Vipi utaichangia CUF

13 10 2008

Mhe. Bwana/Bibi

KULETA MAGEUZI TANZANIA KUNAHITAJIA MCHANGO WAKO. CHANGIA ULICHONACHO UWE SEHEMU YA MABADILIKO

Katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja kuanzia sasa, tutaingia katika harakati za uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapo mwaka 2009 na katika kipindi kisichozidi miaka miwili Uchaguzi Mkuu wa Taifa hapo mwaka 2010. Kipindi hiki si muda mkubwa wa kujitayarisha kwa maandalizi ya chaguzi hizo, ambayo yanashirikisha – pamoja na mengine – kuwatayarisha mawakala wa kusimamia chaguzi na kununua vifaa vya kampeni.

Kutokana na uzoefu wa chaguzi tatu zilizopita, CUF haitegemei kwamba chaguzi za 2009 na 2010 zitakuwa huru, za wazi na za haki. Uzoefu huo unaonesha matumizi mabaya ya nguvu za dola dhidi ya raia wasio na hatia, uvunjwaji mkubwa wa haki za binaadamu na wizi wa kura, ambapo chama chetu hushindwa kuwahudumia waathirika kwa kukosa madawa na huduma za mawakili wanaowatetea kutokana na kesi za kubambikiziwa.

Ili kukabiliana na matukio hayo tusiyoyategemea na kufanikisha matayarisho ya chaguzi, CUF inahitajia shilingi za Kitanzania bilioni 8.4 (sawa na dola milioni 7 za Kimarekani). Kima hiki ni kikubwa kwa chama pekee kukipata, ndio maana CUF inahitaji msaada wa kila mpenda mabadiliko ya kidemokrasia, haki na maendeleo ya nchi yetu.

Tunakuomba mchango wako uingize katika Akaunti yetu:

Account Name: CUF Electoral Commission

Account Number: 011103008834

Bank Name: National Bank of Commerce, Corporate Branch – Dar es Salaam

Au:

Account Name: CUF Foreign Account

Account Number: 011105012592

Bank Name: National Bank of Commerce, Corporate Branch – Dar es Salaam

Swift Code of the Bank: NLCBTZT, XXXXX

Au:

Account Name: CUF – Tume ya Uchaguzi

Account Number: 021101003515

Bank Name: National Bank of Commerce, Zanzibar Branch

Kama mchango unatolewa kwa njia ya hundi, iandikwe:

i. Katibu Mkuu,

The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi)

P. O. Box 10797

Dar es Salaam.

Au:

ii. Katibu Mkuu

The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi)

P. O. Box 3637

Zanzibar.

Kwa fedha taslim au vifaa, tunaomba ujaze kima cha fedha au vifaa unavyokusudia kutoa katika fomu hii Tafadhali bonyeza hapa.

Tunatanguliza shukrani zetu za dhati.

.

JIKUMBUSHE USALITI WA CCM KWA WATANZANIA


Actions

Information

7 responses

16 10 2008
John

kwanini hamuendelezi website yenu? na kuja ktk Blogu? does it means CUF tunaowatarajia wawe madarakani hawajui tofauti ya Blog na official website? Website inakaa hadi porns….maana yake hakuna mtu wa kusimamia…?

CUF inashindwa nini kumlipa mtu alau lk 250 a month ajitolee kusimamia hata updates?

KWanini Gazeti lenu hamlisimamii? lina muda sasa halipo mtaani…Does it mean hamjui umuhimu au la? hamjui watanzania wangapi wana access ya mtandao?…Hivi mnataka watu waamini kuwa mpo serious kuchukua NCHI?..brothers u need to change…

6 11 2009
Bikinunji

Assalam alaykum!

