Kwa nini uichangie CUF

 Hivyo kazi ya CUF na wewe unayechangia ni kujenga chama imara kilicho bora, chenye kuwatetea watu, chenye matumaini mapya kwa ajili ya Watanzania wa leo na wa kesho. Wakati tunafahamu kwamba kuchangia ni jambo gumu, lakini tunaamini kwamba kutoa ni moyo na si utajiri. Ugumu wa kazi hii haulingani na umuhimu wa kuifanikisha. Hivi ni vita ambavyo CUF na wewe – kwa pamoja – lazima tushinde. Tusishindwe maana tukishindwa leo, tutakuwa tumeshindwa 2009, 2010 na tutakuwa, kwa hinyo, tumeshindwa milele kumkomboa Mtanzania kutoka maisha haya mabaya, magumu na ya kidhalilifu.

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Haruna Lipuma

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Haruna Lupin

CUF NI CHAMA CHAKO, CHANGIA ULICHONACHO KWA FAIDA YAKO NA KIZAZI CHAKO

 CUF – Chama cha Wananchi kinasikitishwa na khofu waliyonayo wananchi na familia zao zinazosababishwa na:

 • Umasikini uliokithiri kutokana na kupanda kila siku kwa gharama za maisha,
 • Uhaba wa chakula na ukosefu wa maji safi na salama,
 • Ukosefu mkubwa wa ajira na usalama mdogo wa kazi walizonazo vijana
 • Hali duni ya elimu ya watoto wao ambao wazazi wanashindwa kugharimia
 • Ufisadi na rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma uliokithiri
 • Maradhi yasiyokwisha yaliyozidishwa na ugonjwa wa Ukimwi
 • Kilimo duni kisichopewa umbele katika kusaidia kukuza uchumi
 • Ubaguzi wa tabaka la matajiri wachache na masikini wengi

Nafasi ya CUF kwa Mabadiliko Tanzania:

 • Kwa miaka 15 sasa CUF imeendelea kuwaelimisha Watanzania kukubali kuleta mabadiliko ya uongozi wa taifa letu ili kuibadilisha hali hiyo. Hadi sasa CUF ndiyo chama pekee kilichoweza kujenga upinzani wa kweli katika mabaraza yote mawili ya kutunga sheria – Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
 • CUF imejenga mtandao wake katika Tanzania nzima kutoka visiwa vya Unguja na Pemba hadi Ngara mpakani na Burundi, kutoka Tunduru Kusini mwa Tanzania hadi Babati Kaskazini. Kati ya wilaya 140 za Tanzania, CUF ina uongozi uliokamilika katika Wilaya 120 hadi ngazi ya kata. Kwa wastani wanachama wa chama hiki zaidi ya 750,000 Tanzania nzima.
 • Katika chaguzi tatu za vyama vingi zilizofanyika CUF imebaki nambari mbili baada ya CCM na imebaki ndiyo iliyounda serikali kivuli katika mabaraza yote mawili ya kutunga sheria kwa miaka yote 15. Kati ya wabunge 45 wa upinzani bungeni 32 ni wa CUF. CUF pia kina wajumbe wa uwakilishi 25 katika Baraza la Wawakilishi lenye wajumbe 75 la Zanzibar. Pamoja na ugumu wa chaguzi za Zanzibar, zinazotawaliwa na uvunjaji mkubwa wa haki za binaadamu, matumizi ya vyombo vya dola kukisaidia chama tawala na kutofuatwa kwa taratibu za uchaguzi, bado CUF ina wajumbe 19 kati ya 50 wa kuchaguliwa.

 Kwa hivyo, CUF ndiyo tegemeo pekee la Watanzania, kwa Tanzania Bara na kwa Zanzibar.

