Jikumbushe usaliti wa CCM kwa Watanzania

Jikumbushe kuwa mababu zetu walidai uhuru wa aina ya kwanza. Uhuru wa kuwaondoa wakoloni (wageni) wasituamulie maendeleo yetu na ya nchi yetu. Kazi hii ilifanywa na Julius Mwalimu Nyerere na Mzee Abeid Karume. Tunawapongeza. Uhuru huu ni uhuru wa kuwa huru (freedom for self-determination). Baada ya hapo tuliutafuta uhuru wa aina ya pili – uhuru wa kujikusanya na kutoa mawazo yetu (freedom of assembly and expression).

Chama cha Mapinduzi, CCM

Chama cha Mapinduzi, CCM

Jikumbushe maneno haya ya aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Retzer, alipokuwa akiwaaga Watanzania nyumbani kwake 30.08.2007 Dar es Salaam.

“Kwa bahati mbaya, matatizo ya kiafya yanayolikabili taifa hili, hayajabadilika. Mwaka 1985, Tanzania ilijua kwamba ina tatizo la ugonjwa wa Malaria, na ndiyo kwanza ilianza kutambua ina tatizo la Ukimwi. Leo hii zaidi ya Watanzania 400 wanakufa kila siku kutokana na Ukimwi. Hali hii ni kama kwamba ndege kubwa ya Boeing 747 huanguka kila siku na kila aliyemo humo hufa.

“Cha kusikitisha ni kwamba watanzania 100, 000 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa wa Malaria. Ukweli ni kwamba, mtoto mmoja mwenye umri chini ya miaka mitano hufariki kila dakika 10 katika nchi hii.

 “Kwa upande wa uchumi, Kampuni ya Booz Allen Consulting, wamefanya utafiti kutoa mapendekezo. Katika utafiti huo Tanzania ilichukua nafasi ya 127 kati ya nchi 175 kwenye kundi la ‘urahisi wa kufanya biashara.’ Ni vigumu kufanya biashara Tanzania.”

Kwa hivyo, tambua kwamba hapa ndipo walipotufikisha CCM!

Jikumbushe kuwa mababu zetu walidai uhuru wa aina ya kwanza. Uhuru wa kuwaondoa wakoloni (wageni) wasituamulie maendeleo yetu na ya nchi yetu. Kazi hii ilifanywa na Julius Mwalimu Nyerere na Mzee Abeid Karume. Tunawapongeza. Uhuru huu ni uhuru wa kuwa huru (freedom for self-determination). Baada ya hapo tuliutafuta uhuru wa aina ya pili – uhuru wa kujikusanya na kutoa mawazo yetu (freedom of assembly and expression).

Maandamano ya hapo 2001 kule Unguja na Pemba na Dar es Salaam, yaliyobabisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha ndiyo muhanga wa uhuru huo. Baada ya pale Watanzania sasa wana nafasi ya kufanya maandamano bila kubughudhiwa na Polisi. Tangu wakati huo, Watanzania wamepata uhuru wa kusema wa kutoa mawazo yao hata kama hawasikilizwi wasemayo.

Lakini tambua kuwa bado hatukupata uhuru wa aina ya tatu.

Huu ni uhuru wa sisi wananchi kuamua nani atutawale na vipi atutawale. Huu ni uhuru wa kuchagua viongozi wetu tunaowataka bila kulazimishwa. Huu ni uhuru unaopatikana kwa maamuzi ya wengi na kuwalinda wachache. Tutakapopata uhuru huu, ndipo tutakapokua tumekomboka.

Jikumbushe kuwa ndani ya miaka 45, tangu kupata uhuru wa kwanza, bado Tanzania yetu inaendelea kuwa masikini na tegemezi. Chama cha Mapinduzi (CCM) ndiye dhamana wa umasikini na udhalilifu wako, wewe Mtanzania.

Jikumbushe kuwa ndani ya miaka hiyo, CCM imekufanya yafutayo:

 • Ilikufukuza kwa nguvu nyumbani kwako na kukupeleka msituni kwa kile ilichokiita kujenga ‘Vijiji vya Ujamaa’. Sasa vijiji hivyo vyote vimeshakufa wala CCM hawavitaji katika kueleza maendeleo ya nchi hii.
 • Ilikulisha wewe na ndugu zako simba na hamukuwa na muombezi
 • Ilikunyang’anya mifugo na mali zako chache na kukubadilisha jina ukawa nyang’au ama bepari uchwara.
 • Ilizitaifisha mali na majumba ya Watanzania wenzako wachache walioanza kujimudu kiuchumi na sasa nyumba hizo hizo wanauziana viongozi wa CCM hiyo hiyo.
 • Ilimletea motto wako sera ya Elimu ya Kujitegemea iliyozaa UPE —Usome Pasipo Elimu
 • Imeiuza nchi kwa wageni na viongozi wa CCM na serikali zote mbili wameishia kujilimbikizia mali wenyewe peke yao
 • Imejigeuza kutoka chama cha wakulima na wafanyakazi na kuwa chama cha mafisadi

Kwa hivyo, tambua kwamba CCM imekusaliti wewe Mtanzania, imeisaliti nchi yako na imekisaliti kizazi chako.

Jikumbushe kuwa matokeo ya usaliti huo wa CCM ni:

 • Kuwabakisha Watanzania wengi wakiwa wajinga zaidi, masikini zaidi, na wenye maradhi zaidi
 • Kuwageuza watoto wetu kuwa:

             i. Jeshi la jamii haramia
ii. Jeshi la machinga linalopambana na askari wa jiji
iii. Jeshi la watoto wa mitaani wasio malezi ya wazazi
iv. Jeshi la dada zetu wanaoitwa changu doa
v. Jeshi la mayatima ambao wazazi wao waliofariki kwa Ukimwi
vi. Jeshi la watu wenye njaa, kiu na mateso

Je, pamoja na yote hayo, CCM ina jibu kwa Watanzania?

Haina. CCM imechoka. Vijana wa Mwalimu Nyerere na Mzee Karume wamechoka. Wametusaliti vya kutosha. Wametunyanyasa vya kutosha. Wametukandamiza vya kutosha. Sasa ni wakati wa kusema BASI! Basi kwa uonevu, basi kwa ukandamizaji, basi kwa usaliti, na basi kwa ufisadi!

Kwa hivyo, lazima Mtanzanzia useme BASI na BASI yako ilete mageuzi makubwa kupata uhuru wa aina ya tatu kwa:

 • Kupunguza nguvu ya turufu ya CCM Bungeni na Baraza la Wawakilishi
 • Kuongeza wingi wa wabunge wa CUF Bungeni na katika Baraza la Wawakilishi
 • Kushinda Serikali nyingi za mitaa, na Halmashauri za wilaya 2009
 • Kushinda uchaguzi Mkuu 2010

Kuna kila sababu ya kupata uongozi mpya kutumia rasilimali zetu kuwaletea neema watu wetu. Mabadiliko ni lazima na yatatokea tu pale ukweli unapojuilikana na umma uliochoka kama huu wa Watanzania.

Ndiyo maana tunahitaji msaada wako. Changia CUF kwa faida yako na kizazi chako. Changia sasa tutoke hapa tulipo!

HAKI SAWA KWA WOTE

TUJIAMINI TULETE MABADILIKO

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s