Misingi Mikuu ya Uongozi wa Nchi: Mahakama

Ili Mahakama ziweze kutimiza kikamilifu majukumu yake ya kutafsiri sheria na kutoa maamuzi ya haki ni lazima ziwe huru kikamilifu. Aidha ili mahakama ziwe huru kikamilifu ni lazima kubadili utaratibu wa kuwapata majaji na watendaji wengine wakuu wa idara ya mahakama, pamoja na kuhakikisha kuwa idara ya mahakama inatengewa fedha za kutosha kujiendesha kulingana na mahitaji.

Kasoro za CCM

  • Kwa muda wote ambao imekuwa madarakani serikali ya CCM imeshindwa kabisa kukubaliana na dhana ya uhuru wa mahakama.
  • Mara nyingi mahakama zimekuwa zikitumiwa kama chombo cha CCM cha kuwatilia hofu Wananchi. Sheria zimekuwa zikitafsiriwa kuhalalisha matakwa na mahitaji ya CCM kuliko matakwa ya kikatiba. Hata pale ambapo baadhi ya majaji na mahakimu wameweza kuonyesha ujasiri na kutoa maamuzi yanayokwenda kinyume na matakwa ya CCM na serikali yake, maamuzi hayo yamekuwa yakipuuzwa – tena wakati mwingine kwa kejeli.
  • Vitendo vya rushwa na ufisadi vimeachiwa kukua na kukithiri mno kwa watendaji wa idara ya mahakama.
  • Watuhumiwa mbalimbali wamekuwa wakipewa au kunyimwa dhamana kwa matashi binafsi ya majaji, mahakimu na waendesha mashtaka.
  • Uchache wa majaji na mahakimu umesababisha mlundikano wa kesi nyingi na kusababisha kuchelewesha kutolewa kwa haki.

Ajenda ya CUF ya Kuleta Mafanikio

Serikali ya CUF itaifanyia idara ya Mahakama marekebisho ya msingi ambayo pamoja na mambo mengine:

  • Yatalenga kuihakikishia idara ya mahakama uhuru wa kutosha katika kuendesha mashauri na kutoa maamuzi. Ili suala hili liwe wazi na lisilo na utata wowote, serikali ya CUF itahakikisha kuwa inatoa ushawishi Katiba mpya ya Jamuhuri ya Muungano itamke wazi kuwa Mahakama ndio taasisi yenye uamuzi na usemi wa mwisho juu ya suala lolote la kisheria na kuwa itakuwa ni ukiukwaji wa Katiba kwa serikali kuvunja agizo, amri, au hukumu yoyote ambayo imeshapitishwa na Mahakama. Aidha serikali ya CUF itahakikisha kuwa inatoa ushawishi Katiba mpya ya Jamuhuri ya Muungano itamke wazi kuwa uteuzi wa majaji wote (ikiwa ni pamoja na jaji mkuu) na wasajili wa Mahakama Kuu na ile ya rufani utafanywa na Rais kwa kutumia mapendekezo ya Tume ya Ajira ya Majaji na kisha kuthibitishwa na Bunge.
  • Yatalenga katika kuboresha maslahi ya watendaji wa idara ya mahakama kwa ujumla ili kufifisha vitendo vya rushwa na ufisadi.
  • Yatalenga katika kuhakikisha kuwa haki ya dhamana kwa watuhumiwa inatekelezwa kwa dhati kama katiba na sheria husika zinavyotamka.
  • Yatalenga katika kuiimarisha idara ya mahakama kwa vitendea kazi na watumishi wa kutosha wenye utaalamu na ujuzi unaohitajika.
  • Yatalenga kufanya marekebisho ya sheria ili makosa madogo madogo yasiwe na hukumu za vifungo, na badala yake yawe yanalipiwa faini tu au kufanya kazi yoyote ya maendeleo itakayoamuliwa na mahakama iwapo mtuhumiwa atakuwa hana faini ya kulipa.

PREVIOUS… NEXT…

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s