Watu 500 wanyimwa haki ya kupiga kura Micheweni

8 07 2009

Uandikishaji Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Wilaya ya Micheweni: Taarifa ya Awali – Siku ya Pili 8 Julai, 2009

“Watu 584 wanyimwa haki ya kuwa wapiga kura katika siku ya pili”

Zoezi la uandikishaji wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Zanzibar lililoanza juzi katika wilaya ya Micheweni unaendelea katika hali ya mashaka. Ushirikiano ambao sisi katika Chama cha Wananchi (CUF) tunauita ‘utatu usio mtakatifu’ (trinity of the demons) kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia masheha wake, Idara ya Vitambulisho na Tume ya Uchaguzi (ZEC) unaendeleza azma yake ya kuwanyima Wazanzibari haki yao ya kuwa wapiga kura.

Katika rikodi zilizokusanywa juzi, wapiga kura 830 walinyimwa haki hiyo katika vituo sita vya jimbo la Konde huku wakiandikishwa 133 tu katika vituo vyote hivyo. Rikodi za jana zinaonesha kwamba watu 584 wamenyimwa haki hiyo na walioandikishwa ni 224 tu. Kwa hivyo, kwa juzi na jana tu, watu walionyimwa haki ya kuwa wapiga kura katika jimbo la Konde peke yake ni 1,414. Siku hizi mbili zilikuwa ni za uandikishaji wapiga kura wapya. Sababu inayotumika kwa ZEC kuwanyima watu hao haki ya kuwa wapiga kura ni kutokuwa kwao na vitambulisho vya Uzanzibari, sharti ambalo limewekwa na ZEC kwa kusudi maalum la kuvuruga uchaguzi.

Sharti hili liko kinyume na Katiba ya Zanzibar na misingi ya demokrasia ambayo nchi hii inajaribu kuijenga. Wengi wa watu walionyimwa haki hiyo wanazo shahada nyingine zinazothibitisha uzawa na ukweli kwamba wameshafikia umri wa kuwa wapiga kura.

Tunatuma taarifa hii ikiwa ni indhari ya namna hali inavyoendelea na makisio ya hali inakoelekea. Tutakuwa tukituma taarifa kila siku hadi kumalizika kwa zoezi.

Imesambazwa na:

Kurugenzi ya Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF


Actions

Information

One response

9 07 2009
zahir

mimi ni mzanzibari halisi ninaelewa matatizo ya Zanzibar kwa upeo wangu wa ufahamu napenda kutahadharisha kwa chama changu cuf kuwa ccm na serikali zake hazikubali wala hawatokubali maisha nchi hii kuwa huru kivyake yaani To be Independent Nation Recognise by the U.N as Country watafanya kila njama hila zote mpaka kuuwa wako tayari bila ya woga wowote hivyo basi shughuli za uandikishaji Pemba inaonyesha wazi kabisa kwamba hakuna uchaguzi huru na haki mawazo yangu kwa Kiongozi wangu wa chama chetu naomba haraka kuwepo na MBADALA wowote unaofaa kisheria ili zoezi hili lisitishwe mara moja kurekebisha hali hii ikiwezekana hata kutishia kwa namna inayofaa kama haitoharibu demokrasia Labda nchi wafadhili kuja na kuwashinikiza ccm kuzuia uandikishaji haraka la si hivyo cuf tujiandae kuuliwa nasi tubaki kushukuru,,,, haya ni mawazo yangu binafsi kama yanafaa chukua kama hayafai its okay im glad that i live in democrative years…

Leave a comment