SURA YA SABA
MAUAJI YA JANUARI 26 NA 27, 2001
Mwanzoni tuligusia historia ili tuone kama ina sababu tosha ya kusababisha mauaji katika siasa za leo kama inavyodaiwa na baadhi ya wachunguzi wa mambo ya kisiasa na wanasiasa wa hapa kwetu. Tumeona kwamba hili halina ukweli wowote. Kwa kuwa sababu hii haina ukweli, basi maelezo yaliyofuata tukataja kisa na sababu hasa za mauaji yale. Baada ya hapa tukaendelea na chaguzi za mfumo wa sasa tunaelezea namna mauaji yalivyotokea. Tunaona kwamba ingawa mauaji haya yalifanyika Tanzania nzima, lakin yalifanyika kwa kiwango kikubwa Zanzibar na ambako Pemba yalitia for a. si hayo tu, kwa kuwa mauaji yalianza kutokea tarehe 26 Januari 2001 siku ambayo chama chetu hakikuwa na maandamano, na kwa kuwa zaidi yalitokea msikitini, basi bado inatia wasiwasi iwapo mauaji yaliyoendeshwa na Serikali ya Tanzania yalikuwa na sababu za kisiasa. Sasa endelea kusoma upate maelezo zaidi.
Sehemu ya 1: kwa nini Tuliamua kuandamana?
Mauaji yalitokea Tanzania nzima, hasa Zanzibar na zaidi Pemba. Hapana shaka pamoja na kwamba mapungufu mengi yamekuwa yakichangia kuchafuka kwa mazingira ya kisiasa Zanzibar, lakini tokea kuja kwa mfumo wa vyama vingi, chaguzi zimekuja kuivisha matatizo na kuanzisha migogoro na machafuko. Ingawa kuvurugwa kwa uchaguzi wapili wa vyama vingi ndiko kulikoleta malalamiiko yaliyojibiwa na dola kwa umwagaji damu, lakini huku pia kulikuwa mwanzo wa ishara za kutokubalika kuchezewa demokrasia kwa siku za baadae ndani ya mfumo wa vyama vingi.
Tuliona kwamba uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995 ulivurugwa na sisi tukasusia kumtambua Rais wa Zanzibar aliepewa madaraka na Tume ya Uchaguzi iliyoundwa na Rais mwenyewe kutokana na wajumbe wa chama chake. Vile vile, tulichukuwa hatua ya kutochangia miswada katika Baraza la Wawakilishi. Huu ulikuwa ni uamuzi wa chama chetu uliokusudiwa kuinesha Tanzania na dunia jinsi ya kuchukizwa kwetu na kuvurugwa kwa maksudi misingi na maana halisi ya demokrasia ya mfumo mpya wa vyama pamoja na kupinga ukiukwaji wa hakiza binaadamu uliokithiri katika uendeshaji wa uchaguzi na vile vile wakati wa kushangilia matokeo yaliyopora ushindi wa chama chetu.
Tulitembea kote Tanzania na mwishowe katika pembe za ulimwengu kutafuta namna ya kuboresha hali ya kisiasa iliyoanza kuvurugika baada ya kuapishwa asiekuwa mshindi. Juhudi hii ilikuwa ni ishara ya wazi ya uungwana wetu wa kuwa tayari kuvumilia kadhia yote, pamoja na kwamba ndio tulioonewa. Tuliomba angalau tukae na wenzetu ili tujenge misingi mipya ya maelewano na umoja wa nchi yetu. Pamoja na hili, tilikuwa pia na hoja ya kuangaliwa kwa undani sababu zilizochangia uvurugwaji wa uchaguzi ule, ili kupata fursa ya kuandaa taratibu bora zaidi kwa chaguzi zitakazofuata.
Juhudi za chama chetu kufikia lengo la makubaliano zilikabiliwa na upinzani mkali ndani ya CCM pamoja na Serikali zake mbili za Zanzibar na Jamuhuri ya Muungano. Hii ndio maana ilituchukua karibu miaka minne toke tulipoanza kuwaomba wenzetu tukae tuzungumze, licha ya kwamba hatukuchelea hata kuwaomba wengine watukutanishe ili tuitafakari hali ya kisiasa ya Zanzibar iliyoanza kuchafuka kwa kasi. Tulipohisi katika jitihada zetu hakuba uwezekano wa kufikana tulitegemea sana Muungano wetu utuunganishe. Tuliamua tuijaribu ile falsafa inayoenezwa na Serikali kwamba kwa vile Muungano wetu ni wa watu wote kwa faida ya wote, basi suluhisho ya matatizo yetu yamo ndani ya Muungano wenyewe. Hata hivyo, dhana hii haikutoa jibu la “ndio” kwa mara moja.
Ilikuwa ni mwezi wa Juni 1999 ndipo CCM hatimae ilikubali kukaa, japo “shingo begani”. Safari yetu ya kusihi ilianzia mwezi wa Novemba, 1995, mara tu baada ya uchaguzi wa Oktoba 26, 1996. hata hivyo, ilikuwa ni sahihi tuliposema CCM walikubali shingo begani, kwani mazungumzo yetu hayakutoa cha maana baada ya wao kukataa kutekeleza kila kipengele kilichowahusu cha muafaka wetu wa Juni 9, 1999. haikuwa dhihaka ila kulikuwa na ukweli kwamba hata neno Muafaka walilikataa na wakasisitiza liitwe “Makubaliano”. Hata hivyo pia walikataa kukubaliana.
Baada ya hapo tuliona, kilichobakia ni kukaa na kuangalia nini kingetokea katika uchaguzi wa pili wa vyama vingi uliotukabili siku chache tu baada ya makubaliano yaliyovia. Huu ulikuwa ni Uchaguzi wa pIli wa vyama vingi uliotarajiwa tareh 29, Oktoba 2000. Ingawa kilichotokea tumeshakielezea lakini matokeo ya mwisho yalikuwa, kuzidi kuvurugwa kwa uchaguzi huo kulikoambatana na uvunjwaji mkubwa zaidi wa haki za binaadamu na udhalilishaji wa daraja ya juu. Tulilazimika kama chama chenye malengo na sera zinazokubaliwa na watu ambao ubinaadamu wao haupitani na ule wa CCM, kujitutumua zaidi na kuweka madai yetu ya kuvurugwa demokrasia bayana pamoja na kupinga udhalilishajji kwa sauti kubwa zaidi lakini kwa amani tupu.
Hili halikuwa onesho bali ni jaribio la lazima kwani wakati mwengne, licha ya kwamba jitihada zetu za kidiplomasia zilidharauliwa kwa nje, lakini pia kwa ndani zilisutwa kwa kila aina ya kebehi. Kwa mfano, Maliyamkono (2000) anamnukuu aliekuwa Naibu Waziri Kiongozi Mapuri (1996), na wote wanakubaliana kwamba misururu ya safari za Maalim Serif Sharif nje ya nchi baada ya uchaguzi wa 1995, zilikuwa na lengo la kukutana na aliekuwa kiongozi wa Hizbu Ali Muhsin kwa upande wa Ghuba na vivyo hivyo kwa Uingereza, alikuwa akienda ili kukutana na Mfalme Jemshid aliepinduliwa mwaka 1964. kitabu cha Mapuri kinafundishiwa somo la Historia katika maskuli ya Zanzibar baaa ya somo hilo kufutwa kwa zaidi ya miongo miwili kwa kuonekana kwamba vitabu vya historia vilivyokuwepo havikidhi haja ya kuipotoa historia.
Kwa hivyo basi kujitutumua kulikoamuliwa na chama ni kufanya maandamano na kuwahutubia wananchi juu ya madai yetu ya kutokukubaliana na matokeo ya uchaguzi wa pili, kupinga vitendo vya ukiukwaji wa haki za binaadamu pamoja na kutaka uchaguzi uliochafuliwa urejewe. Si zaidi ya hapo na haya yanathibitishwa na kumbukumbu za azimio la Baraza Kuu la Uongozi la Chama kama lilivyotolewa katika kikao chake cha Novemba 9, 2000 na kutiwa saini na Mwenyekiti wa Chama Profesa Ibrahim Lipumba. Azimio hilo pamoja na mambo mengine, kuhusiana na uchaguzi wa Oktoba 29,2000 lilitamka kwamba:
? CUF inadai kufanyika kwa uchaguzi mpya haraka:
? Tunatamka kwamba Tume ya Uchaguzi (ZEC) iliopo sasa hivi iwajibike na Tume mpya yenye ridhaa ya vyama vyote iundwe;
? Kwa kipindi chote kabla ya uchaguzi mpya, CUF haitamtambua Amani Abeid Karume kama Rais halali wa Zanzibar pamoja na Serikali yake.
? Wawakilishi waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na Wabunge waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) hawatashiriki kula kiapo cha utiifu maana uchaguzi huo sio halali na ulivurugwa kwa Zanzibar.
Kifungu cha 167 cha Taarifa ya Uchunguzi wa mauaji ya Tume ya Mbita kinaeleza kwamba, Tamko letu lilikuwa ndio msingi wa Chama cha CUF kuitisha maandamano ya tarehe 26 na 27 Januari, 2001. huu ni uongo dhahiri, na baya zaidi ni kwamba uongo huu kwa vile umejitokeza mwanzoni mwa uchunguzi wa Tume ya Mbia, basi ndio sawa na msingi wa uchuguzi wake. Tamko letu ni la maandishi na liliweka wazi kuwa Chama kingeshirikiana na watu kudai haki yao kwa njia yoyote watakayo amua. Baada ya tamko hili ndio maana Chama kikaamua kufanya maandamano siku na tarehe moja tu, yaani Jumamosi 27 Januari, 2001. Hili halikuwa jambo la siri na ndio maana vyombo vyote vya Habari nchini vilitoa matangazo ya kuzuia uhuru huu tena vikimaanisha siku hiyo tu na sio Ijumaa ya tarehe 26 januari, 2001 ambapo Serikali ilianza kuuwa bila sababu.
Tuna hakika Mheshimiwa Mbita anazo kumbukumbu hizi kama moja ya vielelezo vya CUF, lakini aliamua kuupotoa ukweli na kuudanganya ulimwengu. Kwa sababu hi ya msingi ni sawa na kusema kwamba mauaji ya Januari 26 hayakuwa nya kisiasa hasa kwa vile hakukuwa na maandamano ya aina yoyote. Yawezekana basi, kwa kuwa mauaki ya tarehe 26 yalifanyika Msikitini, pengine Serikali ilikwisha amua kuendesha mauaji kwa sababu nyengine zaidi ya siasa. Kwa hivyo, ni shida kuamini kuwa siasa ni tatizo linaloweza kufanya maafa kama hayo kwa Zanzibar ya leo bila ya kuchanganya mambo mengine ambayo Serikali inayaelewa zaidi kuliko jamii ya Watanzania.
Tamko lilizidi kusema:
“Kwa kuwa Zanzibar ni sehemu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia CUF hakimtambui Mheshimiwa Benjamin W. Mkapa kuwa ni Rais halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali yake kwa sababu hawakuchaguliwa na wananchi wa Zanzibar. Vile vile, kwa uchaguzi uliofanyika Tanzania Bara, Baraza Kuu la Uongozi linalaani vitendo vyote vya wizi wa kura, udanganyifu, na utumiaji wa nguvu za dola uliojitokeza katika hatua zote za uchaguzi huo. Hivyo basi Chama kinawaagiza Wagombea wote waliodhulumiwa kwa njia moja au nyengine kupeleka malalmiko yao mahakamani”. Mwisho wa kunukuu.
Tunarudia kusema kuwa, ni kufuatia Kikao hicho cha Baraza Kuu Taifa basi ndio Chama kilianzimia kufanya maandamano hayo ya Januari 27,2001 ili kuweka bayana maazimio yake na vile vile kuitumia mikutano ya hadhara kurejesha imani na kujenga matumaini ya wanachama baada ya dharuba kali ya ‘uchaguzi wa kishindo’. Ni bahati mbaya basi, pengine Jeshi la Usalama wa Taifa lilimshauri vibaya Amiri Jeshi Mkuu kwamba maandamano yalikusudia kuondosha tawala zao za enzi na ndio hatimae wakamfikisha kutoa amri mbaya ya kuua raia zake.
Watu wakauliwa bure bila hatia na sisi tuliobaki tumeachiwa zivuka jamani, tumeachiwa mayatima jamani, tumeachiwa vilema jamani. Tukageuzwa wakimbizi wa lazima jamani. Mama na dada zetu waliingiliwa kwa nguvu tena hadharani jamani. Wazee walivutwa ndevu kama siku ya Mapinduzi jamani. Hawakujali ulemavu, uzee, utoto wa ujinsia; walipiga, walinyang’anya, walinajisi na pia kuuwa. Hata Mwenyekiti wetu Profesa Lipumba alipigwa kwa marungu na kurudishwa rumande jamani. Yote haya hayakuwa na bahati mbaya, ingawa pia hayakuwa na sababu za lazima kufanywa na Serikali inayosaidiwa na kutangazwa na mataifa makuu ya dunia kkuwa inaendeleza uchumi na demokrasia. Bado tunazidi kujiuliza, iwapo waliouliwa Januari 27, waliuliwa kwa maandamano yaliyopigwa marufuku na Serikali jee, wale waliouliwa msikitini tarehe 26 kabla ya siku ya maandamano, wao walikuwa na kosa gani? Jee ni siasa tu au kuna jengine? Jee, huku ndiko kukubali mfumo wa vyama kwa hiari? Tanzania twaelekea wapi?
Sehemu ya 2: Matayarisho ya Maandamano
7.2.1 Matayarisho ya awali
Kufuatia tamko la Baraza Kuu, Chama chetu kilitoa taarifa Polisi kwamba kinataka kufanya maandamano ya amani na mikutano ya hadhara siku ya jumamosi Januari 27, 2001 katika sehemu mbali mbali katika nchi. Madhumuni yake ni kama tulivyoeleza katika muhtasari uliotangulia. Yaani, kutamka hadharani kwa wanachama wetu, kutoridhishwa kwa chama chetu, na namna uchaguzi wa mwaka 2000 ulivyoendeshwa na namna baada ya hapo, unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binaadamu unavyochukuwa nafasi ya “amani na utulivu” Tanzania. Ni haya tu basi. Ndio maana tukawaomba waandamanaji kujifunga vitambaa vyeupe kama ishara ya amani.
