Vipi utaichangia CUF

Ili kukabiliana na matukio hayo tusiyoyategemea na kufanikisha matayarisho ya chaguzi, CUF inahitajia shilingi za Kitanzania bilioni 8.4 (sawa na dola milioni 7 za Kimarekani). Kima hiki ni kikubwa kwa chama pekee kukipata, ndio maana CUF inahitaji msaada wa kila mpenda mabadiliko ya kidemokrasia, haki na maendeleo ya nchi yetu.

Maalim Seif Sharif Hamad

Maalim Seif Sharif Hamad

Mhe. Bwana/Bibi

KULETA MAGEUZI TANZANIA KUNAHITAJIA MCHANGO WAKO. CHANGIA ULICHONACHO UWE SEHEMU YA MABADILIKO

Katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja kuanzia sasa, tutaingia katika harakati za uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapo mwaka 2009 na katika kipindi kisichozidi miaka miwili Uchaguzi Mkuu wa Taifa hapo mwaka 2010. Kipindi hiki si muda mkubwa wa kujitayarisha kwa maandalizi ya chaguzi hizo, ambayo yanashirikisha – pamoja na mengine – kuwatayarisha mawakala wa kusimamia chaguzi na kununua vifaa vya kampeni.

Kutokana na uzoefu wa chaguzi tatu zilizopita, CUF haitegemei kwamba chaguzi za 2009 na 2010 zitakuwa huru, za wazi na za haki. Uzoefu huo unaonesha matumizi mabaya ya nguvu za dola dhidi ya raia wasio na hatia, uvunjwaji mkubwa wa haki za binaadamu na wizi wa kura, ambapo chama chetu hushindwa kuwahudumia waathirika kwa kukosa madawa na huduma za mawakili wanaowatetea kutokana na kesi za kubambikiziwa.

Ili kukabiliana na matukio hayo tusiyoyategemea na kufanikisha matayarisho ya chaguzi, CUF inahitajia shilingi za Kitanzania bilioni 8.4 (sawa na dola milioni 7 za Kimarekani). Kima hiki ni kikubwa kwa chama pekee kukipata, ndio maana CUF inahitaji msaada wa kila mpenda mabadiliko ya kidemokrasia, haki na maendeleo ya nchi yetu.

Tunakuomba mchango wako uingize katika Akaunti yetu:

Account Name: CUF Electoral Commission

Account Number: 011103008834

Bank Name: National Bank of Commerce, Corporate Branch – Dar es Salaam

Au:

Account Name: CUF Foreign Account

Account Number: 011105012592

Bank Name: National Bank of Commerce, Corporate Branch – Dar es Salaam

Swift Code of the Bank: NLCBTZT, XXXXX

Au:

Account Name: CUF – Tume ya Uchaguzi

Account Number: 021101003515

Bank Name: National Bank of Commerce, Zanzibar Branch

Kama mchango unatolewa kwa njia ya hundi, iandikwe:

i. Katibu Mkuu,

The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi)

P. O. Box 10797

Dar es Salaam.

Au:

ii. Katibu Mkuu

The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi)

P. O. Box 3637

Zanzibar.

Kwa fedha taslim au vifaa, tunaomba ujaze kima cha fedha au vifaa unavyokusudia kutoa katika fomu hii Tafadhali bonyeza hapa.

Tunatanguliza shukrani zetu za dhati.

.

JIKUMBUSHE USALITI WA CCM KWA WATANZANIA

Advertisements

11 thoughts on “Vipi utaichangia CUF

 1. kwanini hamuendelezi website yenu? na kuja ktk Blogu? does it means CUF tunaowatarajia wawe madarakani hawajui tofauti ya Blog na official website? Website inakaa hadi porns….maana yake hakuna mtu wa kusimamia…?

  CUF inashindwa nini kumlipa mtu alau lk 250 a month ajitolee kusimamia hata updates?

  KWanini Gazeti lenu hamlisimamii? lina muda sasa halipo mtaani…Does it mean hamjui umuhimu au la? hamjui watanzania wangapi wana access ya mtandao?…Hivi mnataka watu waamini kuwa mpo serious kuchukua NCHI?..brothers u need to change…

  • Assalam alaykum!

   Nami iungane na wewe juuya suali la kuwa na oficial webiste. Hizi habari za blog ni mambo ya mitaani. Tunataka kitu cha kuaminika. Zaidi sisi kama wanachama wa CUF ambao tuko mbali na nyumbani, tungependa kupata taarifa za kila siku za chama. Tuna Wawakilishi na Wabunge wetu, ni vyema na wao ama wakawa na webiste zao au kutumia ya makao makuu kwa kutowa taarifa kwa mambo wanayo fanya ndani ya majimbo yao na ndani ya Bunge au Baraza la Wawakilishi.

