MAALIM SEIF, KARUME WAKUTANA IKULU

Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, Ikulu Mjini Zanzibar jana. Kulia ni Msaidizi Maalum wa Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Ismail Jusa. (Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu)
RAIS wa Zanzibar Bw. Amani Abeid Karume jana alikutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad Ikulu, mjini Zanzibar ambayo chama hicho cha upinzani kimesema ni ya ‘maelewano makubwa’. Mazungumzo hayo, kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya Zanzibar, yaligusia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na haja ya kudumisha amani na utulivu nchini na maelewano na ushirikiano kati ya wananchi wote. Endelea kusoma habari hii
ZANZIBAR: TUSIPOZIBA UFA TUTAJENGA UKUTA
HAKUNA anayeweza kukataa kuwa Zanzibar inaelekea kubaya, kuwa hali ya visiwani inatia wasiwasi. Zoezi linaloendelea la kujiandikisha katika daftari la wapigakura limetawaliwa na mabomu, risasi, helikopta, uchomaji moto, mapigano, ukamataji wa raia na vitisho vya kuua. Hapo awali tuliambiwa Pemba ndiko kwenye vurugu. Tukasikia na Unguja nako katika kisiwa cha Tumbatu polisi wanamimina mabomu ya machozi kutoka helikopta. Tunaambiwa polisi inashindwa kuwatawanya wananchi kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi na ndipo risasi za moto zinafyatuliwa. Endelea kusoma makala hii
NYUMBA YA KADA WA CCM PEMBA YALIPULIWA KWA BOMU
MLIPUKO mkubwa umetokea katika nyumba moja huko Wete,Kaskazini Pemba, siku moja baada ya Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, kuwahakikishia wananchi na wageni kuwa hali ya usalama Zanzibar, ni shwari. Mlipuko huo ulitokea saa 4:00 usiku wa kuamkia katika nyumba inayomilikiwa na kada wa CCM, Ramadhan Issa Kipaya, iliyoko katika Mtaa wa Mtemani, wilayani Wete. Ingawa mlipuko huo umesababisha kuta za nyumba kuharibika, lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa. Soma habari kamili
MAMIA ya wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) jana walifanya maandamano makubwa yaliyoanzia Buguruni na kupokewa Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. John Tendwa katika Viwanja vya Kidongo Chekundu. Ulinzi mkali wa polisi wenye sare na wasiokuwa na sare, wakiwamo Askari wa Usalama Barabarani, Kikosi Cha Kuzuia Ghasia (FFU) huku gari ‘la upupu’ lenye maji ya kuwasha likivinjari Barabara ya Uhuru walipokuwa wanapita waandamanaji hao. Soma habari kamili
Maelfu ya wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) wakiongozwa na viongozi wao wa kitaifa, jana walilitikisa jiji la Dar es Salaam kwa kufanya maandamano ya amani yaliyolenga kuwasilisha madai yao kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ya kutaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ivunjwe. CUF inadai kwamba NEC imeshindwa kusimamia uchaguzi ulio huru na wa haki nchini tangu iundwe miaka 17 iliyopita na kwa hiyo, inataka ivunjwe na pia, Mwenyekiti wake, Jaji Lewis Makame ajiuzulu. Soma habari kamili hapa
CUF DEMAND IMMEDIATE DISBANDING OF ELECTORAL COMMISSIONS
The Civic United Front (CUF) party has demanded for the immediate disband of both Zanzibar and National Electoral Commissions before the next general elections slated for October next year. Addressing a multitude of supporters who turned up for peaceful demonstrations at Kidongo Chekundu grounds in Dar es Salaam’s Kariakoo area yesterday, CUF national chairman Prof. Ibrahim Lipumba criticised the commissions saying they were favouring the ruling party. Read more
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimezinduka na kutangaza kuwa hakitasubiri machafuko yaliyotokea Kenya na Zimbabwe yatokee Zanzibar ndipo kiunde Serikali ya Umoja wa Kitaifa visiwani humo. Kauli hiyo ya CCM imetolewa huku zikiripotiwa vurugu za mara kwa mara visiwani humo za kupinga utaratibu wa uandikishaji wananchi kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura kutokana na vikwazo katika utoaaji wa vitambulisho vya ukaazi, kiasi cha kusababisha Jeshi la Polisi kutumia mabomu kutuliza hali hiyo. Soma habari kamili hapa
IGP MWEMA AONJA SIASA ZA CUF, CCM
Juhudi za Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, kutaka kuhakikisha amani inakuwepo visiwani Zanzibar, zimekutana na kigingi. Mwema alikutana na hali hiyo katika kongamano la kujadili demokrasia na mchakato wa uandikishaji wapiga kura Zanzibar, baada ya kumalizika bila ya kupatikana muafaka pale suala la vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi lilipowagawa washiriki. Soma habari kamili hapa
MWANDISHI WA THE GUARDIAN AKAMATWA Z`BAR
Mwandishi wa habari wa magazeti ya kampuni ya Guardian Ltd ofisi ya Zanzibar, Mwinyi Sadallah amekamatwa na maofisa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na kupelekwa kituo cha polisi wakati akiwa kazini. Mwinyi alikamatwa wakati akiwa katika kambi ya wagonjwa wa kipindupindu iliyofunguliwa kimyakimya eneo la Karakana, mjini hapa, baada ya ugonjwa huo kulipuka bila ya serikali kutoa taarifa rasmi kwa wananchi hadi jana. Soma habari kamili hapa
TUNAJIANDAA KUIVURUGA AMANI YA Z’BAR?
NI nani anayesema ukweli na yupi anadanganya? Mkurugenzi wa Idara ya Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi au maelfu ya wananchi ambao hawajandikishwa? Mkurugenzi anasema, tena kwa kujiamini kuwa maelfu ya watu na hasa katika kisiwa cha Pemba wameshapatiwa vitambulisho, lakini idadi kubwa wakiwemo wazee, wanalalamika na kula kiapo kwamba wamenyimwa hivyo vitambulisho. Soma makala kamili hapa
DK BILAL AHOFIA ZANZIBAR INAELEKEA KUBAYA
Waziri Kiongozi wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kipindi cha Dk Salmin Amour, Dk Garib Bilal amesema haelewi siasa za Zanzibar sasa zinaelekea wapi. Dk Bilal alisema hayo juzi katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili alipokuwa ametakiwa kuzungumzia vurugu zinazoendelea visiwani Zanzibar katika zoezi la uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Kudumu. Alisema asingependa kusema lolote kuhusu jambo hilo kwa kuwa haelewi siasa za Zanzibar sasa zinaelekea wapi lakini, akashauri mamlaka husika kufanya kila liwezekanalo kudhibiti mambo yanayotokea sasa na kuharibu taswira ya Zanzibar. ”Sielewi siasa hizi zinaelekea wapi na siko katika nafasi nzuri kuzungumzia hilo kwa undani lakini, kwa kuwa kuna mamlaka za kisheria hali iliyopo inapaswa kushughulikiwa na mamlaka hizo.” Soma habari kamili
President Jakaya Kikwete has said that he has not lost hope on the Zanzibar political situation, saying a lasting peace accord between CCM and Civic United Front (CUF) would be achieved. Kikwete said this on Saturday, when speaking to the United Nations (UN) Secretary General Ban Ki-moon on various issues, including the political situation in the Isles. Read more
Joseph Malembeka, anaripoti kutoka Morogoro kuwa, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, Oktoba mosi mwaka huu, katika viwanja vya Ikulu ndogo mkoani Morogoro, atamkabidhi Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, ujumbe wa kupinga na kulani vitendo vya unyanyasaji Zanzibar. Soma habari kamili hapa
CUF KUFUNGA BARABARA KUSHINIKIZA TUME HURU
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema wakati wa maandamano yake keshokutwa kitafunga baadhi ya barabara za Jiji la Dar es Salaam ili kushinikiza kuundwa kwa Tume huru ya Uchaguzi na kutungwa kwa katiba mpya ambayo itapanua wigo kwa demokrasia nchini. Akizungumza jana Dar es Salaam katika kongamano la wanachama wa CUF, Katibu Mkuu wa chama hicho, Seif Sharif Hamad alisema maandamano hayo yataanzia katika barabara ya Uhuru, Bibi Titi na Maktaba hadi kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw John Tendwa. Soma habari kamili
MAALIM SEIF: UANDIKISHAJI USITISHWE
| C |
hama cha Wananchi (CUF), kimeitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kusitisha zoezi la uandikishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK) hadi hapo wananchi wote wenye sifa watakapopatiwa Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi (Zan ID) ili waweze kuandikishwa. Soma habari kamili
TAHRIRI: TUNASUBIRI KILIO ZAIDI ZANZIBAR?
| S |
aa kadhaa baada ya Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Amer Kificho, kutoa rai kwa Wazanzibari akitaka sheria zifuatwe katika mchakato wa uandikishaji wapigakura, na siku moja tu baada ya kuripotiwa kuchomwa kwa nyumba nne kisiwani Pemba, matukio yanayohusanishwa na mgogoro wa uandikishaji wapigakura, nyumba ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahaya Rashid Bugi, iliyoko kisiwani Unguja imenusurika kuteketea kwa moto baada ya watu wasiojulikana kuimwagia petroli na kuitia kibeirti. Soma tahriri kamili
CUF ISSUES THREAT TO SHUN POLL
| T |
he Civic United Front (CUF) announced yesterday that it is set to boycott General Election next year if the Zanzibar government refuse to review the voter registration exercise. This was said by the party secretary general, Mr Seif Sharif Hamad, at a press conference held at party headquarters. Read more
CUF YADAI ASKARI KMKM WANAJIANDIKISHA
| C |
HAMA cha Wananchi (CUF) kimedai kuwa kimegundua mbinu mpya ya ‘kupandikiza watu’kwa kuwaandikisha askari wa kikosi cha KMKM ili kuongeza idadi ya wapiga kura katika uchaguzi mkuu ujao. Hali hiyo imejitokeza katika kituo cha Shehia ya Nungwi baada ya kundi la watu wanaodaiwa kuwa askari wa KMKM kuongozwa hadi kwa Sheha wa Nungwi, Bw.Kombo Mkuni Ali na kupitishwa kujiandikisha bila ya kuwa na vitambulisho vya ukaazi. Soma habari kamili
| V |
URUGU zinazotokana na Uandikishaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili visiwani zimeanza kuathiri Sekta ya Utalii baada ya baadhi ya wageni hao kutoka nchi mbalimbali, zikiwemo Marekani na Ulaya kuanza kuondoka kwa hofu ya usalama wao. Katika maeneo mbalimbali yenye vivutio vya utalii kama vile Nungwi na maeneo ya mshambani katika Shehia za Paje, Makunduchi na maeneo mengine, hoteli zimebaki wazi hatua inayohusishwa na vurugu hizo. Soma habari kamili
GOVT ACCUSED OF PLANNING TO ARREST CUF`S TOP BRASS
| T |
he Opposition Civic United Front (CUF) has accused the government of planning to arrest its top leaders over the ongoing civil strife linked to voter registration in Pemba. CUF secretary-general Seif Shariff Hamad issued the claims at a news conference he addressed yesterday in Dar es Salaam. “What is happening in Pemba is a planned operation by the government of Zanzibar and its security agents to make sure that the ruling CCM wins the elections in Zanzibar next year.” Read more
US DENIES INVOLVEMENT IN PEMBA CHAOS
| T |
he United States yesterday denied being a party to the chaos that has for weeks now dogged the issuance of Zanzibar residence identity cards on Pemba Island, a condition for Zanzibaris to register as voters. The spokesperson for the US Embassy in Dar es Salaam, Dr Ilya Levin, brushed off suggestions linking the recent US travel alert on Pemba to the commotion associated with the issuance of IDs and the voter registration exercise. Read more
VURUGU ZANZIBAR: MAALIM SEIF AKUNJUA MAKUCHA TENA
| K |
ATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ameibuka tena na kukishambulia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali zake mbili, kwa kuendelea kufanya kile alichokiita ni kuchochea vurugu Zanzibar na hususan katika Kisiwa cha Pemba. Maalim Seif, mwanasiasa mwenye nguvu katika visiwa vya Unguja na Pemba, aliyasema hayo jana wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya CUF, Buguruni, jijini Dar es Salaam. Soma habari kamili
POLISI WATAKA CCM PEMBA WASIWAFUNDISHE KAZI
| J |
ESHI la Polisi kisiwani Pemba limejibu tuhuma za CCM kuwa linafanya kazi kwa kukipendelea chama cha upinzani cha CUF, ikisema kuwa inafuata misingi ya sheria. Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Zainab Khamis Shomari aliwaambia waandishi wa habari wiki iliyopita akisema kuwa chama chake hakina imani tena na polisi wa kisiwani Pemba kwa kuwa idadi kubwa ya askari wamejiingiza katika siasa kwa kuishabikia CUF. Soma habari kamili
VITAMBULISHO VYA UKAAZI VITA PEMBA
| N |
I saa mbili asubuhi. Gari iliyonichukua kutoka mji mdogo wa Chake inakaribia kufika kijiji cha Kiuyu Minungwini, jimbo la Ole, Kaskazini Pemba, masafa ya kilomita 25. Katika kijiji hiki, zoezi la uandikishaji wapiga kura lililosimamishwa mwezi uliopita kutokana na watu kususia kujiandikisha na kuzuia wengine wasifanye hivyo lilikuwa liendelee pamoja na vijiji vya jirani. Soma makala kamili
Z’BAR YAZIDI KUZIZIMA, CUF WAITISHA MAANDAMANO
| C |
