Sekta Muhimu za Uchumi: Madini

Nchi yetu ina madini mengi ikiwa ni pamoja na dhahabu, almasi, bati, chuma, uraninium, phosphate, makaa ya mawe, vito, nickel, chokaa, jasi, jaribosi, chumvi, mfinyanzi na gesi. Madini haya hayajatumiwa kukuza uchumi wa nchi na kuboresha hali ya maisha ya wananchi.

Kasoro za CCM

 • Serikali ya CCM imekuwa na sera ya makusudi ya kuwapiga vita wachimbaji wadogo wadogo wa madini badala ya kuwasaidia kuboresha shughuli zao. Kutokana na sera hii wachimbaji wadogo wadogo wengi wamepoteza ajira zao na mapato ambayo awali yaliwasaidia sana wao wenyewe na jamii iliyowazunguka popote pale walipokuwa.
 • Serikali ya CCM imekuwa na sera ya kukabidhi maeneo yote yanakopatikana madini kwa wachimbaji wa kigeni. Jambo la kusikitisha ni kuwa makabidhiano haya yanaambatana na mikataba mibaya sana kwa maslahi ya Taifa. Takriban madini yote yanayovunwa katika maeneo husika huwanuifaisha wageni hao na kuliacha Taifa likiwa mikono mitupu. Mikataba hii inaonyesha kuwa katika kila shilingi 1000/= inayopatikana baada ya madini hayo kuuzwa ni shilingi 30/= tu ambayo Tanzania inapata kama mrahaba. Katika hatua nyingine ya kushangaza hivi karibuni serikali imeingia mkataba na kampuni moja kuhakiki kiasi cha madini kinachochimbwa nchini na makampuni ya kigeni na mkataba huo unaonyesha kuwa katika mrahaba wa shilingi 30/= ambazo Tanzania imekuwa ikipata, kampuni hiyo itakuwa inachukua shilingi 19/= na kwa hivyo Taifa la Tanzania kubakiwa na kiasi cha shilingi 11/= tu!

Ajenda ya CUF kwa Mafanikio

Serikali ya CUF itachukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa utajiri mkubwa wa madini ya nchi yetu unatumika kikamilifu kuinua hali ya uchumi wa nchi yetu na hivyo kuboresha hali ya maisha ya watu wetu. Miongoni mwa hatua hizo ni hizi zifuatazo:

 • Kuzindua sera mpya ya uwekezaji katika sekta ya madini.
 • Sera mpya ya madini itazinduliwa kwa lengo mahsusi la kulinda maslahi ya wananchi na wachimbaji wadogo wadogo. Pamoja na mambo mengine sera hii itaweka utaratibu ufuatao kwa wawekezaji wa ndani na nje:
 • Mapato ya serikali toka kwenye madini yanayouzwa yataongezwa kutoka asilimia tatu (3) ya sasa hadi kufikia walau asilimia thelathini (30), ili kuwepo na uwiano wa mapato ya migodi yetu na ile ya Kusini na Magharibi mwa Afrika.
 • Thamani ya mitaji ya wawekezaji itasimamiwa na kudhibitiwa kikamilifu ili kuyabana makampuni yanayowekeza yasiongeze thamani hewa juu ya thamani halisi ya mitaji yao (over invoicing of capital expenditure).
 • Migodi yote mipya itasamehewa ushuru wa forodha kwa asilimia 100 kuhusiana na mitambo itakayoingizwa kabla ya kuanza uzalishaji, na baada ya kuanza uzalishaji itapata msamaha wa kodi ya mapato wa asilimia 100 katika miaka miwili ya kwanza. Baada ya kipindi hicho kila mgodi utalazimika kulipa kodi kamili ya serikali kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa.
 • Ili kuweza kuwapatia huduma muhimu ikiwa ni pamoja na masoko mazuri na kuwaendeleza kitaalam, serikali itawasaidia wachimbaji wadogo wadogo wajisajili kama kampuni na kwamba kampuni inayohusika ndio itakayomilikishwa mgodi unaohusika.
 • Vitalu ambavyo vimetelekezwa kwa muda mrefu bila kuendelezwa vitashughulikiwa kwa mujibu wa sheria husika.
 • Wawekezaji watahamasishwa kuanzisha viwanda vya kuboresha madini husika kabla ya kuuzwa nje (polishing industries) ili kuyaongezea thamani na kukuza ajira rasmi.
 • Ili kupunguza tatizo la walanguzi ambao siku zote wamekuwa wanyonyaji wakubwa wa wachimbaji wadogo wadogo na kuikosesha serikali mapato yake utaratibu ufuatao utatumika:
 • Serikali itaweka utaratibu wa kuwapatia wachimbaji taarifa muhimu zinazohusu bei katika masoko ya ulimwengu kila mwanzoni mwa juma.
 • Kila kwenye eneo la machimbo kutakuwa na mnada wa madini mbali mbali yanayopatikana hapo. Wafanyabiashara watakaotaka kushiriki kwenye mnada watatakiwa kukata leseni halali zinazowaruhusu kununua madini.
 • Kupanua wigo wa aina ya madini tunayouza na masoko yake.
 • Pamoja na juhudi zinazoendelea hivi sasa za kuvuna utajiri wa madini tulionao, bado juhudi hizo zimesahau kushughulika na baadhi ya maeneo ambayo yangeweza siyo tu kuongeza ajira, lakini pia kuliingizia taifa mapato. Mathalani, madini ya chumvi na mfinyanzi. Haya ni madini ambayo yanapatikana nchini kwa wingi kabisa na ambayo hayana tatizo la masoko. Wakati chumvi ina soko kubwa katika nchi jirani ambazo hazina vyanzo vingi vya madini hayo, mfinyanzi ni madini yenye soko kubwa katika viwanda vya petroli sehemu mbali mbali ulimwenguni.
 • Serikali ya CUF itahakikisha kuwa wananchi kwa wingi zaidi wanajishughulisha na shughuli za uzalishaji wa madini haya, ikiwa ni pamoja na kuwatafutia masoko.
 • Kuweka juhudi maalum ya kuanza kuchimba mafuta ya petroli yanayosadikiwa kuwepo katika eneo la bahari ya Hindi ndani ya Tanzania. Pamoja na kuwepo kwa gesi, mafuta ya petroli pia yapo katika maeneo ya bahari ya Hindi. Serikali itaingia mikataba ya ubia na makampuni yenye uwezo wa kuchimba petroli baharini ili Tanzania ianze kunufaika na mali ya asili hii yenye bei kubwa katika soko la dunia.
 • Kuchimba chuma na makaa ya mawe yaliyoko kusini ya Tanzania na kuanzisha viwanda vya chuma cha pua.
 • Serikali itaingia mikataba ya uhakika na makampuni yenye teknolojia na mtaji ili yachimbe chuma na makaa ya mawe na kuweza kuanzisha viwanda vya chuma cha pua. Kuna soko kubwa la makaa ya mawe, chuma na chuma cha pua, hasa katika Jamhuri ya Watu wa China.

PREVIOUS… NEXT…

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s