   Sisi licha ya upofu wetu, tuliliona zamani hili tatizo la Daftari… Inshangaza kwa viongozi wa CUF licha ya kuwa wamekuwa pamoja na CCM tokewa wakiwa CCM na sasa hivi Wapizani, lakini bado wanashindwa kujiwa mbinu za CCM!

   CCM hawaleti kitu bure bure, lazima huwa washajuwa kina manufaa kwao. Musitufanye tukawa hatuna imani na nyinyi kwa uzembe wenu!

   • Alaykum Salam Bikinunji,

    Tunaupokea na kuuthamini sana mchango wako wa mawazo juu ya kuwa na website badala ya weblog. Lakini tukuhakikishie kwamba kwetu hadi sasa njia hii ya weblog imekuwa na manufaa zaidi kuliko website. Watembeleaji ni wengi na wanaotuma maoni kama wewe pia ni wengi sana kuliko hata tulipokuwa na website.

    Hata hivyo, si kwamba tunadharau umuhimu wa website. Tunatarajia kuifufua ile tulokuwa nayo hivi karibuni na wakati huo tunaendelea na hii na weblog.

  • Nani kasema kwamba CUF inaongozwa na Seif na Lipumba tu? Inaonekana kasumba ulizolishwa za ki-CCM ndizo tatizo. CUF ni taasisi na kila taasisi ina taratibu zake. Ni kama ilivyo hiyo yenu ya ZIRPP.

   Kwani hakuna mwengine wa kuiongoza ZIRPP isipokuwa Muhammad Yussuf tu? Kwani ZIRPP ni Muhammad Yussuf na Muhammad Yussuf ni ZIRPP? Mbona kila mahala anaonekana na kutajwa yeye? Ukweli ni kuwa yeye ndiye kiongozi kwa sasa na lazima iwe hivyo. Sasa inashangaza nini inapokuwa kwa CUF?

   Hakuna chama chochote chenye demokrasia ya ndani iliyokomaa kuliko CUF Tanzania hii. Tunaku-challenge ufanye utafiti ikiwa kweli unataka kuujua ukweli.

   Uenezi na Mahusiano, CUF

  • Nilikuwa napitiapitia makala fulani katika Weblog yetu nikakuta taarifa hii inayoeleza jinsi ya kuichangia CUF. Nilipobonyeza hapo nikagundua matamshi yanayoonyesha kuwa yalitolewa na ZIRPPO; yaani Taasisi yetu, yanayoituhumu CUF kuwa ni “wababaishaji……” na kadhalika. Kusema kweli, nimeshangazwa sana na kauli hii kwa sababu haikutolewa na ZIRPP. Kwa mujibu wa katiba ya ZIRPP, Taasisi yetu haijafungamana na chama chochote kile cha kisiasa na kwa hivyo haiwezi kabisa kutoka kauli kama hiyo. Kwa hivyo, nimelazimika kuweka hili sawa kwa madhumuni ya kuondoa dhana yoyote ile iliyopo miongoni mwa viongozi na wafuasi wa CUF juu ya msimamo wa ZIRPP katika suala hili. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu kwa kunifahamu vyema. Muhammad Yussuf, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, ZIRPP.

 2. AMA KWAHAKIKA LAZIMA TUJIULIZE,KWANINI WATANGANYIKA WANAINGILIA KATI KATIKA MAAMUZI YETU, WAJUE KUWA DR KARUME NI RAIS WA WAZANZIBAR
  NA WANAOMSHAURI NI WAZANZIBAR SASA LINAWAKERA NINI NYIE?
  MPAKA HII LEO HAKUNA MMOJA ALIYEWAPONGEZA VIONGOZI HAO WALIOPENDANA NA WAKAKUBALIANA KWA KUWAONEA HURUMA WANZANZIBARI WENZIWAO JEE NYIE MNAITAKIA MEMA ZANZIBAR?
  JAMANI TUSHACHOKA TUACHILIENI KIDOGO TUPUMUE.

 3. jee… Wazanzibari mumefurahi maamuzi ya baraza la wawakilishi kupitisha matakwa muliokusudia ili mueze kujikwamua mulipo?