HAMA cha Wananchi (CUF) kimeandaa maandamano makubwa kupinga Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwa madai kwamba tume hiyo si huru na imeshindwa kutenda haki. Akizungumza Dar es Salam jana Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, alisema ZEC na Idara ya Uandikishaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanashirikiana kuendesha hujuma dhidi ya chama hicho. Soma habari kamili
CUF YAJIPANGA KUSHINIKIZA JAJI MAKAME AJIUZULU NEC
MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema chama chake kinajiandaa kuchukua hatua kali za kisiasa ikiwa ni pamoja na kuitisha maandamano na mikutano ya hadhara kote nchini,kushinikiza kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame. Endelea kusoma habari hii
HAMAD: UANDIKISHAJI PEMBA USOGEZWE
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ameitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuacha mpango wake wa kuendelea kuandikisha wapigakura katika daftari la kudumu kisiwani Pemba unaoanza leo. Alisema kasoro zilizosababisha zoezi hilo kusitishwa, bado hazijapatiwa ufumbuzi na kuna dalili za kukwama tena zoezi hilo iwapo litaanza tarehe hiyo. Endelea kusoma habari hii
KAMANDA WA POLISI APIGWA KICHWA
Uandikishaji wapigakura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK) kisiwani hapa, ulioendelea jana, umekwama tena baada ya kuzuka mapambano kati ya wananchi na polisi yaliyosababisha watu wawili kukamatwa, akiwamo mmoja aliyetuhumiwa kumpiga kichwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Rashid Hemed. Endelea kusoma habari hii
WANANCHI PEMBA WAZUIA UANDIKISHAJI
ZOEZI la uandikishaji wapiga kura kisiwani Pemba, jana liliendelea kupambana na vikwazo kutokana na wananchi kuzuia uandikishaji kuendelea kutokana na wengi wao kutopatiwa vitambulisho, hivyo kutoweza kupata haki ya kupiga kura.Vikundi vya watu kati ya 200 na 300 vilikaa karibu na milango ya vyumba vya kuandikisha wapiga kura wakisisitiza wapewe vitambulisho na kuandikishwa au yeyote yule mwenye kitambulisho haandikishwi. Endelea kusoma habari hii
PEMBA VOTER REGISTRATION STILL UNSETTLING
Clashes between civilians and the police erupted yesterday morning at Minungwini School in Wete District of North Pemba Region, leading to the arrests of two persons and halting voter registration as a result. One of the arrested, Mbarouk Ali, is said to have head-butted the region’s Police Commander, Yahya Rashid Hemed, during the clashes. Said Salim Mbarouk who claimed to be defending youths of Ole Constituency was also arrested. Read more
Pemba voter registration exercise still suspended
The registration of eligible residents of Pemba Island in the Permanent Voters’ Register stood suspended for the second day running yesterday following sporadic scuffles between civilians and riot police. Sources said the heavy police presence at various designated registration centres was reported to have fuelled acts of open defiance among opposition Civic United Front supporters in North Pemba Region, and hence the decision to halt the exercise. Read more
CUF WAPIGWA MARUFUKU KUANDAMANA KUPINGA DAFTARI LA WAPIGAKURA
JESHI la Polisi mkoani Kusini Pemba limepiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na CUF ya kupinga kuanza tena kwa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura. CUF ilikuwa imedhamiria kufanya maandamano iliyoyaita kuwa ni makubwa siku ya Jumamosi kwa ajili ya kupinga mpango wa serikali wa kuanza upya kwa zoezi hilo kwa kutumia vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi. Endelea kusoma habari hii
POLISI WATISHIA KUTUMIA SILAHA ZA MOTO Z’BAR
SIKU moja baada ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Rashid Bugi kunusurika kupigwa kichwa, Jeshi la Polisi mkoani humo limetangaza kuwa halitasita kutumia silaha za moto kudhibiti vurugu. Kamanda Bugi alisema jana kuwa, Polisi haitasita kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha kunakuwa na ulinzi na usalama katika vituo vyote vya kuandikisha watu kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Endelea kusoma habari hii
CUF CHAKANA KUWACHOMOA WANAOANDIKISHWA KWA KURA
Chama cha Wananchi (CUF), kimekanusha madai ya kwamba wanachama wake ndio waliohusika kuwachomoa wananchi waliokwenda kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura visiwani Zanzibar. Akizungumza kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa chama hicho, Salum Bimani, amesema wananchi wenyewe ndio waliofanya hivyo baada ya wengi wao kukosa vitambulisho vya ukaazi. Endelea kusoma habari hii
WATU wasiojulikana usiku wa kuamkia jana walichoma moto nyumba mbili
ikiwemo ya Sheha wa Shehia ya Kiuyu Minungwini katika Jimbo la Ole Mkoa
wa Kaskazini Pemba. Mbali na nyumba hizo, pia watu hao wameweka mizinga mitatu ya nyuki katika Kituo cha Uandikishaji wapiga kura cha Kambini Mchanga mdogo katika Wilaya ya Wete usiku huo huo kwa lengo la kuzuia kazi za uandikishaji. Endelea kusoma habari hii
NYUMBA ZAVAMIWA USIKU WA MANANE
Wakati uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
(DKWK) ukiwa umekwama kwa siku ya pili sasa, vitendo vya hujuma na
uvunjifu wa amani vimezidi kushika kasi Jimbo la Ole, Wilaya ya Wete,
Mkoa wa Kaskazini Pemba. Hujuma hizo zinafuatia kundi la watu kuvamia nyumba saa 8:00 usiku na kuvunja baadhi yake, nyingine zikichomwa moto kisha kuwashambulia watu waliomo kwa bakora na magongo. Endelea kusoma habari hii
ZANZIBAR SASA NI BALAA TUPU, MABOMU RISASI ZARINDIMA
MAENDELEO ya uandikishaji wapiga kura kisiwani Pemba, yamezidi kuwa tete baada ya Jeshi la Polisi kulazimika kutumia risasi za moto na mabomu ya
machozi kutawanya wananchi waliokataa kuondoka karibu na vituo vya
uandikishaji wapiga kura.Hatua hiyo ya utumiaji wa nguvu imekuja siku moja baada ya polisi kuonya kuwa, italazimika kutumia nguvu za ziada kutuliza vurugu kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura, baada ya wananchi kuwarushia mawe polisi kwenye moja ya vituo hivyo. Endelea kusoma habari hii
VURUGU UANDIKISHAJI DAFTARI: PEMBA HAPAKALIKI
WAKATI shughuli ya undikishaji Daftari la Kudumu la Wapigakura ikiendelea Zanzibar hali si shwari kisiwani Pemba baada ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kulazimika kurusha risasi za moto na mabomu ya machozi angani kutuliza wananchi. Hatua hiyo ilitokana na baadhi ya wananchi hao kugoma kwenda kujiandikisha na kupinga kile walichodai kulazimishwa kwa nguvu na askari kufanya hivyo. Endelea kusoma habari hii
CCM ZANZIBAR WASHTUSHWA NA MATOKEO YA UTAFITI
BAADHI ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Zanzibar, wameshtushwa na matokeo ya utafiti wa masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yanayoonyesha kuwa katibu mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad anapewa nafasi kubwa ya kushinda kiti cha urais wa visiwa hivyo mwakani. Ripoti hiyo iliyotolewa juzi na kampuni ya Synovate, pia inaonyesha kuwa waziri kiongozi wa zamani wa Zanzibar, Gharib Mohammed Bilal wa CCM ndiye anayefuatia kwa karibu Maalim Seif kumrithi Rais Amani Abeid Karume, ambaye anamalizia muda wake wa miaka 10. Endelea kusoma habari hii
MAALIM SEIF YUKO JUU URAIS WA ZANZIBAR
KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, anapewa nafasi kubwa ya kushinda kiti cha urais visiwani Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa kampuni ya Synovate. Synovate, ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kama Steadman Group Tanzania, imesema katika matokeo ya utafiti huo uliofanyika miezi mitatu iliyopita kwa kuwahoji wananchi wa Zanzibar pekee kuhusu urais wa visiwa hivyo, mtu anayeweza kumfuatia Maalim Seif ni aliyewahi kuwa Waziri Kiongozi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Gharib Mohammed Bilal. Endelea kusoma habari hii
MAFUTA YA ZANZIBAR YAMPALIA KHATIB
WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Muhammed Seif Khatib, amesema hatazungumzia tena uamuzi wa Zanzibar kuliondoa suala la mafuta na gesi katika Muungano. Waziri Khatib alitoa kauli hiyo jana alipoombwa kuzungumzia kama hatua hiyo iliyofikiwa wiki iliyopita si ya kuchokonoa muungano wa Tanzania. “Suala hilo sitaki kulinzungumzia, sitazungumzia tena kwa sasa, wewe andika hivyo hivyo,” alisema Khatib. Endelea kusoma habari hii
PEMBA YAWASIKITISHA WABUNGE EAC
KAMATI ya Sheria ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, imeeleza kusikitishwa na vurugu zinazoendelea kisiwani Pemba, kuhusiana na suala la uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura. Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Abdullah Mwinyi, alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na anashangazwa na kusikitishwa na migogoro ya kisiasa inayotokeza mara kwa mara katika visiwa hivyo. Endelea kusoma habari hii
KAZI ya uandikishaji wapiga kura kisiwani Pemba, imeingia dosari na taarifa kutoka katika kisiwa hicho zimeeleza kuwa wananchi wengi wamegoma kujiandikisha na kuweka vikwazo kuwazuia wachache wanaotaka kwenda kujiandikisha kutokana na kutoridhika na mwenendo wa zoezi hilo. Matokeo yake ni kuwa vituo vitatu vya uandikishaji; Kiuyu, Kiuyu Mjini na Mchanga Mdogo, katika Jimbo la Ole, vilifungwa kwa siku ya pili jana. Endelea kusoma tahriri hii
JESHI la Polisi kisiwani Pemba limekamata na kuyategua mabomu 20 ya kutengenezwa kienyeji, aina ya TNT, ambayo yalipangwa kutumika kufanyia hujuma za kulipua madaraja kisiwani humo. Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba, Said Marekano, siku moja baada ya kuripotiwa kuwapo kwa jaribio la kutaka kulipuliwa kwa mabomu Daraja la Piki, Mkoa wa Kaskazini Pemba. Endelea kusoma habari hii
WABUNGE CCM, CUF ZANZIBAR WAUNGANA, WASHAMBULIA MUUNGANO
“Hatuoni kwamba vikao hivi vya pamoja (Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano na waziri Kiongozi wa SMZ ) vinakuja na suluhisho la tatizo la Muungano, vyenyewe ni sehemu ya tatizo, ili kutimiza wajibu wetu kama Bunge la watu lenye jukumu la kusimamia matumizi ya fedha za walipa kodi, liitake Serikali ya Muungano isitishe mara moja vikao hivi, badala yake Mkataba wa Muungano uletwe hapa bungeni kama nukta kuu ya mjadala, hapo ndipo tuanzie na tumalizie kero za Muungano. Ofisi ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi hazina uwezo wa kujadili Muungano, hapa ni kizungumkuti kinachofanyika. Katika Mkataba wa Muungano, hakuna sehemu inayosema kufutwa kwa Serikali ya Tanganyika.”
UCHAGUZI MAGOGONI LEO, MWAKILISHI WAWI AFARIKI
Wakati wananchi wa Magogoni leo wanachagua mwakilishi wa kuziba pengo lililoachwa kwa kifo cha Mwakilishi wa CCM, Daud Hassan Daud, Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani katika Baraza la Wawakilishi, Mwakilishi wa Wawi, Soud Yussuf Mgeni, 61 (CUF), naye amefariki dunia. Mgeni alifariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU). Soma habari hii..
CUF ZANZIBAR YATAKA ZEC ITENDE HAKI
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuendesha uchaguzi kwa uhuru, haki na uwazi ili kila chama kiridhike na matokeo yatakayotangazwa katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Magogoni unaotarajiwa kufanyika Mei 23 mwaka huu. Hayo yalielezwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa jimbo la Magogoni mkoa wa Mjini Magahribi uliofanyika katika viwanja wa Daraja Bovu. Soma habari hii…
ZANZIBAR: CHAGUZI ZA VURUGU HADI LINI?
Hebu sasa chunguza takwimu hizi kwa makini sana: katika jimbo la Magogoni watu waliojiandikisha kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka 2005 walikuwa ni 9,210 ambapo waliopiga kura ni 7,364. Kinachoweza kuonekana hapo ni tofauti ya watu 1,846 sawa na asilimia 20.04 ya watu wote waliojiandikisha kupiga kura, ambao ama hawakupata fursa ya kupiga kura kutokana na mizengwe iliyozuka baadae ya watu kutoshuhudia majina yao katika daftari la kudumu au ndio kusema kura zao zimeharibika. Hii ni idadi kubwa sana kwa mazingira ya Zanzibar ya watu kukosa kupiga kura burebure. Mashaka yanaanza kwamba chini ya mpango wa makusudi kabisa watu hao walinyimwa haki yao ya kuchagua. Soma makala hii..
SHAABAN MLOO: SHINA LA CUF LISILOSAHAULIKA
“Nakuachieni Chama wajumbe wote wa Mkutano Mkuu huu wa leo mkiwa na jukumu moja kubwa sana. Ingawa sisi tunastaafu, lakini tutaangalia kwa macho mawili utendaji wenu katika kata, matawi, majimbo, wilaya na taifa. Nakuachieni Chama kilichokamilisha theluthi mbili ya mtandao wake katika mikoa 26 ya Tanzania . CUF imeenea kila mkoa. Katika wilaya 130, CUF iko wilaya 117, katika vitongoji 38,000, CUF ina asilimia 20, katika vijiji 11,600, CUF ina asilimia 15. Mitaa yote 3,080, CUF ina asilimia 20.”
SEIF: LIPUMBA LAZIMA AGOMBEE URAIS 2010

