawala kwa uhuru kamili.
HAKI SAWA KWA WOTE
Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti wa Taifa

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s