“Sasa, mimi hapa natamka kwa mdomo mpana. Natamka asikie Pinda huko aliko, kwamba Zanzibar ilikuwa ni nchi, Zanzibar imekuwa ni nchi, Zanzibar ni nchi mpaka sasa hivi na Zanzibar itaendelea kuwa nchi mpaka yaumul-qiyama. Hapa mimi nimesimama kwenye jukwaa lililo kwenye ardhi ya nchi ya Zanzibar. Sasa kama kuna watu wanaona baya kwa hilo, kama wana uhasidi kwa hilo, watafisidika wao. Zanzibar itakuwepo milele na milele. Walikuwepo maadui wengi tu wa Zanzibar, lakini leo wako wapi? Wamepita. Na kila mbaya wa Zanzibar atakwenda na maji”
Msimamo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano uliotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwamba Zanzibar si nchi umewakasirisha Wazanzibari wote, ambao bila ya kujali itikadi zao za kisiasa, wametoka kweupeni kutangaza kupingana na kauli hiyo na kuitambulisha Zanzibar yao kwamba ni nchi. Ifuatayo ni hotuba ya Kiongozi anayechukuliwa na wengi ndani na nje ya chama chake kuwa alama ya ukombozi wa Zanzibar, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kwa Wazanzibari tarehe 16 Julai, 2008, ambapo aliuweka wazi msimamo wa Wazanzibari juu ya hili….. Read the rest of this entry »

Maoni