BAADA YA KUANGUKA, PROF. SAFARI ADAI KUDHALILISHWA

Wajumbe wa CUF wakipiga kura katika uchaguzi mkuu wa Chama hicho. Ni uchaguzi huo ndio uliompa ushindi Prof. Ibrahim Lipumba na kumuangusha Prof. Abdallah Safari
Siku mbili baada ya kuangushwa vibaya katika kinyang’anyiro cha uenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Abdallah Safari anadai kuwa wajumbe wa mkutano mkuu walimdhalilisha na kwamba anaandaa kitabu kueleza udhalilishaji huo. Anasema kwamba katika uchaguzi huo uliomrudisha madarakani Profesa Ibrahim Lipumba, aliyepata kura 646, huku mpinzani yeye akiambulia kura sita tu, alizomewa na baadaye kurushiwa maswali yaliyomtingisha, ikiwa ni pamoja na kutaka ataje jina la katibu wa tawi lake, swali ambalo alibabaika kulijibu. Endelea kusoma habari hii
TAARIFA YA KAZI ZA CHAMA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO (2004 – 2009)

Taarifa ya Kazi za Chama (2004 - 2009)
“Miaka hii mitano imekuwa ya kupanda na kushuka, kupata na kukosa, lakini zaidi ya yote, kama uchambuzi wa ripoti hii unavyoonesha, imekuwa ni miaka ya kujifunza na kujijenga upya. Kwa mfano, ni ndani ya kipindi hiki, ndipo kwa mara ya kwanza CUF ilipojiwekea Mpango Mkakati wa Chama (Strategic Plan – SP), ambao ni wa kisayansi na wenye kutekelezeka. Kwa muda sasa, Mpango huo umekuwa ndio dira, tegemeo, muongozo, na kwa hakika, ndiyo maisha ya CUF. Taarifa hii ya Kazi za Chama kwa Kipindi cha Miaka Mitano inayowasilishwa kama tathmini ya CUF kuanzia 2004 hadi 2009 inaonesha namna ambavyo Chama kimefanikiwa au kutofanikiwa katika kulinda misingi na dhamira ya uanzishwaji wake.” Soma taarifa hii iliyowasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Nne wa Chama.

Mshindi wa uenyekiti, Prof. Ibrahim Lipumba (kushoto) akipongezwa na waliokuwa wagombea wa nafasi hiyo, Prof. Abdallah Safari (katikati) na Koplo Steven Masanja (kulia)
PROFESA wa Sheria, wakili wa kujitegemea na mkurugenzi wa mafunzo na mipango katika Chuo cha Diplomasia, Abdalla Jumbe Safari, ameangushwa katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya uwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) kwa kupata asilimia 0.9 ya kura na kushikilia nafasi ya mwisho. Matokeo hayo yanatokana na uchaguzi mkuu wa CUF uliofanywa jana katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. Mapema wakati wa kujieleza mbele ya wajumbe wa mkutano huo, Prof. Saffari alieleza kuwa lengo lake kuu la kugombea nafasi hiyo lilikuwa ni kukijenga Chama kuwa cha kitaifa, Bara na Visiwani, sambamba na kubuni miradi ya kijamii na kiuchumi ili kukiwezesha chama hicho kikuu cha upinzani kujitegemea. Endelea kusoma habari hii
‘UPINZANI TUMEJIPANGA KULINDA KURA’

Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed
KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, amesema watafanya kila liwezekanalo kulinda kura kwa lengo la kulinda nafasi zao katika chaguzi mbalimbali. Hayo aliyasema jana katika Mkutano Mkuu wa Nne wa Chama cha Wananchi (CUF) ambao unaendelea katika Viwanja vya Diamond Jubilee wakati akiwasilisha taarifa za shughuli za kambi anayoiongoza bungeni na kuongeza kwa sasa wanajipanga vyema ili kuhakikisha kuwa wapinzani wanashinda uchaguzi mkuu ujao. Endelea kusoma habari hii
UCHAGUZI MKUU CUF: MAPROFESA NA KOPLO WAPAMBANA

Koplo Steven Masanja, mmoja wa wagombea wa nafasi ya uenyekiti Taifa
CHAMA cha Wananchi (CUF) leo kinatarajia kufungua ukurasa upya wa historia yake baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa chama hicho. Jambo kubwa linaloelezwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho kuwa litaandika historia mpya ya chama hicho ni mchuano mkali uliopo kwa wagombea wa nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho. Kwa mara ya kwanza katika historia ya chama hicho, Mwenyekiti wake, Prof. Ibrahim Lipumba, ambaye amekiongoza chama hicho kwa muda kwa kipindi kisichopungua miaka kumi amepata upinzani katika wadhfa wake huo. Endelea kusoma habari hii
“CHADEMA HAIJAFUKUZWA MKUTANO MKUU WA CUF”

