CUF Press

CUF YAGUNDUA ‘MADUDU’ MINGINE YA ZEC

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad

“Kwa ugunduzi huu, moja kati ya matatu linadhihirika. Aidha, la kwanza, Tume yako haitumii ZAN ID kama kigezo cha mtu kuandikishwa kuwa mpiga kura, vyenginevyo idadi ya waliopewa ZAN ID na wale walioandikishwa na Tume yako ingelikuwa sawa, au, la pili, moja kati ya taasisi zenu mbili (ZEC na Idara ya ZAN ID) inasema uongo kwenye data zake na au, la tatu, kuna uwezekano mkubwa kwamba watu wanapandikizwa kutoka majimbo mengine na masheha, ambao ni mawakala wenu wanaridhia kwa vile ni njama ya kukibeba Chama cha Mapinduzi (CCM). Kama hili linatokea, hakuna uhakika kwamba waliopandikizwa kuandikishwa katika majimbo ambayo si yao hawataandikishwa tena katika majimbo yao muda utapofikia. Kwa hivyo, mnaandaa mazingira yatakayowaruhusu baadhi ya watu kupiga kura zaidi ya mara moja wakati wengine wananyimwa haki ya kujiandikisha.Soma barua kamili ya Katibu Mkuu kwa ZEC hapa

“HUU SI UBORESHAJI WA DAFTARI, NI UCHAFUZI TU”

Mkurugenzi wa Chaguzi na Oganaizesheni, Juma Said Sanani

Mkurugenzi wa Chaguzi na Oganaizesheni, Juma Said Sanani

Katika ofisi ya vitambulisho Gamba, Mahonda, Amani na Mwera bado kuna watu wengi ambao wamepewa fomu lakini hawapewi huduma kwa sababu tulizoeleza hapo awali.  Utaratibu uliowekwa wa kuwahudumia wananchi wa kila jimbo kwa siku mbili umewaacha kwa mamia bila kuipata huduma hiyo.  Mfano katika ofisi ya Gamba zaidi ya wananchi 1,000 wa majimbo ya Nungwi, Mkwajuni na Tumbatu wameshindwa kuhudumiwa na majimbo yao yameshamaliza kazi ya uandikishaji na, kwa hivyo, wameshapoteza haki ya kupiga kura 2010. Soma taarifa kamili kwa vyombo vya habari

TAMKO LA MAALIM SEIF KUHUSU HALI YA PEMBA

Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad

Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad

Ukweli unabaki pale pale kwamba chanzo na sababu za mgogoro uliopo ni njama ovu kabisa za CCM na Serikali zake kuwazuia wananchi wengi wa Zanzibar wenye sifa zote za kujiandikisha kuwa wapiga kura na ambao wanasadikiwa kuwa wanaunga mkono CUF wasiweze kujiandikisha, lengo likiwa ni kupunguza kura za upinzani. Sambamba na hilo, njama hizo zinahusisha kutumia idadi hiyo ya wapiga kura halali inayopunguzwa kwa kuwajaza watu wasio na sifa ambao ni pamoja na watu wanaoletwa maalum kutoka Tanzania Bara kuja kuandikishwa na baadaye kuipigia kura CCM, vijana malum walioandaliwa na CCM (maarufu kama Janjaweed) waliosajiliwa na chama hicho na baadaye kupelekwa kuandikishwa zaidi ya mara moja katika majimbo tofauti ya uchaguzi, na watoto wadogo wa umri wa chini ya miaka 18.” Soma tamko kamili

VITAMBULISHO: WANANCHI WASONGE MBELE

Hicho kinachoambiwa kimeghushiwa, kwa mfano, ni cheti ambacho mchapishaji mwenyewe wa serikali aliandika jina la Mohammed kwa ama kifupi cha Moh’d au kwa kuondoa ‘o’ na kuweka ‘u’ na hivyo kuwa Muhammed. Katika mifano mingine, jina kama la Haji limeandikwa Hajj au Hamad limeandikwa Hamadi. Wakati mwengine ni mwenye cheti kukozeshea jina lake kwa kalamu baada ya kuwa hati za mchapishaji wa serikali zimefifia kwenye cheti chake. Endelea kusoma taarifa hii kwa vyombo vya  habari

SMZ IWACHE KUSHABIKIA NA KUENDELEZA UBAGUZI DHIDI YA RAIA

“….ni kiwango cha juu cha ubaguzi na upotofu kwa SMZ kuendeleza sera zake za kibaguzi dhidi ya Wazanzibari wa makundi tafauti. Misingi hii ya kibaguzi ilianza kujengwa dhidi ya Wazanzibari wenye asili ya Pemba kwa kuwanyima fursa na haki kadhaa za msingi zikiwemo za kielimu, kiuchumi na kisiasa; na sasa baada ya kwisha kuwabagua Wapemba, SMZ inawageukia Wangazija. Serikali ya kweli ya watu haisimamii ubaguzi na utengano, bali mapenzi baina ya watu wake na mshikamano.” Endelea kusoma taarifa hii

