Sekta Muhimu za Uchumi: Uvuvi

Tanzania ni nchi ambayo ina ukanda mrefu wa bahari na mshirika katika maziwa makuu matatu yaliyomo kwenye Bara la Afrika. Zaidi ya hayo ina maziwa mengine madogo madogo mengi na mito kadhaa mikubwa. Maji yote haya yana utajiri mkubwa wa samaki na bidhaa nyingine za majini. Sekta ya uvuvi pekee ingeliweza kuchangia kiasi kikubwa kabisa katika pato la Taifa na kupunguza umasikini unaoikabili jamii ya wavuvi nchini. Hata hivyo wavuvi wenyewe ni mashahidi kuwa hakuna juhudi za dhati zilizofanywa kuwaunga mkono, kiasi kwamba uvuvi wao wa leo hauna tofauti sana na ule uliofanywa na mababu zao.

Kukosekana kwa zana bora za kisasa za uvuvi kumewafanya wavuvi wengi wasiweze kupata samaki wa kutosha na ili kukabiliana na gharama za maisha zinazoongezeka kila siku wengi wao wamejiingiza katika vitendo vya hatari na vyenye uharibifu mkubwa – uvuvi wa kutumia mabomu na sumu. Ni wazi kuwa siyo tu kwamba mabomu na sumu yanafanya uharibifu mkubwa wa mazingira na kuhatarisha maisha ya walaji wa samaki, lakini uvuvi wa namna hii ukiendelea baada ya miaka michache ijayo hakutakuwa tena na sekta ya uvuvi nchini, na wavuvi waliokuwa wanadhani wanaupiga vita umasikini, watajikuta ni masikini maradufu zaidi.

Kasoro za CCM

 • Serikali ya CCM haijafanya juhudi zozote za makusudi kuwasaidia wavuvi wetu kuingia katika uvuvi wa kisasa. Hali hii imesababisha Taifa lishindwe kufaidika na utajiri mkubwa wa samaki tulionao katika eneo letu la bahari.
 • Wavuvi wa kizalendo kutokana na kuwa na vyombo duni wamekuwa hawawezi kwenda katika maeneo ya mbali na mwambao yenye kina cha bahari cha maji marefu wanakopatikana samaki wengi. Hali hii imesababisha uvuvi katika maeneo haya kuingiliwa na wavuvi wa kigeni ambao wamekuwa wakiendesha shghuli za uvuvi kinyume cha sheria na kuliibia Taifa raslimali hii muhimu.
 • Pamoja na kuwa na utajiri mkubwa wa samaki, kutokana na uchache wa samaki wanaovuliwa, bei ya samaki katika soko ni ya juu kuliko inavyopaswa kuwa.
 • Pamoja na kwamba uvuvi wa uharibifu wa mazingira unafanywa na wavuvi wote; wakubwa na wadogo, serikali ya CCM imekuwa ikitumia dola vibaya kuwanyanyasa wavuvi wadogo wadogo tu.

Ajenda ya CUF kwa Mafanikio

Ili kuiboresha sekta ya uvuvi, Serikali ya CUF itachukua hatua zifuatazo:

 • Kuongeza tija.
 • Utaanzishwa mfuko rasmi wa kudumu wa kulea na kukuza uvuvi ili kuwasaidia wavuvi na wananchi wengine wenye nia ya kujiajiri kwenye sekta hiyo, kwa ajili ya kununulia vifaa vya kisasa vya uvuvi na hifadhi.
 • Huduma ya mafunzo kwa wavuvi itaimarishwa. Kwa kiasi kikubwa italenga katika matumizi ya njia bora za hifadhi ili kuhakikisha kuwa mavuno ya wavuvi hayapotezi ubora wake kabla ya kufika kwenye soko.
 • Shughuli za doria katika maeneo ya uvuvi zitaimarishwa ili kuhakikisha kuwa wavuvi wachache hawaendelei na utaratibu wa uvuvi unaoharibu mazingira na kuleta maangamizi makubwa kwa samaki na viumbe wengine wa majini; na ambao una muelekeo wa kuhatarisha ajira kwenye sekta ya uvuvi.
 • Uboreshaji wa soko na upanuzi wa ajira.
 • Juhudi zitafanywa kuhakikisha kuwa wawekezaji zaidi wa ndani na nje ya nchi wanafungua viwanda vya kusindikia minofu ya samaki katika maeneo yote yenye mavuno makubwa ya samaki, hususan katika mwambao wa bahari ya Hindi.
 • Huduma za ukaguzi na uchunguzi zitaimarishwa ili kuhakikisha kuwa siku zote mavuno yetu ya samaki yanakuwa katika kiwango cha juu cha ubora ili kujihakikishia mauzo mazuri katika masoko, hususan ya nje.
 • Halmashauri za miji na wilaya zilizoko kwenye maeneo ya wavuvi zitahamasishwa kuingia ubia na makampuni binafsi kujenga maghala ya hifadhi baridi (Cold Storage Facilities) kwa ajili ya kuwasaidia wavuvi kuhifadhi mavuno ya ziada kwa kulipa ushuru kidogo.

PREVIOUS… NEXT….

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s