
Hamad Rashid Mohammed, Mbunge wa CUF na Kiongozi wa Upinzani Bungeni
“….baada ya utafiti huu, sasa tunaweza kusema ni katika mwenendo upi taifa letu linakwenda? Kama tunapoelekea ni pazuri au la? Ikichangiwa na kukosekana kwa Uongozi Ulio Makini, viashiria vya siasa huria ya nchi yetu inajikita katika mambo mengine makubwa, ambayo ni mapungufu ya Katiba, chaguzi mbovu pamoja na ufisadi na umasikini, ambavyo vimewanyima Watanzania ajira na ukuwaji wa uchumi unaofikia angalau asilimia 8%. Mustakabali wa taifa haujengwi kwa maneno mazuri, na tabasamu linalovutia bali ni kwa utendaji ulio makini na unaozingatia matatizo ya Mtanzania.”
Kutoka mada “Changamoto za siasa huria na mustakabali wa taifa-Tanzania: Maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni” iliyotolewa na Mhe. Hamad Rashid Mohammed (Mb), Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, kwa Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (Redet) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tarehe 20 Agosti, 2008 Read the rest of this entry »

Maoni