CUF KUONGELEA DAFTARI JUMAPILI

The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi) kinawaalika katika mkutano wake na waandishi wa habari utakaofanyika katika ofisi za Chama zilizoko Vuga, mjini Zanzibar, siku ya Jumapili ya tarehe 31 Agosti, 2009, saa 4.00 asubuhi. Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma, Mhe. Salim Bimani atatoa taarifa maalum ya Chama kuhusu Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura pamoja na hali ya jumla ya kisiasa nchini. Endelea kusoma taarifa hii

UCHAGUZI Z’BAR 2010 MATATANI

“Tumekuwa na makubaliano ya kubadilishana taarifa na Serikali lakini nimeandika barua zaidi ya nne kwa Rais Jakaya Kikwete kuhusu mwafaka huu lakini hakuna majibu hadi sasa. Pamoja na mimi kuandika barua hizo nne pia Katibu wangu Malim Seif Sharif Hamad naye ameandika barua mbili kuhusu utekelezaji wa mwafaka lakini hadi sasa hakuna majibu kutoka kwa Rais.” Anasema Prof. Lipumba. Soma habari kamili

STANDOFF IN ZANZIBAR WORRISOME – MAAJAR

Tanzania’s High Commissioner to the United Kingdom, Mwanaidi Maajar, has cautioned over the belief by some investors that efforts to resolve the post-election political standoff in Zanzibar were slowing down and might not bear fruit. Speaking in an exclusive interview with The Guardian in London recently, the envoy said the investors’ risk analysis was not an issue as such but she was worried over their general perception of developments in the Isles. Read the story

SMZ TEGUA BOMU HILI PEMBA

Linalosikitisha zaidi, masheha ambao walitegemewa kutoa msaada, pia wako kazini kukwamisha wananchi kuandikishwa. Wanakataa kuwapa barua wasiokuwa na Zan ID ili kuthibitisha kwenye Idara ya Vitambulisho ya Zanzibar kuwatambua wapatiwe kitambulisho hicho, wakidai wameelekezwa na wakuu wao. Katika mlolongo huo, Idara ya Vitambulisho Zanzibar, nayo kwa upande wake imejipanga sawa kuhakikisha inawakomoa wananchi. Soma makala kamili

“SMZ/SMT WATUMIA KISINGIZIO CHA KITAMBULISHO CHA MZANZIBARI KUIINGIZA NCHI KATIKA MACHAFUKO”

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana juu ya zoezi la uandikishaji wapiga kura linaloendelea Pemba

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana juu ya zoezi la uandikishaji wapiga kura linaloendelea Pemba

Hoja inayotolewa na ZEC ni kwamba hayo ndiyo matakwa ya sheria ya Uchaguzi ya 1984 kwenye Kifungu 12 (b). Lakini inaeleweka kwamba kifungu hiki cha sheria kimekwenda kinyume na kifungu cha 11 cha katiba ya Zanzibar na hilo limethibitishwa na hata Mkurugenzi wa ZEC alipoongea na waandishi wa habari huko Pemba. Vile vile, sheria Namba 7 ya 2005 inayohusu Vitambulisho inaweka wazi kwamba ni lazima kwa kila Mzanzibari kuwa na kitambulisho hicho na kwamba, kwanza, kutokuwa nacho ni kosa na, pili, kumzuwia Mzanzibari asikipate ni kosa vile vile. Hivi sasa kuna malalamiko na mifano kadhaa ambapo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), kwa kutumia masheha wake, inawazuia Wazanzibari wasipate kitambulisho hicho na wakati huo huo inawapatia wasiokuwa Wazanzibari. Kuna mifano pia ambapo Wazanzibari wanaoonekana na SMZ kuwa wafuasi wa CCM wanapatiwa vitambulisho, lakini wale wanaoonekana kuwa CUF wananyimwa hata kama wanakaa nyumba moja na ni ndugu wa kuzaliwa. Soma taarifa kamili

KARUME AIAMBIE IDARA YA VITAMBULISHO IWAPE WAZANZIBARI ZAN ID

Baadhi ya kinamama wa shehia ya Mjananza, jimbo la Mgogoni waliokataliwa kuandikishwa kwa sababu ya kutokuwa na vitambulisho vya Mzanzibari

Baadhi ya kinamama wa shehia ya Mjananza, jimbo la Mgogoni waliokataliwa kuandikishwa kwa sababu ya kutokuwa na vitambulisho vya Mzanzibari