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amempigia debe Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, kuwa lazima agombee urais wa Jamhuri ya Muungano katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani. Soma habari hii…
TUMEJIPANGA VYEMA KWA 2010 – LIPUMBA

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama, Masoud Abdallah
“Misingi ya chama chetu ilikuwa ni mizuri labda useme kwamba hapa katikati katika mazungumzo, tulipokuwa tumefanya mazungumzo ya CCM na CUF kuhusu mpasuko wa kisiasa Zanzibar hilo jambo lilichukua muda mrefu tukalikamilisha lakini wenzetu hawakuweza kutekeleza. Kwa hiyo, kusema chama kimekosa mwelekeo inakuwa kwa kweli ni kwa sababu shughuli zetu hazielezwi vya kutosha ndani ya vyombo vya habari. Ukienda kama Kusini, Kilwa, Liwale, Tandahimba, ukaenda Newala, ukaenda Nanyumbu, Mtwara Vijijini hali ya chama unaikuta ni nzuri sana, watu wamehamasika wanahitaji mabadiliko. Kanda ya Ziwa, ukienda Muleba, ukienda Bukoba, Bukoba Vijijini hali ya kutaka mabadiliko ni kubwa, hali ya chama ni nzuri katika maeneo mengi. Sasa yeye anazungumzia kwamba kimekosa mwelekeo labda kwamba siku hizi hatuna mafuso, vijana wakawa wanaenda na mafuso kwenye mikutano ya hadhara, lakini hali ya vijana imekuwa ngumu, walikuwa wanakodi magari wenyewe.” Soma mahojiano haya

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Nne wa Taifa
“Mabadiliko hayo yamegusa taratibu za kuwapa wagombea ubunge na uwakilishi kwa upande wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu kutokana na kile kinachoelezwa kuwa taratibu zinazotumika sasa zimekuwa zikisababisha misukosuko na wakati mwingine kutishia uhai wa chama hicho. Ili kukinusuru chama hicho na mipasuko nyakati za kuwapa wagombea ubunge kwa tiketi yake, mabadiliko ya Katiba yanayotajwa kulenga kuziba mianya ya mipasuko, kuimarisha umoja wa chama hicho, kuepusha vitendo vya rushwa na kuhakikisha wanachama wote wanashiriki kikamilifu kumpata mgombea, yanabainisha kuwa kwa upande wa Zanzibar, wagombea wa ubunge au uwakilishi wapigiwe kura za maoni na wanachama katika matawi yote majimboni.” Soma habari hii

Mwakilishi wa Chambani, Abbas Juma Muhunzi
“…kiongozi wa kambi ya upinzani kwenye baraza la wawakilishi, Abubakar Khamis Bakari alisema Mhunzi anashutumiwa kutumia fedha kifisadi na anadaiwa kuchota zaidi ya Sh200 millioni ambazo inadaiwa zilitengwa kwa ajili ya kununulia magari wajumbe wenzake. Bakari alisema mwakilishi huyo anadaiwa kuchukuwa fedha hizo kwa ajili ya kutafuta magari kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi na fedha za michango ya wajumbe wa baraza hilo wa kambi ya upinzani. Kiongozi huyo alisema Mhunzi alipewa kiasi cha Sh72 milioni tangu mwaka 2006 kwa ajili ya kununua magari ya wawakilishi wenzake, lakini hadi sasa ameshindwa kufanya kazi hiyo wala kurejesha fedha alizopewa.” Soma habari hii.

Mjumbe wa Baraza Kuu, Wilfred Lwakatare
“Profesa Lipumba ndiye mwenye madaraka ya kufanya uteuzi na yeye aliamua kuweka majina mapya ya wagombea, hivyo namshukuru Mungu kwamba katika kura za wajumbe wa mkutano mkuu uliopita, mimi ndiye mjumbe pekee niliyeongoza kwa kupata kura nyingi kuliko wote na kufuatiwa na Katibu wa Zanzibar, Juma Duni Haji ambaye amerudishwa katika nafasi hiyo. Naamini Joram Bashange atakuwa anafanya kazi ya kujituma zaidi yangu ili wajumbe wasiwe na maswali zaidi ya kujiuliza, na naamini sisi wote ni wachapakazi, hakuna matatizo.” Soma habari hii.
TAMWA, CUF WAMLILIA REHEMA MWAKANGALE

Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
Kutokana na kifo hicho, CUF wametoa pole kwa Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Media, waandishi wote wa habari nchini, ndugu na jamaa wa marehemu na kusema wanaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na maombolezo. Aidha, mazishi ya mtangazaji huyo yanatarajiwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam. Taarifa zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam, kutoka kwa jamaa wa marehemu Lulu Mwanjesa, mwili wa marehemu utaagwa nyumbani kwa bibi yake, Sinza Makaburini, kabla ya kuelekea Mlalakuwa jirani na JKT kwa baba mkubwa wa marehemu. Soma habari hii. Soma habari hii.
PROF. LIPUMBA: ZIARA YA BUTIKU CUF HAIKUWA NA HILA

Mwenyekiti, Prof. Ibrahim Lipumba
“Kikubwa ambacho tuiliongea na mzee Butiku ni kumshukuru tu kwa kuitikia mwaliko wetu wa kuhudhuria katika mkutano wetu mkuu wa nne wa chama. Ila alipitia hapa kumsalimia Katibu Mkuu, Maalim Seif. Mzee Butiku alitueleza siku ile kuwa tatizo la uongozi Tanzania si la mmoja na alitaka tushirikiane ili kuondoa tatizo hilo kwa mshikamano na umoja wa kitaifa. Lakini kwa bahati mbaya sana baadhi ya vyombo vya habari vilimnukuu vibaya.” Soma habari hii.

