Je, hakuna haki za wanaume?

Na Salim Said

Nakumbuka nilipokua najiandaa na mitihani yangu ya darasa la kumi na mbili (Form IV), nilibahatika kufanya mitihani ya utani (mock exams) kanda ya Dar -es-Salaam ambayo huandaliwa makhsusi kwa wanafunzi wanaojiandaa mitihani yao ya taifa.

Katika karatasi ya maswali ya mtihani wetu wa somo la Kiswahili, sehemu ya mwisho ambayo kwa kawaida hukaa maswali ya fasihi, tulibahatika kukutana uso kwa uso na suali lililosomeka hivi! “Kwa kutumia vitabu viwili ulivyosoma, jadili nafasi ya mwanaume katika jamii”. Nimesema tulibahatika, kwani kupata suali kama hili halikua jambo linalodhaniwa katika vichwa vya watahiniwa wengi kwa muda huo, tulizoea tu kupata maswali yanayohusu nafasi ya mwanamke tu katika jamii na si kinyume chake kama ilivyotokea.

Tukio hili ndio nimependa liwe kianzio cha makala yangu  kwani katika akili, macho na hata masikio ya wanafunzi ni jambo lisilotarajiwa kukumbana na swali kama hilo katika mtihani yao ya taifa, utani (mock), muhula, nusu muhula na hata mazoezi ya darasani..

Ndugu yangu msomaji endelea kusoma ili uweze kujua yaliyojiri katika chumba cha mtihani baada ya watahiniwa kupewa, kufunua, kuanza kusoma na hatimae kukutana na suali nililolitaja hapo mwanzo katika mtihani wa Kiswahili. Kwa hakika lilikua ni suali gumu, geni, la ajabu na lisilowahi kuonekana au kusikika katika macho na masikio ya watahaniwa hao hata katika mitihani iliyopita (past papers). Jambo hilo lilimfanya moja kati ya watahiniwa kushindwa kuvumilia na kuamua kugonga meza kama kiashirio cha kumuita msimamizi (ivigilator) ili amweleze shida yake kwani kulingana na taratibu na kanuni za mitihani, mtahiniwa haruhusiwi kuongea akiwa katika chumba cha mtihani.

Kama wajibu wake alifika katika meza ya yule mtahiniwa kwa lengo la kutaka kujua shida yake, mtahiniwa alimueleza msimamizi kua suali hilo lilikua limekosewa na usahihi wake alidai kua ni nafasi ya mwanamke na si nafasi ya mwanaume katika jamii. Lakini msimamizi alikataa. Muda mfupi mtahiniwa mwengine alimuita msimamizi na kumueleza kesi hiyo hiyo.

Kuona hivyo msimamizi aliamua kututoa wasiwasi mbele ya chumba cha mtihani kua suali hilo lilikua sahihi na halikua na kosa lolote, hivyo aliwataka watahaniwa waendelee kufanya mtihani wao.

Wahenga walisema “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”. Kwa upande moja tulikua na haki ya kuhoji kuepo kwa suali kama hilo katika mtihani kwani ndivyo tulivyolelewa kua suali kama hilo haliwezi kutokea katika mtihani. Hii ni kutokana na ukweli kua walimu na hata wanafasihi na wasomi mbali mbali wanaochambua vitabu vya fasihi na kuuza kazi zao katika maduka mbali mbali ya vitabu kushindwa kuweka wazi au kutogusia kabisa nafasi ya mwanaume katika jamii na badala yake wanaelezea nafasi ya mwanamke tu katika jamii.

Hivi ni kweli mwanaume hana nafasi, umuhimu au kazi yeyote  katika jamii iwe nzuri au mbaya? Ni wazi kua mwanaume ana kazi, nafasi na umuhimu mkubwa katika jamii kisiasa, kiuchumi, kijamii na hata kiutamaduni.

Lakini kwa upande mwengine ambao nasema ndio sahihi ni kwamba hatukua na haki ya kuhoji wala kuuliza kuhusu usahihi wa suali hilo, kwani ukweli ni kwamba kuliko mwanamke na mwanaume ana nafasi kubwa na muhimu katika jamii, ila tatizo ni kwamba mfumo na kiwango cha elimu kimeshuka na wanafunzi wameegemea zaidi katika kukariri (cramming) kuliko kuelewa (understanding) na kupanua wigo wa mawazo yao, jambo ambalo linawadumaza kimawazo.

Pia kutokana na mambo yanayojitokeza katika Mashirika, Asasi na Taasisi mbali mbali za kitaifa na hata kimataifa zinazojishughulisha na kutetea haki za binaadam kwa ukaribu mambo yao yanalandana na haya yaliyojitokeza kwa wanafunzi.

Tumezoea tu kusikia aina mbali mbali za haki za binaadam na siku zao za kuadhimisha zikitangazwa katika redio na runinga kama si kuandikwa katika magazeti na vitabu pamoja na majarida mbali mbali, kama vile haki za watoto (children’s rights), haki za waandishi wa habari (journalists’ rights), haki za wanawake (women’ rights) na nyengine nyingi za makundi mbali mbali ya watu katika jamii, lakini cha ajabu na kweli ni kwamba sijawahi kusikia katika redio na runinga au kusoma katika magazeti wakitangaza kuhusu haki za wanaume au siku ya wanaume duniani au hata Taasisi au Asasi yeyote inayojishughulisha na utetezi wa haki za wanaume (men’s rights).

