Maendeleo ya Jamii: Vijana

Vijana ambao ni wananchi wa chini ya umri wa miaka 30 wanaunda asilimia sabini (70%) ya wananchi wote nchini. Vijana ndiyo kundi lenye mchango mkubwa katika uzalishaji kuliko kundi jingine lolote, na kwa maana hiyo umuhimu wa kundi hili kwa jamii ni mkubwa mno.

Kasoro za CCM

 • Serikali ya CCM imelipuuza kundi hili kwa muda mrefu mno. Sehemu kubwa ya vijana hawana fursa za ajira za kueleweka kitu ambacho kinawasababisha walio wengi kujikuta wakilazimika kuingia katika vitendo viovu kupambana na umasikini unaowakabili. Vijana wengi wamekata tamaa kabisa kiasi kwamba wanadhani kwamba njia pekee iliyobaki ya kujiletea maendeleo ni wao kuondoka nchini. Kwa kweli hali hii haiashirii mazingira mazuri kwa maendeleo ya nchi na vita dhidi ya umasikini.
 • Mkabala wa serikali za CCM kwa vijana ni wa ubabaishaji na mara nyingi huwa unalenga pale tu vijana wanapohitajika ili kufanikisha malengo fulani fulani ya serikali hizo, hususan wakati wa chaguzi.

Ajenda ya CUF ya Kuleta Mafanikio

 • Elimu. Pamoja na azma ya CUF kuhakikisha kuwa kila kijana anapata elimu ya darasani (formal education) kwa upeo wa uwezo wake, serikali ya CUF itachukua pia hatua zifuatazo:
 • Itaongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi katika maeneo yote ya nchi kwa lengo la kuwashawishi vijana walioshindwa kuendelea na mfumo wa masomo ya darasani kujipatia ujuzi mbalimbali wa ufundi.
 • Itaanzisha huduma ya ushauri nasaha kuhusu chaguo la ajira na matatizo ya kijamii ili kukabiliana na matarajio ya vijana.
 • Afya. Pamoja na azma ya CUF kuhakikisha kuwa kunakuwa na mkakati unaoigusa jamii nzima katika kuhakikisha kuwa afya za wananchi zinaboreshwa, serikali ya CUF pia itachukua hatua zifuatazo:
 • Itaanzisha programu zitakazohusisha makundi ya vijana katika ngazi ya mtaa na kitongoji kukutana na kuelimishana juu ya:
 • Njia bora za kuepukana na maambukizo ya ukimwi.
 • Tatizo la matumizi ya madawa ya kulevya na njia za kuepukana nalo.
 • Utamaduni na michezo. Pamoja na azma ya CUF kuhakikisha kuwa kunakuwa na mkakati unaoigusa jamii nzima katika kuhakikisha kuwa viwango vya ubora wa ushiriki wa Taifa letu katika medani za michezo na burudani vinapanda, serikali ya CUF pia itachukua hatua zifuatazo:
 • Itaboresha huduma za burudani na michezo vijijini na mijini na kusambaza wataalamu wa fani mbalimbali katika medani hizo ili kusaidia kutambua vipaji na kuviendeleza.
 • Itashawishi ushiriki zaidi wa sekta binafsi katika kuwekeza katika huduma za burudani na michezo.
 • Itashawishi vijana kuwa mstari wa mbele kuendeleza yale yote mazuri yanayopatikana katika tamaduni zetu, na kupiga vita tamaduni mbaya za kigeni.
 • Itashawishi vijana kushiriki kwa hiari yao katika harakati mbalimbali za kijamii kama vile uboreshaji wa mazingira na kuwasaidia wagonjwa, watoto, wazee, na mayatima.
 • Utumishi wa Taifa. Madhumuni makubwa ya uanzishwaji wa makambi ya JKT yalikuwa ni kutoa mafunzo ya awali ya ulinzi na uchapa kazi kwa vijana ili kuwatayarisha kwa maisha yao ya baadaye. Lakini ni dhahiri kuwa kiutendaji madhumuni haya yalivurugwa kwani wale ambao kweli wanahitaji mafunzo ya awali ndio ambao hawakulazimika kushiriki na wale ambao walikuwa na uhakika wa ajira ndio waliolazimika kujiunga. Waliosamehewa ni wale wanaomaliza darasa la 7 na 12 bila kujiunga na chuo chochote, wakati waliolazimika ni wale waliomaliza Kidato cha sita ama wenye elimu ya juu zaidi. Ni wazi basi kuwa mfumo uliotumika haukuwa na tija.

Pili, uendeshaji wa programu mbalimbali katika makambi hayo ulilenga zaidi katika kukomoana na kudhalilishana na hivyo matumizi ya akili yalizingatiwa kwa kiwango kidogo. Haishangazi basi kuwa makambi ambayo kimsingi yalitakiwa yawe na uwezo wa kuzalisha kwa ajili ya kujiendesha na ziada, hatimaye yalionekana kuwa ni yenye kuliingizia Taifa hasara kubwa na kulazimika kusitisha sehemu kubwa ya programu zake – hususan ile ya kuwachukua vijana kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo bado umuhimu wa utumishi kwa Taifa upo ila kinachohitajika ni marekebisho ya msingi. Serikali ya CUF itachukua hatua zifuatazo ili kuleta marekebisho haya:

  1. Utaratibu wa uendeshaji wa programu kwenye vituo hivi utabadilika ili kuondoa dhana kwa vijana, wazazi, na watoa mafunzo kuwa hivyo ni vituo vya ‘Mateso’ kwa vijana wanaomaliza masomo yao. Katika kutekeleza azma hiyo, kwanza kabisa muundo wa awali utabadilishwa na badala ya kujulikana kama makambi sasa yataitwa ni ‘vituo vya maandalizi kwa vijana ili kulitumikia Taifa’.
  2. Itatenganisha kabisa masuala ya uajiri, fursa za masomo na suala la kujiunga na vituo hivi.
  3. Itavifanya vituo hivi kuwa ni huduma muhimu ya miaka miwili katika kutoa mafunzo ya awali ya kijeshi, ukakamavu, kazi za uzalishaji (Vocational Training), lugha za Kiingereza na Kifaransa, huduma ya mwanzo (First Aid), sanaa mbalimbali, udereva, michezo, pamoja na stadi zinazohusiana na shughuli za uokoaji (Rescue Operations).
  4. Itatoa ruzuku mwanzoni wakati wa maandalizi, na mikakati itawekwa kukiwezesha kila kituo kiwe kinajiendesha chenyewe.
  5. Itaweka vituo katika kila mkoa kwa ajili ya uandikishaji wa wale wote ambao wangependa kujiunga na vituo hivi na itawashauri vijana wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne na kukosa nafasi ya kuendelea na masomo katika shule za kawaida na vyuo wajiunge.
  6. Itaweka utaratibu kuhakikisha kwamba fedha zote zitakazozalishwa na vijana kutokana na miradi mbalimbali ya uzalishaji baada ya kuondoa gharama za kuendeshea kambi inayohusika zinahifadhiwa kwa ajili ya kupewa vijana wakati wa kuhitimu ili ziwasaidie kununulia zana mbali mbali zinazohusiana na stadi walizojifunza.
   • Ajira. Serikali ya CUF itahakikisha kuwa vijana wanatumia kikamilifu fursa ya kuwepo kwa mifuko ya kulea na kukuza uzalishaji (Incubator Funds) ambayo serikali itaianzisha kwa kila sekta ya uzalishaji mali, kupata mitaji kwa madhumuni ya kujiajiri.

   PREVIOUS… NEXT…

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s