Tujiamini tulete mabadiliko

CUF inakusudia kufanya kila lililo kweye uwezo wake kushinda uchaguzi na kuunda Serikali itakayohakikisha utawala wa sheria wenye kutekeleza haki sawa kwa wote chini ya misingi ya haki za binaadamu. Serikali hiyo haitohakikisha tu upatikanaji wa mahitaji ya msingi kama afya na elimu na maji safi, bali pia itahakikisha kuzingatia vipa umbele vya kitaifa kwa kutumia vyema kodi na rasilmali za nchi kwa faida ya wananchi. Serikali hiyo itajenga misingi ya uchumi itakayowezesha kukua kwa uchumi unaotokana na kuwekeza katika sekta ya kilimo na sekta isiyorasmi ambayo ndiyo tegemeo kubwa la wananchi wanyonge wa taifa hili. Kuendeleza sekta hizi ndiko kutatoa ajira zaidi kwa kuendeleza viwanda vidogo vidogo kwa kuwasaidia na kuwaendeleza wajasiria mali.

Maalim Seif Sharif Hamad

Maalim Seif Sharif Hamad

Mhe. Bwana/Bibi

TUMEKOSA UONGOZI WENYE HEKIMA, KWA HIVYO TUJIAMINI TUFANYE MABADILIKO

Ahsante kwa kusoma waraka huu na hivyo kuwa sehemu ya wale wanaoiona haja ya kuwa na uongozi mpya kwa nchi yetu.

Inaeleweka na sote kwamba katika kipindi kisichozidi miaka miwili kuanzia sasa, tutaingia katika harakati za uchaguzi wa serikali za mitaa hapo 2009 na uchaguzi mkuu wa taifa hapo 2010. Tukizingatia ukubwa wa nchi yetu, hali mbaya ya barabara na miundo mbinu mengine, ukosefu wa uhuru wa vyombo vya habari unaofika kwa wananchi vijijini, mfumo usioaminika wa kuendesha uchaguzi, miaka miwili si muda mkubwa kujitayarisha kwa chaguzi hizo. Maandalizi ya chaguzi yanahusisha, pamoja na mengine, kuwatayarisha mawakala wa kusimamia uchaguzi huo, kununua vifaa vya uchaguzi pamoja na magari ya kampeni.

Kutokana na uzoefu wa chaguzi tatu zilizopita, haionekani dalili yoyote kwamba chaguzi wa 2009 na 2010 kuwa huru, za haki na za wazi. Uzoefu wa miaka 15 umetufunza kwamba uvunjwaji wa haki za binaadamu unaofanywa na vyombo vya dola huwa mkubwa mno. Chama chetu hushindwa kuwahudumia waathirika kwa kukosa madawa na huduma za mawakili wanaowatetea kutokana na kesi za kubandikizwa.

Kwa lengo la kupunguza mwanya wa uharibifu huo wa chaguzi, na kujiandaa na maafa tusiyoyategemea, tunalazimika kutafuta fedha na vifaa vingine kukabiliana na hali hiyo. Kiwango cha mahitaji hayo kwa chama chetu hakitapungua dola 7,000,000 za Kimarekani. Kima hiki ni kikubwa sana kwa chama pekee kukipata. Ndipo tunapohitaji msaada wa kila mpenda mageuzi na mpenda maendeleo ya nchi yetu kutusaidia.

CUF inakusudia kufanya kila lililo kweye uwezo wake kushinda chaguzi hizo na kuunda Serikali itakayohakikisha utawala wa sheria wenye kutekeleza haki sawa kwa wote chini ya misingi ya haki za binaadamu. Serikali hiyo haitohakikisha tu upatikanaji wa mahitaji ya msingi kama afya na elimu na maji safi, bali pia itahakikisha kuzingatia vipa umbele vya kitaifa kwa kutumia vyema kodi na rasilmali za nchi kwa faida ya wananchi. Serikali hiyo itajenga misingi ya uchumi itakayowezesha kukua kwa uchumi unaotokana na kuwekeza katika sekta ya kilimo na sekta isiyorasmi ambayo ndiyo tegemeo kubwa la wananchi wanyonge wa taifa hili. Kuendeleza sekta hizi ndiko kutatoa ajira zaidi kwa kuendeleza viwanda vidogo vidogo kwa kuwasaidia na kuwaendeleza wajasiria mali.

CUF itafanya hayo kwa sababu ndicho chama pekee kilichosimama na umma wakati wote kwa shida na raha na hasa wale wanaoteseka kotokana na huduma duni za serikali iliyopo. CUF itaendelea kuwa jasiri pekee katika kusimamia na kutetea maslahi ya wananchi bila woga, rushwa au kuvunja haki za binaadamu.

Ili tuweze kuyafanya hayo tunaomba msaada wako wa hali na mali. Kwa hili sisi tunakuamini kwamba una moyo wa kujitolea. Tunaomba ujiamini na utuamini, ili tulete mabadiliko kwa kuiondoa CCM madarakani. Sababu tunazo, nia tunayo na uwezo tunao. Tutimize tu wajibu wetu.

Mtumishi wako mtiifu,

KWA NINI UICHANGIE CUF

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s