Waheshimiwa Wananchi,
Hii ni mara ya tatu kuteuliwa na Mkutano Mkuu wa Chama chetu kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) Niliamua kujaza fomu ya kuomba kuwa mgombea Urais kwa kuamini kuwa nina nia, sababu, na uwezo wa kutoa ushawishi kwa Watanzania kunichagua kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuunda serikali itakayopambana na saratani ya rushwa, kusimamia upatikanaji wa haki sawa kwa wananchi wote, kukuza uchumi utakaokuwa na manufaa na kuleta neema kwa wananchi wote, kuharakisha maendeleo yetu na kuondoa umasikini. Kama mnavyojua mzigo mzito hupewa Mnyamwezi. Read the rest of this entry »
Maoni