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Chama chake hakikufukuzwa kwenye mkutano mkuu wa CUF
“Wageni wetu wote waliohudhuria shughuli yetu ya ufunguzi walipokelewa na kutambuliwa rasmi kwenye Mkutano wetu na tunawashukuru sana. Hakuna kiongozi wala mwakilishi wa kiongozi yeyote wa CHADEMA ambaye aliwasili mbele ya walinzi wetu na kuzuiwa. Hiyo si sera wala msimamo wa CUF panapohusika mahusiano yetu na taasisi nyengine za kisiasa ama za kijamii. Hakuna uhasama wowote baina yetu na chama chochote cha kisiasa, CHADEMA ikiwemo, na hata kama panaweza kuwapo tafauti kati yetu na baadhi ya vyama vya kisiasa, utamaduni wa Chama chetu ni kuzizungumza tafauti hizo kistaarabu. Kwa mfano, kisiasa hakuwezi kuweko Chama cha siasa ambacho tunatafautiana sana kuliko Chama cha Mapinduzi (CCM), lakini washiriki wa Mkutano wetu ni mashahidi wa namna mwakilishi wa Chama hicho kwenye ufunguzi, Mhe. John Guninita, alivyopokelewa, kutambulishwa na kushangiliwa kwa heshima zote.” Soma taarifa hii…
CUF DOUBTS GOVT`S STAND ON CORRUPTION

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Serikali yake haina dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi
Addressing hundreds of CUF members and invited representatives of the government, political parties and foreign diplomatic missions, Prof Lipumba said it would be suicidal for anyone to pay lip-service to the anti-corruption crusade as a ploy to lead Tanzanians and the international community into believing that such a thing was indeed on when it was not true. “I do not believe that these court cases will reach anywhere. I suspect that they will be used merely as a political game to deceive Tanzanians and the outside world that the CCM government is taking measures on corruption when nothing will ultimately come out of it.” Read more…
CUF SASA WATISHIA KUSUSIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed
Akifungua mkutano mkuu huo juzi, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, aliisihi serikali kuhakikisha kuwa chaguzi za mwaka huu zinaendeshwa kwa mujibu wa makubaliano ya wadau. “Ninaisihi serikali uchaguzi wa mwaka 2009 uzingatie makubaliano ya wadau vikiwemo vyama vya siasa, serikali na asasi za kiraia uliofanyika Morogoro Febuari 19, mwaka huu. Wadau wote walikubaliana kuwa mambo mengine yasiwahusishe watendaji wa vijiji na kata (VEO na WEO) katika zoezi la kuandaa orodha ya wapiga kura.” Soma habari hii…
PROFESA LIPUMBA KUPAMBANA NA WAWILI NAFASI YA UONGOZI CUF

Prof. Abdallah Jumbe Safari, mmoja wa wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa CUF Taifa
CHAMA cha Wananchi (CUF), leo kinachagua viongozi wapya katika ngazi ya taifa ambapo upinzani mkali unatarajiwa kuwepo kwa wagombea nafasi ya Mwenyekiti Profesa Abdallah Safar, Profesa Ibrahim Lipumba na Steven Masanja. “Nisingependa kutaja asilimia ngapi ya kura ambazo nitapata katika uchaguzi wa kesho (leo), ila kwa kawaida ndani ya uchaguzi wa CUF, ushindi ni zaidi ya asilimia 50,” anasema Masanja. Soma habari hii…
TANZANIA INAHITAJI MABADILIKO NA CUF IKO TAYARI KUONGOZA NJIA – LIPUMBA

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye Mkutano Mkuu wa Nne wa Taifa tarehe 23 Februari, 2009
“Kwa hakika, mwaka wa nne sasa tokea Rais Kikwete aingie madarakani, ni wazi kwamba Taifa limekabiliwa na ukosefu wa uongozi kutokana na CCM kushindwa kuongoza. Maeneo tisa yanadhihirisha jinsi CCM ilivyoshindwa kuongoza na kuwafanya Watanzania wasijue wanakopelekwa. Maeneo hayo ni pamoja na kupanda kwa kasi ya kutisha kwa gharama za maisha, kuongezeka kwa ufisadi, kuyumba kwa uchumi, migomo ya wafanyakazi, migomo ya wanafunzi, kuongezeka kwa nyufa katika Muungano, kuibuka kwa mpasuko wa kidini, kuporomoka kwa maadili ya Taifa, na kushindwa kuumaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar. Lakini ni bahati mbaya kwamba achilia mbali kuyatafutia ufumbuzi matatizo haya ambayo yakiachiwa yanaweza hata kuhatarisha usalama wa Taifa, Rais Kikwete anaonekana kufanya usanii wa kutoyaona. Katika hotuba aliyoitoa Bungeni tarehe 21 Agosti 2008, Rais Kikwete alieleza kuwa mambo ni mazuri katika nchi, kwamba uchumi unakua, ajira zinaongezeka na ahadi alizozitoa kwa Watanzania amezitekeleza na anaendelea kuzitekekeza.” Endelea kusoma hotuba ya Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nne wa Taifa.
Maoni