Naibu Mkurugenzi wa Siasa, Dkt. Juma Ameir Muchi
“Chama cha CUF hakitakubali kurudi kwenye meza ya mazungumzo yaliyokwishamalizika, labda rais kama anaona kutakuwa na umuhimu wa hilo awakutanishe wagombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif na Rais Karume. CCM wanaendelea kulipwa ruzuku zao bila usumbufu, lakini sisi tunaendelea kusumbuliwa, tunaogopa suala hili kulipeleka mahakamani kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wakatuzungusha bila kupata mafanikio yoyote kwa vile mahakama zetu zinajulikana zilivyo.” Soma habari hii.
“BAINA YA VIONGOZI WA CCM NA CUF, NANI WALEVI WA TENDE!?”
“Viongozi wanakuja kueleza, lakini mimi nasema moja tu: Rais Kikwete, sisi si walevi wa tende. Walevi wa tende ni wale wal’owaua Wazanzibari kwa bunduki siku ya Januari 26 na 27, 2001. Na tunakushangaa sana, kwenda Pemba, ukaja Unguja katika mwezi huu wa huzuni, lakini ukashindwa hata kusema “Poleni” kwa wale waliofikwa na maafa haya. Umeshindwa kabisa kutamka hayo.” Soma kauli ya Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu na Mahusiano ya Umma, Salim Bimani
“WANAOUA ALBINO WAUAWE, WALIOUA WAZANZIBARI JE?”

Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Juma Duni Haji: "Anayeua albino auliwe, anayeua Wazanzibari afanyweje?"
“Nikasema lo, Mashallah! Anayeua albino anaye auliwe, aliyewaua Watanzania na Wazanzibari tarehe 27, afanywe nini? Maana kama ni mwanaadamu na ni uchungu wa roho, roho ya albino na roho ya Mzanzibari ni sawa sawa. Tafauti iliyopo ni kwamba yule aliyemuua albino hajapatikana, bado anasakwa, lakini walowaua Watanzania na Wazanzibari tarehe 27 wanajuilikanwa. Tena wengine, baada ya kuua, Mheshimiwa Mkapa kawatunza vyeo, ati wamefanya kazi nzuri kutuua.” Soma kauli ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Juma Duni Haji
“KIKWETE AKOME KUTUFITINISHA WAZANZIBARI!”

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad: "Kikwete akome kuwafitinisha Wazanzibari!"
“Linamuuma sana tu, kwa sababu wao wamo katika kutekeleza mkakati tangu aliouwacha Julius Nyerere kwamba Zanzibar itoweke katika ramani ya dunia. Sasa mshikamano wenu Wazanzibari unawafanya wao wasifanikiwe. Kwa hivyo, alilokuja kufanya Kikwete ni kujaribu kuwagawa tena Wazanzibari kwa kutumia wimbo wa Mapinduzi. Tena, mimi nashukuru Mungu, kasema ‘Mapinduzi yetu,’ katumia wimbo wa Mapinduzi yao. ‘Mapinduzi yao’ si Mapinduzi ya Wazanzibari, jamani. Mujuwe hilo! Kwa hivyo, anataka kutumia wimbo huo atugawe, lakini kachelewa. Kachelewa. Hatugawiki tena ng’o! Tena namwambia Jakaya wa Mrisho wa Kikwete akome, akome, akome! Akome kutuletea fitna katika nchi yetu. Akome, akome kuja kutugawa Wazanzibari. Fanya chokochoko zako huko huko Bara. Namna gani, bwana!?” Soma kauli ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad
“IKIWA KUWALINDA ALBINO KUMEMSHINDA, KIKWETE ATAWEZAJE KUYALINDA MAPINDUZI?”

Makamo Mwenyekiti, Machano Khamis Ali
“Nasema kama Kikwete anao uwezo wa kuyalinda Mapinduzi, kwanza angewalinda Albino wanaouliwa kama wadudu. Hawa ni binaadamu, wanakufa katika nchi yake, anashindwa kuzuwia. Ataweza kuzuia watu wakitaka kuyapindua Mapinduzi? Kwa hivyo ni usanii tu. Au atwambie, kwa sababu magazeti yanaandika kuwa albino wanakufa kwa sababu ya ushirikina wa watu kutafuta mali na vyeo, ni miongoni mwa hao wanaotafuta vyeo na hivyo anaruhusu wale wauliwe? Kama harusu, hana uwezo wa kuyalinda Mapinduzi. Kwanza atuoneshe mfano, awalinde albino wasiuliwe. Akituonesha mfano kwamba albino hawafi – na kawazuia yeye – basi tutaamini anao uwezo wa kuyalinda Mapinduzi. Nawalinde wale.” Soma kauli ya Makamo Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali
HAMAD RASHID AFAFANUA MSIMAMO WAKE KUHUSU ALBINO

Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed: "Hatuwezi kuzuia mauaji kwa kushajiisha mauaji. Ni kiyume na Katiba na ni kinyume na mantiki!
“Ikiwa kauli ya Pinda ingefanya kazi kwa kumuua aliyetuhumiwa kumua albino ni wangapi wangeuawa? Je, sheria ndivyo inavyotaka? Au ukiwekewa kidole cha albino nyumbani mwako, halafu ukauliwa, huyo aliyekuua ana uhakika gani kuwa na yeye siku moja hatauliwa na ndugu zako? Kwa hiyo tungetengeneza msururu wa mauaji kwa jazba tu.” Soma habari hii…
MIAKA NANE BAADA YA MAUAJI, WAZANZIBARI WAENDELEA KULIA

Said Hamad akighani utenzi wa maombolezo
Wamekuja na wazazi
Wamejawa nasimanzi
Sikitiko na majonzi
Kwa yale tulofanyiwa
Wapo mbele Mayatima
Waso baba wala mama
Twawaonea huruma
Yawanamia dunia
Kila tunapokumbuka
Mambo yaliyotufika
Machozi humiminika
Hushindwa kujizuia
Elfu mbili na moja
Bara, Pemba na Unguja
Tulifikwa ni miuja
Ya kuuliwa Raia
Soma utenzi huu wa Wazanzibari wakiomboleza miaka nane ya kuuliwa kwa wenzao na serikali ya CCM
“TUMECHOKA, TUNATAKA MABADILIKO” – WANAWAKE WA ZANZIBAR

Msomaji wa Risala ya Wanawake wa Zanzibar katika Kumbukumbu za Miaka Nane ya Mauaji ya Dola dhidi ya Wazanzibari
“…kama vile haya hayajatosha, na sasa wakati tunaelekea katika uchaguzi mkuu wa 2010, matayarisho ya mipango kama hiyo tayari inaonekana kuandaliwa. Wiki iliyopita tu, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, alipofanya ziara hapa Zanzibar alitoa kauli kali zilizofichua rangi zake halisi dhidi ya Wazanzibari na zinazokwenda kinyume na misingi ya umoja na demokrasia. Sisi, kama ilivyo dunia nzima, imemsikia Rais Kikwete akiwa Pemba akitutangazia kwamba wapinzani tutasubiri muda mrefu sana kabla ya kupata nafasi ya kuunda Serikali nap engine tusiipate kabisa nafasi hiyo katika uhai wetu. Na hapa Unguja, alikuja kukoleza chuki na kuendelea kutugawa Wazanzibari pale aliposema kwamba eti sisi wapinzani ni wapinga Mapinduzi na hivyo hatuwezi kamwe kupewa fursa ya kuiongoza Zanzibar…kauli hizi hazina maana nyengine yoyote zaidi ya kuwa ni maandalizi mengine ya kuja kutumia nguvu za kijeshi na wizi wa kura kulazimisha CCM iendelee kutawala huku wakijua kwamba chama hicho kimepoteza mvuto na hakikubaliki tena kwa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla.” Soma risala hii ya wanawake wa Zanzibar katika Kumbukumbu za Nane za Mauaji ya Januari 2001
HAMAD: KIKWETE ACHA KUTUVURUGA

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad: "Kikwete ukome, tena ukome..."
“Viongozi wa Tanzania Bara wapo katika mkakati wa Mwalimu Julius Nyerere wa kuitokomeza Zanzibar, tunamwambia Kikwete kachelewa Wazanzibari hatugawiki tena ng’o tena namwambia akome akome akome kutuletea fitna katika nchi yetu, afanye chokochoko huko huko Bara.” Soma habari hii…
SPIKA SITTA, PINDA WAMETUPOTOSHA

Samuel Sitta, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amepotosha kuhusu Rais kutumia ndege ya serikali kwa shughuliza chama chake
“Tatu, hatukubaliani na upotoshaji wa Spika Sitta kuwa haiwezekani kwa rais kutenganisha majukumu yake kama rais na kama mwenyekiti wa CCM, kwani sisi tunaamini kuwa inawezekana, kinachotakiwa ni kwa mhusika (Rais Kikwete) kuwa na utashi na utayari wa kutodharau misingi ya utawala bora wala kuwa mwepesi wa kubagua wafuasi wa vyama vingine vya siasa pindi awapo kwenye ziara za kiserikali.” Soma tahriri hii ya Tanzania Daima…
PROFESA LIPUMBA AMTAKA JAJI MAKAME AJIUZULU
Siku chache baada ya uchaguzi mdogo wa ubunge wa Mbeya Vijijini, mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameibua shutuma nzito dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kumtaka mwenyekiti wake, Jaji Lewis Makame, ajiuzulu. Soma habari hii…
KIKWETE AAMBIWA HAJUI MAANA YA MAENDELEO

Juma Duni Haji, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
“Kama maendeleo yanapimwa kwa kuangalia barabara za kwenda uchochoroni na kuvalishwa kofia ya kiua na wananchi wa Nungwi, basi tunampongeza Rais wetu. Barabara zote zilizopo Zanzibar ambazo Rais anasema kuwa ni maendeleo, kwa ubora hazikaribii hata barabara moja tu ya kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma. Lakini sisi tumeshazishtukia kauli hizi ni za kilaghai, zinalenga na kujipendekeza kwa SMZ na Rais Amani ili wanyonye petroli yetu, hatukubali.” Soma habari hii…

