
Pamoja na waandamaji kuonesha kila dalili ya amani, vyombo vya dola vilitumia nguvu kupita kiasi dhidi yao
The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi) kilikuwa na kila sababu ya kufanya maandamano yake Januari 27, 2001, na vyombo vya dola havikuwa na sababu yoyote ya kuwamiminia risasi waandamanaji wale walioandamana kwa amani. Hoja kuu, kuliko zote, inayoyafanya maandamano haya kuwa halali ni ukweli kwamba maandamano hayo yalikuwa yanalalamikia uharamu wa uchaguzi wa 2000: uendeshaji wake na matokeo yake. Kwa hivyo, maandamano haya yalikuwa haki na halali katika kiwango kile kile ambacho uchaguzi huo ulikuwa haramu na batili. Read the rest of this entry »




Maoni