Azma ya pili ilikuwa ni kuamsha hamasa za chama pamoja na kujenga imani na matumaini kwa wanachama wetu baada ya kuvunjikka moyo kutokana na uendeshwaji mbaya wa uchaguzi na mapishi ya matokeo yake. Barua ziliandikwa na kila wilaya ya chama chetu, il kuwaarifu Polisi katika sehemu zao watupatie mapema kabla ya wiki tatu ili kuipa nafasi Serikali kupanga mipango yake ya kiusalama. Kwa kawaida sisi huwa hatuhitaji walinzi katika mikutano yetu kwani walinzi wetu wa chama yaani Blue Guards na White Guards wanatosha kuweka hali ya utulivu katika mikutano yetu. Wanatosha hasa kwa kuwa mikutano yetu haina fujo. Tulitoa taarifa kwa kuwa sheria ndivyo inavyotutaka tutoe taarifa kwa Polisi si chini ya masaa 48. Tena sheria inasema kutoa taarifa na sio kuomba ruhusa. Kwa hivyo, anaeomba ruhusa waweza mzuia, lakini anaetoa taarifa na sio kuomba ruhusa. Kwa hivyo, anaeomba ruhusa waweza mzuia, lakini anaetoa taarida kwa wingi waweza mshauri wakati mzuri wa kudanya jambo na sio kumzuia kabisa. Serikali za Tanzania zimezoeza kuweka vifungu vya Katiba na sheria zinazoruhusu mambo ili kuuhadaa ulimwengu tu na inapokuja hatua ya utekelezaji, amri ya kiongozi huwa juu kuliko matakwa ya Katiba na sheria. Ndio maana Serikali ilipozuia maandamano ilisema kwa “amri halali” na sio kwa mujibu wa vifungu vya “Katiba na Sheria”.
Kutokana na barua yetu ya taarifa, Polisi walijibu baadae kwamba, maandamano yetu yalipigwa marufuku. Hakukuwa na sababu za mapungufu ya kiusalama kama kawaida yao, maana mara nyingi pakiwa na sabau hizo basi Serikali husema pangeni siku nyengine, lakini mara hii ilikuwa ni kupiga marufuku moja kwa moja bila hoja zaidi. Vikwazo hivi vya vyombo vya dola havikubuniwa tu, lakini ilikusudiwa kutekeleza matakwa ya kibinasi ya Amiri Jeshi Mkuu Benjamin Mkapa. Licha ya kuwa ndo Amiri Jeshi Mkuu, pia ndie Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano; na kwa mujibu wa Baba wa Taifa katika siku za kumnadi, ndie Bwana Msafi (Me. Clean) Tanzania. Kauli ya kupiga marufuku harakati za kisiasa alizotoa mbele ya umma wa Tanzania zikishuhudiwa pia na Jumuiya za Kimataifa mara tu baada ya kuapishwa kwa mara ya pili kuwa Rais. Kwa ufupi alisema kwamba, mara tu baada ya kurejeshwa tena Ikulu asingependa kuona harakati za vyama vya upinzani kwani alihitaji wasaa wa kutekeleza sera za CCM kama alivyoahidi katika ilani ya uchaguzi. Huu ndie “Bwana Msafi” anavyotekeleza demokrasia Tanzania.
Rais Mkapa anamaliza muda wake wa Urais, lakini kwa kawaida ya mila na desturi zetu Tanzania, Rais anaeondoka madarakani ndie anaemuonesha kidole yule anaetarajiwa kuwa Mgombea katika chama chake. Ndivyo alivyofanya Baba wa Taifa, Mwalimu na bila shaka ndivyo atakavyofanya Bwana Msafi. Na iwapo Msafi katufikisha hapa, sijui Mtanashati atakae muelekeza kidole ataifikisha wapi Tanzania iwapo atapewa ridhaa ya watu! Sisi hatumjui ndio maana tuna wasi wasi na tunatoa wasi wasi wetu mapema sana ambapo leo ni miaka miwili kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Tatu wa vyama vingi wa Oktoba, 2005. tunawajibu wa kusema hivyo kwa kuwa tunaambiwa na wana historia kuwa historia hujirudia.
Amri hii ya Amiri Jeshi Mkuu licha ya kwamba ilipingana na misingi yote ya demokrasia na haki za kujumuika, lakini pia ilishtusha kutolewa na Rais Mkapa. Itakumbukwa kwamba, ni yeye aliemiminiwa sifa tele kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa na vyombo vya fedha hasa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani kwa jitihada zake za kurejesha demokrasia, uongozi bora na kufufua uchumi, katika kipindi cha awamu yake ya kwanza (a995 – 2000). Kauli ya Mkapa iliendana na ile “ushindi wa kishindo” katika nchi ya siasa za ushindani. Hata hivyo, kauli ya Mkapa ilipokelewa kwa mshangao mkubwa na vyama vingine hadi wengine kufikiria kwamba ni kigugumizi cha kuteleza kwa ulimi tu. Kwa urasmi wa vyama kutokana na kusajiliwa na Serikali na kwa umuhimu wa harakati zao za kuirekebisha, kuikosoa na kuielekeza Serikali, wengine walidhani Tais aliogopa Serikali kukosolewa. Hata hivyo, wapinzani walidhani Rais angewaandikia rasmi katika vyama vyao kuthibitisha utaratibu huu mpya ya awamu yake.
Pamoja na vitisho na kauli kali za vyombo vya dola, sisi tuliendelea na matayarisho yetu ya maandamano kwani tulijuwa kuwa nchi hii haiendeshwi kwa amri, bali inaendeshwa na sheria. Tulijuwa kwamba Wafalme wakivaa kofia mbili kwa wakati mmoja, hutokeza shida ya namna ya kuzidengua. Mkapa yeye ana kofia mbili, na hivyo hatukujua alikuwa akitumia ipi wakati ule, ama ya Uenyekiti wa chama au Uamiri Jeshi Mkuu. Tena tukumbuke kwamba Rais aliapishwa mwezi wa Novemba 2000, na sisi tulitaaribu tufanye maandamano mwisho wa mwezi wa Januari mwaka uliofuata. Hivyo, kwa vyovyoe vile maandamani yetu hayakukusudiwa kumzuia asifanye kazi zake za Urais.
Haki ya uhuru wa mawazo na kujumuika imeelezwa katika vifungu vya 18 hadi 21 vya katiba. Kwa mfano Kif. 20(1) cha Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinasema, “Kila mtu anastahiki kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, tkuo mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo”. Ni Katiba hii ndio Rais alioikamata na kuapa kuitumikia na kuilinda. Ndio tukasema wengi hatukuamini kuwa alikuwa hadhiri alipokuwa akitoa kauli ili.
Bila shaka maneno “bila kuathiri sheria za nchi” katika Katiba haina maana kwamba sheria ndio zilizo juu ya Katiba, lakini Sheria zinakuwepo kutandika utaratibu bora wa kuitekeleza Katiba na sio kuifanya isifanye kazi. Na ikitokea kuna sheria huathirika kwa matakwa ya Katiba au inazuia Katiba isifanye kazi, basi sheria hiyo ni miongoni mwa sheria kandamizi (oppressive laws) ambazo Jaji Mkuu Mstaafu Fransis Nyalali alishauri zifutwe ili kuwa na mazingira bora ya kutekeleza demokrasia. Hata hivyo, kwa kuwa Tanzania haina ukweli katika kutekeleza demokrasia ya vyama vingi, ndio maana ikakataa kuzifuta na leo inazitumia sio tu kwa kuzuia demokrasia ya kweli ya vyama vingi, bali inazitumia kwa visingizio vya kumaliza maisha ya Watanzania. Imekuwa mara nyingi ikidaiwa na vyama vya upinzania kwamba kunahitajika angalau badi kuzifanyia marekebisho sheria za ukandamizaji lakini Serikali hujibu hakuna sheria za namna hiyo Tanzania.
Kama hii ndio imani thabit ya Serikali, basi hii na maana kwamba huku ni kukubali kwa Serikali kuwa Sheria zilizopo zintia nguzu Katiba na zaidi zinasaidia Katiba hiyo ifanye kazi. Kwa mantiki hii, Serikali inaamini kwamba hakuna katika Tanzania, uwezekano wa matakwa na haki za kikatiba kuathiri sheria zilizopo. Ukweli huu ndio uliotuongoza sisi katika CUF kutoa notisi ya taarifa ili kutumia haki yetu ya kikatiba tena kwa mujibu wa sheria ambayo inataka muombaji wa mkutano atoe taarifa (sio ombi) ya masaa 48 kwa Polisi kabla ya shughuli yenyewe.
Hivyo, hatukuona mantiki kwa dola kusema tulivunja sheria, ila tulijua tu kwamba vyombo vya dola vilitumika kusaidia matakwa ya CCM na kwa hili lilionekana na chama chetu kama kebehi ya mwisho ya demokrasia. CUF kama chama kikuu cha upinzani kina jukumu tangulizi (leading role) katika jamii ili pia kulinda hadhi ya vyama vingine. Vyama vya upinzani vyenye upinzani wa kweli hawatasahhau kujitosa na kujitoa muhanga kwa wanachama wetu katika kuitetea demokrasia. Sote tulikwisha pigwa mweleka kwa kauli ya Mkapa, lakini baada ya maandamano tulisimama tena kwa pamoja. Zaidi ya yote chama chetu ndicho chama mbadala kwa mujibu wa maoni ya wananchi yaliyojitokeza katika uchaguzi uliopita licha ya mizengwe yote ya CCM na vyombo vya dola ya udanganyifu katika kura. Hivyo, tunajukumu la kuona kwamba imani hii haipotei bali inashamiri ili kupata uwezo wa kuiongoza dola. Zote hizi ni sababu za kuwa na haja ya kuzungumza na watu kila mara na kwa nafasi tena bila vizingiti. Haya ndio mambo ya msingi yaliyotulazimisha kuwa na mikutano na maandamano ili kushajiisha na ujumbe wetu upate kusikika vyama. Hatukuwa na jengine zaidi ya hili.
Tabia za kulazimisha ushindi zina hasara zake, na zaidi ushindi wa kishindo ni “ushindi shinda” na athari zake kwa mshindi wa kishindo ni kuogopa vishindo vya baadae vya ushindi bandia. Ukweli wa ushindi wa aina hii ni kwamba, akubalipo mmoja wenu kuwa kashinda kwa kishindo, hili haliwezi kumuondoshea hofu mshindi wa aina hii ya kuwa pia anaweza kuondoshwa kwa kishindo. Hofu ya kulazimisha ushindi huikosesha Serikali ilioko madarakani imani kwa wananchi. Na kwa hivyo, Serikali hujizatiti kujijengea imani (confidence) kwa rungu ya dola kwani Serikali kama hii siku zote hutaka iogopwe.
Mambo mawili makubwa yalichangia kupandisha munkari kwa dola baada ya uchaguzi. Kwanza ni ile tabia ya baadhi ya vyama kukataa maoni ya wanachama wao walio wengi juu ya nani awe mgombea. Mgombea wa namna hii hukataliwa na wanachama wake pamoja na wale wa vyama vingine. Anaelezimisha huwa kajifedhehesha kwani huambukia kura chache na mwishowe hutafuta wapi kwa kusukumia lawama. Hivi ndivyo Mkapa alivyotaka kuhakikisha kwamba Mgombea wake anatawala kwa hali yoyote. Na hili ndilo hasa lililomlazimisha ahiari kuuwa ili kunyamazisha kila kilichojitokeza kuwa ni bghudha kwa utawala wa kishindo.
Sababu nyengine ni ule ukweli kwamba Tanzania Bara nako mara hii kulikuwa kumeimarika kwa chama chetu kuwa mbele kwa utetezi wa demokrasia inayovurugwa na chama tawala na dola yake. Kwa vyovyote vile, mtu hawezi kujenga imani kulazimisha chochote katika mfumo unaotoa fursa kwa watu kuamua wapendalo. Ndio maana katika kumjengea imani mgombea wake, Rais Mkapa hakupata njia isipokuwa kulazimisha kama alivyolazimisha ushindi. Mauwaji haya hatuyakumbushi kwa nia ya kuandika historia ya matukio tu, lakini kumbukumbu hii ni pamoja na tangazo la kuyalaani kwa nguvu zetu zote. Hata katika enzi ya ukiritimba wa chama kimoja, bado bunduki haikuwahi kuitumiwa “hadhiri nadhiri” kuua raia kama ilivyokuwa Januari 26 na 27. Aidha, haikufikapo Serikali kutumia majeshi ya nchi kutesa na kunajisi raia hata Watanzania wakahiari hifadhi ya ukimbizi kwa makundi kuliko nchi yao inayojulikana ulimwenguni kwa utulivu.
Haya ndiyo yaliyojiri chini ya utawala wa Rais Benjamin William Mkapa, ‘Bwana Msafi’. Wakati mauaji yanatokea Rais Mkapa alikuwa nje ya nchi kwenye ziara. Aliachia madaraka yake yashikwe kwa muda na Makamp wake, Dr. Omar Juma. Hatukujua iwapo ukimwacia Urais mwenza, pia unamwachia na Uamiri Jeshi, lakini angalau twajua kwamba dola hua chini ya anaeachiwa madaraka. Mauaji yalitokea wakati Dr. Omar akiwa kazini na leo “sisi sote tuna msiba kwa roho za ndugu zetu na wake waliopotea”. Tulidhani CCM itakaa na kutoa kauli ya kukubali jukumu na kuwafariji waliobakia miongoni mwa wafiwa, vizuka na mayatima. Hata hivyo, kubwa tuliloambiwa ni kwamba tulistahili kufa kwa kuwa hatukutii amri halali. Watawala na baadhi ya Wanafalsafa wa Tanzania Bara, wao wanasema kwa kisingizio cha historia kuwa ni kitendo cha marudia kwa Wazanzibari kufa kwa makundi baada ya chaguzi.
7.2.2 Alkhamis tarehe 25 Januari, 2001 Dar es salaam
Kabla ya siku ya maandamano kufika, itakumbukwa kuwa Serikali ilizuia mkutano uliokuwa uhutubiwe na Mbunge wa CUF wa Jimbo la Kigamboni Mhe. Frank Magoba uliokuwa ufanyike tarehe 25 Januari, 2001, Polisi walitoa taarifa ya ghafla kuzuia mkutano huo. Wananchi walikuwa wamefika kwa wingi kwenye eneo la mkutano na hata Mwenyekiti wetu wa Taifa Mhe. Lipumba nae pia alikwishawasili akiwa kama mgeni mwalikwa wa mkutano huo. Baada tu ya kuwasili hapo aliona bora kuahirisha mkutano na kuwataka watu waondoke na warejee majumbani. Ijulikane tu kuwa taarifa ya Mwenyekiti ilikuwa ni kuahirisha na sio kuvunja mkutano ule, na alifanya hivyo kwa kuwa watu wengi walikwisha ondoka. Siku za nyuma iwapo kulikuwa na matatizo ya usalama baada ya sisi kupeleka taarifa yeu, Polisi walikuwa wakiwasiliana nasi na kutuomba tuahirishe na tupange siku nyengine. Siku zote tulikubaliana na mashirikiano kama haya. Katika mkasa huu, Polisi walitupillia mbali utaratibu wao wa kiungwana na wakahiari „kufanya uharibifu katika ardhi“.