Jaji Lewis Makame, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC). Amevurunda.
Uchaguzi mdogo wa Mbeya Vijijini jana asubuhi ulianza kwa vituko baada ya kubainika kuwa baadhi ya masanduku ya kura yalihifadhiwa katika nyumba za watu, huku yakihamishwa kiholela kutoka sehemu moja kwenda nyingine huku vituo vingine vikichelewa kubadikwa majina ya wapiga kura. Katika tukio mojawapo, mwanafunzi, Severine Gama wa shule ya msingi alikutwa akiwa amebeba sanduku la kupigia kura na alikuwa hana msimamizi wala polisi wakati akipeleka sanduki hilo katika kituo cha kupigia kura cha eneo la Mbalizi katika Kata ya Utengule Usongwe. Soma habari hii…
KAULI ZA KIKWETE, PINDA ZAWEKA UFA

Matokeo ya CCM kutokujifunza kwa mauaji iliyoyafanya Januari 2001. Hii ni picha ya mwaka 2005, ambapo kijana huyu - Nassor Ali - alivamiwa na kupigwa na kundi la Janjaweed, Mikunguni Unguja
Mwenendo wa mambo nchini unazidi kuwa tata, baada ya viongozi wakuu wawili wa kitaifa kutoa kauli zilizotafsiriwa na wachambuzi wa mambo kuwa zinaweza kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini. Viongozi hao, Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu wake, Mizengo Pinda, wiki iliyopita, kwa nyakati tofauti, walitoa matamshi yenye kuashiria kwamba serikali wanayoingoza haiko tayari kuachia madaraka na kuchochea mauaji miongoni mwa wanajamii. Soma habari hii…
RAIS KIKWETE ANAPOZOMEA WAPINZANI

Rais Jakaya Kikwete. Kauli zake alizozitoa Zanzibar zinaifanya dhamira yake kutiliwa mashaka
Sasa hapa kuna matatu: Ama Rais ameshindwa kutekeleza ahadi yake ya ‘kumaliza mpasuko Zanzibar na sasa anakiri;’ au kauli yake ilikuwa inathibitisha kuwa hakuwa na dhamira ya kweli pale alipoahidi kumaliza mpasuko; au kauli hii ilikuwa njia isiyo rasmi ya kuvunja kamati yake. Na kauli ya Rais Kikwete haina utata. Ina maana iliyokusudiwa. Imetolewa katikati ya ngome ya upinzani, Pemba. Inapata nguvu kutokana na ukweli kwamba, tangu mparaganyiko ulioletwa na wajumbe wake katika Kamati ya Muafaka, hamasa ya ‘kumaliza mpasuko’ inaonekana kuyeyuka. Soma habari hii…
PROFESA LIPUMBA ASEMA CCM NI KIKWAZO
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema kukwamishwa kwa juhudi za kuleta mwafaka baina yao na CCM Zanzibar kwa mara ya tatu, ili kuepusha maafa kama yalitokea Januari 26 na 27 mwaka 2001 kisiwani Pemba, ni ishara tosha kwamba Chama hicho hakikujifunza chochote kutokana na maafa hayo. Aidha kimeitaka serikali ya Jamhuri ya Muungano iseme basi kwa ukandamizaji wa haki za binaadamu huku kikiitaka tume za ucvhaguzi kusema basi kusimamia chaguzi zisizokidhi viwango vya demokrasia kwa maslahi ya wachache. Soma habari hii…
CUF HAIYATAMBUI MATOKEO YA UBUNGE MBEYA VIJIJINI

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF
“Tatizo kubwa ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa wananchi kutopata haki ya kupiga kura, ni watendaji wa baadhi ya vijiji waliohodhi shahada za kupigia kura za wananchi kwa madai kuwa watapata vocha ya mbolea ya ruzuku. Mwananchi wa Kijiji cha Msituni, Kata ya Iwindi, Ezekieli John alituambia kwamba hawezi kupiga kura kwa sababu shahada yake ilichukuliwa na balozi wa nyumba kumi na taarifa hiyo tumeipeleka polisi.” Soma habari hii…
“HASIRA ZA WAPEMBA ZINATOKANA NA KUFELI KWA SERIKALI ZA CCM”

Salim Bimani, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu na Mahusiano na Umma
“…ikiwa kweli Rais Kikwete ana dhamira ya kuisaidia Zanzibar kuondokana na ule aliouita ‘Mpasuko wa Kisiasa’ anapaswa kuliangalia suala hili kwa uadilifu. Kuendelea kwake kupiga mifano ya watu ‘waliogomewa’ kupata huduma za kijamii kutoka kwa wenzao lakini asigusie kabisa sababu halisi zilizopelekea hao waliogomea kugomea, ni kuwabagua watu na ni kuendeleza mpasuko. Tunakusudia kusema, ikiwa Rais Kikwete anaongelea kisa cha mwanachama wa CCM kususiwa biashara yake na wana-CUF, kwa mfano, basi pia na azungumzie kuwa mwana-CCM huyo aliyesusiwa ndiye aliyeshiriki kuwabaka watoto wa wana – CUF, kuiba mali zao na kuwaletea makundi ya Janjaweed kuwavunjia nyumba zao. Je, Rais Kikwete yuko tayari kuueleza ukweli huu pia?” Soma taarifa hii…
CUF: JK ANAONGEZA MPASUKO ZAIDI

Waandamanaji wakiwa na mabango yao, Zanzibar, kushinikiza kuwekwa saini kwa Muafaka kati ya CCM na CUF, Machi 2008. Sasa ni wazi kwamba Rais Jakaya Kikwete hakuwa na dhamira ya kuupatia ufumbuzi wa kudumu mgogoro wa Zanzibar
“Kauli ya Rais Kikwete ni tatizo linaloongeza matatizo, rais lazima asimamie demokrasia na nafasi ya uhuru wa nchi na watu wake, lakini badala yake yupo kinyume. Anatonesha vidonda na majeraha makubwa ya kisiasa… anaonyesha wazi sera yake ni kuendeleza wizi katika uchaguzi visiwani Zanzibar. Hana nia ya kuziba mpasuko wa kisiasa ulio Zanzibar ambao alisema anaushughulikia. Huko ni kukosa uongozi bora na kuhatarisha amani na uhuru wa kweli wa wananchi kwa njia ya demokrasia ya uchaguzi. Rais hana nia njema na demokrasia.” Soma habari hii…
CUF YANGUNDUA MAJINA HEWA MBEYA

Naibu Mkurugenzi wa Blue Guards, Rajab Mazee
“Tumegundua kasoro mbalimbali, kwa mfano katika kata za Santilya, Iwiji na Ilembo kuna majina 252 ya watu ambao tayari walishafariki dunia, na katika kata ya Ilembo kuna majina 25 ya watu ambao wamejiandikisha mara mbili. Matatizo kama hayo pia yako katika kata ya Iyunga Mapinduzi.” Soma habari hii…
CCM YATUMIA MBOLEA KUHADAA WAPIGA KURA MBEYA
“Jana nilikuwa kijiji cha Isupo na mjumbe wa serikali ya kijiji nikiongea na wananchi. Wengi wanalalamika kutorudishiwa kadi zao walizoambiwa wazipeleke kwa uongozi wa kijiji. Hadi juzi kadi hizo zilikuwa hazijarudishwa, na huenda wasipige kura. Juzi, ofisa wa kata ya Iyunga Mapinduzi alitangaza punguzo la bei ya mbolea kutoka Sh100, 000, hadi Sh45, 000. Hii ni rushwa, kwa nini punguzo la bei lisubiri wakati wa uchaguzi?”
CUF YAISHUSHIA CHADEMA KOMBORA

Ismail Jussa, Msaidizi Maalum wa Katibu Mkuu (Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa) na Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF
“Viongozi takribani wote wa CUF tumeonja sulubu za CCM na serikali zake katika kupigani mabadiliko. Mwenyekiti Prof. Ibrahim Lipumba, Makamu Mwenyekiti Machano Khamis, Katibu Mkuu Seif Sharif Hamad, Manaibu Katibu Mkuu, Juma Duni na Wilfred Lwakatare, Kiongozi wa Upinzani Bungeni Hamad Rashid na wajumbe wengi wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa wa CUF wamekwenda jela na hata kuchezea vipigo vya vyombo vya dola kuleta mageuzi hapa nchini. Ni kiongozi gani wa Chadema aliyejitoa muhanga kama huu kwa ajili ya Watanzania?”
MREMA AWA KIVUTIO KATIKA UCHAGUZI MBEYA

Augustine Mrema, Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP)
MWENYEKITI wa TLP, Augustino Lyatonga Mrema juzi alikuwa kivutio katika mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mbeya Vijijini kwa tiketi ya CUF, Daudi Mponzi uliofanyika kwenye kiwanja cha stendi ya mabasi cha Mbalizi alipodai kuwa wamejitakia maisha ya shida kwa kuichagua CCM.
VIONGOZI WA CUF KUCHAGULIWA FEB 23-27

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF
“Tunataka hadi kufikia mwaka 2010 wagombea wa CUF katika chaguzi zote nchini wawe wanapigiwa kura na wanachama majimboni mwao. Lengo ni kuondoa malalamiko na lawama kwa wanaoshindwa. Sambamba na hilo la kupokea na kujadili taarifa hiyo, pia baraza kuu litaandaa kazi za chama kwa miaka mingine mitano kuanzia mwaka 2009 hadi 2014.”
RAIS KIKWETE JUA LINATUA LINI?

Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kukwama kwa mazungumzo hayo kumezaa mazingira mapya ya Watanzania kuanza kuhoji juu ya dosari za muungano na serikali kutoa majibu rahisi kwa maswali magumu. Mazingira ya mwafaka wa kisiasa ni ajenda inayopuuzwa kila mara lakini matokeo ya uchaguzi mkuu ndiyo yanayotuumbua na wanasiasa hutumia mwafaka kama mtaji wao kisiasa. Mgogoro wa Zanzibar si wa kubeza, mabilioni ya fedha na muda mrefu vimetumika kuwezesha mwafaka kufanikiwa. Ahadi ya Rais Kikwete bungeni tunadhani haikuwa porojo, ndio maana wanahabari walishinikiza kutekelezwa mwanzoni mwa muda wa uongozi. Kadri muda unavyokwenda ukingoni lisipotekelezwa na kuzaa machafuko basi Kikwete atalaumiwa.
VIONGOZI TLP, PPT WATINGA MBEYA VIJIJINI KUISAIDIA CUF
IKIWA imebaki wiki moja kufanyika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Mbeya Vijijini, wenyeviti wa taifa wa vyama vya CUF, Tanzana Labour (TLP) na PPT Maendeleo, wamewasili mkoani Mbeya kuongeza nguvu katika kampeni za mgombea wa CUF, Daud Mponzi. Viongozi hao wa ngazi ya kitaifa waliowasili jana pamoja na Mweyekiti wa CUF Taifa, Prof Ibrahimu Lipumba ni Augustino Mrema wa TLP na Peter Mzirai PPT Maendeleo.
“SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA INAWEZEKANA ZANZIBAR”

George Washington
“Nashawishika kusema kwamba kiasi kikubwa cha maumivu ya kisiasa ya Zanzibar yamechipuka kutokana na kutengwa kisiasa. Enzi za utawala wa Omani, Ureno, Sultani na Uingereza, madaraka yalikuwa mikononi mwa wachache. Hakukuwa na mashauriano au kufikiria maslahi ya Wazanzibari walio wengi, au kama kulikuwepo ni kwa kiasi kidogo sana. Upande mmoja ulikuwa na madaraka yote na upande mwingine haukuwa na kitu. Kupoteza madaraka ilikuwa ni kupoteza kila kitu. Kwa kiwango fulani utamaduni huu bado upo hadi leo. Ingawa mfumo wa Serikali umebadilika na sura ya namna ya utawala imebadilika, dhana ya kukosa ama kupata, utamaduni wa kisiasa wa mshindi kujitwalia kila kitu haujabadilika. Ninaamini kwamba ili nchi ya Zanzibar na uchumi wake viweze kustawi, na ili Zanzibar iweze kuzitumia raslimali zake kiukamilifu, utamaduni huu inabidi ubadilike kwa kuwepo maafikiano, heshima kwa kila upande na kugawana madaraka.” Soma hotuba ya Balozi wa Marekani anayemaliza muda wake nchini Tanzania, Mark Green, katika kuwaaga Wazanzibari, aliyoitoa Januari 8, 2009, mjini Zanzibar.
ZEC INASHIRIKIANA NA CCM KUPANDIKIZA WAPIGA KURA PEMBA

Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF. Picha kwa hisani ya Global Publishers.
“Ni bahati mbaya kwamba nchi nyingi za Afrika zimetumbukia katika majanga na hata mauaji kutokana na Tume za Uchaguzi kutokuwa makini katika usimamizi na uendeshaji wa chaguzi na kukubali kutumiwa na Serikali zilizoko madarakani au kukosa udhibiti wa Sekretarieti na maofisa wake wa ngazi za chini. Tume ya Uchaguzi ya Kenya na ile ya Zimbabwe ni mifano hai ya hali kama hizo na matokeo ya kuvurunda kwake sote tumeyashuhudia. Hatutaki Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ifuate mkondo kama ule wa Kenya na Mwenyekiti Mwinchande awe Samuel Kivuitu wa Zanzibar. Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ina nafasi ya kujirekebisha ili ijenge imani ya vyama vya siasa na Wazanzibari kwa jumla. Wito wetu kwao ni kuchukua hatua za haraka za kurekebisha makosa haya niliyoyataja na mengine.” Soma tamko la CUF kuhusiana na njama za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Vyombo vya Dola kuharibu uchaguzi wa 2010.
ZEC INAFANYA KAZI KWA MAAGIZO YA VYOMBO VYA DOLA
“Kampuni iliyoteuliwa kufanya kazi na Tume katika uboreshaji wa Daftari kwa kile kinachoitwa ubadilishaji wa shahada za wapiga kura kutoka mfumo wa ‘analogue’ kuja ‘digital’ ni kampuni iitwayo ‘On Track Innovations (OTI)’ kutoka Israel. Kampuni hii ndiyo pia iliyopewa kazi ya kutayarisha na kutoa vitambulisho vya Mzanzibari bila ya kufuata taratibu za Serikali za utoaji zabuni. Walioileta ndiyo wanaoijua na ni kwa ‘maelewano’ gani ililetwa hapa Zanzibar. Mkurugenzi wa Idara ya Uandikishaji na Utoaji Vitambulisho vya Mzanzibari, Bwana Mohamed Juma Ame, anafahamika kuwa ni afisa wa ngazi ya juu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Hivi Sekretarieti ya Tume ya Uchaguzi inaposhikilia kampuni hii ya ‘On Track Innovations (OTI)’ kutoka Israel ambayo iliingizwa kinyemela hapa Zanzibar katika utayarishaji na utoaji wa vitambulisho vya Mzanzibari kuwa ndiyo pia ipewe jukumu la uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura ina maslahi gani? Inapokuwa mkuu wa shughuli za kampuni hii katika utoaji wa vitambulisho vya Mzanzibari ni afisa wa ngazi ya juu wa Idara ya Usalama wa Taifa, tutaweza kukwepa ukweli kuwa kuna kiungo kikubwa kati ya Sekretarieti ya Tume na Maafisa wa Usalama wa Taifa? CUF hivi sasa inafuatilia kupata ukweli kamili kuhusu taarifa kwamba kampuni hii ya ‘On Track Innovations (OTI)’ ilihusika na uvurugaji wa Daftari la Wapiga Kura wa Guinea wakati wa utawala wa Rais Lansana Conte.” Soma uthibitisho wa CUF kwamba Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) inashirikiana na Vyombo vya Dola kuhakikisha ushindi wa CCM Zanzibar
SERIKALI YA MSETO SULUHU PEKEE ZANZIBAR’

Balozi Mark Green
“Hakuna kiongozi atakayeweza kuendesha kila kitu anavyotaka yeye milele. Hakuna chama kinachoshinda madaraka kwa asilimia 100. Hakuna chama kilicho nje kabisa ya mfumo wa madaraka. Mpinzani wa leo anaweza kuwa rafiki wa kesho. Haipaswi kundi moja la kisiasa lijisikie limetengwa na Serikali.” Soma habari hii…
HAMAD ATHIBITISHA ZEC YAPEWA MAELEKEZO
“Mkurugenzi wa Idara ya Uandikishaji na utoaji vitambulisho vya Mzanzibari, Mohammed Juma Ame, anafahamika kuwa ni afisa wa ngazi ya juu wa Usalama wa Taifa.” Soma habari hii…
MREMA ATAKA CUF KIUNGWE MKONO UCHAGUZI WA MBEYA

Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema (kushoto) na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad
“CCM ikishinda uchaguzi huo, aibu itakuwa kwetu wapinzani wote… nawaomba sana wapinzani wenzangu, wenye nia ya dhati ya kuiondoa CCM madarakani, waunganishe nguvu na kuwaunga mkono wenzetu wa CUF katika uchaguzi wa Mbeya Vijijini.” Soma habari hii…
BENDERA ZA CCM ZASHUSHWA Z’BAR
Wakaazi wa kijiji cha Uroa wameshuhudiwa wakiteremsha bendera za CCM zilizokuwa zimetundikwa katika makazi yao na sehemu nyingine na kupandisha bendera za Chama cha Wananchi (CUF) kwa madai kwamba wamevunjwa moyo na viongozi wao kwa kushindwa kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo. Soma habari hii…
CUF WALALAMIKA KUSUSIWA KAMPENI MBEYA VIJIJINI

Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Wilfred Lwakatare
“Hii ni aibu, nchi imefikia hatua mbaya kabisa, hakuna maadili ya habari sasa, leo wandishi wanagoma kwa makusudi kuripoti taarifa za uchaguzi wa chama chetu kwa umma bila sababu yoyote.” Soma habari hii…

Chama cha Mapinduzi, CCM
“Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema baadhi ya makamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na watendaji wameanza kupotosha sheria ya uchaguzi kwa maslahi yao.” Endelea kusoma habari hii…
“Rais hayuko juu ya sheria na kinga yake ni sheria, hivyo naye achunguzwe endapo itabainika kama alihusika kwenye rushwa katika ununuzi wa rada ambao umeliingizia taifa hasara ya sh bilioni 40, basi hana budi kushtakiwa.” Endelea kusoma habari hii… KHATIMA YA ZANZIBAR NA MUSTAKBALI WA MUUNGANO

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akitoa mada juu ya Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano
“Wazanzibari wanafahamu kwamba Serikali ya Tanganyika imefutwa kwa makusudi na Bunge la Tanganyika kinyume na Makubaliano ya Muungano ili kujipa nafasi kuitumia Serikali ya Muungano, kama kwamba ndio Serikali ya Tanganyika. Lengo ni hatimaye kuiuwa Serikali ya Zanzibar na kufanya Tanganyika mpya ikiwa na jina jipya la Tanzania lenye mipaka mipya, yaani kuwa nchi moja yenye Serikali Moja. Hiyo ndio ghilba iliyofanywa na viongozi wa Tanganyika mara baada ya kuwekwa saini makubaliano. Kwa kusaidia kufichuwa ukweli wa hadaa hii, msomaji anashauriwa asome Sheria Na. 22 ya mwaka 1964 inayoitwa “Union of Tanganyika and Zanzibar Act, 1964.”- Maalim Seif Sharif Hamad, Disemba 4, 2008, Zanzibar
Angalia picha za Kongamano hilo
“Chama makini kinatakiwa kuwa na viongozi makini wanaoweza kuleta maendeleo, lakini kama Makamba ataendelea kuwa Katibu Mkuu, ni usanii mtupu viongozi badala ya kuangalia shughuli za maendeleo watakuwa wanalumbana wao kwa wao.” Soma makala hii…
LIPUMBA ATAKA MKAPA NAYE APANDISHWE KIZIMBANI
“Mkapa naye awekwe ndani, alikuwepo wakati wa mchakato…yeye ndiye alikuwa Rais, bila kuwekwa ndani, hakutakuwa na haki iliyotendeka…wahusika wote pia wa EPA wawekwe ndani kuanzia mdogo hadi mkubwa.” Soma habari hii…
MNYAA AISHANGAA SERIKALI KUHUSU RICHMOND
“Mimi kama mmoja wa wajumbe wa kamati ya Richmond, siridhiki na jinsi serikali inavyoshughulikia maagizo ya Bunge kuhusu Richmond kwa sababu baadhi ya vipengele muhimu havijatekelezwa. Bunge lilipendekeza utekelezaji wa suala hilo ufanyike ndani ya miezi mitatu kuanzia Februari mwaka huu, lakini serikali ilianza kuzungumzia utekelezaji Agosti na imeanza utekelezaji kwa kuchagua vipengele rahisi na kuacha vipengele vigumu ambavyo ndivyo msingi wa matatizo.” Soma habari hii…
CUF YAZOA WAPIGA KURA 700 WA KARAMAGI
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi amepata pigo kwenye jimboni lake la Bukoba Vijijini, baada ya wapigakura wake 700 kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF). Wapiga kura hao walifikia uamuzi huo baada ya wabunge wa CUF, Habib Mnyaa (Mkanyageni), Shoka Khamis Juma (Micheweni) na Severina Mwijage (viti Maalum) wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CUF Seif Hamad kumchambua Karamagi katika mkutano wa hadhara kwa kumhusisha na kashfa ya kampuni ya Richmond. Soma habari hii…
“HAKUNA SABABU CCM IENDELEE KUTAWALA”