Malengo ya CUF:

 • Kujenga upinzani imara, wenye nguvu na wenye kujitegemea kwenye Bunge na Baraza la Wawakilishi
 • Kuipunguzia CCM nguvu ya turufu wanayoitumia vibaya na kuzaa kibri cha kutetea waovu
 • Kujenga nguvu ya kuvunja ukuta uliojengwa na CCM unaosababisha kutugawa katika makundi ya kikabila na kidini
 • Kushinda uchaguzi 2010 na kujenga Tanzania mpya yenye neema kwa wote, kwa kumpa kila Mtanzania haki sawa mbele ya sheria na kutoa nafasi kwa kila mwananchi ya kujiendeleza na kupata maisha bora
 • Kuwajengea watoto wetu mazingira mazuri, si ya maisha bora ya baadae tu lakini pia mazingira mazuri ya maisha bora ya sasa
 • Kuwabadilisha askari wawe askari wa watu badala ya kuwa askari wa Dola
 • Kutoa elimu bora inayojenga umoja bila kuzingatia itikadi
 • Kuwaunganisha Watanzania wasahau yanayowatenganisha na kuhimiza yale yanayowaunganisha.

Imani ya CUF

 • CUF itafanya yote hayo kwa sababu inaamini kwamba wanaadamu wote ni sawa
 • CUF inaamini kwamba silaha kubwa ya kujenga Taifa moja ni kupendana na ndiyo maana itikadi yake ni “Haki Sawa kwa Wote” na “Neema kwa Wote”
 • CUF ina viongozi shupavu na wanaojiamini, wenye uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli kwa faida ya wote
 • CUF ndiyo sauti ya wasio sauti, wawe matajiri au masikini

Malengo haya na imani hii yataweza kutekelezwa kama CUF itaweza kuongeza uwezo wake kifedha, vitendea kazi na nguvu akili (human resources).

Katika haja ya kufikia malengo hayo, CUF inaanzisha mfumo wa kupata michango ya uingizaji wa mapato kutoka kwa wanachama, wapenzi na wale wote wanaoguswa na hali mbaya ya maisha ya Watanzania walio wengi. Lengo ni kukusanya fedha na hata vifaa ndani na nje ya nchi kwa muda mrefu bila kuwapa udhia wale walio tayari kuchangia.

Hivyo kazi ya CUF na wewe unayechangia ni kujenga chama imara kilicho bora, chenye kuwatetea watu, chenye matumaini mapya kwa ajili ya Watanzania wa leo na wa kesho. Wakati tunafahamu kwamba kuchangia ni jambo gumu, lakini tunaamini kwamba kutoa ni moyo na si utajiri. Ugumu wa kazi hii haulingani na umuhimu wa kuifanikisha. Hivi ni vita ambavyo CUF na wewe – kwa pamoja – lazima tushinde. Tusishindwe maana tukishindwa leo, tutakuwa tumeshindwa 2009, 2010 na tutakuwa, kwa hinyo, tumeshindwa milele kumkomboa Mtanzania kutoka maisha haya mabaya, magumu na ya kidhalilifu.

Hivyo basi tunahitaji kuwa na uhakika wa kukusanya fedha kidogo kidogo katika kipindi hiki kila mwezi ili kufanikisha programu ya malengo hayo. Mafanikio ya michango hiyo ndiyo yatayoweza kutupatia pato lenye kutosheleza na kulitumia kutupatia ushindi wa uchaguzi wa mwaka 2009 na 2010 ili kujenga Serikali yenye kujiamini au upinzani wenye kujitegemea utakaopunguza kura ya turufu ya CCM Bungeni na katika Serikali za Halmashauri za Wilaya.

CUF iko tayari kukutumikia kwa kuwatumikia wasio sauti.

Tunahitaji uongozi mpya kutumia rasilimali zetu kuleta neema kwa watu wetu.

Inawezekana, timiza wajibu wako

NAMNA YA KUCHANGIA

Advertisements

One thought on “Kwa nini uichangie CUF

 1. aslam alykumu marafiki nandugu wote pamojanawanachama wa cuf jemimi nimekuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kupigakurakwanjia compyuta je wana cuf mushajiandaa kwa hilo kwasabu hawo ccm niwizi nawanatafutakilanjia waibe kura zetu 2010 kwahiyo kuhusu upigaji kura kwa ID uwangaliwe vizurisana kwasabu hawo wenzetu hawana zamana

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s