Wakati wanarajea majumbani , Polisi walisimamisha msafara wa Mhe. Mwenyekiti, Mbunge na baadhi ya viongozi wetu wa kitaifa na kuteremshakwenye magari yao. Polisi wetu, bila ya kuwauliza „kala wa la kalamu“ walianza kuwashambulia kwa marungu na watu wengi wakijeruhiwa vibaya sana. Kitendo hiki kilifanywa na Polisi wa FFU wlaiokuwa wakiongozwa na Afisa aitwae Afande Toss na kwa kweli, mtu mmoja ambae alijeruhiwa kupita kiasi alifariki siku ya tatu yeke katika Hospitali ya Muhimbili. Kwa jiji la Dar es salaam si rahisi hata kidogo kumtambua majeruhi mara moja katika kizaa zaa kama kile walichokisababisha walinzi wetu wa usalalma wa raia. Baada ya mkong’oto wa kishindo viongozi wengine (akiwemo Mwenyekiti wa Taifa), Prof. Lipumba walikamatwa na kupelekwa rumande hapo Police Central wakiwa pamoja na wananchi wengine ambapo sasa jumla yao ikiwa ni zaidi ya hamsini.
Polisi baadae waliwapeleka Mahakamani suku ya Jumatatu tarehe 29 Januari, 2001. Kitu kimoja kinajieleza. Polisi hawa hawa wanaongozwa na Mahita mmoja na Sheria moja walichuwa hatua na kuwapelwka mahakamani mapema kidogo ikilinganishwa na Zanzibar ambako mtu humpelekwa rumande wastani wa wiki siku kabla ya kufunguliwa mashtaka. Hatusemo kwamba siku 3 kukaa ndani bila hatia ni vizuri, lakini inaonesha namna sheria moja inavyotumika kwa kuwahudumia watu wamoja katika Tanzania moja. Hatimae, ili kupunguza idadi ya washitakiwa katika kesi ambayo Serikali haikuwa na hamu nayo, basi Polisi walianza kuwaachilia baadhi ya mahabusu kinyemela bila ya kuwapeleka mahakamani.
Ukiachilia mbali wale wananchi waliokamatwa na kuachiliwa kinyemela siku ya pili yake na ambao hatukuweza kupata majina yao, viongozi na baadhi ya wanachama wafuatao ndio waliokamatwa na kufikishwa mahakamani:
Jadweli Na. 1: waliokamatwa na kufikishwa Mahakamani
|
S/No.
|
JINA
|
WADHIFA
|
PAHALA
|
|
1
|
Prof. Ibrahim H. Lipumba
|
Mwenyekiti Taifa
|
Sinza
|
|
2
|
Ernest J. Lyanga
|
Naibu Mkurugenzi
|
Ilala
|
|
3
|
Annia Said Chaurembo
|
Naibu Mkurugenzi wa Fedha
|
Kariakoo
|
|
4
|
Shaban Ngozi
|
Afisa Mipango na uendeshaji
|
Vingunguti
|
|
5
|
Hussein Ali Alawi
|
Dereva
|
Buguruni
|
|
6
|
Hussein H. Iddi
|
Mlinzi
|
Buguruni
|
|
7
|
Ali Shaali
|
Afisa Mnadhimu
|
Magomeni
|
|
8
|
Yussuf M. Karama
|
Mpiga Picha (camera man)
|
Temeke
|
|
9
|
Abuu baker Rakesh
|
Mwanachama
|
Magomeni
|
|
10
|
Salum Said Kikugio
|
Mwanachama
|
Tandika
|
|
11
|
Kassim Said
|
Mwanachama
|
Mbagala
|
|
12
|
Khamis Mohammed
|
Mlinzi
|
Tandale
|
|
13
|
Frank G. Magoba
|
Mbunge
|
Kigamboni
|
|
14
|
Fred Kabisama
|
Kaimu Katibu wa Wilaya
|
Ilala Vingunguti
|
|
15
|
Swaleh Sudi Ally
|
Mwanachama
|
Buguruni
|
|
16
|
Mussa Rashid
|
Mwanachama
|
Buguruni
|
|
17
|
Omary Ally
|
Mwanachama
|
Buguruni
|
- Waliomia na kupata matibabu
Jadweii Na.2: Walioumia na kupata matibabu
|
S/No
|
Jina
|
Walivyoumia
|
|
1
|
Prof. Ibrahim H. Lipumba
|
Mkono wa Kulia na kuibiwa saa na Polisi
|
|
2
|
Ernest J. Lyanga
|
Kichwani (ngeo)
|
|
3
|
Hussein Ali Alawi
|
Miguu
|
|
4
|
Hussein Hamad Iddi
|
Miguu
|
|
5
|
Yussuf Mohammed Karama
|
|
|
6
|
Abuubakar Rakesh
|
Kichwani (ngeu)
|
|
7
|
Salum Said Kikugio
|
Kuvunjika mkono wa kulia
|
|
8
|
Kassim Swedi Kitunda
|
Alivunjika mguu wa kulia
|
|
9
|
Khamis Mohammed
|
Kichwani na mguuni
|
|
10
|
Fred Kabisama
|
Aliumizwa kichwani
|
|
11
|
Omary Ally
|
Aliumizwa kichwani
|
|
12
|
Shaban Shomari
|
Aliumizwa miguuni
|
Chanzo: Kurugenzi ya Mipango (CUF – Ofisi Kuu DSM)
* Angalia: Abubakar Rakesh sasa ndie Mkurugenzi wa vijana na Haki za Binaadamu, Taifa
7.2.3 Ijumaa Tarehe 26 Januari, 2001
Wakati tumeshapeleka barua zetu kungojea majibu ya Polisi wa kila wilaya, wote walijibu, tena kwa lugha inayofanana kwamba, walipiga marufuku maandamano yetu ya amani. Vyombo vya habari baadae vilianza kunguruma kwamba maandamano yalipigwa marufuku. Vyombo vya habari vya Dola (hasa sauti Tanzania Zanzibar) navyo vilitapika vitisho, na kejeli iliyoongeza mori na munkari kwa askari ili wafanye unyama wao iwapo tungekhalifu amri. Sio kwamba vilisema kwa sauti ya kukhofisha watu, lakini vilisema kwa kushonganiza. Sisi kuhusu hili la kuuliwa ovyo, hatukufikiria kwamba askari wangekuwa na ukatili wote na wakalitekeleza. Hatukwenda kwenye vita sisi tulikuwa kwenye mstari wa uhuru wa maoni ambao ni msingi wa Katiba yetu. Hatukutarajia hata kupigwa marungu, ingawa huu ndio mtindo wao kwetu sisi, iwe tuna kosa au la. Ama kwa wakati ule Sauti ya Tanzania Zanzibar ndio iliyotia fora kwa kazi chafu, kama vile Radio Intarahamwe ilivyoshonganiza mauaji ya Rwanda na Burundi. Hadi tunaandika kitabu hiki, ikiwa leo ni miaka mitatu baada ya mauaji na miaka miwili baada ya muafaka, bado vyombo vya habari vya Serikali havijabadilika hata shubiri katika majukumu yao ya kudhoofisha demokrasia nchini. Hii ndio maana tukisema mazingira ya mateso na mauaji bado yapo huwa tunatumia vigezo kama hivyo na ingawa mifano yake iko mingi, lakini vyombo vya habari vya Serikali ndio vinavyoongoza kwa kuvizisha demokrasia.
Kwa hivyo basi, vitisho hivyo vya dola na vyombo vya habari vilianza mapema wiki nzima kabla ya siku ya mauaji. Huku vyombo vya habari vikitoa matangazo, Polisi walianza kumiminwa na wengi wao wakitokea Tanzania Bara. Silaha nzito nzito zilielekezwa Unguja na Pemba. Huku askari wakiivamia miji mikuu ya Tanzania, bosi wao Mkuu Alhaj Omar Mahita, alijitutumua kwa kauli ya dhihaka akasema iwapo „CUF wao ni ngangari basi Polisi ni Ngunguri“. Ngangari kwa CUF si chengine isipokuwa ni ukakamavu na mtu anaweza kujiuliza basi ilikuwaje Polisi wageuze taswira na maana ya bango lenye usemi wetu huu kiasi cha kufikia uamuzi wa kutekeleza sheria wakiwa na kasumba za kiitikadi za chama tawala? Alipokuwa akimpigia kampeni Dr. Salmin, Rais Mstaafu Mwinyi, alikuwa akimnadi Mgombea Mwenza wa CCM, Dr. Omar kwamba yeye ni „Chinja chinja“, lakini Polisi hawakutoa tafsiri kwamba yeye alikuwa anahubiri hatari na mauaji. Iweje leo basi, Mahita aitafsiri kauli ya CUF aiwache ile yenye maana ya wazi wazi ya Mwinyii. Sisi tulielewa kwamba pengine mafuta ya madaraka yalikuwa hayajakolea, kwani wakati ule kulikuwa na ustaarabu mwengine katika Jeshi la Polisi chini ya IGP Mahundi.
Kama utamaduni wa kazi wakati wa Ispector General Mahundi ungekuwa wa kuua kama wa mrithi wake mahita, basi alikuwa na nafasi na uwezekano mkubwa zaidi wa kuua. Katika kipindi kile mfumo wa vyama vingi ndio kwanza ulikuwa unaingia nchini na kila mmoja aliupokea kwa namna ya ufahamu wake. Hii ni tafauti na miaka mitano baadae ambapo watu walianza kuufahamu kwa mtazamo wa aina moja. Wakati ule Polisi hawakuwahi kabisa kutiwa kasumba wazi wazi hata wakapoteza imani kwa ndugu zao na kuua ovyo. Hivyo, hawakufurutu asa wakaua kama walivyofanya wakati wa Mahita. Wengine wanadhani,pengine kwa kuwa Mwalim alikuwa hai, yawezekana ndio sababu wauaji walificha makucha yao. Kumbe hatukujua kwamba warithi wake walikuwa wanaomba Mungu aondoke haraka ili wadhihirishe yaliyomo vifuani mwao.
Kabla ya mauaji wakubwa wa nchi walifanya kazi kubwa kusaidia mauaji yatekelezeke. Tuna mifano ya kauli za uchochezi zilizotolewa na viongozi wakuu wa CCM kutoka pande zote za Muungano. Mfano wa kauli hizi ni kama zifuatazo:
Ndugu Mohammed Seif Khatib, Waziri wa Mambo ya ndani wa Tanzania alifanya ziara Zanzibar na kutoa maelekezo kwa Polisi na kama kawaida yao, kukutana na viongozi wa Chama Tawala na Serikali kuweka mikakati yao sawa.
Ndugu Fredric Sumaye, Waziri Mkuu wa Tanzania naye kama kawaida yake alitoa kauli katika Bunge mjini Dodoma, sio tu ya vitisho lakini pia ya kuwamkinisha askari kwa kazi ya kuua ambayo Kamati yao ya Ulinzi na Usalama ilikwisha kaa na kuithibitisha kauli yake. Kikao hicho kiliitisha na Makamo wa Rais, Dr. Omar Ali Juma ambae kupitia kikao hicho alitoa onyo kali la kutaka maandamano hayo na mikutano isifanyike.
Kauli nyengine kwa utngo zilikuwa zikitolewa na Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Makamanda wa Polisi katika sehemu zao. Wanasiasa wa Chama tawala pia nao hawakuwa nyuma kutoa maoni yao ambayo yalizidi kuwaunga mkono Polisi wafanye ambayo wengi wa wanachama hawajayaona katika uhai wao na uzoefu wa kisiasa.
Ushahidi huu ni tosha kwamba majeshi yetu yalitayarishwa kivita na sio kuzuia fujo. Ni bahati mbaya sisi hatukuwa na kikosi wala silaha na ndio maana hata pale Serikali walipotoa takwimu ya waliokufa basi walisema, walipoteza askari mmoja aliechinjwa kwa kisu. Miaka ya nyuma majeshi ya CCM yaliwahi kuuchakaza mji mzima wa Shengejuu eti kwa shutma kwamba wananchi wa hapo walikuwa na silaha waliyomnyang’anya askari. Kama hii lingekuwa kweli, basi huyo askari mmoja wanaesingizia kuuliwa na CUF asingekufa kwa kuchinja kwa kisu.
Baada ya kutolewa kauli za kuzuia maandamano ambazo zote zilikusudiwa kubinya demokrasia pamoja na kwamba zilikuwa ziko kinyume na Sheria na Katiba ya Nchi, kiburi cha Polisi kilizidi na kauli za Wakubwa wa Jeshi la Polisi zilianza kutolewa kwa nguvu na kuashiria kwamba ni Askari wenyewe ndio waliotayarishwa kuanzisha vurugu siku hiyo ya Januari 27, 2001. Hata hivyo, juu ya vitisho vyote, wana CUF wa Tanzania nzima waliendelea na maandalizi ya maandamano na mikutano ya hadhara tu, siku hiyo ya Januari 27, na katu haikukusudiwa jambo jengine.
Wakati tunasubiri kwa hamu maandamano yetu, mara tulisikia kwamba Mheshimiwa Juma Othman Juma ambar ni Katibu wetu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama alikamatwa na kuwekwa rumande. Unguja, Mheshimiwa Muhammed Ali Yussuf, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje nae alikamatwa usiku wa manane siku ya Alhamis tarehe 25 Januari. Yeye pamoja na viongozi wengine wakuu, Mheshimiwa Ali Haji Pandu na Dk. Maulid Makame Abdalla ambao walikamatwa siku iliyofuata, wote waliwekwa rumande kitu cha Mwembe Madema kwa muda wa zaidi ya wiki mbili na baadae kupelekwa mahakamani kuanza utaratibu mwengine mrefu wa sheria za kimapinduzi. Mtindo huu wa kukamata watu usiku ni hatua iliyochukuliwa kwa raia siku za harakati za Mapinduzi tu, lakini zilirejea tena mwaka 2000. hatukushangaa kwani tuliambiwa Amani atakwenda hakukutuvunja moyo, tuliendelea tu na mipango yetu huku tukisubiri Jumamosi kwa hamu. Masikini , kumbe tulishatayarishiwa karamu ya misiba.