Prof. Ibrahim Lipumba (kulia) akiongoea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza Kuu la CUF, Oktoba 30, 2008, Buguruni - Dar es Salaam
OKTOBA 29 hadi 30 mwaka huu Chama Cha Wananchi (CUF) kilikuwa na kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, chini ya Mwenyekiti wake Prof. Ibrahim Lipumba,kwenye makao makuu ya chama hicho Bugurudi jijini Dar es Salaam. Kupitia kikao hicho wajumbe walijadili pamoja na mambo mengine, kile walichokiita mikakati mizito ya kuhakikisha Rais Jakaya Kikwete pamoja na Serikali yake, haendelei na kipindi cha pili cha uongozi mara baada ya kumaliza kipindi cha kwanza mwaka 2010. Endelea kusoma makala hii…
“…Zanzibar ipo katika hali mbaya, hakuna dawa katika vituo vya afya zaidi ya Panadol. Zanzibar inahitaji mabadiliko ya kiutawala, ili kuleta fikra mpya ya kupunguza umaskini ulioota mizizi kwa wananchi wake hususan wa vjijini. Na wala msivunjike moyo na vitendo tulivyofanyiwa tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi kwa sababu ipo siku lengo la kuleta mabadiliko litafanikiwa. One day yes!” Maalim Seif Sharif Hamad. Soma habari hii…
CUF YAANZA KUZIBOMOA NGOME ZA CCM Z’BAR
Baada ya mialiko ya Chaani na Kizimkazi Mkunguni, sasa wazee wa Donge na Uzini nao wamemualika Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akawahutubie kuhusu hadhi ya Zanzibar kwenye Muungano na awaeleze muelekeo wa chama chake katika kujenga maisha ya vijana wao. Huu umekuwa mtiririko wa matukio ya kihistoria katika siasa za hapa, ambapo haikutarajiwa kwa wazee kutoka sehemu zilizoaminiwa kuwa ngome madhubuti za CCM, kukikunjulia mikono chama cha CUF. Soma habari hii…
TUKITAKA TUNAWEZA KUIONDOA CCM
Chama Cha Wananchi (CUF) kimewataka wananchi kubadilika na kuachana na kasumba za kuwa mabadiliko ya kweli hayawezi kufanyika Zanzibar kutokana na kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chenye mamlaka ya kuendelea kushika madakara milele. Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Kizimkazi Mikunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Machano Khamis Ali, alisema ni wakati wa wananchi kukubali mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa umefika. Soma habari hii…
MAALIM SEIF ACHUKUA FOMU YA UKATIBU MKUU
“Hii ni haki yangu ya msingi. Mimi bado uwezo wangu wa kuwaongoza wananchi ninao na uwezo wa kusaidiana na wenzangu wa kukiimarisha chama chetu ninao, akili zangu bado ni nzuri sana kwa kukitumikia chama changu na nchi yangu.” Soma habari kamili…
CUF YALAANI WAZEE WA EAC KUPIGWA, KUSHTAKIWA
”Tunalaani vikali hatua ya serikali kuwamwagia maji ya kuwasha, kuwapiga, kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wazee wetu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki…Mafao ni haki yao kwa kuwa waliitumikia sana nchi hii na wamevumilia vya kutosha… kwa nini wapigwe na kufunguliwa mashtaka wakati wezi wa EPA wanadunda barabarani?” Endelea kusoma habari hii…

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, akisoma maazimio ya Baraza Kuu kwa waandishi wa habari, Buguruni tarehe 31 Oktoba, 2008
“…CUF kikiwa ni chama cha siasa makini hapa nchini kinachojali na kuheshimu misingi ya umoja, amani, utulivu, haki, uadilifu, maendeleo na ustawi wa nchi yetu na watu wake kimejipanga vyema kuwaongoza Watanzania katika kuleta mabadiliko ya uongozi wa Serikali ifikapo mwaka 2010 yatakayowapatia Watanzania uongozi na utumishi wa dhati utakaoheshimu utu wao na kulinda maslahi yao chini ya misingi ya haki sawa kwa wote na uchumi imara unaotoa neema na ajira kwa wananchi wote. CUF inasema TANZANIA BILA YA CCM INAWEZEKANA.” Endelea kusoma Maazimio ya Kikao Cha Baraza Kuu La Uongozi La Taifa Kilichofanyika Ofisi Kuu, Buguruni, Mjini Dar Es Salaam Tarehe 29 – 30 Oktoba, 2008

