Makaazi

Pamoja na kwamba Tanzania ina Wizara nzima inayoshughulikia masuala ya Ardhi, ina Chuo Kikuu kishiriki kinachoshughulikia masuala ya Ardhi tu na kuna Idara za Mipango Miji katika kila Halmashauri na Mabaraza ya Miji, hali ya makazi ya wananchi inazidi kuwa mbaya siku hadi siku. Uhaba mkubwa wa viwanja vilivyopimwa umewalazimisha wananchi wengi kujenga makazi kwenye maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu na ambayo hayana huduma za msingi kama vile mitaro ya maji machafu, vyoo vya umma, barabara, viwanja vya kuchezea watoto na sehemu za kuzikia za uhakika.

Mathalani, inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wote wa Jiji la Dar es Salaam wanaishi kwenye maeneo yaliyojengwa holela na yenye msongamano mkubwa. Aidha hali hii imewalazimisha baadhi ya wananchi wengine kujenga sehemu za mabondeni na hivyo kuhatarisha usalama wa maisha na mali zao wakati wa mvua za masika.

Ukosefu wa sehemu za uhakika wa biashara za ‘Machinga’, na uhaba wa vituo bora vya mabasi, na maegesho rasmi kwa ajili ya vyombo vya usafiri – hususan magari, umetokea kuwa ni kero kubwa kwa wananchi wengi hususan katika Jiji la Dar es Salaam. Pamoja na yote haya pia kuna udhaifu mkubwa sana katika kusimamia sheria zinazotawala makaazi.

Pamoja na matatizo haya, sheria ndogondogo zinazotungwa na halmashauri na mabaraza mengi ya miji hazizingatii hali halisi ya kimaisha ya wakaazi wa miji husika. Mathalani, katika baadhi ya miji kuna sheria inayowakataza wakaazi kufanyia matengenezo nyumba zao zinazochakaa kwa maelezo kwamba maeneo ziliko nyumba hizo yametengwa kwa ajili ya kujenga maghorofa. Matokeo ya sheria hii ni kwamba katika miji mingi kuna nyumba nyingi chakavu zinazokaribia kuanguka huku wamiliki wake wakisubiri zianguke na wao kupoteza haki ya kumiliki viwanja husika kwa sababu hawana uwezo wa kujenga maghorofa. Ni wazi kabisa kuwa sheria ya namna hii siyo tu kwamba ni ya kikandamizaji, lakini pia ni yenye kuongeza kiwango cha umasikini miongoni mwa wananchi.

Kasoro za CCM

 • Shirika la Nyumba la Taifa ambalo kinadharia lilianzishwa kwa malengo ya kutatua tatizo la makazi kwa wananchi, hususan wale wanaoshi mijini limeshindwa kabisa kutimiza azma hiyo. Kasi ya ujenzi wa majengo mapya imefifia kabisa, na majengo yake mengi ya zamani, ikiwemo yale liliyoyarithi kutoka kwa wamiliki wake halali baada ya kutaifishwa, yako katika hali mbaya sana kutokana na kutokuwa na uangalizi mzuri. Hivi sasa shirika hilo liko kwenye mgogoro mkubwa na baadhi ya wapangaji wake kutokana na kupandisha kodi bila kuzingatia hali halisi.
 • Pamoja na kwamba hivi karibuni serikali imebuni mradi wa viwanja elfu ishirini (20,000) katika jiji la Dar Es Salaam, bei za viwanja hivyo ni za juu mno kwa watu wa kawaida kuweza kuzimudu. Matokeo yake ni kwamba vingi kati ya viwanja hivyo vitaangukia katika mikono ya watu wachache wenye uwezo, na wananchi wa kawaida (ambao ndiyo wengi) wataendelea na ujenzi holela katika maeneo yasiyofaa.
 • Kasi ya kuboresha maeneo ya makazi amabayo hayajapimwa kwa kukata barabara, kuweka maeneo ya ujenzi wa shule, vituo nya afya, na viwanja vya kuchezea watoto ni ndogo mno. Matokeo yake ni kwamba huduma muhimu, mathalan za magari ya zima moto na magari ya wagonjwa bado ni vigumu kuwafikia wakazi walio wengi katika maeneo hayo.
 • Kuna udhaifu mkubwa katika kuandaa maeneo ya biashara za ‘machinga’ na maeneo mengine muhimu kama vituo vya mabasi ya daladala. Kutokana na hali hii kuna baadhi ya mitaa ambayo wakazi wake wanapata adha kubwa kutokana na msongamano mkubwa wa biashara hizo na wingi wa daladala zilizogeuza mitaa hiyo kuwa stendi za kupakia na kushusha abiria.
 • Kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria ndogondogo zinazotawala makazi na hususan katika maeneo ya mijijini, bila ya hatua zozote kuchukuliwa.
 • Sheria katika baadhi ya miji na manispaa zinazokataza wakazi wa baadhi ya maeneo kufanyia matengenezo nyumba zao kwa kisingizio kuwa maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa maghorofa ni za udhalilishaji, zinalenga kuongeza umasikini katika jamii, na zinakiuka haki za binadamu.
 • Serikali imeshindwa kabisa kukitangaza kitengo chake cha mradi wa utafiti wa nyumba za bei nafuu na matokeo yake ni kwamba wananchi walio wengi hawanufaiki na kuwepo kwa kitengo hicho.