 4. Ni lazima chama kiwe na vision na hiyo vision iskirudishe kuwa chama kisicho na matumaini kama hivi sasa bara. Mikoa ya kanda ya ziwa hakuna harakati za kukiendeleza kilipokuwa na nguvu kama MIKOA YA mWANZA NA kAGERA Nna wala kabla ya uchaguzi mkuu ujao 2010 hakuna wakurugenzi wanao kuna wagombea katika majimbo semina pia hazipo hizo sheria hazieleweki na jinsi tu ya kujaza fomu za wagombea huwa tatizo.
  vaiongozi wetu waelewe kuna watu wanpoteza mali na hata kupata madhara baada ya kuwa mbadara wa chama kutulia.
  Viongozi wameshindwa kusimami a uchaguzi huru ndani ya chama migogoro haishi katika wilaya kam Tanga na Nyamagana .
  Katiba ya chama ilindwe ili chama kiendelee na sikuwa na viongozi wanaojaribu kuhakikisha chama kinashindwa uchaguzi na kuthibitishwa na viongozi wakuu wa chama katika mikutano wa ndani

 5. MADHAMBI WANAYOFANYIWA WAFANYAKAZI NA WAKULIMA WA NCHI HII.
  YAPO madhambi mengi wanayofanyiwa wananchi wa nchi hii na baadhi yake ni kama yalivyo hapa chini,
  -kuchota fedha kwenye mabenki, mifuko ya hifadhi, wizarani, mikoani na
  kwingineko kwa faida binafsi ya wanasiasa na wala sio wananchi,
  -watoto wetu kuteseka wakati wa kwend ana kurudi shule wakati wa kwao raha
  tupu,
  -kuthaminiwa matajiri na wanasiasa kiasi ambacho haki ya mnyonge huporwa akapewa tajiri mwenye mtaji, magari au majumba au mwanasiasa kwa cheo chake kikubwa bila watu kuona aibu, haya au kuogopa kumkosea muumba,
  -kulipishwa gharama za afya na tiba wakati wakwao wanatibiwa nje,
  -wanajenga mahekalu na makasri wakati wanashindwa kutuwezesha kile wakina Bryceson
  walichokifanya kwenye 1960,
  -siasa zinabomoa miji, biashara na uchumi mikoani,
  -wameachia mashule binafsi kupandisha mno ada kiasi fedha wanayochaji
  hailingani na gharama za uendeshaji wao,
  -imekuwa ni kawaida ya nchi hii kuongeza mafuta bila mpango hususan
  kutokana na ule ukweli kuwa kuwaachia watu binafsi peke yao kuendesha
  biashara ya mafuta ulikuwa uamuzi wa kuwatajirisha wachache na
  kuwamasikinisha wengi,
  -Isitoshe hakuna mikakati yoyote ile ya kuhifadhi mafuta achilia mbali
  kutafuta mafuta bara ili kuzalisha kile tunachostahili kutumia na kuuza ziada nje,
  -kutumia mabilioni ya fedha za wananchi kuendesha televisheni, redio na magazeti kihasara hasara bila faida yoyote ya maana wakati vyama vya siasa, watu binafsi na makampuni yanaweza kuifanya kazi hiyo vizuri zaidi na kwa faida kifedha kwa nchi,
  -kutumia magari ya kifahari yanayotumia mabilioni kwa ajili ya matengenezo na mafuta wakati inawezekana kabisa kuwa na magari mbadala imara na ya bei nafuu kutoka nchi kama Brazil, China, India na nchi nyingine kama hizo kuliko yale ya Japan na Ulaya,
  -Kulipa mabilioni kwa masurufu ya misururu ya safari kwa mamia ya maofisa ambao hakuna wanalochangia katika kupunguza umaskini nchini,
  -manispaa za miji zinazokwaza wakazi wa sehemu husika katika kuchangia maendeleo ya maeneo yao kwa kudai vibali vya kijinga hata pale mtu anapotaka kuchimba mtaro, kujenga barabara au daraja badala ya jambo hilo kushangiliwa kama kitendo cha wananchi kujitegemea na hususan hapa Dar es salaam,
  -Kuanzisha miradi inayofadhiliwa na watu na nchi za nje halafu serikali na wanasiasa kula fedha hiyo badala ya fedha hiyo kutumika kufanikisha malengo ya miradi,
  -kuwazuia wananchi kuuza mazao yao nchi za nje na kuwawekea bodi na mamlaka ambazo zimekuwa zikiwaibia tokea huko nyuma badala ya kufuta vyombo vya kilanguzi na wizi kama hivyo,
  -kushindwa kusaidia kwa vitendo maendeleo ya Mtanazania binafsi au vikundi vya ushirika na kulifanya jambo hilo kuwa na sura ya ksiiasa zaidi badala ya kijamii na kiuchumi,
  -kulazimisha shirika la ndege kufanya kazi ya kupeleka abiria badala ya kubeba mizigo ambayo ingelikuwa na tija zaidi na pengine kuigeuza nchi soko la kati kwa bidhaa zitokazo China, Mashariki ya Kati, Ulaya Mashariki na Marekani ya kUsini na ya kati,
