CCM walalamikia maofisa ZEC

Na Mwanne Mashugu, Zanzibar

Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema baadhi ya makamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na watendaji wameanza kupotosha sheria ya uchaguzi kwa maslahi yao.

Hayo yalielezwa na Katibu Mwenezi wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya CCM, Kisiwandui, Zanzibar.

Alisema makamishna hao wamekuwa wakipotosha sheria ya ukaazi kuwa mtu anaweza kujiandikisha hata bila ya kuwa na sifa ya Uzanzibari ukaazi katika eneo husika.
Alisema sheria ya ukaazi katika majimbo lazima izingatie kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi kwa sababu ni kielelezo cha Mzanzibari mwenye sifa ya kushiriki uchaguzi wa Zanzibar.

Vuai alisema CCM itaingia katika zoezi la uandikishaji wapiga kura katika daftari la kudumu kwa kuona katiba na sheria za uchaguzi zinafuatwa.

”Hatupo tayari kuona baadhi ya makamishna na watendaji wakitaka kupindisha sheria kwa maslahi yao,” alisema na kusisitiza sheria ya ukaazi katika majimbo inaheshimiwa.
Alisema tayari CCM imeanza kupokea malalamiko kutoka kwa wanachama wao kuwa baadhi ya makamishna wameanza kupotosha sheria za mpiga kura anazopaswa kuwa nazo kabla ya kuandikishwa katika jimbo husika.

Hata hivyo, aliwataka wanachama wao kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wapiga kura lililopangwa kuanza Januari mwakani.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ina makamishna saba, wawili kati ya hao wanatoka chama cha Wananchi (CUF).

Aidha, alitanabahisha CUF hakina hati miliki za majimbo ya Pemba kwa hivyo kila chama kina haki ya kufanya kampeni ya kushinda viti Pemba.

Alisema kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na CCM, mabadiliko ya kisiasa hayakwepeki kisiwani Pemba kwa kuwa mambo yaliyokuwa kero kubwa kwa wananchi yametafutiwa ufumbuzi.

Alizitaja baadhi ya kero kuwa ni usambazaji wa umeme vijijini, mradi wa maji vijijini na uhifadhi wa mazingira, miundo mbinu ya barabara na kuunganisha umeme katika gridi ya taifa kutoka Tanga hadi Pemba.

Alisema CCM imesikitishwa na watu wanaopotosha historia ya Zanzibar na kuwataka kuacha mara moja tabia hiyo kwa vile mapinduzi ya Januari 12, mwaka 1964, ndiyo yaliyowakomboa Wazanzibari.

Alisema kusheherekea uhuru wa Desemba 10, mwaka 1963 ni sawa na kupoteza muda kwa sababu ulikuwa hauna faida yoyote kwa taifa.

Alisema Mapinduzi ya Zanzibar ndiyo yaliyomkomboa mnyonge kwa kupata elimu na kumiliki ardhi.

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad alidai kuwa CCM kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama vimeandaa njama ya kuchafua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa lengo la kuisaidia CCM kushinda viti sita Pemba.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma alipinga madai yaliyotolewa na Hamad kwa kusema “Hamad anaota ndoto za mchana na homa ya uchaguzi imempanda mapema

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s