Kwa upande mmoja tunataka tuamini kwamba Mhe. Karume alimaanisha hasa alichokuwa anakisema na kwamba ni haja yake kuona kwamba kila Mzanzibari mwenye haki na sifa anapata kitambulisho hicho. Kwa upande mwengine tunataka tuamini kwamba, anatoa kauli hiyo kufurahisha wahisani tu, ambao wameshajulishwa kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia mtandao wake usio mtakatifu (unity of the demons) unaowajumuisha masheha, Tume ya Uchaguzi (ZEC) na Idara yenyewe ya Vitambulisho, inafanya kila lililo kwenye uwezo wake kuhakikisha kuwa Wazanzibari wengi ambao inaamini kwamba hawaiungi mkono serikali na chama chake tawala hawapatiwi vitambulisho hivyo na hatimaye wanaenguliwa katika zoezi la uandikishaji kwa ajili ya kushiriki kwenye chaguzi. Taarifa kamili

CUF YALAANI USALAMA WA TAIFA KUINGILIA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA

Itakumbukwa kwamba Usalama wa Taifa ni miongoni mwa mambo ya Muungano na, kwa hivyo, ni idara inayosimamiwa moja kwa moja na Serikali ya Jamhuri  ya Muungano. Kwa mantiki hiyo, hakuna namna yoyote ambayo Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wanaweza kujivua na lawama za kuchafuliwa kwa uchaguzi wa Zanzibar, maana inaonesha wazi kwamba ama wanaridhia utendaji wa vyombo vilivyo chini ya mamlaka yao Zanzibar au hawajali kile kinachofanywa na vyombo hivyo. Lolote kati ya hayo mawili linamaanisha kwamba wao ndio wanaopaswa kubeba dhamana na lawama za hali ya juu katika jambo hili. Taarifa kamili

CUF YABAINI MBINU YA ZEC MICHEWENI

“Tatizo jengine ni la kasi ndogo ya uandikishaji kwa siku ya jana na leo. Maafisa wa ZEC wanatoa sababu kwamba kompyuta zao hazina chaji, yumkini kutokana na tatizo sugu la umeme kisiwani Pemba, lakini sisi katika CUF tunaamini hiyo ni njama nyengine inayolenga kuhakikisha kuwa siku tatu za kubadilisha shahada zinamalizika huku maelfu ya wapiga kura ikiwa imetengwa kando kutokana na sababu ya muda.” Endelea kusoma taarifa hii…

584 WANYIMWA HAKI YA KUWA WAPIGA KURA MICHEWENI

“Katika rikodi zilizokusanywa juzi, wapiga kura 830 walinyimwa haki hiyo katika vituo sita vya jimbo la Konde huku wakiandikishwa 133 tu katika vituo vyote hivyo. Rikodi za jana zinaonesha kwamba watu 584 wamenyimwa haki hiyo na walioandikishwa ni 224 tu. Kwa hivyo, kwa juzi na jana tu, watu walionyimwa haki ya kuwa wapiga kura katika jimbo la Konde peke yake ni 1,414. Siku hizi mbili zilikuwa ni za uandikishaji wapiga kura wapya. Sababu inayotumika kwa ZEC kuwanyima watu hao haki ya kuwa wapiga kura ni kutokuwa kwao na vitambulisho vya Uzanzibari, sharti ambalo limewekwa na ZEC kwa kusudi maalum la kuvuruga uchaguzi.” Endelea kusoma taarifa hii…

ZEC ’YAKATA VICHWA’ 800 MICHEWENI

“Tathmini ya jana inaonesha kwamba katika Jimbo la Konde, ambako uandikishaji huo umeanza, watu walioandikishwa kwenye vituo sita vya jimbo hilo ni 133 tu huku wengine 830 wakikataliwa kuandikishwa kwa sababu ya kutokuwa na vipande vya Mzanzibari Mkaazi. Wengi wa watu hao wana vielelezo vyengine vinavyothibitisha uzawa na ukaazi wao katika jimbo hilo na kwamba tayari wamefikisha umri wa miaka 18, vikiwemo vyeti vya kuzaliwa.” Endelea kusoma taarifa hii…

PROF. LIPUMBA AZINDUA OPERESHENI ZINDUKA

Katika kuzindua operesheni maalum ijulikanayo kama “Zinduka”, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema:

“Chama Cha Wananchi (CUF) kina historia ya kuwaongoza Watanzania kudai na kuleta mageuzi ya kisiasa. Ndiyo chama pekee cha upinzani chenye misingi ya kitaifa kuwawezesha Watanzania kulifikia lengo lao kuu la kuleta mabadiliko ya kisiasa hapa Tanzania. Ni vuguvugu la mageuzi la watangulizi wa CUF lililofanikisha kurejeshwa kwa haki ya msingi ya Watanzania ya kuwa na mfumo wa siasa unaowaruhusu kujiundia vyama vya siasa na kuchagua mfumo wa utawala na uongozi wanoutaka kupitia vyama hivyo. Ilikuwa ni vuguvugu la kisiasa la CIVIC MOVEMENT iliyokuwa ikiongozwa na Mheshimiwa James Mapalala kwa upande wa Tanzania Bara na Kamati ya Mageuzi ya Mfumo wa Vyama Huru (KAMAHURU) iliyokuwa ikiongozwa na Marehemu Shaaban Khamis Mloo kwa upande wa Zanzibar lililowazindua Watanzania kudai na kuipata haki yao hiyo ya kuzaliwa.” Kuedelea kusoma taarifa hii ya uzinduzi wa “Operesheni Zinduka” uliofanywa na Prof. Lipumba katika hoteli ya Peackock, Dar es Salaam, tarehe 5 Julai, 2009, tafadhali bonyeza hapa.