  -kwenda nje na kushindwa kuona hali ilivyo huko na kuiga angalau machache kama vile usafi wa mji, miundo mbinu bora na mipango miji ambayo ingelichangia si haba kukuza biashara ya utalii na biashara nyinginezo,
  -kumuachia Mtanzania kuwa anatumia jembe la kisegerema miaka 50 baada ya uhuru,
  -kujilipa fedha nyingi zaidi wao wenyewe bila kuwa na uwiano wa michango yao kwa maendeleo ya watu na nchi,
  -kuachia makamapuni na migodi ya dhahabu na madini mengine kuinyonya nchi kutokana pengine na wao kunufaika na hisa, ukurugenzi au mapato ya makampuni hayo ya nje,
  -kushindwa kuendesha mashirika ya usafiri na kutegemea wakorofi wachache wanaofanya biashara hiyo sio kwa huduma ila kwa kutaka utajiri wa haraka haraka,
  -kuachia wananchi kula mafuta, sukari, maziwa ya watoto na vyakula vingine vinavyohatarisha afya ya watoto,
  -kushindwa kujenga viwanja vya michezo na burudani kwenye kata ili watoto wetu angalau wajiendeleze kwa michezo mbalimbali mitaani waliko,
  -kuachia kizazi kizima cha Watanzania kuwa kizazi kisichoajiriwa na hivyo kufanya hata waliojikwamua wenyewe kutoka umasikini kurudi tena kwenye umasikini,
  -kukubali na kuhimiza miradi ya kula fedha ambayo haiwezi kamwe kuchangia kuondoa kabisa tatizo linalotaka kumalizwa na mradi husika,
  -kuwaruhusu wachache kuiba au kukopa toka kwenye benki kuu na benki zinginezo na watu hao kujenga maghorofa yatakayowanufaisha wao binafsi na sio wananchi,
  -kuwadhulumu wale wanaohamishwa toka maeneo mbalimbali ili kupisha ujenzi wa miradi ya umma au binafsi isiyo na faida kwa muathirika baada ya yeye kudhulumiwa,
  -kushindwa kutumia rasilimali za bahari, maziwa na mito na hivyo kutia nchi umasikini zaidi,
  -kutumia mabilioni kufanya kazi mbalimbali kwa namna ambayo zinakuwa mbovu na zisizofaa wakati robo ya fedha inayotumika ingeweza kufanya kazi kubwa na bora zaidi kuliko iliyofanyika kwa kuwa wanaopewa kazi hizo wanatumia ujanja huu au ule na wana uhusiano na wakubwa,
  -kushinda kuiruhusu mikoa kujiendesha kiuchumi na mikoa kuendelea kuwa kama idara za serikali badala ya kampuni zinazojitegemea na kujiendesha kifaida,
  -kushindwa kuwadhibiti viongozi mbalimbali ili kila mmoja afanye kazi iliyokusudiwa toka ngazi ya chini hadi juu kabisa, kwa maneno mengine, serikali haina udhibiti wa siku kwa siku, mwezi kwa mwezi na robo mwaka kwa robo mwaka na ule wa kila mwaka kiasi mambo ovyo yanafanyika leo yasigundulike hadi baada ya miaka mitatu,
  -kushindwa kuhakikisha upatikanaji maji na umeme kwa kila mkulima na kila mfanyakazi na hivyo kuongeza ughali na ugumu wa maisha kwao,
  -kushindwa kuwasaidia Watanzania kwenda kufanya kazi za nje kama Kenya inavyofanya na hivyo kuwakosesha ajira malaki ya watoto wetu eti tu kwa sababu sio watoto wa viongozi au wa matajiri,
  -kuziachia benki kuwanyonya wananchi na kuwa na riba za viwango ambavyo vinachangia kuturudisha nyuma badala ya kutuendeleza,
  -serikali kushindwa kuhamia Dodoma na kuuza majengo yake hapa Dar es salaam ili jiji liwe la kibiashara na dodoma iwe ya kisiasa na hivyo kupunguza shida za usafiri kwa wananchi wa kawaida jijini,
  -kuendelea kujenga kila kitu katikati ya jiji badala ya kuwa na miji pembezoni kwenda maeneo ya Rufiji, Kibaha, Bagamoyo na Chalinze….
  Kubwa zaidi ni kuwa maendeleo katika nchi yoyote ile hayawezi kuaptikana kama VIONGOZI NA WANASIASA NDIO WANAOTAKA KUTAJIRIKA KWANZA KABALA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI HAWAJATAJIRIKA. Nendeni mkajifunze Imarati, kwingineko Uarabuni, China, Vietnam muone viongozi wanavyokubali kuwa masikini na chini ya wananchi ili wananchi wanyanyuke kwanza kisha wao ndio baada ya wananchi kuwezeshwa waanze kula nchi!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s