Nami iungane na wewe juuya suali la kuwa na oficial webiste. Hizi habari za blog ni mambo ya mitaani. Tunataka kitu cha kuaminika. Zaidi sisi kama wanachama wa CUF ambao tuko mbali na nyumbani, tungependa kupata taarifa za kila siku za chama. Tuna Wawakilishi na Wabunge wetu, ni vyema na wao ama wakawa na webiste zao au kutumia ya makao makuu kwa kutowa taarifa kwa mambo wanayo fanya ndani ya majimbo yao na ndani ya Bunge au Baraza la Wawakilishi.

Sisi licha ya upofu wetu, tuliliona zamani hili tatizo la Daftari… Inshangaza kwa viongozi wa CUF licha ya kuwa wamekuwa pamoja na CCM tokewa wakiwa CCM na sasa hivi Wapizani, lakini bado wanashindwa kujiwa mbinu za CCM!

CCM hawaleti kitu bure bure, lazima huwa washajuwa kina manufaa kwao. Musitufanye tukawa hatuna imani na nyinyi kwa uzembe wenu!

12 11 2009
hakinaumma

Alaykum Salam Bikinunji,

Tunaupokea na kuuthamini sana mchango wako wa mawazo juu ya kuwa na website badala ya weblog. Lakini tukuhakikishie kwamba kwetu hadi sasa njia hii ya weblog imekuwa na manufaa zaidi kuliko website. Watembeleaji ni wengi na wanaotuma maoni kama wewe pia ni wengi sana kuliko hata tulipokuwa na website.

Hata hivyo, si kwamba tunadharau umuhimu wa website. Tunatarajia kuifufua ile tulokuwa nayo hivi karibuni na wakati huo tunaendelea na hii na weblog.

16 10 2008
John

Wenzenu Tanzania Daima la Chadema sasa income yake hadi 250million a month..where are u?

29 09 2009
zirppo

Nyinyi CUF wababaishaji tu, why there is no democracy only Seif na Lipum inamaana wengine wajinga au hawafai kuongoza?

29 09 2009
hakinaumma

Nani kasema kwamba CUF inaongozwa na Seif na Lipumba tu? Inaonekana kasumba ulizolishwa za ki-CCM ndizo tatizo. CUF ni taasisi na kila taasisi ina taratibu zake. Ni kama ilivyo hiyo yenu ya ZIRPP.

Kwani hakuna mwengine wa kuiongoza ZIRPP isipokuwa Muhammad Yussuf tu? Kwani ZIRPP ni Muhammad Yussuf na Muhammad Yussuf ni ZIRPP? Mbona kila mahala anaonekana na kutajwa yeye? Ukweli ni kuwa yeye ndiye kiongozi kwa sasa na lazima iwe hivyo. Sasa inashangaza nini inapokuwa kwa CUF?

Hakuna chama chochote chenye demokrasia ya ndani iliyokomaa kuliko CUF Tanzania hii. Tunaku-challenge ufanye utafiti ikiwa kweli unataka kuujua ukweli.

Uenezi na Mahusiano, CUF

30 10 2009
zirppo

Nilikuwa napitiapitia makala fulani katika Weblog yetu nikakuta taarifa hii inayoeleza jinsi ya kuichangia CUF. Nilipobonyeza hapo nikagundua matamshi yanayoonyesha kuwa yalitolewa na ZIRPPO; yaani Taasisi yetu, yanayoituhumu CUF kuwa ni “wababaishaji……” na kadhalika. Kusema kweli, nimeshangazwa sana na kauli hii kwa sababu haikutolewa na ZIRPP. Kwa mujibu wa katiba ya ZIRPP, Taasisi yetu haijafungamana na chama chochote kile cha kisiasa na kwa hivyo haiwezi kabisa kutoka kauli kama hiyo. Kwa hivyo, nimelazimika kuweka hili sawa kwa madhumuni ya kuondoa dhana yoyote ile iliyopo miongoni mwa viongozi na wafuasi wa CUF juu ya msimamo wa ZIRPP katika suala hili. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu kwa kunifahamu vyema. Muhammad Yussuf, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, ZIRPP.

Leave a comment