Misingi Mikuu ya Uongozi wa Nchi: Ulinzi na Usalama

Suala la Ulinzi na Usalama wa Taifa linapaswa kupewa uzito unaostahili.

Kasoro za CCM

 • Kwa muda mrefu sasa serikali ya CCM imetelekeza wajibu wa kuhakikisha kuwa vikosi vyetu vya Majeshi ya Ulinzi na Usalama – JWTZ, Polisi, Magereza, Zimamoto, Uhamiaji, na JKT vinaimarika na kuwa vya kisasa zaidi.
 • Vikosi hivi vimeathiriwa na ukosefu wa vifaa vya kutendea kazi, mafunzo duni na maslahi yasiyoridhisha.
 • Makaazi ya walio wengi miongoni mwa askari wetu ni ya udhalilishaji mkubwa na yanakwenda kinyume na haki za msingi za binadamu.
 • Mishahara na marupurupu mengine ya askari ni ya chini mno ukilinganisha na wito na maadili ya kazi zao.
 • Askari wengi wastaafu wanaishi maisha yaliyojaa udhalilishaji mkubwa uraiani kutokana na kutokuwepo na mipango madhubuti ya kuuenzi muda walioutumia kulitetea Taifa.
 • Huduma za uokoaji nchini ziko katika hali mbaya kabisa. Udhaifu mkubwa uliojionyesha wakati wa kushughulikia majanga kama ya MV Bukoba na mafuriko ya Mererani ni kielelezo halisi cha hali hii.

Ajenda ya CUF ya Kuleta Mafanikio

Taifa linapaswa kuhuisha upya umuhimu wa vyombo vya ulinzi na usalama, na kurekebisha kasoro ambazo zimeachiwa kujijenga kwa muda mrefu. Serikali ya CUF itafanya mambo yafuatayo ili kuondoa kasoro hizi:

 • Itaviimarisha vikosi vya ulinzi na usalama kwa kuvipatia mafunzo bora na vifaa vya kisasa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa vyombo vya usafiri, vyombo vya mawasiliano, na sare vinatosheleza mahitaji ili:
  1. Viweze kukidhi haja ya ulinzi dhidi ya mashambulizi ya ardhini, baharini na angani.
  2. Viweze kuimarisha usalama wa raia na mali zao.
 • Itakiimarisha kikosi cha wanamaji cha polisi (police marine) ili mbali ya kutoa msaada kwa kikosi cha jeshi cha wanamaji dhidi ya mashambulizi ya baharini pale yatakapotokea, kiweze kuboresha doria katika ukanda wote wa pwani na kwenye maziwa makuu kwa madhumuni ya:
  1. Kutoa msaada kwa vyombo vya kiraia vya uvuvi na usafirishaji wakati wa matatizo (Rescue Operations).
  2. Kuzuia magendo, uvuvi haramu, biashara chafu kama za madawa ya kulevya, uharamia wa majini na utupaji wa takataka zenye sumu katika eneo la bahari yetu.
 • Itahakikisha kuwa askari wa vikosi vyote nchini wanalipwa vizuri na kuhudumiwa ipasavyo ili waweze kutekeleza majukumu na wajibu wao kwa ari.
 • Itahakikisha kuwa askari wote wanapatiwa makazi ya kuheshimika na kupewa mafunzo ya kutosha juu ya wajibu, sheria na maadili ya kazi yao.
 • Itahakikisha kuwa inakihuisha, kukipanua na kukiimarisha kikosi cha Zima Moto ili kiweze kutoa huduma za uokoaji kikamilifu. Hii itakuwa ni pamoja na kuongeza idadi ya askari, kutoa mafunzo ya kisasa yanayohusiana na shughuli zote za uokoaji na kukipatia vifaa vya kisasa vya uokoaji.
 • Itahakikisha kuwa inapitia upya viwango vya pensheni za wastaafu kutoka vikosi vya ulinzi na usalama, na kusimamia kuona kuwa wanapata haki zao stahiki bila ya kusumbuliwa.
 • Itaanzisha mafunzo ya kijeshi ya hiari kwa Wananchi wote watakaopenda ili wawe askari wazuri pindi itakapohitajika.
 • Muundo wa jeshi la polisi utaangaliwa upya ili kuondoa ukiritimba wa madaraka ya IGP na hivyo kuongeza ufanisi wa jeshi hilo.

PREVIOUS… NEXT…

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s