Hata hivyo, Polisi hawakusubiri Jumamosi ifike kwani ilipofika Ijumaa ya 26 januari, 2001 mauaji yalianza. Ijumaa kwa Waislamu ni Siku Kuu ya Ibada. Ilikuwa ni majira ya saa saba na nusu mchana siku hiyo, ndio kwanza Waislamu wanamaliza sala zao misikitini. Misikiti mingine ilikuwa imeshamaliza kusali na watu wako milangoni wakitakiana kheri na kuagana. Bila shaka wengine walikuwa njiani tayari wakielekea majumbani kwani misikiti mingine hutangulia kusali kidogo. Siku hiyo haikuwa ya maandamano kabisa, maana maandamano yalipangwa siku ya pili yake, tena barua zetu kwa Polisi zilionesha hivyo.
Siku ya Alhamis ya tarehe 25 Januari, 2001, Dr. Omar alihutubia Taifa kupitia vyombo vya habari akisema haya „…… hawa CUF ndugu zanguni hamuwajui nyie, ni wajanja sana hawa, na kwa vile wamesema watafanya maandamano siku ya Jumamosi, yawezekana wakafanya Ijumaa hawa“. Wengi hadi leo tunajiuliza kwanini aseme moja kwa moja maelezo ambayo hayawezi kuthibitishwa na ushahidi wa aina yoyote! Lakini hapana la ajabu sana na wala mtu hapaswi kushangaa sana kwani hapa ndipo tulipopata jibu kwa nini CCM walikuwa wakipakaza kuwa CUF ni chama cha Waislamu. Yawezekana basi, kwa kuwa sasa wamepitisha sheria za kigaidi, siku moja wakataka kuifanyia kazi, na bila sha, kwa mantiki hiyo basi, kazi ya kwanza huenda itaelekezwa kwenye chama chetu. Ndio maana tukasema mazingira ya kuua Watanzania bado yapo na kila uchao yanaimarishwa.
Tunasema hivi kwa sababu hapo nyuma, hata kabla ya sheria hii kutungwa, tayari CCM kwa kutumia vyombo vyake na vyama vyake tegemezi walitoa kauli kwamba CUF ni chama cha magaidi. Hizi zilikuwa ni shutma nzito kuwasakamizia wanasiasa wenzako. Yawezekana walifanya hivyo ili Watanzania watuogope na wao ‚waendelee kula nchi na kuwaletea wananchi maendeleo ya umaskini’. Hata hivyo, hili tuna wasi wasi nalo kuwa ndio lilikuwa lengo, kwani tulitangazwa kuwa sisi ni magaidi hata kabla tafsiri na sheria ya ugaidi kutungwa. Si hasha basi siku moja CCM wakatuhukumu hata kabla hatujafanya huo ugaidi waliotubebesha mgongoni. Wanafanya hivyo il kuficha makucha yao yalioroa damu ili wajipendekeze kwa vyenye kuleta maafa kwa raia katika Afrika. Diplomasia inageuzwa rushwa ili kutengeneza tawala zenye madhambi kwa raia. Hatujui iwapo kweli ulimwengu waungana au wamong’onyoka.
Tukirejea habari za siku ya Ijumaa ni kwamba, majira ya kama saa nane kasorobo za mchana hivi, waumini wa dini ya kiislamu walikuwa ndio kwanza wanamalizia sala ya Ijumaa hapo katika Msikiti wa Mwembe Tanga. Msikiti huo uko ubavuni tu mwa ofisi ya CUF wilaya ya mjini. Wakati huo watu walikuwa wamechanganyika changanyika kwa kusalimiana na kutakiana kheri ya Ijumaa na kuagana karibu na msikiti wao. Mara Polisi waliokuwa na silaha walifika ghafla na kuvamia kikundi kile cha waislamu. Kikosi kile kilikuwa kinaongozwa na Ofisa wa Polisi kwa jina la Mahmoud Juma, maarufu hapa Unguja kwa jina la Mrema. Watu walipowaona kundi hilo la Polisi wakiwa na silaha katika hali ya tahadhari walianza kufadhaika. Ofisi yetu ya wila ilifungwa kwani tulijua pale ndio palipokusudiwa, lakini haikuwa hivyo. Na kwa nini wakusudie wilaya wakati Makao Makuu iko karibu mita 200 tu kutoka pale! Naam; hawakuwa na haja ya Makao Makuu wala ya Ofisi ya Wilaya na kwa hivyo hawakuwa na haja ya siasa siku hiyo. Walikuwa na haja ya msikiti kama ilivyokuwa siku ya Mwembechai.
Hali hii ya mfadhaiko ilimshitua kila mtu na tukajua sasa ndio kishindo cha ushindi kinaaza. Mara kufumba na kufumbua tukasikia amri kutoka kwa Mrema ikisema ‚shoot’ na punde amri ikapokewa kwa kumfayatulia mtu mmoja risasi. Hadi leo twajiuliza hivyo ndie waliemkusudia kweli! Maana huyu alieandguka na kufariki pale pale alikuwa ndie Imamu wa msikiti ule wa Mwembetanga. Kwa Askari kama Mrema ndio maana hadi leo anatanua kama vile aliua tumbili tu; kwani kama ingekuwa mwnye vita ukifanikiwa kuua kamanda huwa umefanya kazi nzuri. Ndio hivyo hivyo basi, kumuua Imam msikitini Mrema alistahili aliyopewa baada ya kitendo kile. Imam walietunga na kumtungua na kumuua Mwanazuoni chipukizi Ustadh Juma Khmais Mohammed akiwa katika umri wa miaka 30 akiacha kizuka na familia kubwa iliyomtegemea, lakin bila ya mtoto wa kuzaa. Ndio mwanzo alianza kufunga ndoa jamani. Maskini Mrema alimkata roho kufumba na kufumbua, na kufungua na baadae akarudi kwake akafura mikono damu akakaa kitako na familia yake akicheka. Famlia ya mwenziwe ikilia na sasa inahangaika. Ustadha Juma hakuwahi hata siku moja kuwa kiongozi wa chama chetu, lakini yawezekana kabisa alikuwa mwanacham wetu. Na kwani kuna kosa gani? Au ndio hukumu ya kuchanganya dini na siasa inayokatazwa sana na CCM? Haijulikani kama Ustaadh Juma aliuliwa kama mwana CUF aliekuwa karibu na Ofisi ya wilaya au walimuua kama Kiongozi wa Waislamu aliekuwa karibu na Msikiti. CCM ndio wanaojua zaid na siku moja wataulizwa.
Kama hii haitoshi mara risasi nyengine kama mvua zikamwagwa kundini mwa watu waliokuwa wakikimbia. Mara hii ilikuwa zamu ya Ustadh Seif Juma Said. Huyu alianguka na kuzimia na wakadhani amekwisha. Baadae alizinduka lakini kumbe risasi iliathiri sana mguu wake, na ilibidi akatwe. Ni kiwete sasa, angalau yeye ana uwezo wa kumuona Mrema bado, Juma hamuoni tena Mrema ingawa kesho wataonana. Risasi zile zilizomiminwa kama mvua katika kundi la watu ambao walikuwa wako mbioni kujisalimisha ziliangusha na kujeruhi vibaya watu wengi. Salama iwapi tena, watu walianguka na kuwa majeruhi na wengine hadi leo ni vilema. „Kila kitu ni cha Mungu, na kila kitu kitarejea kwake“. Ama inaonesha kama vile waliambiwa waje waue msikitini na zaidi wamuuw Imam, kwani baada ya hapo Mrema na kikosi chake walielekea msikiti wa Mchangani na Mbuyuni. Kama walikuwa wakitafuta maimamu, basi bila shaka walikuwa wakiwatafuta akina Sheikh Aliani. Lakini hakumkuta. Zake zikeeko. Kwa kawaida Mchangani wao saa saba huwa hawapo tena.
Punde tukasikia mlio mzito wa bunduki. Wakatupita vijana wakihema kwa mbio. Hawauliziki lakini baadae tukapata habari kuwa Mrema kachomoka kumwaga damu. Hapa tukapata habari kuwa mti mmoja aitwa Hamad Said nae alitunguliwa na kufa hapo hapo. Tukauliza ni mwanachama wa tawi gani, lakin vijana wakatujibu kwamba huyu ni mwanachama mkereketwa wa CCM. Kwa yoyote „mwenye macho“ na anaetaka kujua ukweli sasa ataamini kwamba siku ile watu kwa misingi ya kisiasa bali walikusudiwa kuuliwa watu kwa misingi ya Uzanzibari, na kwa kuwa yalifanywa misikitini basi ni nani atakaebisha kuwa pia yawezekana mauaji yalifanyika pia kwa misingi ya Uislamu. Ndio maana ya CCM kupandikiza chuki ndani na nje ya Tanzania kuwa CUF ni chama cha Waislamu, na kwa hivyo wakitaka kuishughulikia CUF kwanza huwenda misikitini.
Haya yakitokea chini, huko juu ya anga basi Bwana Mahita yuko na Helkopta kuangallia kama kazi yake ilikwenda vizuri. Tuna kumbukumbu kwamba helkopta hizi zililetwa kutoka Afrika ya Kusini na zilizinduliwa kwa kuwashughulikia Waislamu Mwembechai. Kazi ya pili ilikuwa kuwashughulikia Waislamu Mwembetanga, hatujui jamani kazi ya tatu itakuwa Mwembe upi. Lakini haya twende, tutafika. Mtu atashangaa, tokea helkopta hzi kuja hapa nchini, jahazi nyingi zimezama zikitokea Tanga (kwao Omar Mahita) kuelekea Pemba (Kwao Dk. Omar) na kupoteza maisha ya mamia ya watu, lakini hatujaziona wala kusikia kwenye vyombo vya habari kwamba zimejihusisha kutoa msaada wa kuokoa maisha ya wale ndugu zao wa damu. Si kwa sababu nyengine, ile kwa kuwa ni Wapemba, na ni wakorofi kwa kuwa wamesimama kidete kupinga udhalimu wa CCM kwa Watanzania walio wengi. Ndio amani na utulivu hii, ndio umoja wa mshikamano. Ndio udugu wa damu huu wa wenzetu, na si wote, lakini CCM
Matukio haya ya Ijumaa kabla ya siku ya maandamano yalitendwa na Polisi huku sababu za msingi wakizijua wao wenyewe. Ina mahusiano gani mikusanyiko ya ibada ya dini ya Kiislam na chama cha CUF? Ndio dhana za CCM, kwa kuwa wamesema CUF ni chama cha Kiislam na kwa sababu Uislamu ni kero kwa CCM na Serikali zake, basi naam, yachukuliwa kwamba ukiwa Muislamu ndio eti utakuwa ni CUF, na kwa hivyo ukiua Waislamu basi ndio umeua CUF, na ndio hivyo hivyo wema hautendwi kwenye Waislamu wengi kwani kwa dhana yao, ukiwatendea wema Waislam utakuwa umeitendea CUF. Hii ndio hisia iliyojengeka kwa wenzetu na si hisi tena lakini ni mkakati unaofanyiwa kazi. Mkakati huu siyo tu kwamba unashadidiwa na watawala wa CCM lakini pia hushereheshwa na baadhi ya wasomi wao. Tanzania hakuna magomvi ya kidini kwani pamoja na Serikali kuwaelekeza watu katika mkondo wa misuguano ya kidini, lakini Watanzania wanazidi kuvumiliana kwa masuala haya. Twamuomba Mungu azidi kutuepusha nayo, lakini pia atuepushw na wale watutatkiao kadhia hio.
Baada ya kumaliza kuwashughulikia Waislamu kwenye ibada yao, sasa ndio walianza kuwashughulikia Watanzania kama wana CUF. Na tunataka ieleweke hivyo kwamba shughuli ya Ijumaa ilikuwa tafauti tena sana na shughuli iliyofuatia. Mauaji ya Mwembetanga na Mbuyuni hayana uhusiano wowotena siasa na kwa maana hiyo, mauaji ya wanachama wa CUF yaliyotokea baada ya siku hiyo. Hata hivyo, sisi kama chama kinachopigania haki za binaadamu yanatugusa sana mauaji haya, na kwa hivyo ni misiba yetu ya kuhuzunisha kweli kweli. Hivi ndio sahihi kwani katika misikiti huwa hatajwi Lipumba wala Seif. Anaetajwa mule mara nyingi kwa baadhi ya misikiti ni Sheikh Amani Abeid Amani Karume, ili apate maisha bora na fadhila za Ijumaa. Ndivyo baadhi ya Masheikh wanavyoamini. Na pengine yawezekana basi, kwa kuwa Mwembetanga hawana utaratibu wa kumtaja kiongozi, hii pekee yaweza kuwa ndio sababu ya kukumbushwa. Tunazidi kutoa ushahidi kwamba Ustaadh Juma na wenziwe walipotezewa maisha kwa sababu ya Uislamu na sio kwa sababu ya uwanachama wao wa CUF. Mungu awalaze peponi.
Kwa hivyo, kuanzia hapo askari Polisi waliendelea kuwakamata viongozi wa juu wa Taifa na wa Wilaya ya Mjini na kuwaweka rumande. Tulifikiri iwapo Polisi walikuwa wakiuwa CUF, basi na hawa wasingerudi rumande. Huu ni ushahidi mwengine kuwa mauaji ya Ijumaa ya kabla ya maandamano, hayakukusudiwa CUF. Baadhi ya viongozi aliokamatwa mkesha wa tarehe 27 ni viongozi wa Taifa na wa Ofisi ya wilaya. Baadhi yao ni: Mhe. Mohammed Iddi Makame (Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa), Mhe. Masoud Khamis (Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Wanawake wilaya ya Mjini), Mhe, Fat –hiya Zahran (Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa), Mhe, Mohammed Ali Shamte (Mwandishi wa Kamati Tendaji), Mhe. Zahor Tamal (Ofisi katika Kurugenzi ya Mpiango) na Mhe. Fatma Said (Sekreteri wa Ofisi ya Wilaya ua Mjini). Hawa,, tunasema ndio waliochukuliwa na kuwekwa ndani kwa imani zao kama wanaCUF na yawezekana ilifanywa hivyo ili kupunguza nguzu za maandamano ya tarehe 27 Januari, 2004.
