Uchumi: Hali ya Maisha ya Mtanzania kwa Ujumla

UMASIKINI wa kupindukia unazidi kuongezeka siku hadi siku. Inakisiwa kuwa kiwango cha watu masikini wanaoishi kwa matumizi yasiyofikia dola moja kwa siku kimeongezeka kutoka asilimia arobaini na nane (48%) iliyokuwepo mwaka 1992 hadi kufikia asilimia sabini na tano (75%) hivi sasa. Kwa maneno mengine ni kwamba mpaka kufikia mwaka 2005 Katika kila Watanzania 100, 75 walikuwa ni masikini wa kupindukia.

Makosa ya CCM kwa Ujumla

 • Sera mbaya za CCM zimechangia sana katika kuwatumbukiza wananchi wa nchi hii katika dimbwi la umasikini.
 • Serikali ya CCM imeshindwa vibaya katika suala zima la kuangalia vipaumbele; Mabilioni ya shilingi yamekuwa yakitumika katika semina, warsha, na makongamano ya kuzungumzia umasikini bila kupatikana kwa suluhisho la uhakika zaidi ya kutunisha mifuko ya walengwa.
 • Mfumo mbovu wa kodi unaowanyanyasa walipa kodi wadogo wadogo na kuwapendelea walipa kodi wakubwa unalipotezea Taifa mabilioni ya shilingi ambayo yangetumika katika programu za kupambana na umasikini.
 • Sera mbovu ya ubinafsishaji imesababisha mashirika mengi ya umma kuuzwa kwa bei ya kutupwa na kulipotezea Taifa mabilioni ya shilingi ambayo yangetumika katika programu za kupambana na umasikini.
 • Sera mbovu ya uwekezaji inatoa mwanya kwa wawekezaji kutoka nje kutorosha kutoka nchini mabilioni ya shilingi ambayo yangetumika katika programu mbalimbali za kupambana na umasikini.
 • Serikali ya CCM imeshindwa kutumia jiografia nzuri ya nchi yetu kuinua uchumi wa nchi na kuliongezea Taifa mapato.
 • Serikali ya CCM imekitelekeza kilimo ambacho kimsingi ndio uti wa mgongo wa Taifa letu.
 • Serikali ya CCM imekumbatia sera ya kupunguza watu kazi badala ya kuwa na sera ya kuongeza ajira. Katika jiji la Dar es Salaam, watu 46 katika kila 100 hawana ajira hata ya kubangaiza.

Ajenda ya CUF ya Kuleta Mafanikio

 • Zaidi ya robo tatu ya Watanzania wote ni wakaazi wa vijijini. Hii ina maana kwamba kimsingi tunapozungumzia umasikini wa Mtanzania, kwa kiasi kikubwa mlengwa ni Mtanzania wa kijijini. Kwa maana hiyo basi vita yoyote ya kuondoa umasikini nchini haiwezi kufaulu bila kipaumbele kutolewa kwa maeneo ya vijijini.
 • Watanzania wengi walioko vijijini au ni wakulima, wafugaji, wavuvi, au ni wenye kufanya shughuli mchanganyiko. Sehemu kubwa ya shughuli zote hizi inahusu uzalishaji na kwa hivyo basi kusudio la kupunguza au kuondosha umasikini ni lazima lilenge kwanza kwenye kuboresha uzalishaji; na pili, kutafuta masoko ya uhakika. Kuboresha uzalishaji kuna maana ya kuboresha mipango, miundombinu, na ushauri wa kitaalamu.
 • Masoko ni kitu kinachoundwa kwa makusudi baada ya kusoma mazingira na kugundua kuwepo kwa mahitaji.
 • Serikali ya CUF itaelekeza nguvu kubwa katika kupambana na umasikini nchini. Hii ina maana kuwa itaelekeza nguvu kubwa katika:
 • Kuboresha uzalishaji vijijini na kuunda masoko ya uhakika ya vile vitakavyokuwa vinazalishwa. Halmashauri za Wilaya zitakuwa ni vituo muhimu katika kufanikisha mkakati huu.
 • Kutafanyika mabadiliko ya msingi ambapo Halmashauri zitabadili mwelekeo kutoka kuwa ni asasi zinazoshughulikia zaidi huduma za kiutawala na kuwa ni asasi zinazoshughulikia zaidi masuala ya kupambana na umasikini.
 • Chini ya mwelekeo huu mpya kila halmashauri itawajibika kuweka mazingira yatakayovutia uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo vitakavyotumika kuongeza thamani ya mazao mbalimbali yanayozalishwa vijijini, ili kuweka mazingira ya masoko ya uhakika zaidi kwa mazao hayo, na hivyo kutoa ushawishi kwa Wananchi wengi zaidi wa vijijini kujiajiri katika uzalishaji wa mazao hayo. Aidha ajira itakayopatikana kwenye viwanda hivi itaongeza mzunguko wa fedha wa kudumu kwenye maeneo ya vijijini na hivyo kuchochea ukuaji wa ajira katika sekta zingine zisizo rasmi.
 • Mfumo usioridhisha wa kodi utafanyiwa marekebisho ili mabilioni ya shilingi yanayopotea hivi sasa kutokana na misamaha holela ya kodi yaokolewe na kuelekezwa kwenye mapambano dhidi ya umasikini.
 • Jiografia nzuri ya nchi yetu inayoruhusu kuibua vyanzo vya mapato takriban katika kila nyanja itatumika kukuza uchumi na kuliongezea Taifa mapato.
 • Kilimo kitapewa msukumo mkubwa.
 • Serikali itaanza kushughulikia uwezekano wa kuwalipa mafao ya uzeeni wazee wote wanaofikia miaka 70 na kuendelea kupitia idara ya ustawi wa jamii.

PREVIOUS … NEXT…..

Advertisements

One thought on “Uchumi: Hali ya Maisha ya Mtanzania kwa Ujumla

 1. Pingback: Tupe nafasi tuibadilishe Tanzania | Haki Sawa kwa Wote

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s