UJUMBE WA MAALIM SEIF KWA WAPEMBA

Ujumbe huu wa Maalim Seif unakuja katika wakati ambapo tayari CUF imekusanya ushahidi wa kutosha unaothibitisha kuwa kuna ‘utatu’ usio mtakatifu (trinity of the demons) baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na Idara ya Vitambulisho Zanzibar, unaopanga njama za kuhakikisha kuwa wakaazi wengi wa Pemba hawaandikishwi kuwa wapiga kura. Katika mtandao huu, njama iliyopangwa ni hii: SMZ iwatumie masheha wake kuhakikisha kuwa hawatoi baru za uthitisho kuwapa watu wanaodai vitambulisho vya Uzanzibari, Idara ya Vitambulisho isimpe kitambulisho hicho mtu ambaye hana barua ya sheha na ZEC isimuandikishe kuwa mpiga kura mtu ambaye hana kitambulisho. Hadi sasa watu 18,000 kisiwani Pemba pekee wamesharipoti kunyimwa vitambulisho hivyo vya ukaazi huku hata zoezi la uandikishaji wapiga kura likiwa halijaanza. Lakini, licha ya kuwepo kwa taarifa hizo, ujumbe wa Maalim Seif kwa wananchi wa Pemba unabakia kuwa ule ule: lazima wahakikishe kuwa kila mwenye haki ya kuwa mpiga kura anaingia kwenye Daftari hilo. Endelea kusoma ujumbe huu…

BURIANI PROF. HAROUB MIRAJ OTHMAN

Marehemu Prof. Haroub Miraji Othman katika siku ya mwisho ya uhai wake akisoma wasifu wa kitabu Race, Revolution and the Struggle of Human Rights in Zanzibar, mjini Zanzibar

Marehemu Prof. Haroub Miraji Othman katika siku ya mwisho ya uhai wake akisoma wasifu wa kitabu Race, Revolution and the Struggle of Human Rights in Zanzibar, mjini Zanzibar

Ulamaa maarufu wa fani za siasa na sharia, Prof. Haroub Othman, amefariki dunia mjini Zanzibar asubuhi ya tarehe 28/6/2009 na maziko yake yanatajiwa kufanyika tarehe 29/6/2009 saa 10.00 alasiri katika Msikiti wa Quality mjini Unguja.

Marehemu Prof. Haroub alikuwa mjini hapa kuhudhuria uzinduzi wa kitabu kiitwacho Race, Revolution and the Struggle for Human Rights in Zanzibar kilichotungwa na Bw. Ali Sultan Issa, Maalim Seif Sharif Hamad na Prof. B. Burgess. Kitabu hicho kilizinduliwa tarehe 27/6/2009 hapa mjini Zanzibar na aliyekuwa  Katibu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika, Dkt. Salim Ahmed Salim, ambayo yeye Prof. Haroub alisoma wasifu wa kitabu hicho.

Mola amlaze mahala pema peponi. Amin!

Zaidi juu ya kitabu hicho tembelea www.ohioswallow.com na kuhusu picha za tukio la uzinduzi wa kitabu hicho, tembelea CUF Picha.

CUF YALAANI WAANDISHI KUFUKUZWA

Kurugenzi ya Uenezi na Mahusiano na Umma ya The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi) imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia Idara ya MAELEZO kuwazuia waandishi wa habari kuingia kwenye eneo la tukio la ajali ya meli ya MV Fatih bandarini Zanzibar, hapo jana. Kurugenzi inalaani vikali kitendo hicho kilichotekelezwa na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa maagizo kutoka afisa wa MAELEZO, kwa kuwa haki ya kukusanya habari na kuzisambaza ni ya msingi sana kwa taifa linalojali misingi ya utawala wa sheria na uwajibikaji. Kuvumilia vitendo kama hivi ni kukubali kuizamisha Zanzibar katika enzi za giza na usiri usiokuwa na maana. Endelea kusoma taarifa hii kwa vyombo vya habari

