CCM imechoka, imechoka, imechoka

28 08 2008

Prof. Ibrahim Lipumba akizungumza katika Kongamano la Diamond Jubilee, Agosti 28, 2008

Prof. Ibrahim Lipumba akizungumza katika Kongamano la Diamond Jubilee, Agosti 28, 2008

Wakati nchi ikitumbukia katika majanga makubwa ya kitaifa kama vile migomo ya wafanyakazi, migogoro ya wanafunzi, mfumko wa bei, nyufa katika Muungano, uchumi dhaifu, ufisadi mkubwa, mgawanyiko mkubwa na kushindwa kwa Rais Jakaya Kikwete kuutatua mpasuko wa Zanzibar, Chama cha Wananchi (CUF) kinaona kwamba kuna haja ya lazima sasa kuliziba ombwe hili la kiuongozi. Hii hapa ni hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Mhe. Prof. Ibrahim Lipumba, katika Kongamano Maalum la Kujadili Ukosefu wa Uongozi na Hatima ya Tanzania, Ukumbi Wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, tarehe 28 Agosti, 2008 Read the rest of this entry »





CUF yainyooshea kidole SMZ kutumia vikosi vyake kisiasa

28 08 2008
Mhe Abdalla Juma Abdalla - Mwakilishi wa CUF Jimbo la Chonga

Mhe. Abdalla Juma Abdalla, CUF, Chonga

“…..Naomba niitumie fursa hii kuihadharisha SMZ kwa mara nyengine tena IACHE MARA MOJA mpango wake huo kwani sio tu unaidhalilisha DEMOKRASIA, lakini pia ni hatari, sio tu kwa wananchi wa jimbo la Chonga pekee lakini ni kwa Zanzibar nzima. Mimi, na kwa niaba ya Kambi ya Upinzanii, siko tayari hata siku moja kuona pesa za walipa kodi wa nchi hii zinateketezwa kwa kurundika vijana wa maskani katika makambi haya kwa ajili ya kuipigia kura CCM na kwa mantiki hiyo ni vyema tukaziba ufa kabla hatujalazimika kujenga ukuta.”

Hotuba ya Waziri Kivuli Wizara ya Nchi Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ. Mhe. Abdalla   Juma Abdalla kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2008/2009: aliyotoa kwa Niaba ya Kambi ya Upinzani katika Baraza la Wawakilishi Read the rest of this entry »