Sekta Muhimu za Uchumi: Utalii

Ziko nchi nyingi ulimwenguni ambazo zinategemea kwa kiasi kikubwa biashara ya utalii kuweza kufidia gharama za mahitaji ya wananchi wake. Nchi hizi zimefanikiwa kwa sababu zimewekeza kwa dhati kwenye sekta hii, pamoja na kwamba baadhi yake hazina vivutio vingi vya watalii. Bahari ya Hindi, Visiwa vya Zanzibar na Mafia, Delta ya mto Rufiji, mbuga za wanyama za Serengeti, Ngorongoro, Lake Manyara, na Selous, milima Kilimanjaro na Meru na ukarimu wa wananchi wetu na tamaduni zao, unaifanya Tanzania kuwa nchi ya pekee kwa mapumziko murua kwa wageni watokao nchi za Ulaya, Marekani na Asia. Gazeti la Financial Times la Uingereza katika moja ya matoleo yake limeelezea kuwa Tanzania “Offers one of the world’s most complete holiday destinations”. (Ni moja ya nchi za dunia zinazofaa kutembelewa na anayehitaji mapumziko murua ya uhakika). Hata hivyo hatujautumia urithi huu kikamilifu kuinua hali ya maisha ya Watanzania tuliopo sasa na wale wa vizazi vijavyo.

Kasoro za CCM

 • Kwa muda mrefu serikali ya CCM ilitelekeza kuwekeza katika miundo mbinu muhimu inayohitajika kwa huduma ya utalii.
 • Kwa muda mrefu dhana ya utalii kwa serikali ya CCM imejikita katika utalii wa asili, yaani ule wa kuja kuangalia mbuga za wanyama au kupanda mlima Kilimanjaro, na kusahau kuendeleza maeneo ya utalii ya aina nyingine.
 • Serikali ya CCM imeshindwa kuhamasisha utalii wa ndani kiasi cha kutosha.
 • Kwa kiasi kikubwa serikali ya CCM imetelekeza kutoa huduma za kutosha kwa wafanyakazi wa idara ya wanyama pori na matokeo yake ni kwamba wafanyakazi hawa wanashindwa kutoa huduma stahiki kwa wanyama pori.
 • Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko kuwa ugawaji wa maeneo maalum ya uwindaji hauzingatii maslahi ya Taifa na serikali ya CCM imechagua kukaa kimya.
 • Wananchi waishio katika au kandokando ya maeneo ya vivutio vya kitalii hawashirikishwi katika kutengeneza mipango ya kulinda mazingira na hawafaidiki na mapato ya utalii

Ajenda ya CUF ya Kuleta Mafanikio

Serikali ya CUF itachukua hatua zifuatazo ili kuipa sekta ya utalii msukumo unaotakiwa:

 • Kuimarisha miundo mbinu.
 • Serikali itahakikisha inaimarisha mawasiliano ya aina zote katika maeneo mbali mbali ya nchi yetu ambayo kwa hivi sasa yako kwenye ukanda wa utalii.
 • Serikali itatafuta wawekezaji zaidi kuwekeza katika huduma za watalii kama vile mahoteli, usafirishaji, uandaaji wa ziara n.k.
 • Serikali itawashirikisha wananchi waishio katika maeneo ya vivutio vya utalii katika kuandaa sera za kulinda mazingira na kuhakikisha wananufaika waziwazi na mapato ya utalii
 • Kupanua shughuli za utalii
 • Hivi sasa shughuli za kitalii nchini zimeelemea sana kwenye utalii wa kiasili, yaani ule unaohusu watalii wa kawaida wanaofika kuangalia mbuga za wanyama, kupanda mlima Kilimanjaro, na kuzuru fukwe zetu za Zanzibar na Bagamoyo. Hata hivyo nchi yetu bado ina nafasi kubwa sana ya kuweza kujiongezea mapato yatokanayo na utalii na kupanua ajira kwa kukuza aina nyingine za utalii. Serikali ya CUF pamoja na kuchukua hatua za kuimarisha utalii wa kiasili, pia itasimamia kwa karibu uanzishwaji na ukuzwaji wa utalii wa kimazingira na kiutamaduni (eco-tourism & cultural tourism). Utalii wa aina hii utawavutiwa wageni wengi wenye nia ya kujua Watanzania wanavyoishi na mazingira yao, hususan wanafunzi na watafiti. Aidha serikali itafanya juhudi kubwa kuhamasisha na kutoa vichocheo kwa watalii wa ndani. Matarajio ni kuongeza pato linalotokana na utalii kutoka wastani wa dola za kimarekani milioni 700.00 kwa mwaka za sasa, hadi wastani wa dola milioni 1500.00 kwa mwaka katika miaka 5 ijayo.
 • Kukuza na kupanua soko la utalii.
 • Pamoja na kuimarisha miundo mbinu ya kitalii na kupanua vivutio vya utalii, serikali ya CUF itafanya juhudi kubwa kuitangaza biashara yetu ya utalii nchi za nje, ikiwa ni pamoja na kuanzisha kituo kikubwa cha utalii kwenye mtandao wa internet ambacho kitakuwa na habari zote muhimu kwa wageni wenye nia ya kuizuru nchi yetu.
 • Huduma kwa wafanyakazi wa idara ya wanyamapori zitaimarishwa kwa kiasi kikubwa kwa kutoa maslahi zaidi na vitendea kazi. Kuimarishwa huku kwa huduma kutakuwa ni motisha kwa wafanyakazi hawa kutoa huduma bora na ya uhakika zaidi siyo kwa wanyamapori tu, bali pia na kwa watalii wanaouzuru maeneo yao.
 • Kusimamia maeneo ya uwindaji
 • Serikali itachunguza tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa katika maeneo haya na kuchukua hatua muafaka kurekebisha matatizo yaliyopo.

PREVIOUS… NEXT…

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s