Ama kuanzia hapo tena hali ya nchi ilivurugika na Polisi hawakuwa wakiongozwa tena na sheria kama vile bosi wao walivyoacha hekima na busra na badala yake kuongozwa na kibri na jabza. Kamata kamata na kupiga watu ovyo ilikuwa ndio hali iliyotawala miji yote Tanzania. Wakati wote huu tulikuwa Makao Makuu, Mtendeni kupotea habari kutoka kila pembe ya nchi. Ole wako, uwe na rangi nyeupe kidogo au ndevu. Ukiweza kuvutwa kama vile mkulima anavyonyoa mahindi mabichi. Haikuwa bahati mbaya hii, ndio kukumbushia ya 1964, ndio maana ya Mapinduzi Daima; ndio namna ya kudumisha ushindi wa kishindo na ndio kuwajengea heshima na kuwaenzi Mzee Karume na Mwalim Nyerere. Lakini si tuliambiwa? Ndugu Amani, huyu ndie mwenzetu, ni mwenetu, atakwenda mwendo kama wa babaake. Sadakta, kwani baada ya mwezi mmoja tu wa kuingizwa madarakani mauaji haya yalikuja kuthibitisha maneno ya mpiga debe wake maana hata babaake ndivyo alivyo anzia. Kwa kifupi sana hivyo ndivyo ilivyokuwa kabla ya siku ya maandamano
Sehemu ya 3: Maandamano ya Amani Januari 27,2001
7.3.1 Maandamano Dar es Salaam
Serikali hii haina washauri wazuri, na CCM nayo, kwa kuwa maamuzi yao hata yawe ya kisiasa, lazima kwanza yapate baraka ya vyombo vya dola basi mara nyingi dola ndio inayoanza kuvurunda. Na kwa sababu rushwa ya vyombo vya dola hutegemea kwa kiasi kikubwa wingi na uzito wa fitna, basi vyombo hivyo vya dola hutaka kuhakikisha kwamba kile walichoshauri kwa Serikali kinatokea vile vile. Hii ni kusema, ikiwa wametia fitna kwamba maandamano yatakuwa na fujo, basi ni lazima kila kitu kitafana lakini fujo itokee. Ndio maana mara nyingi wamekuwa wakiwashauri CCM wasishughulike kwani CUF ni mali ya Lipumba, Mloo na Seif. Na ndio vivyo hivyo walipowashauri kwamba wakikamatwa viongozi wakuu wa CUF na kufunguliwa kesi ya uhaini basi CUF nayo itamalizika. Walisahau kwamba ikiwa CCM ina wenyewe, CUF ni Chama cha Wananchi.
Ilikuwa asuhubi mapema Januari 27 kama tulivyopanga, wananchi wa jiji kuu la Dar es Salaam walimiminika kwa wingi katika sehemu tulizopanga maandamano yafanyie. Tatizo tulilolipata pale ni kwamba mgeni rasmi alikuwa awe Mwenyekiti wetu Profesa Lipumba, lakini ndio bado alikuwa rumande anashikiliwa tokea siku ile ya Alhamis. Pamoja na yeye, viongozi wetu wengi walikuwa bado wako rumande. Ingawa kuwakosa viongozi hawa kulikusudiwa kushusha ule msisimko na hamasa lakini hali haikuwa hivyo. Wanachama waliongeza kasi ya ungangari na maandamano yalifana sana. Wananchi waliweza kufika kwa wingi katika viwanja vya Kidongo Chekundu ambapo tulipaamua kabla.
Baadae ya kufika kule Kidongo Chekundu, Polisi wa FFU wakiwa na vifaa vyote vizito vya kuzuia fujo na kuua walifika na kuanza kumpiga kila mtu aliyeonekana kwenye eneo hilo na katika barabara iliyokaribu na hapo. Hii haikuwa kuzuia fujo, kabisa. Katika vurumai hiyo jumla ya 99 walikamatwa. Baadae wengine waliachiwa lakini wengine 40, akiwemo mwanamke mmoja aliyekuwa mgombea Udiwani katika kata ya Upanga Magharibi walifikishwa mahakamani. Orodha kamili ya waliofikishwa mahakamani ni kama hii hapa chini.
Jadweli No. 3: Waliokamatwa na Kufikishwa mahakamani Dar
|
S/No.
|
JINA
|
ATHARI
|
MAELEZO
|
|
1.
|
Hamza Lema
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Rukia Moh’d Ali
|
Kipogo na kupoteza fahamu
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Salim Said Kibwena
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Coolnine Yahya
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Said Hassan
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Ramadhan Amran Moh’d
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Frank Martin Raphael
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Twalib Abdalla
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Mrisho Juma Upatu
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
James Ali
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Mussa Mwinyijuma Kishashu
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Athuman Juma
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Waziri Juma Kijembe
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Salum Rashid Kipara
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Nassor Suleiman Chambuso
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Shokate Suleiman
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Omary Ali
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Hussein Juma Kidesu
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Moh’d Abdalla Ali
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Jumanne Membe
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Suleiman Salum
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Abdul Shaaban
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Rajab Phillemon
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Kiasi Mtipa
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Said Alisi
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Wilson Francis
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Ramadhan Kaziba
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Yussuf Abdalla
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Juma Yahya Kijazi
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Jarome Dioniz Mishi
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Madarizir Rajamula
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Waziri Mhina
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Abdalla Halfan Hamad
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Mussa Hamad Mtani
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Philipo Joseph
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Moh’d Shomari Pazi
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Rwebangira Kataraia Cleofasi
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Kazembe Rashid
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Nassor Ramadhan
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
|
1.
|
Hassan Kiswagale
|
Kipigo
|
Shitaka la kuandamana
|
Wakati huo huo, tulipokea taarifa kuwa yule kijana aliepigwa siku ya tarehe 25 Januari alikuwa akiitwa Jaffar Said na alifariki siku hiyo ya tarehe 27 Januari, 2001 na kuzikwa kijijini kwao Tanga.
7.3.2 Maandamano ya Tanga
Maandamano yalifanyika katika Mkoa wa Tanga. Halikadhalika, mamia ya wananchi walihudhuria na kushambuliwa na Polisi. Baada ya kipigo hicho,, wengine walikamatwa na kuwekwa rumande kabla ya kufikishwa mahakamani. Watu hawa ndio waliokamatwa na kushtakiwa:-
Jadweli No. 4: Waliokamatwa na kushtakiwa Tanga
|
S/No.
|
JINA
|
WADHIFA
|
MAELEZO
|
|
1
|
Adellastella Mkilindi
|
Katibu wa wilaya
|
Shitaka la kuandamana
|
|
2
|
Rashid Jumbe
|
Mjumbe, Baraza Kuu Taifa alipigwa sana
|
Alipigwa na kushtakiwa kwa kuandamana
|
|
3
|
Suleiman Muro
|
|
Shitaka la kuandamana
|
|
4
|
Moh’d Khamis
|
diwani
|
Shitaka la kuandamana
|
|
5
|
Omar Aden
|
|
Shitaka la kuandamana
|
7.3.3 Maandamano Jimbo la Mwibara
Katika Jimbo la Mwibara taarifa tulizozipata ni kwamba Bwana Laurenti Mayenjwa alipigwa na Polisi hadi kufa.
7.3.4 Maandamano Lindi
Lindi nako kulirindima kwa maandamano, wanachama walihamasika na kuitikia wito wa chama chao. Viongozi wetu wa wilaya ndio wa kwanza kukamatwa na kushtakiwa.
Jadweli No. 5: Waliokamatwa na kushtakiwa LIndi
|
S/No.
|
JINA
|
WADHIFA
|
MAELEZO
|
|
1
|
Mhe. Moh’d Mussa Barwan
|
Mwenyekiti wa CUF wilaya
|
Shitaka la kuandamana
|
|
2
|
Mhe. Abubakar Twahir
|
Katibu wa CUF wilaya
|
Shitaka la kuandamana
|
7.3.5 Maandamano Bunda
Bunda haikuwa nyuma kwa maandamano. Huko wanachama walichachamaa na kuhamasika kikweli kweli kama kawaida ya dola, waliwakamata viongozi wetu mashuhuri na kuwapeleka mahakamani.
Jadweli No. 6: Waliokamatwa na kushtakiwa Bunda
|
S/No.
|
JINA
|
WADHIFA
|
MAELEZO
|
|
1
|
Mhe. Ernest Binna
|
Katibu wa wilaya
|
Shitaka la kuandamana
|
|
2
|
Mhe. Manyama Makunja
|
Mkurugenzi Vijana CUF wilaya
|
Shitaka la kuandamana
|
|
3
|
Mhe. Kukiko Maginda
|
Mwanachama
|
Shitaka la kuandamana
|
7.3.6 Maandamano wilaya ya Kaskazini B
Wanachama wa Kaskazini B, Unguja nao walijitokeza kuandamana kuunga mkono kauli na wito wa Chama chao.
Jadweli No. 7: Waliokamatwa na kushtakiwa katika maandamano ya wilaya Kakazini B
|
S/No.
|
JINA
|
WADHIFA
|
MAELEZO
|
|
1
|
Ramadhan Ali
|
Mwenyekiti wa wilaya
|
Kuandamana
|
|
2
|
Abdi Salum Ali
|
Katibu wa wilaya
|
Kuandamana
|
|
3
|
Ali Haji Ali
|
Kiongozi
|
Kuandamana
|
|
4
|
Ali Abdi Ali
|
Kiongozi
|
Kuandamana
|
|
5
|
Moh’d Kombo
|
Kiongozi
|
kuandamana
|
7.3.7 Maandamano wilaya ya Kati
Polisi wakiwa na magari ya dereva walifika vijijini na kumkamata Mheshimiwa Ali Khamis Ali ambae alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na viongozi wengine wa CHama katika wilaya
Viongozi hao waliotajwa walipokamatwa walipelekwa na kufunguliwa kesi katika kituo cha Polisi cha Mahonda. Kama kawaida ya Polisi wetu, utaratibu wa kisheria wa kimahakama ukavunjwa hali iliyopelekea kupata usumbufu mkubwa hapo kituoni. Baada ya wiki moja watuhumiwa waliachiliwa bila ya kufunguliwa shitaka lolote. Ilikusudiwa tu polisi wapitishe ada yao ya kuendeleza uvunjwaji wa Haki za Binadamu kwa kuwakamata watu bila kosa na kuwarundika rumande.
7.3.8 Maandamano Mjini Unguja
Wanachama wetu na wapenzi wakajitokeza kwa wingi sana kuitikia wito wa chama chao na walielekea pale palipotayarishwa kwa kuanzia maandamano. Kawaida hua tunaanzia kwa Biziredi. Pamoja na Polisi kuweka udhibiti mkubwa pamoja na vizuizi vingi vya njiani, takriban mji mzima, bado watu walimiminika kama kawaida ya mikutano yetu. Palikuwa na vikosi vya CCM. Polisi, FFU, KMKM, Askari Magereza, JKU pamoja na vikosi maalim vya Volantia na Umawa. Wakiwa na bunduki, mawe na mapanga walikuwa wakiyashambulia makundi ya watu ambao walikuwa wakielekea kwenye maandamano ambai wamejifunga vitambaa vyeupe wakionesha ishara ya amani. Hata hivyo, hawakujali ishara ile ya kitambaa cheupe na waliendelea kuwasakama wanachama wetu kwa kila aina ya adhabu.
Hapo ndipo vurugu lilipoanzia na vurumai lilikuwa kubwa kwani makundi ya askari yalizidi kumiminika na kutesa kwa zamu kwa mashirikiano mazuri. Waliwarushia risasi wanachama wetu ambao walikuwa hawana cha kujibu isipokuwa kurudi nyuma na kukimbia. Baadhi ya njia na maeneo muhimu ya kuelekea Biziredi kama vile Mfereji wa wima baina ya Mwembe mamba na Hospitali ya Utapoa iliopo Mikunguni palikuwa na makundi makubwa ya Polisi waliokuwa wakiwashambulia wa nguvu sana wanachama wetu na katika eneo hilo wanachama wetu wawili walikufa hapo hapo na huku watu wengi walijeruhiwa kwa risasi. Baadae maiti hizo zilipelekwa Hospitali ya Mnazi mmoja.
Baada ya wanachama wetu kwa maelfu kuona kuwa hujuma hizo zilikuwa zikiongezeka, huku vifo vikianza kutokea na udhibiti wa askari ukizidi wanachama wetu walibadili mwelekeo na kubuni njia za kuyaendeleza maandamano hayo bina ya kupafikia pale ilipoamuliwa awali, yaani kwa Bizeredi. Maelfu ya wanachama wetu walifanikisha pale walipoandamana katika njia kuu ya Daraja Bovu na kwa huku mjini wengi wao walijikusanya Mtendeni Makao Makuu ya CUF na kuelekea Darajani ili kwenda katika viwanja vya Mkutano vya Malindi. Lakini hii pia haikusaidi kwani huku wakiandamana kwa amanni na mabango yenye kuonyesha malalamiko yao, Polisi waliwatawanya waandamanaji wetu kwa risasi za moto na hapo hapo walimuua Mwanachama wetu mmoja kwa kumpiga risasi ya kichwa. Huyu akiitwa Mwalim Nassor. Huyo ndie shahidi mkuu kwani ndie alieshikilia bango la maandamano wakati akiuliwa.
Baada ya mwanachama huyu kufa hapo hapo, wengi wengine walijeruhiwa hali ambayo ilileta fadhaa kubwa kwa wananchi walioshiriki katika maandamano na raia wengine wanaoishi maeneo ya karibu. Huku fadhaa ikizidi, polisi walizidisha risasi za moto na za machozi na idadi ya majeruhi ilikuwa kubwa sana. Askari walipoona watu wengi walikwisha changanyika walichukuwa hatua ya kupitisha mabomu ya machozi ndani ya majumba. Walisahau kwamba ndani ya majumba walikuwemo pia watoto wachanga, watoto wadogo, kinamama waja wazito na vikongwe wa kike na wa kiume na wagonjwa wa maradhi mbali mbali. Na kwa kuwa hujuma za raia zilifanywa hata kwa raia ambao hawakuwa katika maandamano, hili nalo linatoa ushahidi kwamba CCM iliwatumia askari kufanya unyama mkubwa na uvunjaji wa haki za binaadamu kwa raia walio huru katika nchi yao kwa kisingizio tu cha siasa. Na hapa wengi wanajiuliza, jee hawa ni askari wa Taifa hili hili au ni majeshi ya uvamizi. Watu wengi waliathirika sana na kupata maumivu makali na afya zao kudhoofishwa na wengi walipoteza nuru ya macho kwa mabomu. Katika Mkoa wa mjini waliojeruhiwa ni wengi sana kiasi kwamba hatukuandika majina makusudi ili kuepusha kuwaacha baadhi yao. Tulisikia idadi ya waliojeruhiwa vibaya sana kufikia 3600. tunawashukuru wote waliofanikisha huduma kwa majeruhi.
Tulikuwa kabla ya hapo tuna kituo cha huduma za Afya chini ya usimamizi wa Dr. Juma Ameir Muchi na wasaidizi wake Bw. Nassor Khalid na madaktari wengine kadhaa. Wote tuliwashukuru na tunaendelea kuwashukuru sana kwa kutoa msaada usiosahaulika katika maisha ya kisiasa Zanzibar, ingawa kwa ujumla tunaishukuru Kurugenzi nzima ya haki za Binaadamu ya CUF chini ya Mkurugenzi Mheshimiwa Hamad Masoud Hamad na Naibu wake Mhehimiwa Lyanga kwa mashirikiano na kazi nzuri licha ya kutokwa na nyenzo.