CUF YAMTAKA WAZIRI WA MAWASILIANO Z’BAR AJIUZULU

Kuangalia picha za ajali hii ya meli ya Mv Fatih, bonyeza hapa

Kuangalia picha za ajali hii ya meli ya Mv Fatih, bonyeza hapa

Kwa makosa haya makubwa kwa Serikali, makosa yanayotokana na uzembe, kutokuwa makini, dharau katika kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kulinda usalama wa watu na mali zao, na ili wananchi waone kwamba Serikali hii haikufurahishwa nayo. Tunapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe haraka iwezekanavyo. Waziri wa Nchi katika Afisi ya Rais anayeshughulikia mawasiliano na uchukuzi awajibike kwa kujiuzulu. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari naye ajiuzulu au awajibishwe. Mrajisi wa Meli naye awajibishwe kwa kuondolewa katika wadhifa huo. Serikali katika Bajeti ya mwaka wa 2009/2010 ihakikishe kuwa imetenga fedha za kutosha kwa ununuzi wa vifaa vya uokozi na vya kukabiliana na ajali za baharini. Serikali iunde kamati maalum ya uchunguzi inayojitegemea (Independent Commission of Inquiry) kuchukunguza sababu za ajali hii na taarifa ya kamati hii iwe tayari kwa umma katika kipindi cha wiki mbili. Miongoni mwa wajumbe wa kamati hii wawe ni wajumbe wa Baraza la wawakilishi kutoka vyama vya CCM na CUF. Soma taarifa hii ya msemaji wa CUF kuhusu Mawasiliano kwenye Baraza la Wawakilishi hapa

RIPOTI YA AWALI KUHUSU UCHAGUZI WA MAGOGONI

  1. Aliyekuwa OCD wa wilaya ya Mjini, Bwana Nurdin, amewapeleka watu ambao si wakaazi halali wa jimbo la Magogoni kwa sheha wa shehia ya Welezo, Bi Mgeni, kwa ajili ya kupatiwa shahada za kupigia kura.
  2. Sheha, Bi Mgeni, anapeleka watu wasiokuwa na shahada za kupiga kura na anasimamia kuwapigisha kura. Angalau watu watatu (miongoni mwa hao waliopelekwa) wamesharipoti katika ofisi zetu kuthibitisha hili.
  3. Katika Chumba Na. 4, wapiga kura wanapewa shahada mbili za kupigia kura. Kwa uchache, watu wanne wamesharipoti kwetu kwamba wamepewa shahada mbili mbili. Endelea kusoma ripoti hii…

MAALIM SOUD HATUNAYE TENA

Marehemu Soud Yussuf Mgeni katika uhai wake

Marehemu Soud Yussuf Mgeni katika uhai wake

Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF), Mheshimiwa Soud Yussuf Mgeni (61), amefariki dunia leo hii, majira ya saa 4.00 asubuhi, katika sehemu ya wagonjwa mahututi (ICU) ya Hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa takriban wiki tatu sasa. Endelea kusoma taarifa hii…

TANZIA: MZEE SHAABAN KHAMIS MLOO

Marehemu Shaaban Khamis Mloo

Marehemu Shaaban Khamis Mloo

Kwa hivyo, CUF iliyosimama leo hii kama taasisi imara ya kisiasa, imewezekana kuwa hivi kwa sababu ya juhudi kubwa zilizofanywa na Mzee Mloo na wenzake. Hakuna chochote tunachoweza kukifanya kukumbuka mchango uliotukuka wa Mzee wetu huyu, zaidi ya kutimiza ile ndoto yake ambayo daima aliishi nayo, yaani kuiona CUF kikiwa kinaongoza Serikali za Muungano na Zanzibar, kikitekeleza sera yake ya neema na haki sawa kwa wote. Sisi tuliobakia nyuma yake, tunaahidi kwamba tutaitimiza dhamira na azma hiyo ya waasisi wa Chama hiki, akiwemo Mzee Mloo, kwa manufaa ya nchi na vizazi vijavyo. Tunaahidi kuwa CUF aliyoiasisi, kuijenga na kuisimamia kwa siku zote za uhai wake itaendelea kuwa taasisi imara ya kisiasa.” Soma tanzia hii…

ZEC YAANDAA KUPANDIKIZA WAPIGA KURA 2000 MAGOGONI

Kundi la watu waliotambulika kuwa askari wa vikosi vya SMZ ambao walikusudia kuandikishwa katika kituo cha Viwanda Vidogo Vidogo. Hata hivyo, katika jimbo zima la Magogoni hakuna kambi ya vikosi vya SMZ

Kundi la watu waliotambulika kuwa askari wa vikosi vya SMZ ambao walikusudia kuandikishwa katika kituo cha Viwanda Vidogo Vidogo. Hata hivyo, katika jimbo zima la Magogoni hakuna kambi ya vikosi vya SMZ

“Taarifa ambazo tunazo ni kwamba ZEC imekusudia kuongeza wapiga kura 2,000 ili kufikia hisabu ya wapiga kura 7,000 ambao walipiga kura mwaka 2005. Kwa upande mmoja, hatua hiyo inakusudiwa kuziba aibu ya 2005 ambapo ZEC ilipandikiza wapiga kura zaidi katika jimbo la Magogoni. Mara hii, kutokana na umakini wa mawakala na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, ‘utatu usio mtakatifu’ wa ZEC, CCM na SMZ (kupitia masheha) ulishindwa kupandikiza idadi hiyo na sasa wanataka kuona kwamba aibu yao inasitirika kwenye takwimu. Kwa upande wa pili, uongezaji huo wa wapiga kura unakusudiwa kuibeba CCM, kwani ZEC imepanga kutokubandika orodha ya wapiga kura kwa ajili ya pingamizi hadi siku za mwisho mwisho, ambapo orodha hiyo haitawekwa kwa mfumo wa alfabeti na wala kwenye vituo husika na, hivyo, kufanya iwe vigumu kwa watu kuwabaini ‘mapandikizi’ na kuwawekea pingamizi. Itakumbukwa kuwa mbinu kama hiyo ndiyo iliyotumiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika chaguzi ndogo za Tarime na Mbeya Vijijini.” Soma taarifa hii…


