Ni wakati wa kuwa na jeshi la kisasa

18 08 2008
Mhe Masoud A Salim

Mhe Masoud A Salim

“Kambi ya Upinzani, inalitaka jeshi letu lifikirie kwa   kina namna ya kuongeza kasi ya kuleta mapinduzi ya maendeleo katika nchi yetu kama wanavyofanya wenzetu kwa ajili ya kunyanyua uchumi wa nchi zao jambo litakalosaidia kupatikana kwa fedha za kutosha kwa bajeti ya jeshi letu…Kambi ya Upinzani ilikwishashauri jinsi ya kupata vijana wenye vipaji maalum ambao tunaamini kama vipaji hivyo vikitumiwa vizuri jeshi letu litakuwa ndiyo hazina kubwa ya chimbuko la teknolojia mpya na rahisi kwa maendeleo ya watanzania. Jeshi waanze kuwatafuta vijana wenye vipaji tangu wakiwa mashuleni…”

Hotuba ya Mhe. Masoud Abdalla Salim (Mb) Msemaji Mkuu Kambi ya Upinzani Wizara ya Ulinzi wa JKT kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya wizara kwa mwaka wa fedha 2008/2009 Read the rest of this entry »





Kwa nini serikali imemilikisha ardhi kwa mgeni?

18 08 2008

Mhe Magdalena Sakaya

Mhe Magdalena Sakaya

“Sheria ya ardhi ya mwaka 1999 inakataza ardhi kumilikishwa kwa wageni. Wawekezaji wageni wanakodishiwa ardhi kwa muda fulani wa makubaliano. Kitendo cha Serikali kummilikisha mwekezaji ‘reserve’ ya Grumeti na akajenga VIP Hotel ndani ya ‘reserve’ hiyo yenye eneo la kilomita za mraba 149 ni kinyume na utaratibu na kanuni za nchi. Kambi ya Upinzani inataka majibu kutoka kwa Serikali ni taratibu gani zilifuatwa kumilikisha ardhi ya wananchi wa mkoa wa Mara kwa mwekezaji huyo raia wa Marekani, Johnes Tudor? Kuna usiri mkubwa wa shughuli zinazofanywa kwenye eneo hili na mtu yeyote haruhusiwi kuuliza. Tuna wasiwasi hata mapato yanayokusanywa na serikali kutoka eneo hili siyo sahihi. Mwekezaji huyu amekuwa anawanyanyasa sana wananchi wanaozunguka eneo hilo. Amekuwa anatumia askari wake kuwapa kipigo kikali mwananchi yeyote anayekutwa hata jirani na eneo lake. Kumekuwepo na malalamiko kuwa askari hawa wanawalazimisha wananchi kula nyama mbichi pale wanapokamatwa na mnyama. Hii ni haki kwa nchi inayoendeshwa kisheria?”

Hotuba ya Mheshimiwa Magdalena Sakaya, Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2008/09 Read the rest of this entry »