Hospitali ya Serikali ya Mnazi mmoja ilizuiwa isihudumie majeruhi. Tulilazimika kuwapeleka majeruhi lakini hawakuwa wakihudumiwa kwani haukuwa ukatili wa madaktari bali ulikuwa woga wa kupoteza kazi. Nao tunawashukuru kwani walihisi na mara nyengine kujali shida zetu, lakini dola ilijizatiti kukandamiza hadi mwisho. Ni vyema tu kufahamu kwamba wakati wote haya yanatendeka wasimamizi wakuu walikuwa ni Jeshi la Polisi na Inspector General Omar Mahita alikuwa juu akiranda na helkopta ya Afrika ya Kusini ili kusaidia kwa maangamizi pale ambapo palikuwa na upinzani. Kama tulivyosema hatukujitayarisha kwa fujo wala mapambano na kwa hivyo, hatukutoa upinzani wowote. Kabla ya kuelekea Pemba, sasa tunawauliza wasomaji jee hivi ndivyo ilivyofanywa katika machafuko ya Juni, 1961 chini ya utawala wa madhila wa kifalme? Jibu, hapana. Basi ingawa Mkoloni mbaya lakin CCM imekithiri kwa unyanyasaji.
Tukio jengine baya lilitokea katika maandamano ya Mjini Unguja ni pale askari Polisi walipokwenda katika nyumba ya Bwana Mtumwa Haji Mati wakuvunja mlango na kuingia ndani. Mule ndani waliwanyanyasa watoto wake na baadae wakampiga Mtumwa hasi akawa taabani. Hapo wakamchukua hadi rumande wakati anamwagika damu. Familia yake iliomba apelekwe hospitali, lakin polisi walimzidishia kipigo cha mbwa dume hadi akapoteza fahamu. Kutokana na hali hii mbaya, Mtumwa alifariki tarehe 16 Februari, 2001. aliacha vizuka wawili, Amina Khamis na Tatu Mosi pamoja na mayatima kumi na moja. Haji, Tama, Khamis, Khalfan, Shaib, Awadh, Ibrahim, maryam, Mwanaharusi, Hafsa na Husna. Kitendo alichofanyiwa Mati hakufanyiwa mtu siku za siasa za ukoloni.
Sehemu ya 4: Maandamano Pemba
Kwa maumbile ya kisiwa cha Pemba kijiografia, ni vigumu kuwashirikisha watu katika maandamano pahala pamoja hasa katika hali isiyokuwa ya kawaida. Maandamano kwa upande wa Pemba yalipangwa kimikoa iko kuepusha misururu mikubwa ya wanachama. Serikali ilikusudia tokea siku ya nyuma kuyafanya maandamano yetu kuwa si ya kawaida kwa kuwa walitangaza kuyazui. Kama tungekuwa na nia mbaya ya kufanya fujo na mauaji, basi tungewaita watu wote sehemu moja kupata wingi wa watu. Kwa kuwa hatukuwa na nia mbaya ndio maana iliamuliwa kuwa kwa Kaskazini maandamano yafanyike Wete na Micheweni, na kwa Mkoa wa Kusini basi wilaya ya Mkoani ijiunge na wilaya ya Chake chake kwa maandamano yaliyopangwa kuanzia Machomane Chae chake hadi viwanja vya Tibirinzi. Wilaya zote zilikamilisha lengo kama walivyopangiwa na kwa kweli maandamano hayo yaliitikiwa kikweli kweli licha ya mauaji yaliokwisha tokea Dar es Salaam na Zanzibar. Wanachama wetu walipata habari mapema kupitia Radio za BBC na Ujerumani pamoja na utaratibu wetu wa ndani wa mtandao maarufu wa „Radio Kifua“. Pamoja na hayo hatukushituka wala kuogopa.
Kama tulivyosema awali jiografia ya Kisiwa cha Pemba ni ya aina yake kwa Zanzibar, kwani kule kazi ya Polisi kuzuia watu huwa rahisi kwani bara ipitayo magari ni moja tu kuingia kila mji wa wilaya. Katika hali kama hiyo, waandamanaji nao walipata shida kubwa ya kujikusanya kwa vile kila njia kubwa ilikuwa na vikwazo zaid ya vitatu. Hata ukisema upite maporini ili kuwepa askari basi ukizukia juu unakutan kikwazo chengine. Hali hii ni mbaya zaidi kwa wilaya ya Mkoani hasa kwa majimbo ya Mkoani, Mkanyageni na Mtambile. Hata hivyo, pamoja na yote hayo wananchi walijitokeza kwa maelfu kutoka kila jimbo kwa nia ya kuandamana kwa amani. Kabla hatujatoa tathmini ya kila wilaya basi kuna msanii katuomba tufupishe yaliyotokea kwa beti hizi za ushairi wa kuhuzunisha sana.
7.4.1 Shairi
Ilienea maafa jamii Pemba nzima
Watu wengi walikufa Baba na akina mama
Hapakua takhfifa bali yekuwa nakama
Kieleacho huzama kizamacho kikazuka
Kizamacho kikazuka kieleacho huzama
Na kile kilo anguka baadaye husimama
Si kazi kubadilika mabaya yakawa mema
Kieleacho huzama kizamacho kikazuka
Wingwi hadi Micheweni ilikithiri nakama
Ilikuwa tafrani hapakuwa na salama
Basi Wete Utaaani wakipigwa kama Kima
Kieleacho huzama kizamacho kikazuka
Mkanjuni na Madungu kulikuwa kukivuma
Watu kupigwa marungu na risasi iko nyuma
Hukumu iko kwa Mungu Ghafuru ndiye Rahima
Kieleacho huzama kizamacho kikazuka
Akikujia Polisi huna pumzi wahema
Aifyatua risasi na bebeti akuchoma
Katu hupati nafasi utapigwa kama ngoma
Kieleacho huzama kizamacho kikazuka
Dola iliiingia hofu aibu hata kusema
Dola kubwa maarufu kwenda pigana na chama
Dola haikusadifu kwa dalili ishakwama
Kieleacho huzama kizamacho kikazuka
Kweli ilipodhihiri wakubwa wengia homa
Wenyeviti Zanzibari wakataraji ujima
Wakakodi maayari kutoka Dar es salaam
Kieleacho huzama kizamacho kikazuka
Watu wakidhalilishwa na kuvunjiwa heshima
Pigo na kuhangaishwa hashimna Mahshuma
Baadaye kufikishwa korti kwenye mahakama
Kieleacho huzama kizamacho kikazuka
Kidogo nitaeleza kuficha kweli si vyema
Wala sitayanyamaza nitayasema daima
Kubwa lilojitokeza ni chuki na uhasama
Kieleacho huzama kizamacho kikazuka
Alohai duniani ajue kuna kiama
Alofika kaburini na hesabu iko nyuma
Moja kwa moja motoni kama hakufanya mema
Kieleacho huzama kizamacho kikazuka
Kila mtu ajijue asijione mzima
Uzima una mwishowe na tena una alama
Jepesi huwa ni jiwe laini huwa ni chuma
Kieleacho huzama kizamacho kikazuka
Mengineyi siyasemi hadi tamati wa tamma
Nafunga wangu ulimi nafika pakusimama
Kenda imekuwa kumi upepo sasa wavuma
Kieleacho huzama kizamachp kikazuka.
Kwa kuyapa mapana maelezo ya msanii huyu kuhusu mambo yalivyokuwa basi tunachukua nafasi kueleza kwa ufupi sana hali ya kila wilaya, Pemba
7.4.2 Wilaya ya Wete
Tokea usiku wa manane wa kuamkia mkesha wa maandamano askari walikwishaweka vikosi na vifaa vyao barabarani katika maeneo tofauti ambayo yangetokea watu kwa kuja kujikusanya palipo kusudiwa kuanzia maandamano. Katika eneo la Madenjani hadi Chwale ilikusudiwa kuwashambulia watu waliotoka Ole, Kangagani, Kiuyu, Kambini, Mchanga mdogo, Chwale, Kojani na Kiungoni. Humu walijua kuwa ndimo mwenye hazina ya wanachama wetu wengi. Kwa hivyo, askari hapa walikuwa wengi na wengine walioneka katika vichaka mbali na barabara wakiwa tayari kuchukuwa amri za kuua kutoka kwa wakubwa wao. Halikushitua wanachama wetu hili kwani Dar es Salaamu na Unguja walikwishaua na tulikuwa hatuwajui kwani walikuwa ndugu zetu kutoka Tanzania Bara, ingawa pia walikuwepo Wazanzibari tena wengine kutoka Pemba.
Kikosi cha pili kiliwekwa Limbani ili kushambulia watu waliotokea Kisiwani, Piki, Matuuni, Mzambarauni, Pandani, Machengwe na Tungamaa. Kikosi chengine kilikuwa Kizimbani kuwashambulia watu waliotokea Kizimbani, Kwale na Pandani. Na kikosi chengine kilikuwa Bopwe kushambulia watu waliotokea Gando, Junguni, Ukunjwi, Chanjaani Madaniwa na Raha. Hivyo, ni kusema kwamba Wilaya nzima ya Wete ilikwisha zungukwa na askari wakiwa katika mavazi ya kivita kabisa. Wakati wote tokea kuelezea taarifaa hii hatukuwataja kabisa Jeshi la Wananchi (JWTZ), lakin hapa sasa tunaanza kuwataja. Kwa wao kuingilia mwisho katika kisiwa cha Pemba, yawezekana fitna ilikuwa kali zaidi. Tulisema yaelekea walielezwa kwamba sisi tutakuwa na vita na pengine tutakuwa na majeshi kutoa nchi za nje wakitusaidia. Hivi ndivyo viongozi wa CCM walivyo wakiwaambia wananchi kuwa sisi tunatumiliwa na watu wa nje.
Kwa Wete, mauaji yalianza Limbani ambapo waandamaji pamoja na kuwaona wenzao watatu wameshauliwa ghafla mbele yao, hawakurudi nyuma bali walizidisha mori na kusonga mbele kiasi ya kuwafanya askari wakimbie kidogo baada ya kumalizikiwa risasi. Baadae waliongezwa askari waliofika kwa magari baada ya kuwasiliana na kuomba msaada na vifaa. Hapa ndipo majeshi ya ulinzi nayo yalipoingilia na kuanza kuwashambulia raia bega kwa bega na Polisi. Huku yakitokea haya ardhini, angani helikopta ilikuwa ikiranda na kunyesha „mvua ya risasi“. Baada ya muda Polisi waliweza kuwakimbiza misituni kundi la waandamanaji waliotokea upande wa Limbani kuja kuungana na wenzao wa Mjini.
Kwa kuwa hatukuwa na silaha yoyote basi hapakuwa na askari alieshambuliwa na kujeruhiwa au kuuwawa, kama ilivyothibitishwa na Serikali zote mbili kwamba walipoteza askari mmoja tu aliekufa kwa kuchinjwa. Pamoja na taarifa hii CUF inakanusha kwa nguvu zote kwamba haikuhusika na kifo cha huyo askari mmoja iwapo alikufa kweli. Maandamano yetu yalitangazwa na vyombo vyote kwamba yalikuwa ya amani na ndio maana isingestahiki kwa waandamanaji kuwa na silaha. Matukio matatu ya kushtusha yalitokea hapo katika mauaji ya Wete. Kwanza, baada ya watu wote kukimbia, askari walikuwa wakipita kila nyumba na kupiga risasi madirishani. Katika mbinu hii ya kivita waliofundishwa, bila shaka nchi za ng’ambo, walipita kwenye nyumba moja na kumuona kijana ambae alikuwa kaketi barazani akipumzika. Bila kumuuliza walimfyatulia risasi na kumkata roho hapo hapo. Huyu ni kijana Salum Masoud Al – Miskry ambae alifika Pemba wiki moja kuangalia wazee wake akitokea Sweeden ambako anaishi tokea mwaka 1985.
Pili, askari walikwenda kwenye nyumba nyengine na kuwaona watu wakiosha maiti na kuwakung’uta risasi na wawili wakafa na maiti wao. Kilichostaajabisha ni kwamba walipiga „radio call“ na papo hapo gari ikafika na kupakia maiti, na hatujaziona hadi hii leo. Tukio la tatu ni kule kumpiga mama mmoja ambae alikuwa migombani kajilaza ili askari wapite wasimuone na baadae akimbie. Huyu walimpiga risasi ya matako hakufa lakini ilichana kuanzia nyuma hadi mbele ya sehemu zake za siri. Na kwa CCM, huku ndiko kuwapenda wanawake. Kwa ujumla basi takwimu sahihi ya maiti waliowashuhudia wao tu ni 26 kwa Wete. Wako waliopigwa na helkopta na kufa, lakini hawa walikuwa misituni wakikimbia mauti, ingawa huko Mahita aliwafuta. Mji ulizizima na waliokuwa na kamandi ni askari ambao walikuwa wakipita kila kona ya mji na kuchukua na kamandi ni askari ambao na watu waliokuwa wakichunguza kwa makini mwenendo wa askari hao watii kwa CCM na Dola lakini makatili kwa raia wasio na hatia.
Wananchi watakumbuka kwamba mara tu baada ya aliekuwa Mwenyekiti wetu wa mwanzo, mkongwe wa siasa Mapalala kukiasi chama chetu alitumiwa na dola kubuni na kusambaza uongo kwamba Libya inatusaidia kupanga njama za kumpingua Dr. Salmini. Basi yawezekana usalama wa Taifa waliishauri Serikali vibaya na kuwaona Wapemba wanahitaji kushughulikiwa zaidi. Vile vile Pemba ilishughulikiwa sana kuliko sehemu nyengine kwani tumeshaona mpishi wa historia, Profesa Mmuya alivyosema, it is conceded by CUF leaders and the members a like that Pemba is the preasure centre and the rest are action zones, [Mmuya, 1998:37]. Maana yake ni kwamba, inachukuliwa na viongozi wa CUF pamoja na wanachama kwamba, Pemba ndipo pahala pa shindikizo na sehemu nyengine hufuata tu kwa vitendo. Kwa kuwa vitendo vya unyanyasaji na mauaji (vya Polisi) vilianzia unguja na Dar es salaam tarehe 26 Januari kabla ya Pemba, basi hapa unaonekana uongo na fitna za kifalsafa ambazo husinginiziwa historia. Ingetarajiwa pale pahala pa shindikizo ndipo kungekuwa mwanzo wa matukio hayo ya kutisha kama yanavyotabiriwa na mchunguzi aitwae Profesa.