Ajenda ya CUF ya Kuleta Mafanikio

Ili kuboresha makaazi, Serikali ya CUF itachukua hatua zifuatazo:

 • Kubinafsisha Shirika la Nyumba la Taifa. Kwa kuwa kwa muda mrefu sasa serikali ya CCM imesharuhusu watu binafsi kujenga na kumiliki majengo yenye thamani yoyote ile, na pia imekuwa na utaratibu wa upendeleo wa kurejesha baadhi ya majumba yaliyotaifishwa kwa wamiliki wake wa awali, hakuna sababu za msingi kwa serikali kuendelea kumiliki majumba ya watu wengine ambayo iliyapora katika miaka ile ya utaifishaji. Serikali ya CUF itaweka utaratibu wa kuwarejeshea majumba yao wale wote waliokuwa wametaifishiwa na hawakulipwa fidia, na baada ya zoezi hili italibinafsisha shirika la nyumba la Taifa.
 • Upatikanaji wa viwanja vilivyopimwa. Serikali itahakikisha kwamba katika kipindi cha miaka miwili tu, katika miji yote nchini viwanja vilivyopimwa na vinavyopatikana kwa bei ndogo ndivyo vitatafuta wajenzi; badala ya hivi sasa ambapo wananchi mbalimbali wenye nia ya kujenga ndio wanaohaha kutafuta viwanja hivyo. Huduma za barabara, maji na umeme kwenye makaazi zitakwenda sambamba na upimwaji wa viwanja vipya.
 • Uboreshaji wa mazingira ya miji. Serikali itasitisha mara moja ukiukwaji mkubwa wa sheria za mipango miji uliopo hivi sasa. Aidha kwa kushirikiana na serikali za mitaa, serikali itaweka mkakati imara wa kuhakikisha kuwa kila penye makaazi na hasa kwenye maeneo ambayo yamejengwa kiholela, barabara zinapitishwa, mitaro ya maji machafu inakuweko au kufanyiwa ukarabati, vyoo vya umma vinasambazwa, taka zinazolewa kwa wakati na madimbwi yanayotuama maji wakati wa mvua yanatoweka. Serikali pia itahakikisha kuwa uhaba wa sehemu za kuzikia, vituo bora vya mabasi, sehemu za uhakika kwa biashara za ‘Machinga’, viwanja vya kuchezea watoto, na bustani za mapumziko unapatiwa ufumbuzi wa haraka.
 • Gharama za ujenzi. Gharama za ujenzi kwa kiasi fulani zitapungua kutokana na azma ya serikali ya kurekebisha viwango vya kodi. Serikali itakiimarisha na kukitangaza kwa nguvu zote kitengo chake cha mradi wa utafiti wa nyumba za bei nafuu na kuwahamasisha wananchi wote – wa mijini na vijijini – wakitumie kujengewa nyumba bora kwa gharama nafuu. Aidha katika maeneo ya mijini makampuni zaidi yatahamasishwa kwa ajili ya kujenga nyumba za gharama nafuu na kuzigawa kwa Wananchi mbali mbali kwa mikopo ya masharti nafuu.
 • Sheria ndogo iliyotungwa na baadhi ya manispaa inayowakataza wakazi wa baadhi ya maeneo kufanyia matengenezo nyumba zao kwa madai kwamba maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya maghorofa itafutwa.

PREVIOUS… NEXT…

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s