Polisi yashindwa kuizuia CUF kuandamana Alhamisi Dar

Na Kizitto Noya

 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limeruhusu maandamano yaliyopangwa na Chama cha Wananchi (CUF) kufanyika kesho jijini Dar es Salaam.Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliliambia gazeti hili jana kuwa polisi haina sababu ya kuwazuia CUF kuandamana, kwa kuwa ni haki yao.

 

”Waache waandamane kwa kuwa ni haki yao kwani ukiwazuia unawapa umaarufu usiokuwa na sababu. Wako huru kuandamana kama walivyotaka,” alisema Kamanda Kova.

 

Kova alisema hayo alipotakiwa kueleza endapo polisi itayazuia maandamano hayo kutokana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Idd Nyundo kuizuia CUF kutumia uwanja wa Mnazi Mmoja katika maandamano yao.

 

Kova alisema CUF wako huru kuandamana kwa utaratibu waliojiwekea kwani kikwazo cha kutotumia uwanja wa Mnazi Mmoja kimeondolewa baada ya polisi kuwasiliana na mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.

 

”Hakuna kikwazo tena tayari tumewasiliana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhusu suala la uwanja na tumekubaliana awaache wautumie,” alieleza Kamanda Kova.

 

Siku mbili baada ya CUF kuiarifu polisi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhusu nia ya kufanya maandamano yatakayoishia viwanja vya Mnazi Mmoja Septemba 9 mwaka huu, Mkurugenzi huyo aliwajibu kwamba uwanja huo hauruhusiwi kutumika kwa shughuli za siasa wala dini.

 

Lakini juzi Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alipuuza zuio hilo la uwanja na kusisitiza kwamba maandamano hayo yatafanyika siku na maeneo yaliyopangwa kwa kuwa suala la mkurugenzi huyo kuzuia uwanja ni hila.

 

CUF imepanga kufanya maandamano kesho kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa lengo la kuishinikiza serikali itaje majina ya watuhumiwa wa EPA na kisha kuwafikisha mahakamani.

 

Profesa Lipumba alieleza kuwa maandamano hayo yataanzia Buguruni kupitia barabara ya Uhuru hadi Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambako viongozi wa chama hicho taifa watahutubia.

Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=7330

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s