KAULI YA CUF KUMUHUSU MUHUNZI

Makamo Mwenyekiti, Machano Khamis Ali: "CUF inachunguza kadhia ya Muhunzi"

Makamo Mwenyekiti, Machano Khamis Ali: "CUF inachunguza kadhia ya Muhunzi"

“Kwamba Mhe. Muhunzi aliitwa na Chama mara tatu kuzungumza naye kuhusu kadhia ya fedha za waheshimiwa Wawakilishi wenzake. Mara mbili ilikuwa ni katika mwaka uliopita na mara ya mwisho ni katika mwezi Februari, 2009 – siku chache kabla ya Mkutano Mkuu wa Chama chetu. Mara zote hizo tatu aliitwa na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.” Soma tamko hili la CUF kama lilivyotolewa na Makamo Mwenyekiti, Machano Khamis Ali<!–[if gte vml 1]> <![endif]–><!–[if !vml]–><!–[endif]–>

IDARA YA VITAMBULISHO YASHIRIKI KUHARIBU UANDIKISHAJI

Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad: "Idara ya Vitambulisho na ZEC wana uhusiano"

Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad: "Idara ya Vitambulisho na ZEC wana uhusiano"

“Ushahidi wa madai haya ni kuwa kwa kipindi kirefu sasa ofisi yako imesitisha kutoa vitambulisho vya Uzanzibari ukaazi. Nathibitisha hili kwani Wazanzibari wengi ambao wameshakamilisha utaratibu wa kupatiwa vitambulisho na tayari walipewa risiti ambazo zinaonyesha nambari za Vitambulisho lakini wanapofika kwenye ofisi yako ili wapatiwe vitambulisho, wanajibiwa kwamba zoezi la kutoa vitambulisho limesitishwa. Mfano wa hili ni risiti ya Bwana JUMA HAMAD AMANI yenye namba ID 070118355.” Soma barua hii ya CUF kwa Mkurugenzi wa Vitambulisho

KAULI YA ABUBAKAR KWA MUHUNZI

Kiongozi wa Upinzani (BLW), Abubakar Khamis Bakary

Kiongozi wa Upinzani (BLW), Abubakar Khamis Bakary

“Baada ya hayo tulikubaliana tufanye uchunguzi kwa kuwaandikia Benki halafu tukwite. Kabla hatujapata majibu ya Benki wakati mimi nikiwa Dodoma ukanitumia “message 15” kwenye simu yangu. Message hizo zote ni mbaya ukanitukana ukisema maneno ya kijinga na yasiyomaana kwangu mimi na kwa Wawakilishi wengine. Message zote hizo ninazo.” Message zote hizo sikuzijibu kutokana na uungwana wangu na heshima yangu, na bado ninazo sijazifuta. Message nilioijibu ni moja tu ulipouliza niko wapi unahaja na mimi; na nikakujibu niko Dodoma, wewe baadae ulisema kuwa hukunikusudia mimi, bali ulimkusudia Mhe. Hamad Masoud.” Soma taarifa hii

BARUA YA ABUBAKAR KWA IGP MWEMA VITISHO VYA MHE. MUHUNZI

IGP aliyetangulia, Omar Idi Mahita. Anatambulika kwa rekodi mbaya ya kutumikia siasa badala ya taalum yake

IGP aliyetangulia, Omar Idi Mahita. Anatambulika kwa rekodi mbaya ya kutumikia siasa badala ya taalum yake

“Ninajiuliza “action” hiyo ni kuzusha mambo dhidi ya Serikali, Nchi au Tanzania kwa ujumla? Au action hiyo ni kukodi majambazi wakanihujumu na kupoteza maisha yangu au vipi? Lakini zaidi najiuliza, kweli “wakubwa” hao wa Zanzibar ni wakubwa wa Serikali au niwachama au wakumbwa wepi? Lakini pia message nyengine alizoniletea, ambazo ninazo ni kama hivi: (a) “…. Mie nitazinya (akimaanisha fedha alizozitapeli) lakini na wewe (yaani mimi) lazima kufa….” (b) “kama hujawahi maishani kwako kula bumbwi jitayarishe kula chokaa…..” n.k.” Soma barua hii

TANZIA: REHEMA MWAKANGALE

Marehemu Rehema Mwakangale

Marehemu Rehema Mwakangale

“Ulimwengu wa habari nchini utamkumbuka Rehema kwa umahiri wake wa hali ya juu katika utendaji kazi, hasa hasa katika uwasilishaji wa taarifa za habari. Sura na sauti yake itabakia nasi daima milele. Kwa hakika, wanahabari na Watanzania wote tumempoteza mtu muhimu katika fani hii.” Soma tanzia hii.

