Kuyaendeleza Makundi Maalum kwa Lengo la Kunyanyua Maendeleo ya Jamii

18 09 2008

WANAWAKE

Wanawake wanafanya asilimia 51 ya idadi ya Watanzania. Hivyo, kuwawezesha wanawake kutapewa umbele na Serikali ya CUF.

 

Kasoro za Serikali ya CCM

  • Baada ya miaka ya 40 ya utawala uliopo madarakani, wanawake bado wako nyuma kwa kila hali.
  • Imeshindwa kuweka mfuko maalum kusaidia elimu ya juu kwa wanawake na kutetea hatua thabiti za kuongeza kuingizwa wanawake katika taasisi za masomo ya juu.
  • Kuna uwakilishi mdogo wa wanawake katika vyombo vyote vya kutoa maamuzi ikiwa ni pamoja na Baraza la Wawakilishi Read the rest of this entry »




Kutunza Afya za Wananchi Wetu na Kupambana na UKIMWI

18 09 2008

Afya ni haki ya msingi ya binaadamu. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilirithi mfumo wa huduma za afya imara 1964, Zanzibar ikijitegemea kwa madaftari, wauguzi na wahudumu wengine wa afya. Hivi sasa kuna upungufu mkubwa wa wafanyakazi waliopata mafunzo. Kwa sababu usimamizi mbaya wa wataalamu, fedha na vifaa, huduma za afya zinaporomoka mno. Read the rest of this entry »





Kukuza Kiwango cha Elimu kwa Kutoa Huduma za Uhakika katika Sekta ya Elimu

18 09 2008

Mara tu baada ya Mapinduzi ya 1964, Serikali ya CCM ilianza na sera ya kutoa elimu bure. Utekelezaji wake umekuwa wa mashaka makubwa kuanzia kipindi cha miaka ya 80 na 90 na hatimaye elimu bure kubadilishwa jina na kuitwa elimu bila malipo. Pamoja na marekebisho ya jina kukimbia aibu, watoto wamekuwa wakikaa chini, madarasa yamesheheni wanafunzi kuliko uwezo na kama hayo hayatoshi wameendelea kutakiwa kujinunulia vitabu vya kusomea na vya kuandikia. Mara nyingi hulazimika kutoa michango mbali mbali kwa huduma za skuli zao. Read the rest of this entry »





Kuwekeza katika Kuimarisha Huduma za Kiuchumi na Huduma za Kijamii

18 09 2008

ARDHI

Zanzibar ni nchi yenye ardhi finyu inayohitaji kulindwa, kuendelezwa na kutumiwa kwa uangalifu mkubwa sana.

 

Kasoro za Serikali ya CCM

  • Kuna mengi yanahitaji kufanywa juu ya kutumia ardhi, lakini Serikali ya CCM imeshindwa kuunda sera na mikakati yoyote ya maana. Matokeo yake ni matumizi mabaya ya ardhi na migogoro isiyokwisha.
  • Kwa miaka 41 ya utawala wake, Serikali ya CCM imeshindwa kutengeneza mpango madhubuti wa matumizi ya ardhi (land use plan). Matokeo ya hili, matumizi ya ardhi yamekuwa ni ya holela na ya kushitukiza.
  • Imeshindwa kufuata ‘master plan’ ya mji. Read the rest of this entry »




Kuendeleza Kilimo, Kuimarisha Uvuvi, Mifugo, Misitu na Kutunza Mazingira

18 09 2008

UKULIMA WA MAZAO

Kasoro za Serikali ya CCM

  • Katika miaka ya sitini Zanzibar ilikuwa inazalisha wastani wa tani 14,000 za karafuu kwa mwaka; sasa uzalishaji umeshuka mpaka wastani wa tani 4,000 kwa mwaka.
  • Serikali ya CCM imekuwa ikiwanyonya wakulima wa karafuu. Imefika hadi kuwalipa asilimia 7 ya bei ya zao hilo katika soko la dunia: wakoloni wa Kiingereza waliwahakikishia wakulima asilimia 65 ya bei. Read the rest of this entry »