Kwa hakika jambo hili ndilo lililonifanya kuchukua kalamu na karatasi kuandika makala hii. Kimsingi nimeamua kuandika makala hii si kwamba ni mwanasheria laa, mimi si mwanasheria bali nimeamua kuandika makala hii ya “haki za wanaume” kutokana na sababu kuu mbili:-

Mosi, nimeamua kuandika makala hii kwa sababu mimi mwenyewe ni mwanaume lakini pili nimeamua kuandika makala hii kwa sababu mimi ni mwanafunzi ninaesomea shahada ya mawasiliano ya umma (Mass Communication).

Wanaotetea haki za wanawake kama vile TAMWA, TAWLA na mashirika ya kimataifa yanayotetea haki za wanawake wanapinga mambo mbali mbali anayofanyiwa mwanamke katika nyanja mbali mbali kama vile kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Miongoni mwayo ni kwa mwanamke kuachiwa au kufanyishwa kazi zote za nyumbani, kukatishwa masomo, kubakwa, kulawitiwa, unyanyasasaji katika maeneo ya kazi au katika ndoa na kudhulumiwa.

Suali ni je wanaume hawakumbani na matatizo kama hayo? Jibu ni kwamba na wanaume pia wanakumbana na matatizo kama kudhulumiwa, wapo wanaolatiwa, wapo wanaoolewa, wapo wanaonyanyaswa kazini, wapo wanaofanyishwa kazi nyingi za nyumbani (house boy). Kuna ushahidi wa kila aina kua wapo wanaume wanaofanyiwa mambo ambayo yanawanyanyasa na kuwadhalilisha lakini mashirika yote hayo na hata wanaume wenyewe wanatetea haki za wanawake na kusahau za kwao au za wanaume wenzao.

Kwa mfano, gazeti la “The Express” la tarehe 26/04/2005 liliandika na kuweka wazi jinsi wanaume wanavyonyanyaswa kijinsia kama vile kubakwa na kulawitiwa, kunyimwa huduma muhimu pamoja na kupigwa katika magereza makubwa kama vile Ukonga na Segerea.

Hili nalo vyombo vya kutetea haki za binaadam hawalioni na hawaliwaumizi vichwa sana lakini hukereka na kuumia sana pale wasikiapo vitendo kama hivi kafanyiwa mwanamke, utasikia tu katika kila aina ya chombo cha habari, mikutano, semina na makongamano wakilaani vitendo hivyo.

Ni wanaume wangapi wanaowa wanawake wenye uwezo wa kiuchumi na kujikuta wanafanywa kama mama wa nyumbani badala ya kua baba wa nyumba, lakini watu hawasemi kitu, wakati kitendo hiki hiki akifanyiwa mwanamke ni kinyume na haki za binaadam.

Na je mwanaume na mwanaume kuoana au kulawitiana ni sawa? Ni nani anakubali au kufurahi kuona au kusikia mumewe, mtoto wake wa kiume, kaka, mjomba, ami au jamaa yake yeyote wa kiume akiolewa au kufanyiwa vitendo vya liwati? Jibu ni kwamba hayupo anaependa, kukubali au kufurahia kuona hilo . kama hivyo ndivyo basi vitendo hivyo si vizuri kwani vinamnyanyasa mwanaume kijinsia na isitoshe linakwenda kinyume na maadili ya jamii.

Sasa kwa nini kazi ya kulaani vitendo hivi tunaiachia Misikiti na baadhi ya Makanisa? Nimetumia neno baadhi najua wasomaji watajiuliza kwani kuna baadhi ya makanisa duniani yanaruhusu vitendo kama hivyo kwa mwanaume? Naam ni kweli kabisa yapo baadhi ya makanisa Duniani yanaruhusu na kukubali kuongozwa na hata Askofu au Padri ambae ni shoga (anaelawitiwa). Tunamshukuru Mungu kwa Tanzania bado halijatokea hilo la kuongozwa na mtu ambae ni shoga katika nyumba za ibada na tunamuomba Mungu atuepushie mbali laana hiyo.

Jamani ni lazima ikumbukwe kua mwanaume ana haki, nafasi, majukumu na umuhimu sawa kama si zaidi na/kuliko makundi mengine ya watu katika jamii, ambayo yametengewa mpaka siku za maadhimisho, kama vile siku ya wanawake, wafanyakazi, wakulima, watoto na nyenginezo duniani. Kwa hiyo ipo haja na sababu ya kuwepo pia na taasisi, asasi na hata mashirika yatakayotetea haki za wanaume na siku ya kuadhimisha ambayo itawakutanisha wanaume katika kona mbali mbali duniani na kujadili mambo yao.

UKURASA 1 – KIKWETE AMEZUNGUKWA NA WAHAFIDHINA

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s