Rais Jakaya Kikwete. CUF inamhakikishia kuondoka madarakani 2010 kwa kuwa ameshindwa kabisa kuwa kiongozi
LIPUMBA AMVAA KIKWETE, MWANYIKA
“Utendaji duni wa Serikali ndiyo chanzo cha matatizo yote haya, hivyo hakuna haja ya kuhukumu magazeti, yenyewe ni lazima yaandike kila wanachoona.” Endelea kusoma habari hii…
“Wastaafu walishaahidiwa pesa zao kwanini kila siku maandamano, pigo la jana linapaswa kuwa fundisho kwa taifa hili na jumuiya za kimataifa zichukue hatua sasa. Walimu nao waliahidiwa kulipwa kwa kipindi kirefu na serikali ilishakiri kudaiwa na walimu inapaswa kuwalipa…” Endelea kusoma habari hii…
EPA: LIPUMBA, WARIOBA WAIJIA JUU SERIKALI
“Nchi hii inaongozwa kwa misingi na taratibu za kisheria ambazo kwa mujibu wa katiba, hakuna mtu aliye juu yake…Kwa mujibu wa sheria, wizi ni kosa la jinai na kurudisha mali iliyoibwa si mwisho wa adhabu ya kosa hilo, bali sheria inaelekeza kuwa mtuhumiwa wa kosa la jinai lazima afikishwe mahakamani…Nashangaa kusikia kwamba (mkurugenzi wa mashtaka) DPP anasubiri maagizo ya mwisho kutoka kwa rais ili kuona atawafanye watuhumiwa wa EPA. Nashangaa kwa sababu si rais anayeelekeza nani afikishwe mahakamani kwa kosa gani. Sheria zipo na hii ni kazi ya polisi, Takukuru na mwendesha mashataka.” Endelea kusoma habari hii…
LIPUMBA AMUHUSISHA KIKWETE NA UFISADI WA IPTL
“Ndugu zanguni wana-Mwanza kuzorota kwa utendaji wa kazi wa shirika la kuzalisha umeme nchini (TANESCO), kumetokana na mkataba mbovu wa kampuni ya IPTL iliyoruhusiwa kufanya kazi na Rais Kikwete wakati huo akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Rais Kikwete amehusika pakubwa sana katika kuliingiza taifa kwenye hasara na mikataba mibovu kama huu…lazima alaumiwe! Hivi sasa Tanesco ipo hoi haijiwezi kumudu uendeshaji wake wa kazi sababu ya Kikwete huyu!” – Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF.
BILA YA IDHINI YA ZANZIBAR, MAFUTA HAYACHIMBIKI
“Makampuni hayo yameleta ujumbe kwangu kwamba wao hawana shaka kuwa serikali itakubali suala la uchimbaji mafuta na gesi, lakini khofu yao ni Upinzani. Mimi nikawaeleza kupitia kwa mjumbe wao kuwa, ikiwa watachimba chini ya Serikali ya Muungano hatukubali na iwapo watachimba kwa kibali cha SMZ tutawaunga mkono.” – Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF.
CUF ina kurugenzi maalum ya Haki za Binaadamu na Mahusiano ya Umma na pia ina sera maalum kuhusu watu wenye ulemavu, maalbino wakiwa miongoni mwao. Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi hiyo, Mbaralah Maharagande, ambaye aliongozana na Prof. Lipumba katika maandamano hayo, amesema kwamba ni jukumu la kuwalinda na kuwatetea maalbino maana wao ni sehemu ya raia wa nchi hii. Soma habari kamili hapa…
TUIKOMBE TANZANIA KUTOKA UFISADI WA CCM
“Pamoja na Serikali ya Uingereza kuileza Serikali ya Tanzania, lakini pia walileta makachero wao kumuhoji hapa hapa nchini, naye Vithlan alikiri kupokea fedha hizo. Pamoja na kuwepo kwa ushahidi na kuwepo kwa maafisa wa serikali, lakini badala ya kumkamata Vithlan na kumuweka ndani, wao wakamwachia mpaka ameondoka. Cha kusikitisha kuwa baada ya kuondoka Vithlan, ndipo TAKUKURU eti inajikakamua inapeleka mafaili mahakamani, tena bila haya inatangaza kwa waandishi wahabari ili wawe na taarifa kwamba sasa wanapeleka Mahakamani kesi nzito ya rushwa iliyokamilika na kumshitaki Salileth Vithlan ambaye hayupo na wanachukua hatua kumtangazia duniani kote, akamwate arudishwa kujibu kesi. Huu ni usanii, kwani mtu alikuwepo hapa hapa nchini mpaka anahojiwa na chombo cha nje, kwa nini wasimkamate akaeleza fedha hizo amekula nani? Halafu tena Rais Jakaya Kikwete bila haya katika mafanikio aliyoyataja Bungeni mojawapo ni kuwa wamempeleka Vithlan mahakamani.” Hotuba ya Prof. Ibrahim Lipumba kwa waandamanaji wa Dar es Salaam waliomshinikiza Rais Jakaya Kikwete kuwataja na kuwapeleka mahakamani mafisadi, Oktoba 9, 2008
CUF TAYARI KUKUTANA LAKINI SI KWA USANII
CUF imesema kipo tayari kukutana na wenzao wa CCM ili kumalizia hatua iliyobaki ya kupata muafaka wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar lakini si kurudishwa nyuma kujadili mambo ambayo tayari yashajadiliwa…”CUF inaungwa mkono na Wazanzibar na Watanzania walio wengi ambao wanataka kuona suala la mgogoro wa Zanzibar linapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Kutokana na hali hiyo CUF ipo tayari kukutana na CCM hata kesho ili mradi kumalizia hatua iliyobaki ya kupata muafaka.” Soma habari kamili…
MAALIM SEIF KUZUNGUMZIA MAMBO MUHIMU Z’BAR
Jumapili ya kesho, 19 Oktoba, 2008, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad atazungumza na Wazanzibari, Watanzania na walimwengu kwa jumla kuhusu mambo muhimu yanayohusu muelekeo wa siasa na uchumi wa Zanzibar katika kipindi hiki ambapo kuna kila dalili za kubadilika kwa hali ya siasa na uchumi wa nchi. Tafadhali usikose kuhudhuria mkutano huo wa aina yake. Soma taarifa kamili hapa.
IMF INACHOCHEA UFISADI – LIPUMBA
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, alilaumu Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa kuchochea ufisadi nchini Tanzania kutokana na kauli ya Mkurugenzi wa Shirika hilo, Dominique Strauss-Kahn, kama ilivyonukuliwa na gazeti la serikali la Daily News. Soma habari kamili.
POLISI WASHINDWA KUIZUIA CUF ISIANDAMANE
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limeruhusu maandamano yaliyopangwa na Chama cha Wananchi (CUF) kufanyika kesho jijini Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliliambia gazeti hili jana kuwa polisi haina sababu ya kuwazuia CUF kuandamana, kwa kuwa ni haki yao. Endelea kusoma habari hii.
LWAKATARE AMKATIA RUFAA KAGASHEKI
ALIYEKUWA mgombea ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare (CUF), amekata rufaa Mahakama ya Rufani Tanzania-Mwanza, kupinga hukumu ya Mahakama Kuu ya Kanda ya Bukoba iliyomtangaza Balozi Khamis Kagasheki (CCM) kuwa mbunge halali wa jimbo hilo. Endelea kusoma habari hii.
CUF YAWAKINGIA KIFUA WANA-CCM WANAOTETEA UZANZIBARI
“Ninyi viongozi wa CUF nawaambieni kwamba hakuna kuwakejeli wana CCM wanaotetea masilahi ya Zanzibar ambayo ni yetu sote. Wenzetu walikuwa hawajafahamu lakini sasa alhamdulilah wamefahamu kabisa.” Endelea kusoma habari hii
CUF YASISITIZA SERIKALI YA PAMOJA Z’BAR
“Ni kweli Zanzibar inahitaji umoja na mshikamano na ili kuondosha tofauti zilizopo na kusahau yaliopita ipo haja kubwa ya kufanya kazi pamoja kati yetu kwa lengo la kuondosha ile dhana na kuwa mmoja anaweza kulipiza kisasi. Lakini pia tutakapofanya kazi pamoja, tunajenga mazingira mazuri ya kuaminiana hasa katika kipindi hiki kinachokuja cha matayarisho ya uchaguzi mkuu wa 2010.” Endelea kusoma habari hii
KIKWETE MJENGA NJE MBOMOA NYUMBANI
“NINA rais anayetajwa kwa umaarufu wake hadi Marekani ambako ameshafanya ziara mara sita – wastani wa safari moja kwa kila baada ya miezi mitatu – tangu Desemba 2005 alipoingia ikulu na kula, kunywa na kuteta na George W. Bush, kiongozi wa taifa hilo tajiri zaidi duniani.” Endelea kusoma makala hii.
“CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepata pigo baada ya wagombea wake wawili waliokuwa wakiwania udiwani katika Kata ya Ngamiani Kati na Chongoleani, wilayani hapa kubwagwa kwenye uchaguzi mdogo. Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi, Chama cha Wananchi (CUF) kilipata ushindi kwa wagombea wake kuongoza katika kata zote mbili.” Endelea kusoma habari hii.
ASKARI KUANIKA SIRI YA USHINDI WA CCM Z’BAR
“Hapa kinachoonekana hawathamini mchango wetu, tumetumika sana kwenye uchaguzi na tunajua mambo mengi, hiki ni choyo cha watendaji wa Wizara ya Fedha.” Endelea kusoma habari hii.
CUF YAWEKA MASHART KURUDI KWENYE MAZUNGUMZO NA CCM
“Nani alisema hayo? Sisi hatujapata taarifa ya mdomo wala maandishi. Lakini hata kama tungepata, msimamo wa CUF sasa ni kwamba, mazungumzo hayo yamemalizika kwenye ngazi ya kamati na sasa yanatakiwa kufanywa na viongozi wakuu wa vyama hivyo yaani, Maalim Seif na Karume kwa upande wa Zanzibar au Jakaya Kikwete na Profesa Lipumba.” Endelea kusoma habari hii
HATA KAMA NI KINIBU, NI MAFUTA YETU
“Hata kama watajipaka mwilini au wengine watatumia kama dawa ya kuchulia misuli, itakuwa bora zaidi kuliko suala la mafuta kuwa la Muungano.” Endelea kusoma habari hii
POLISI ACHENI UCHOCHEZI KISIASA
“Vitisho dhidi ya raia Zanzibar huanza hivyo. Hutokea tukio na kada wa CCM akatoa kauli ambayo vyombo vya ulinzi na usalama huichukua ni amri. Inapokuwa wahusika ni wafuasi wa upinzani, inajengwa kesi. Hizi zote ni fitna. Lengo lake ni kukengeuka tatizo la msingi linaloikabili nchi, Muafaka, ili kulaghai wananchi kwa kupakaza ubaya wanaopigania haki zao.” Endelea kusoma makala hii
“Kusema kwamba CCM kukubali kukaa mezani na CUF ni fadhila tu kwa chama cha upinzani na kwamba Rais Kikwete hana uwezo wa kumaliza mgogoro huo bila ya kushirikisha vikao vya chama chake, ni dharau kwake na kubeza kile anachokisimamia. Rais anayo mamlaka tena makubwa, hasa ukizingatia kwamba alipotoa ahadi ile aliitoa kama kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baadaye amekuja kuvikwa na uenyekiti wa taifa wa chama chake. Hayo ni mamlaka.” Endelea kusoma tahriri hii ya MwanaHALISI.
SIASA-MZAHA ZINAZIDISHA TU MGOGORO ZANZIBAR
“Iwapo CCM imekubali “kimsingi” makubaliano iliyofikia na CUF, kura ya maoni inasaidia vipi kuendeleza utaratibu wa kuyatekeleza? Kenya palikuwa na kambi inayotaka katiba mpya na nyingine inayoikataa kwa kuona haikidhi matarajio ya Wakenya. Hapa Kura ya Maoni ilikuwa muhimu. CCM imeridhia makubaliano yaliyofikiwa kutokana na mazungumzo yaliyoanzishwa na kiongozi wao mkuu ambaye ndiye Rais wa Watanzania. Sasa hoja ya Kura ya Maoni ambayo haikupata kujadiliwa pamoja na wenzao imetoka wapi?” Endelea kusoma makala hii.
UTATA WA MUUNGANO, BOMU KILO 1,000
“ANDAA swali hili: Taja orodha ya mambo ya Muungano. Irudufu karatasi ili upate nakala nyingi na ugawie wabunge pale mjini Dodoma. Nyingine wapatie wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, mjini Zanzibar. Waambie majibu yao utayakusanya kesho yake ofisini kwa maspika. Haki ya Mungu, majibu utakayopata yatakushtua.” Endelea kusoma makala hii.
“Mpasuko wa kisiasa Zanzibar ulilipuka baada ya kufanyika Uchaguzi Mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, ambapo mgombea wa urais wa CCM, Dk. Salmin Amour alishinda kwa asilimia 50.2 dhidi ya Hamad aliyegombea kwa tiketi ya CUF na kupata asilimia 49.8. Matokeo hayo yalikataliwa na CUF kwa madai kuwa kura za mgombea wao ziliibwa na CCM na hivyo kusababisha mpasuko mkubwa wa kisiasa.” Endelea kusoma habari hii.
MANIFESTO YA UCHAGUZI MKUU WA ZANZIBAR 2005
“Mfumo wetu wa kisiasa unahitaji upepo mpya wa mabadiliko wenye nguvu ya kuisafisha jamii yetu na kuleta mawazo na fikra mpya, kuleta viongozi na watu walioungana na wenye dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko ya maana, na ambao wanathamini utu na heshima ya binaadamu,wanaofahamu maana hasa ya utumishi wa umma na uwajibikaji. Ni CUF pekee inayoweza kuyaleta haya.” Ni ipi Ajenda ya CUF kwa maendeleo ya Zanzibar?
FEDHA ZA EPA ZITUMIKE KULIPA NAULI YA WANAFUNZI
“Idadi ya wanafunzi wote wa shule za msingi na Sekondari kwa sasa ni takriban milioni 9 (darasa 1-VII ni 8,31,925 na Sekondari Form I-VI ni 765,672). Hesabu hizi zinajumuisha hata wale walioko katika mashule ya bweni. Tuchukulie kuwa robo tatu yao kuwa wako shule za kutwa ambao ni wanafunzi milioni 6. Waziri wa Fedha alikwishatamka kuwa fedha za EPA hazina mwenyewe na wahusika wamerudisha, basi nusu yake ambao ni shilingi bilioni 66.5 zitumike kama ruzuku ya mafuta, jambo ambalo litasababisha bei ya mafuta kutokupanda na hivyo kisingizio cha bei ya mafuta kupandisha nauli hakitokuwepo tena.” Taarifa maalum ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohammed (Mb), kuhusu maandamano ya wanafunzi wa Dar es Salaam dhidi ya kupandishwa kwa nauli ya daladala
“Hizi ni dalili za kuwa watawala wanatapatapa kutokana na wananchi walio wengi kukata tamaa na uongozi wa CCM ambayo imeshindwa kuwaondolea matatizo ya msingi Watanzania na jinsi inavyoyumba katika kukabiliana na rushwa iliyokithiri kiasi kwamba wananchi kila kukicha wanazidi kutokwa imani na uongozi wa CCM. Wanadhani ikiwa mimi nitasingiziwa kusema maneno nisiyoyasema, labda hiyo inaweza kuiokoa CCM, na labda watapata nafuu. Naona kwa hili Mzalendo imeshika kuti kavu.” Taarifa ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kwa vyombo vya habari kufuatia kuchapishwa habari za uzushi na gazeti linalomilikiwa na CCM la Mzalendo juu ya safari yake ya London, Uingereza, ya Mei, 2008
Wakati nchi ikitumbukia katika majanga makubwa ya kitaifa kama vile migomo ya wafanyakazi, migogoro ya wanafunzi, mfumko wa bei, nyufa katika Muungano, uchumi dhaifu, ufisadi mkubwa, mgawanyiko mkubwa na kushindwa kwa Rais Jakaya Kikwete kuutatua mpasuko wa Zanzibar, Chama cha Wananchi (CUF) kinaona kwamba kuna haja ya lazima sasa kuliziba ombwe hili la kiuongozi. Hii hapa ni hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Mhe. Prof. Ibrahim Lipumba, katika Kongamano Maalum la Kujadili Ukosefu wa Uongozi na Hatima ya Tanzania, Ukumbi Wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, tarehe 28 Agosti, 2008.
CUF MWENYEJI WA MKUTANO WA WALIBERALI AFRIKA
“Chama Cha Wananchi (CUF) kimepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Vyama vya Siasa vya Kiliberali Afrika (Africa Liberal Network-ALN) ambao unafanyika Golden Tulip Hotel, mjini Dar es Salaam.” Endelea kusoma taarifa hii.















Maoni