CUF mwenyeji mkutano Kiliberali Afrika

The Civic United Front (CUF - Chama cha Wananchi)

The Civic United Front (CUF - Chama cha Wananchi)

Chama Cha Wananchi (CUF) kimepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Vyama vya Siasa vya Kiliberali Afrika (Africa Liberal Network – ALN) ambao unafanyika Golden Tulip Hotel, mjini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa siku tatu unaojumuisha washiriki 17 kutoka vyama vya siasa vinavyofuata mrengo wa kiliberali unafanyika huko Golden Tulip Hotel, mjini Dar es Salaam kuanzia Jumamosi, tarehe 2 Agosti hadi Jumatatu, tarehe 4 Agosti, 2008.

Agenda kuu za mkutano huo ni kupanga mikakati ya kuuimarisha Umoja huo na kuongeza kasi ya mashirikiano kati ya vyama vya kiliberali katika kuleta mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika nchi ambamo vyama hivyo vinafanya kazi lakini pia na katika bara zima la Afrika.

Siku mbili za awali (2 – 3 Agosti), mkutano utakuwa katika mfumo wa warsha yenye lengo la kupokea mapendekezo yaliyotayarishwa kwa ajili ya kuuimarisha muundo na utendaji kazi wa Umoja huo ambayo yalitokana na maamuzi ya mkutano kama huu uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini mwezi Machi, mwaka huu.

Siku ya tatu (4 Agosti) kutakuwa na Mkutano Mkuu (the General Assembly) ambao pamoja na kupitisha marekebisho ya muundo na katiba ya Umoja huo kama itakavyokubaliwa, pia utachagua viongozi wapya wa Umoja huo.

Wajumbe watakaoshiriki na vyama vya siasa na nchi wanazoziwakilisha nikama ifuatavyo:

 1. Prof. Ibrahim Lipumba – National Chairman- CUF Tanzania
 2. Ismail Jussa – Director International Affairs – CUF Tanzania
 3. Juma Duni Haji – Deputy Secretary General – CUF Tanzania
 4. Raul Domingos – Leader- PDD Mozambique
 5. Aly Toure – ALN President – RDR Cote d’Ivoire
 6. Yaya Kaba Fofana – President of the Technical Commission for Culture and Tourism – RDR Cote d’Ivoire
 7. Jonathan Moakes – Executive Director-Resources and Development – DA South Africa
 8. Tiens Kahenya – Secretary General – UPND Zambia
 9. Roger Mancienne – Secretary General – SNP Seychelles
 10. Abdrrahmene Mlahouah – International Affairs Officer- PSD Tunisia
 11. Albi Bweya – International Affairs Officer- ANADER DRC
 12. Kabore Jean Pate – Vice-President- ADF-RDA Burkina Faso
 13. Clement Stambuli – MP and National Campaign Director – UDF Malawi
 14. Abdeslam Nihrane – Member of Political Bureau – UC Morocco
 15. Mamadou Lamine Ba – Advisor to President Wade – PDS Senegal
 16. Imen Trabelsi – ALN Coordinator
 17. Peter Schroeder – Facilitator

Kwa maelezo zaidi kuhusu Umoja wa Vyama vya Kiliberali Afrika (Africa Liberal Netwrok – ALN), tembelea: http://www.africaliberalnetwork.org/

Imetolewa na:

Ismail Jussa

Ofisa wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa

Ofisi ya Katibu Mkuu – CUF

01 Agosti, 2008

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s