7.4.3 Wilaya ya Micheweni
Askari waliweka kizuizi kimoja tu kabla ya kufikia kituo cha Polisi cha Wilaya. Kizuizi kilikuwa Kilindini kwenye mpaka wa Micheweni na Konde, katikati ya msitu wa Micheweni katiya njia inayotoka Mjin Wingwi na kwenda kituo cha polisi, kizuizi kikubwa kiliwekwa mita 10 kutoka kituo cha polisi. Na hapo ndipo walipouliwa watu wengi. Baada ya kutoa amri Mkuu wa Wilaya Ramadhan Juma Shaibu ambae pia yeye mwenyewe ni Ofisi wa Polisi. Kwa kawaida Wakuu wa Wilaya na Mikoa ni Majeshi, Polisi na Usalama. Hizi ndizo nafasi walizotengewa na Baba wa Taifa. Kwanza majeshi yalikuwa katika siasa wazi wazi kwa muda wote wa kipindi cha mfumo wa chama kimoja. Baada ya Tume ya Nyalali kupendekeza kuwatoa katika siasa, basi shea yao ya uongozi iliongezwa katika Mikoa na Wilaya ingawa pia wanaweza kuwa Wabunge.
Kwa hivyo, maendeleo ya Mkoa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na ikaonekana kuwa na viongozi walio malinza ni bora kwa kuimarisha ulinzi na usalama. Hii ndio maana basi majeshi wengi (kama si wote) ni wanasiasa kuliko hata Wabunge wengine, na ndio sababu wanashindwa kuwa waadilifu wa kazi zao, kwa kuwa maadaili ya kiulinzi yamechanganywa na siasa. Hivyo basi ukali wao wa kuvita huanzia kufanya mazoezi juu ya migongo ya Wazanzibari, hasa Wapemba; maana ndivyo wanavyo ambiwa asubuhi na jioni na hata na Amiri Jeshi mwenyewe kwamba Wapemba ni maadui na hawaitakii mema nchi hii. Kwa hivyo, askari hawakufanya kosa, walikuwa wakitekeleza “amri halalli” ambayo huanzia kwenye Kamati ya Ulinzi chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri, Mheshimiwa Ben Mkapa.
Tukirudi basi, katika mfululizo ule wa risasi ulitokea pale penye kizuizi cha kwanza jumla ya watu 10 walikufa kufumba na kufumbua. Mkimbizi mmoja alieleza kamsikia Ramadhani, Mkuu wa wilaya ya Michweni, akisema “mwasubiri nini kama hamjaua”. Na kule Wete pia kulikuwa na Mkuu wa wilaya akiitwa hivyo hivyo Ramadhan lakini baba yake ni Feruzi. Huyu ndie alietoa amri kwa askari ambae alimuua Shahidi wa kwanza wa demokrasia marehemu Omar Ali wa Shumba Mjini mwaka 1992, wakati akipachika bendera ya kwanza ya CUF Kaskazini. Baada ya kufanya kazi zao vizuri, Ramadhan wote wawili sasa wamepimzishwa kazi ya Ukuu wa Wilaya kama kawaida yao hawaachishwi ila hupewa uhamisho na kurudia kazi zao za ulinzi. Baadhi ya askari wa Zanzibar ambao walilazimishwa kuuwa na wakauwa baba na mama wa wenzao, hawa wamechukuliwa na kufichwa Bara. Yule alieuwa vizuri zaidi yuko Arusha kwenye mandhari safi ya hewa baridi.
Alipokalia kiti Bwana Amani Karume, aliamua kuwabakisha kazini Wakuu wote wa Wilaya lakin baada ya kama miezi sita hivi Ramadhan wote wawili akawaondoa. Hii ni hukumu ya kimya kimya kwa zile wilaya zilizouwa kupita kiasi lakini alie akisimamia mauaji Mahita, tunaambiwa na Mbita tumsamehe. Hii ni dhihaka, na iwapo hili litekelezwe Tanzania basi lianzie kwenye Mahkama ya Kimataifa ya Mauaji Rwanda na Burundi kule Arusha ili iwe mfano sio tu kwa Zanzibar lakin kwa Afrika nzima. Tunawaka Watanzania waelewe kwamba huu tunaoueleza leo ndio ukweli na ukweli unauma lakini haumi kuliko risasi zilizoondosha ndugu zetu. Jambo moja la kuhuzunisha hapa Wilaya ya Micheweni lilitokea kama ilivyokuwa kule Wete. Msitu wa Maziwa Ng’ombe ulikuwa na sehemu chafu kupitika. Hapa palipotea watu wengi. Helkopta ilikuwa ikiwamwagia risasi watu waliokuwa wakikimbia ovyo kujisalimisha. Wengi waliokuwa wakipita sehemu chafu ni wale watu wa vijiji jirani wasio na uzoefu wa sehemu hizi.
Baada ya helkopta kuona kwamba hakukuwa na watu wengi tena barabarani na misituni, bosi alishuka Wapemba waliokwisha kata roho. Pia walioondosha maiti na sisi hatukujua wapi walienda nazo. Tulizungumza hapo awali kuwa kulikuwa na kaburi la siri lakin Serikali haikutaka awali pafanyike uchunguzi kwani wakati ule siri ingefichuka. Sisi hatumshangai Mbita kwa kusema hakuona makaburi ya halaiki, huu si utamaduni wao CCM. Na kwa kweli haitafika siku CCM na Serikali zikaungama kukubali kuwa Zanzibar kuna makaburi ya halaiki na siri, hadi pale siku watakapoonesha makaburi ya akina Kassim Hanga wenziwe. Jee haya hayako, na iwapo haya hayako wao wako wapi?
Hivi ndivyo CCM inavyowapoteza Wazanzibari, na ndio maaana halisi ya “Mapinduzi Daima”. Ilikadiriwa basi, baada ya wale 11 wa uhakika, wapo wengine kama 31 walihofiwa ama kufa au kupotea. Hesabu hii ilipatika wiki moja hivi baada ya kuendesha sensa ya siri katika wilaya nzima. Na iwapo kuna Mtanzania anasema CUF inatia chumvi au uchochezi (kwa maana hizi ndizo lugha za CCM wakificha madhambi yao) basi wailaumu taarifa ya Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu la Human Right Watch ambayo ilitoa matokeo ya uchunguzi wake mara tu baada ya mauaji. Taarifa hiyo iko katika nyaraka mbalimbali zinazotunzwa na chama.
7.4.4 Wilaya ya Chake chake
Chake chake kulikuwa na vizuizi vitano. Kizuizi cha kwanza kiliwekwa Mkanjuni ili kuwazuia watu waliotokea Ziwani, Kidemeni, Mchanga wa Kwale, Semewani, Mavungwa, mbuzini, Niyapi, Kwale, Gombani, Ng’ambwa na Mkoroshoni. Kizuizi cha pili kiliwekwa Machomane ili kuwazuia watu waliotokea Vitongojji, Wawi, mgogoni, Furaha, Mvumoni, Pujini na Vikunguni. Kizuizi cha tatu kiliwekwa Shamiani ili kuwazuia watu ambao wangetoka sehemu za Mkoani ili kuja kujiunga na wenzao kwa kujipanga Mkanjuni na kuelekea Tibirinzi. Vile vile kulikuwa na kizuizi kwenye makutano ya barabara itokayo Vitongoji na Mgogoni ili kuwazuia awote ambao wangetoka Pujini, Mtangani na Chambani. Kulikuwa na kikosi cha askari polisi na jeshi katika sehemu za Chanjaani kuzuia watu ambao wangetoka sehemu za Chanjamjawiri na kuendelea.
Pamoja na askari kutumia silaha na nguvu za kupita kiasi ili kuwadhuru wanaandamanaji, lakini watu hawakurudi nyuma waliendelea kusonga mbele. Polisi waliposhindwa kuwazuia waandamanaji waliomba msaada kwa kambi ya Jeshi ya Vitongoji na mara tukawaona Polisi, FFU na JWTZ wakiwa sambamba na kuanza kupiga risasi za moto. Kama kkawaida, juu kulikuwa na helkopta ikipita hadi karibu ya mabonde ya nyuma ya nyumba za Serikali za machomane. Juu ya majumba hayo kulikuwa na askari ambao walitoa mawasiliano moja kwa moja kwa askari popote katika Mji wa Chake, hasa kwa vile ukikaa juu ya nyumba zile unaona karibu mji mzima. Mara moja Helkopta ilikuja karibu sana na mava yaliopo kwenye kituo cha mafuta cha Sahrif Kassim. Askari walitoka mlangoni na kutengeneza bunduki ili wapige lakkini halafu ikaruka biila kuangusha risasi plae.
Watu waliokuwepo kwenye mava mara wakasikia risasi. Wakatikiri ni za machozi wakataka kutoka mavani kuelekea Tibirinzi moja kwa moja. Walikuwepo vijana waliokuwa wakijua milio ya risasi na hawa wakawazuia wenzao wasitoke. Mra tukasikia mamaangu wee! Mtume! Mara kimya, watu wameingia misituni, lakini wengine walikwisha kufa zamani. Pale vurumai jengine lilitokea sehemu za misituni kukimbia helkopta na Polis wakawakurupusha ili warudi kule kule na hapo watu wengi walipigwa risasi wakafa na wengine kujeruhiwa. Taarifa ya wilaya ilionesha kwamba Chake chake walikufa watu 13 na wengine wengi walijeruhiwa. Kuanzia hapo watu walianza kutawanyika na baada ya kusafika hapo ndio askari wakajikumbusha shughuli ya kimapinduzim kubaki wanawake na watoto wao tena mbele ya waume zao. Askari walishangaza sana kwani watu wengi waliokuja kwa maandamano walitoka sehemu mbali mbali, na Machomane walikutana tu. Hata hivyo baada ya watu kukimbia ghadhabu za askari walizitoa pale Machomane.
7.4.5 Wilaya ya Mkoani
Kama tulivyosema awali wanachama wa wilaya ya Mkoani walitakiwa wafike Chake kujiunga na wenzao wa kule na kuendelea na maandamano. Hali ya kijiografia ndio iliowafanya watu wengi wa Mkoani kutoweza kufika Chake. Ili watu wa Mkoani wafike Chake, ni lazima kutumia usafiri wa magari. Kwa kuwa huwezi kufika Chake bila kupita Mtambile ambako kuna kituo cha Polisi, hii iliwafanya watu wengi wasifike. Hata hivyo, wako watu wengine walifika Chake kwa kupita maporini. Wengine walitueleza kwamba iliwalazimu kulala Chake chake ili kuwahi. Na ushahidi ni kwamba kuna orodha ndefu ya watu waliojeruhiwa na humo tuliona majina ya watu kutoka Kengeja, Kiwani na sehemu nyengine.
Hata hivyo, kwa kuwa mpango wa mauaji na kujeruhi ulikuwa umepangwa tayari na CCM na dola yake, basi watu wa wilaya ya Mkoani hawakukwepa virungu ingawa hawakuuliwa hata mmoja. Siku ya pili yake, wakati hakuna tena dalili ya maandamano, askari waliweka vizuizi katika sehemu za Mtambile na Changaweni. Kwa Mtambile ndio waliambiwa kuwa hapo kulikuwa na Hizba na Shirazi, basi hapa waliwaandama watu wenye ndevu na kuwavuta. Ilikuwa akipita mtu mwenye ndevu anaitwa Sefu; huyu anavutwa chini na juu, lakini ukiwa huna ndevu unaitwa Mkapa; utasalimika. Iliendelea hivi kwa karibu wiki tatu. Watu wanashushwa kwenye magari na kupekuliwa hadi sehemu za siri, mke na muume bila kuchagua. Mzee mmoja licha ya kwamba walikuwa na vyama vilivyopinduliwa, lakiini hawakupata shida kama ya siku ile.
Wakati huku askari wananyanyasa hakukuwa na namna ila kupita na kuwapeleka wagonjwa hospitali kuu ya Mkoani. Kule watu wa Mkoani ndio waliokuwa na kazi kubwa ya kuwahudumia wagonjwa kwa kuwapatia chakula na madawa. Shukrani ziwaendee kwa kazi kubwa ya kusaidia chama. Hata Makao Makuu walifurahi sana kwani hakukuhitajika msaada mkubwa kutoka kule. Watu wenyewe wakiongozwa na kijana aitwae Meneja Asaa walifanya kazi hiyo ngumu.
Sehemu ya 5: Matokeo Baada ya Maandamano
Maafa ya mauaji na majeruhi yaliyotokea kwa wilaya zote zilizofanya maandamano ni makubwa. Idadi inayooneshwa ni ya wale waliopatikanwa kuzikwa na majeruhi kutibiwa. Itachukua muda mrefu kwa ulimwengu kupata idadi halisi na habari kamili ya vitendo vingine vya uvunjaju wa haki za binaadamu vilivyopitishwa na vyombo vya ulinzi, kama ambavyo Tume ya Mbita ilishindwa. Kuna habari walizotuletea wenzetu wa Dar kuwa wakati wa mauaji Zanzibar, manuwari ndogo za kijeshi ambazo hukaa Kigamboni ziliwahi kuteremsha masanduku ambayo yalifanana kama yale yanayotumiwa kwa kuchukulia maiti. Wao walifikiri kwamba nao askari walikufa wengi, lakini baada ya kusikia kuna askari mmoja tu kafa kwa mujibu wa taarrifa za Serikali, basi pengine hali hii inatoa dalili kwamba pengine zilikuwa maiti za Wazanzibar zilikimbizwa ili kukwepa ushahidi wa wazi. Huu ndio mtindo wa Zanzibar tokea Mapinduzi kwa ndugu na jamaa waliopotea. Tunadumisha mapinduzi kwa kazi kama hii iliyoanzishwa na wazee wetu.
Tatizo jengine kubwa tulilopata ni la wakimbizi. Kwa mara ya kwanza Tanzania ilijitia aibu kubwa ya kuwa na wakimbizi nje ya nchi makundi kwa makundi, hasa kutoka Zanzibar. Suala hili liliiweka Serikali njia panda na ndio maana lilifanywa kila liwezekanavyo, lakini suala la wakimbizi lisitokee. Katika kuhakikisha hili ndipo helkopta ilipotumiwa kuwaangamiza watu waliokuwa wakisafiria madau kwenye nchi ya jirani, Kenya. Bada ya kuzamisha jahazi moja taarifa zilienea nje na ndani na ndio wakasimamisha ukatili huu wa dhahiri. Kwenda Mombasa ilikuwa ni lazima kwani wagonjwa wengi walikoseshwa huduma kwenye hospitali za serikali na hakuna hospitali za binafsi kisiwani Pemba. Sisi tulikuwa na hofu kwamba kwa siasa za Afrika Mashariki, watawala wana tabia ya kusaidiana ili kuziweka tawala zao bila ya bughudha. Hii ndio maana, Tanzania na Kenya zilitiliana mkataba wa kubadilishana wakimbizi wakati wa jaribio la kuangusha serikali ya Tanzania miaka ya sabiini. Hata hivyo, wakimbizi wetu walipata mashirikiano mazuri kutoka kwa Serikali na wananchi wa Kenya. Tunalishukuru Shirika la Ukimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) kwa huduma nzuri, pamoja na matatizo madogo madogo ambayo yanavumilika.
