Sekta Muhimu za Uchumi: Maliasili, Misitu na Mapori ya Asili


Tanzania ni nchi ambayo imejaaliwa misitu na mapori mengi ya asili yenye mchanganyiko mkubwa wa mimea. Pamoja na kwamba mimea hii imekuwa ikichangia uchumi wetu kwa kiasi fulani, bado mkazo wa kutosha haujawekwa kuhakikisha kwamba faida yote iliyomo kwenye mimea hii inapatikana. Mathalani, madawa asilia ambayo nchi nyingine, kwa mfano Costa Rica, ni sekta inayoingiza mabilioni ya Dola kwa mwaka, hapa kwetu haijaendelezwa. Hali kadhalika, uchumi wa mimea yetu ya asili kwa matumizi yasiyo ya kitiba nao haujaimarishwa. Mfano mzuri ni uvunaji wa Gum Arabica ambayo ni utomvi mgumu utumikao kuimarisha vinywaji vya aina mbalimbali. Mbali ya kwamba kuna soko kubwa la bidhaa hii ulimwenguni, na bidhaa yenyewe inapatikana kwa wingi nchini hasa katika mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, na Shinyanga mpaka sasa hakuna hatua madhubuti ambazo zimekwisha chukuliwa kukuza mauzo yake.

Kasoro za CCM

  • Hakuna juhudi za dhati za kuhakikisha kuwa uvunaji endelevu wa mali asili iliyoko katika misitu na mapori ya asili yaliyoko nchini unatumika kunyanyua pato la Taifa.
  • Hakuna taratibu zinazotabirika zinazosimamia uvunaji na uuzaji wa bidhaa zinazotokana na mali asili yetu. Matakwa binafsi ya viongozi wa serikali bado yanachukua sehemu kubwa ya maamuzi yanayofanywa kuhusiana na biashara ya mali asili. Mfano mzuri unahusu biashara ya magogo. Wafanya biashara ya magogo hivi karibuni walijikuta katika wakati mgumu baada ya serikali kupiga marufuku biashara ya magogo wakati baadhi yao magogo hayo waliyashayavuna na tayari yalikuwa bandarini kwa ajili ya kusafirishwa nje.
  • Serikali kwa kiasi kikubwa imezitelekeza taasisi zetu zinazoshughulika na tafiti zinazohusu mimea asilia, na hususan katika nyanja ya madawa. Matokeo yake ni kwamba taasisi hizi zinafanya kazi kikamilifu tu pale zinapopata wafadhili wa nje ambao huja kuhodhi matokeo na manufaa yanayotokana na tafiti hizo.
  • Kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika maeneo yote yanayozunguka hifadhi za Taifa. Wanavijiji wamekuwa hawana haki ya kulinda mazao yao dhidi ya wanyama waharibifu, na pale wanapochukua hatua dhidi ya uharibifu wowote wamekuwa wakinyanyaswa, kupigwa, na hata kubambikiziwa kesi na askari wa wanyama pori.

Ajenda ya CUF ya Kuleta Mafanikio

Ili kuhakikisha kuwa Taifa linanufaika kikamilifu kutokana na misitu na mapori yake, Serikali ya CUF itachukua hatua zifuatazo:

  • Kufanya tathmini ya mimea asilia inayopatikana nchini. Tathmini hii itafanyika kwa lengo la kujua aina, wingi, mahali inapopatikana na matumizi yake ya kijadi. Tathmini hii itafanywa na idara husika katika chuo chetu Kikuu cha Dar-es-Salaam kwa kusaidiwa na Wananchi mbali mbali wenye ujuzi mbali mbali wa kijadi. Aidha vitengo vya matumizi ya miti asilia katika Taasisi ya Madawa Asilia ya Chuo Kikuu kishiriki cha Tiba, na Idara ya Kemia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam vitaimarishwa.
  • Kuanzisha benki maalum ya kuhifadhi viasili (Gene Bank). Kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kimataifa na idara zinazohusika katika vyuo vyetu vikuu vya Dar-es-Salaam na Sokoine, serikali itaanzisha benki maalum ya kuhifadhi kila aina ya mmea asili unaopatikana nchini, kama kinga endapo janga lolote laweza kusababisha aina yoyote ile ya mmea kutoweka.
  • Kuandaa sera ya kitaifa kuhusu uvunaji endelevu wa mimea asilia. Sera hii itasaidia sana katika kuweka taratibu za wazi na zinazotabirika za kusimamia uvunaji na biashara ya mimea asilia, hususan kwa ajili ya masoko ya nje.
  • Kutafuta masoko. Ili wananchi mbalimbali hususan wale ambao tayari wana ujuzi wa matumizi mbalimbali ya mimea ya asili waweze kunufaika kikamilifu na ujuzi wao, serikali itawatafutia masoko ya nje ya nchi na kuwaelimisha juu ya viwango vya ubora unaohitajika. Pamoja na mambo mengine serikali itafungua kituo katika mtandao wa internet ambapo wote wenye leseni ya kufanya biashara hii wanaweza kuorodhesha bidhaa zao na kuwasiliana na wateja.
  • Serikali ya CUF itahakikisha kuwa Wananchi wanalipwa fidia kwa mali na mazao yao yanayoharibiwa na wanyamapori wanaotoroka kutoka katika hifadhi za Taifa. Aidha elimu ya uraia itatolewa kwa watendaji wote wa hifadhi za Taifa ili waweze kuzingatia haki za binadamu.

PREVIOUS… NEXT…

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s