RIPOTI YA AWALI YA UANDIKISHAJI WA MAGOGONI

Mohammed Abdallah Khamis aliyepigwa mapanga na Janjaweed, Kinuni, 3 Machi 2009

Mohammed Abdallah Khamis aliyepigwa mapanga na Janjaweed, Kinuni, 3 Machi 2009

“Tunasikitika kukutumia taarifa kwamba wakati zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Magogoni kwa nafasi ya uwakilishi unaendelea kwa siku ya tano sasa, tayari Chama chetu cha Wananchi (CUF) kimeshabaini vitendo vya wazi wazi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Tume yako ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuuharibu uchaguzi huo.” Soma ripoti hii

“ZANZIBAR INA ARDHI NDOGO, LAZIMA ILINDWE”

Bendera ya Zanzibar. Zanzibar nzima, kama nchi, ina ardhi ya 0.29 ya ardhi yote ya Tanzania

Bendera ya Zanzibar. Zanzibar nzima, kama nchi, ina ardhi ya 0.29 ya ardhi yote ya Tanzania

“…Zanzibar ina eneo dogo la ardhi kulinganisha na Tanganyika, ni vyema basi kukawa na udhibiti wa umiliki wa ardhi kwa wasio kuwa Wazanzibari maana ardhi hiyo ni ndogo. Zanzibar nzima ina ukumbwa wa kilomita 2,232 za mraba. Kwa mujibu wa sensa ya taifa ya mwaka 2002, Zanzibar ina asilimia 2.9 tu ya Watanzania wote na ardhi yake ni asilimia 0.25 tu ya ardhi ya Tanzania. Ukweli ni kuwa kuna hata baadhi ya wilaya tu za Tanzania Bara ambazo ni kubwa zaidi kuliko nchi nzima ya Zanzibar. Hii ni kusema kuwa ardhi na rasilimali nyengine za Zanzibar ni chache sana (so limited) kuweza kugawanywa kwa wengine wanaotoka nje ya Zanzibar. Hata ukichukua mfano wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki: Siku zote Watanzania tumekua tukipiga kelele kuwa ushirikiano huu wa “free movement” na “mtu kuishi atakapo” usiwe wa kuwaruhusu Wakenya, Waganda, Warundi na Wanyarwanda kuingia tu na kuishi katika ardhi ya Tanzania kama watakavyo. Kilio chetu Watanzania panapohusika hili ni kwamba pawe na utaratibu mzuri wa kuingia na kuishi. NILICHOKISEMA NI KUWA UTARARIBU UWEKWE WA WATU KUINGIA NA KUISHI ZANZIBAR NA VILE VILE WATU KUINGIA NA KUISHI TANGANYIKA.” Endelea kusoma taarifa hii…

“CHADEMA HAIJAFUKUZWA MKUTANO MKUU WA CUF”

“Wageni wetu wote waliohudhuria shughuli yetu ya ufunguzi walipokelewa na kutambuliwa rasmi kwenye Mkutano wetu na tunawashukuru sana. Hakuna kiongozi wala mwakilishi wa kiongozi yeyote wa CHADEMA ambaye aliwasili mbele ya walinzi wetu na kuzuiwa. Hiyo si sera wala msimamo wa CUF panapohusika mahusiano yetu na taasisi nyengine za kisiasa ama za kijamii. Hakuna uhasama wowote baina yetu na chama chochote cha kisiasa, CHADEMA ikiwemo, na hata kama panaweza kuwapo tafauti kati yetu na baadhi ya vyama vya kisiasa, utamaduni wa Chama chetu ni kuzizungumza tafauti hizo kistaarabu. Kwa mfano, kisiasa hakuwezi kuweko Chama cha siasa ambacho tunatafautiana sana kuliko Chama cha Mapinduzi (CCM), lakini washiriki wa Mkutano wetu ni mashahidi wa namna mwakilishi wa Chama hicho kwenye ufunguzi, Mhe. John Guninita, alivyopokelewa, kutambulishwa na kushangiliwa kwa heshima zote.” Endelea taarifa kusoma hii…

“SMZ YAVUNJA NYUMBA ZA WANANCHI”

