Taarifa ya Kamati ya Utendaji ya Taifa

31 12 2011

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba

“Kamati ya Utendaji ya Taifa imeridhika kwamba kuna hoja za msingi na ushahidi wa kutosha dhidi ya wanachama hao 14 unaoonesha kuhusika kwao na njama hizo.” Read the rest of this entry »





SUKZ yaenda mwendo wa mbwa-kachoka?

31 12 2011

Rais Ali Shein akikutana na serikali watendaji wa serikali yake. Je, watendaji hawa wanaifanya serikali iende mwendo wa mbwa-kachoka: hatua moja mbele, tisa nyuma?

Kwa kiasi kikubwa wengi tumekuwa na imani na kazi ambayo imekuwa ikifanywa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) katika kipindi chake cha mwaka mmoja na kidogo hivi. Kumekuwa na dalili kuwa kuna nia nzuri ya kuleta mabadiliko makubwa ya kisiasa, kijamii na hata ya kiuchumi na kwa hilo pamoja na kuwepo kwa amani na utulivu ndani ya Zanzibar iliyozoea vurugu, SUK imekuwa ikienda vizuri. Read the rest of this entry »





Muungano sasa uwe wa mkataba, sio wa Katiba

31 12 2011

Wazanzibari wakiwa katika mjadala wa wazi kuhusu mchakato wa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA)

KUNA sababu moja kuu inayowafanya Watanzania waukaribishe kwa msisimko mwaka mpya wa 2012. Nayo ni kwamba, mwakani ndipo suala la Katiba mpya ya nchi hiyo litapoanza hasa kutokota. Hatuhitaji wapiga ramli kutwambia kwamba mwaka ujao hilo ndilo litalokuwa suala kubwa la kisiasa nchini Tanzania. Read the rest of this entry »





Haki ya misaada ya mafuriko iwe kwa wote

30 12 2011

Na Julius Mtatiro

Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro

Jana (29 Disemba 2011) tumeimaliza siku nzima kwa kazi ya kuzungukia kambi za wahanga wa mafuriko Dar es Salaam. Nimeongoza ujumbe wa viongozi waandamizi wa chama taifa na wilaya na tumepita katika kambi mbilimbili katika kila wilaya ya Dar es salaam.

Zoezi hili limekuja baada ya kupita kwa mara ya kwanza mara baada ya mafuriko. Leo tulikuwa na kazi moja kubwa, KUTOA MISAADA KWA WAHANGA. Katika kila kambi tuliyopita tumewafariji wahanga na kutoa misaada ya UNGA, MCHELE,  SUKARI, MAFUTA YA KULA, DAGAA, SABUNI, MAJANI YA CHAI, NGUO, MAHARAGE, n.k. Read the rest of this entry »





Zanzibar iwe na Benki Kuu yake – Maalim Seif

28 12 2011

Maalim Seif Sharif Hamad

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema ni muhimu kwa sasa Zanzibar kuwa na benki kuu yake ikiwa inataka kutumia kikamilifu rasilimali zake kujenga uchumi wake. Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, akizungumza katika viwanja vya Kibandamaiti mjini hapa juzi alisema kuendelea kutegemea Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kunainyima Zanzibar kutekeleza mipango yake ya maendeleo kwa ufanisi. Read the rest of this entry »





Wazanzibari tuungane – Maalim Seif

27 12 2011

Maalim Seif Sharif Hamad

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema hana tatizo la wanaotetea serikali mbili lakini kuwepo na mfumo maalumu utakaokubalika na wananchi wote. Alisema wale wanaotetea mfumo wa Serikali mbili, kama ni hivyo yeye hana tatizo. Ila ziwepo Serikali mbili, moja ya Zanzibar na Katiba yake na mambo yake yote, na ya pili ya Tanganyika na Katiba yake na mambo yake yoye. “Halafu tutaamua yepi tunataka tushirikiane na kwa mfumo upi” alisisitiza Maalim Seif. Read the rest of this entry »








Follow

Get every new post delivered to your Inbox.