Kwa ujumla idadi ya vifo na majeruhi kwa wilaya za Pemba ni kama itavyoonekana hapa chini, ingawa idadi hiii haikuweza kuwaingiza wale wanaohofiwa kufa kwenye mapori na wengine bahrini wakati wakielekea Mombasa kwa ukimbizi na matibabu. Kwa kweli suala la ukimbizi lilisababisha kutopata takwimu sahihi ya waliokufa, lakini vile vile, unyanyasaji wa karibu mwezi mzima baada ya mauaji ualisababisha mtu asiweze kufanya uchunguzi wa kina. Aidha katika mazingira haya, mtu angefikiriwa kakimbia kumbe ameshakufa. Taarifa zilizopatikana ni zile tu zilizoshuhudiwa na vijana wetu wa Blue Guards wakati wa kadhia hii. Vile vile kuna watu wengi waliokufa siku za baada ya marukio haya, lakini bado sababu ni zile zile za unyanyasaji wa majeshi kwa raia wao zilizotokana na matukio ya siku za mauaji. Pamoja na yote hayo majeshi yetu yalipora mali na vyakula kama ilivyokuwa siku za vita vya Ugandana Tanzania. Hatukutaja habari ya mali kwani roho na damu vilikuwa bora zaidi kutupotezea muda kuelezea kuliko mali.
7.5.1 Takwimu za maafa
Jadweli Na 8: Takwimu za maafa
|
Wilaya
|
Waliouliwa na kutambuliwa
|
Waliohofiwa kufa/kutooneka tena
|
Majeruhi
|
Vilema
|
|
Wete
|
16
|
13
|
109
|
37
|
|
* Micheweni
|
11
|
17
|
203
|
42
|
|
Chake
|
6
|
5
|
67
|
21
|
|
Mkoani
|
-
|
-
|
16
|
-
|
|
Unguja
|
10
|
-
|
178
|
35
|
|
**Bara
|
3
|
-
|
85
|
-
|
|
Jumla
|
46
|
35
|
658
|
135
|
• Micheweni kuna maiti mmoja hakutambuliwa na maiti mmoja (Mohd Amour) alikutwa ufukweni baada ya siku sita. Hii ilithibitisha kwamba wako watu wanaohofiwa kufa majini au katika mapori au katika mazingira ya kutatanisha.
** Wawili walikufa Bara, na mmoja (Mariam Kyango) alifia Mbeya baada ya kuondolewa Zanzibar akiwa taaban. Huyu ni wa tatu.
7.5.2 Majina ya Marehemu
Jadweli Na. 9: Majina ya marehemu
|
S/No.
|
MAREHEMU
|
WILAYA
|
|
1
|
Mjaka Salim Ali (Kiuyu)
|
Wete
|
|
2
|
Hassan Omar Hassan (Mtambwe)
|
Wete
|
|
3
|
Haji Kombo Ali (Mchanga Mdogo)
|
Wete
|
|
4
|
Said Abdalla Suleiman El Ruweihy
|
Wete
|
|
5
|
Ahmed Said Othman El Khaif
|
Wete
|
|
6
|
Kombo Ali Abdalla (Aliuliwa akienda shamba)
|
Wete
|
|
7
|
Salum Juma Salum (36, Chasasa; aliuliwa wakati akimuosha maiti Kombo Ali)
|
Wete
|
|
8
|
Moh’d Masoud Seif El Miskry
|
Wete
|
|
9
|
Juma Bakar Juma
|
Wete
|
|
10
|
Haji Muslim
|
Wete
|
|
11
|
Salum Masoud El Miskry (aliuliwa akiwa nyumbani akiangalia maandamano, alikuja kutoka Sweden ili kuoa)
|
Wete
|
|
12
|
Haji Kombo Ali
|
Wete
|
|
13
|
Abdalla Moh’d Salum El Mazrui
|
Wete
|
|
14
|
Abdalla Moh’d Abeid
|
Wete
|
|
15
|
Mjaka Ali Msonga
|
Wete
|
|
16
|
Ali Omar Kibabu (Mtambwe)
|
Wete
|
|
17
|
Mchande Saidi Mchande (35, Msuka)
|
Micheweni
|
|
18
|
Hemed Saidi Omar El Kindy (45, Wingwi)
|
Micheweni
|
|
19
|
Ali Juma Makame (40, Mjini Wingwi)
|
Micheweni
|
|
20
|
Abdalla Hamad Rajab (30, Kinyasini)
|
Micheweni
|
|
21
|
Khatib Omar Othman (30, Wingwi)
|
Micheweni
|
|
22
|
Haji Hassan Makame (30, Tumbe)
|
Micheweni
|
|
23
|
Moh’d Amour Salum El Khaif (26, Kinyasini)
|
Micheweni
|
|
24
|
Aliripotiwa na Polisi na hakutambuliwa jina
|
Micheweni
|
|
25
|
Mbarouk Kh. H (20, Wingwi)
|
Micheweni
|
|
26
|
Hemed S. Omar (36, Njuguni Wingwi)
|
Micheweni
|
|
27
|
Ali Haji Kombo (44,Mtoni)
|
Chake Chake
|
|
28
|
Malik Mbarouk Hamad (25, Mvumoni)
|
Chake Chake
|
|
29
|
Said Moh’d Kassim (30, Gombani)
|
Chake Chake
|
|
30
|
Habib Salim Kassim (30, Furaha)
|
Chake Chake
|
|
31
|
Ali Juma Ali (Machomane)
|
Chake Chake
|
|
32
|
Said Kombo Haji
|
Chake Chake
|
|
33
|
Ali Haji Mdungi (53, Magogoni)
|
Unguja
|
|
34
|
Mwalim Nassor Mwalim (31, M’kwerekwe)
|
Unguja
|
|
35
|
Abdalla Said Moh’d El Ghassany (37, Magomeni)
|
Unguja
|
|
36
|
Mtumwa Haji Mati (57, M’makumbi)
|
Unguja
|
|
37
|
Gharib Salim Hamad El Mindhir (26, Hurumzi)
|
Unguja
|
|
38
|
Kombo Rashid Ali (32, Daraja bovu)
|
Unguja
|
|
39
|
Hamad Said Hamad (58, Jang’ombe0
|
Unguja
|
|
40
|
Juma Khamis Moh’d (32, El Jahadhmy)
|
Unguja
|
|
41
|
Haji Ali
|
Unguja
|
|
42
|
Bakar Ali Hamad (25, Misufini, kafia mikononi mwa Polisi, Ng’ambo)
|
Unguja
|
|
43
|
Maryam Kyando (alikufa kijijini kwao Mbeya, baada ya kupigwa na Polisi, Zanzibar)
|
Mbeya
|
|
44
|
Jaffar Said (Kafa siku 2 baada ya kipigo)
|
Tanga
|
|
45
|
Laurenti Mayenjwa
|
Mwibara
|
7.5.3 Vizuka (wajane) na Mayatima
Ifuatayo chini ni idadi ya wanawake waliouliwa waume zao pamoja na mayatima wao:
Jadweli Na. 10: Waliouliwa Waume zao na mayatima
S/N MAREHEMU/KIZUKA WILAYA KIJIJI YATIMA
|
S/N
|
MAREHEMU/KIZUKA
|
WILAYA
|
KIJIJI
|
YATIMA
|
|
1
|
Ustadh Juma khamis Mohammed/Biubwa
|
Mjini
|
Mkamasini
|
Hana
|
|
2
|
Ali Juma Makame/ Fatma K. Makame na Mwanakhamis
|
Micheweni
|
Mjini/Wingwi
|
Mwamize A. Juma (16), Sharif A. Juma (13), Salim A. Juma (miezi 4), Hadiya A. Juma (5)
|
|
3
|
Kombo Rashid Ali/Time Khamis na Amina Said
|
Micheweni
|
Micheweni
|
Rashid k. Rashid (7) Time K. Rashid (5), Asha K. Rashid (2), Zawadi K. Rashid (3)
|
|
4
|
Abdalla Hamad Rajab/ Asha M. Omar na Bitumu A. Moh’d
|
Micheweni
|
Kinyasini
|
Hassan A. Hamad (miezi 6), Pili A. Hamad (7), halima A. Hamad (6), Time A. Hamad (2)
|
|
5
|
Hemed Said Omar/Maryam A. Omar na Maram A. Nassor
|
Micheweni
|
Wingwi
|
Sada H. Said (14), Mboga H. Said (8), Salama H. Said (12), Juma H. Said (15), Wardat H. Said (7)
|
|
6
|
Khatib Omar Othman/ Mwajuma Shaaban
|
Micheweni
|
Wingwi
|
Khadija Khatib Omar (3), Sabra Khatib Omar (1)
|
|
7
|
Hamad Said Hamad/ Salma O. Mbwana
|
Mjini
|
Jang’ombe
|
Hussein H. Said (17), Fatma H. Said (6), Hafsa H. Said (4)
|
|
8
|
Mtumwa Haji Matti/ Amina Kh. Shaaban na Tatu Mosi
|
Mjini
|
Mwembe Makumbi
|
Khalfan M. Haji (13), Abdulwahid M. Haji (7), Shaib M. Haji (10), Hafsa m. Haji(3), Husna M. Haji (3), Mwanaharusi M. haji (10), Ibrahim M. Haji (7).
|
|
9
|
Abdalla Said Moh’d/Fatma Aman Hamad
|
Mjini – Unguja
|
Magomeni
|
Nasra A. Said (13), said A. Said (11), Latifa A. Said (10), Khadija A. Said (7), Ali A. Said (5), Kauthar A. Said (3), Safia a. Said (1), fadhila A. Said (2)
|
|
10
|
Mwalim Nassor Suleiman/Rukayya Abdalla
|
Mjini Unguja
|
M’kwerekwe
|
Nassor M. Nassor (2), Maryam M. Nassor (miezi 2)
|
|
11
|
Mjaka Salim Ali/Fatma Ali Hamad
|
Wete
|
Kiuyu
|
Hamad Mjaka Salim (10), Mwanaisha M. Salim (8), Ali M. Salim (7), Salim M. Salim (4), Rehema M. Slaim (miezi 3)
|
|
12
|
Salum Juma (Fundi)/Shufaa A. Moh’d
|
Wete
|
Chasasa
|
Juma S. Juma (11), Fatma S. Juma (9), Ahmed S. Juma (7)
|
|
13
|
Ahmed Said Othman/Khadija Ali Othman (Siti)
|
Wete
|
Mtemani
|
Rahma A. Said (17), Said A. Said (15), Aziza A. Said (13), Maryam A. Said (1)
|
|
14
|
Abdalla Moh’d Salim
|
Wete
|
Kizimbani
|
Walid A. Moh’d (8), Nasra A. Moh’d (7), nasria A. Moh’d (7)
|
|
15
|
Haji Kombo Ali/Fatma H. Moh’d
|
Wete
|
M’mdodo
|
Riziki Haji Kombo (16)
|
|
16
|
Ali Haji Kombo/Dalila Moh’d Ali
|
Chake chake
|
Shamiani
|
Maryam A. Haji (7), Seif A. Haji (8), Moh’d Ali Haji (12), salum A. Haji (10), Yahya A. Haji (14), Mustafa A. Haji (miezi 3)
|
|
17
|
Habibu Salum Khamis/Bimkubwa Moh’d Khamis
|
Chake chake
|
Furaha
|
Nasra Habib Salum (3), Husna H. Salum (2), Warda H. Salum (1), Haytham H. Salum (miezi 6)
|
|
18
|
Said Moh’d Kassim/Zuhura N. Humud
|
Chake chake
|
gombani
|
Nayrat Said Moh’d (3), Ahmed S. Moh’d (1)
|
|
19
|
Ali Haji Mdungi/Maryam Nyange na Maryam Said
|
Magharib Unguja
|
Magogoni
|
Issa A. Haji (13), Salum A. Haji (11), Mwajuma A. Haji (15), Khadija A. Haji (9), Said A. Haji (6), Mgeni A. Haji (2), Is – hak A. Haji (1)
|
Angalia: marehemu wasioorodheshwa hapa hawana au hawakuacha vizuka.
Katika stilahi, neno “Binaadamu” au “Mwanadamu” ni “tamyizi”, yaani upambanuzi au sifa ya kumtafautisha baina yake na viumbe wengine. Kwa maana hiyo binaadamu ni aina ya kiumbe – kiumbe mwanadamu kwa lugha nyengine “human being”. Na inapoondoka sifa hii ya ubinaadamu (humanity) ukabali neno “kiumbe” kwa lunga nyingine “being”, kiumbe hiki huwa hakina tafauti na vitendo vya viumbe wengine na hata mara nyengine kuzidi. Ni kwa kuikosa sifa hii ya ubinaadamu (humanity) yaani UTU kwa maana ya huruma kwa wengine, ndio katika jamii ya wanyama, mwenye nguvu ndiye mwenye haki na wa chini ndiye anamiwaye hata kama ndiye mwenye haki.
Katika jamii ya majibwa kwa mfano, yule mnyonge akionekana kaokota mfupa basi hupigwa na mwenye nguvu, na endapo atapiga mayowe ya kuomba msaada basi wakija wenye nguvu wengine na kumkuta chini akipigwa, basi wale wengine hawaulizi bali hujiamulia tu kuwa wa chini ndiye mkosa na kwa hivyo ndiye anamiwaye zaidi. Matendo ya Polisi waliyofanya Tanzania dhidi ya raia baada ya kuyavunja maandamano sio kwamba yalikosa kabisa ubinaadamu bali vilikuwa ni vitendo vya unyama wa jamii ya majibwa waliopata amri ya “Shike” kutoka kwa mambwana zao.
Bado tunasema mawili zaidi. Kwanza mauaji yaliitwa na chaguzi mbovu na sio historia. Pili na mwisho, maneno haya ya ukweli mtupu yatauma, lakini kwa vyovyote maumivu yake hayatafikia yake ya risasi zilizowapiga wazee, baba, mama na watoto wetu. Aidha maumivu ya maneno haya hayarafikia yale maumivu ya kunajisiwa wake na dada zetu kama mithili ya mnyama wa Serengeti. Sisi tunaendelea kuvumilia lakini kamwe hatusahau. Tunatarajia pia anaeguswa na maneno haya ya ukweli na yeye atavumilia. Ndivyo, tulivyo aswa na Tume ya Mbita kuwa tuvumiliane.
SURA YA NANE
Maoni