Sisi, Chama cha Wananchi (CUF), tunalichukulia suala hili kama ni uvunjaji wa haki za binaadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala wa sheria ambao unahimiza kutokuchukuliwa hatua zozote za kisheria bila kupitia ngazi ya mahakama. Rikodi ya SMZ ya haki za binaadamu inafahamika kuwa ni mbaya kwa miaka mingi sasa na serikali hiyo haionekani kujifunza kwa makosa kadhaa inayoyafanya katika eneo hili. Mambo haya mawili – uvunjaji wa haki za binaadamu na utawala usiojali sheria – si mambo ya kuyaonea fakhari katika dunia ya sasa inayozungumzia demokrasia na utawala bora. Kwa hivyo, tunaitwisha SMZ lawama zote za tukio, matokeo ya tukio hili na athari zake. Miongoni mwa athari hizo ni kudhalilika kiafya na kisaikolojia kwa wahanga wa mkasa huo na kupotezwa kwa mali. Endelea kusoma taarifa hii…

“SMZ HAIKUPASWA KUTUMIA MSAMAHA WA MADENI KWA ANASA”

“Si sawa kusema kuwa fedha zinazotokana na msamaha wa madeni si fedha za serikali na, hivyo, si za wananchi. Ukweli ni kuwa serikali inaposamehewa deni huwa waliosamehewa hasa huwa ni wananchi ambao ndio wao waliokuwa wakatwe kodi zao kulipwa deni hilo. Kwa hakika hasa mzigo wa deni la serikali hubebwa na wananchi, kwani serikali husema kwamba zinakopa kwa ajili ya kuwaendeleza au kuwahudumia wananchi hao. Kwa hivyo, kama zilivyo fedha za kodi, fedha za msamaha wa madeni pia ni miliki asilimia mia moja ya wananchi na, hivyo, lazima zitumike ipasavyo kwa ajili ya wananchi ni si kwa starehe na anasa.” Endelea kusoma taarifa hii…

“WAZIRI HAROUN AJIUZULU”

“Sisi, CUF tunasikitishwa sana na tabia kongwe ya SMZ kupuuzia hatima ya Zanzibar kwa kudharau umuhimu wa elimu bora kwa vijana wetu, ambayo matokeo yake yamekuwa ni kuwafelisha vijana hawa na hivyo kulifelisha taifa zima kwa ujumla. Hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na SMZ, kwa mfano kulundika wanafunzi katika skuli za msingi na kati kwa wingi ili kutaka kujiengea sifa ya kuwa kila mtoto wa Kizanzibari anakwenda skuli, bila ya kujali hali halisi ya upatikanaji na utoaji wa elimu katika skuli hizo, zimekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya kielimu ya Zanzibar na sio msaada kwa watoto wetu.” Endelea kusoma taarifa hii…

KAMA FEDHA ZA EPA ZIPO, ZIKO WAPI? – HAMAD RASHID

“Kambi ya Upinzani inasikitika kuwa majibu yaliotolewa na Serikali sio tu yalipingana na ushauri wetu, bali hata Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, jambo ambalo linaidhalilisha sana Serikali. Ushauri wetu kwa siku za mbele ni kuwa Serikali iongeze umakini katika kutoa majibu na hasa pale ambapo ushauri wa Kambi ya Upinzani na Mdhibiti na Mkaguzi wa Serikali (kwani yeye katika taarifa yake alizionyesha fedha za EPA kuwa ni fedha za Serikali zilizotakiwa zirudishwe na Serikali ikazikana), au taasisi zinazoheshimika maoni yao kwa kiasi fulani yanaoana, maana leo Watanzania watajiuliza hivi ni nani mkweli?” Soma maoni ya Msemaji Mkuu wa Upinzani Bungeni kuhusu Fedha na Uchumi, Hamad Rashid Mohammed, juu ya nyongeza ya Bajeti ya 200/2009

“CCM YAADHIMISHA KUZALIWA KWAKE KWA FUJO, VURUGU”

“Pamoja na kulishukuru jeshi la Polisi kwa utendaji wake katika tukio hili, ni matumaini yetu kuwa jeshi hilo litadumisha misingi ya ufanyaji kazi wake katika siku zinazokuja. Pia tunapenda kuwakumbusha ndugu zetu wa CCM kwamba wawe wastaarabu wakitambua na kukubali ukweli kuwa, sisi sote ni vyama halali vya siasa, vilivyopo kisheria na ambavyo vina haki ya kutekeleza shughuli zao za kisiasa kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi. Kwenda kinyume na hayo, ni kuiweka rehani amani ya nchi hii, ambayo sisi kama raia tunaihitaji na tunachelea kuipoteza. Kuwa mstaarabu hakuhitaji gharama kubwa!” Soma taarifa hii ya CUF

Ni miaka saba sasa tangu Vyombo vya Dola vya Tanzania kutumia mabavu yake kukandamiza maandamano ya amani yaliyoandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF). Wakati huo, CUF ilikuwa na hoja kuandaa maandamano hayo na bado ingali na hoja hadi leo hii ikiwa itaamua hivyo, maana makubaliano iliyofikia mwaka 2001 (Muafaka II) kati yake na chama kinachotawala, CCM, yamevunjwa na CCM na kwa mara nyengine tena Uchaguzi wa 2005 uliharibiwa kwa makusudi… Endelea kusoma hoja hii