Ile Real Madrid inakuja lini?

12 08 2008
Timu ya Real Madrid ya Hispania ambayo Rais Kikwete aliahidi kuileta mwaka jana. Iko wapi hadi sasa?

Timu ya Real Madrid ya Hispania ambayo Rais Kikwete aliahidi kuileta mwaka jana. Iko wapi hadi sasa?

“…miongoni mwa mafanikio ambayo yalisemwa kuwa ni kutokana na ziara za Mheshimiwa Rais nje ya nchi, ni pamoja na ujio wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid ya Hispania. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitoa tamko la kuthibitisha kuwa timu ya Real Madrid ingelifika Tanzania rasmi kwa michezo ya kirafiki Julai mwaka 2007 ikiwa na msafara wa watu wapatao 80. Hili ni tamko rasmi la Serikali ndani ya Bunge. Kambi ya Upinzani inauliza ujio wa timu hii ni lini? Je, Rais alipotoshwa? Kuna jambo gani hapo? Kama imeshindikana, ni kwanini Serikali inakosa ujasiri wa kulieleza Taifa kilichojiri kama ilivyotamka rasmi na kwa mbwembwe wakati wa kutangaza uwepo wa utaratibu huo?”

Hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani – Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2008/2009 iliyosomwa Bungeni na Mhe. Mwanawetu Said Zarafi (Mb) tarehe 28 Julai, 2008 Read the rest of this entry »





Kwa nini Polisi iliwavamia Wapemba usiku wa manane?

12 08 2008

Mhe. Khamis Juma Shoka, mbunge wa CUF, Micheweni, aliyesoma hotuba ya Kambi ya Upinzani kuhusu Mambo ya Ndani kwa niaba ya Mhe. Muhammad Sanya

“…Sote tunaelewa kuwa taratibu mahali pengi duniani ambapo heshima na haki za binadamu zinathamniwa, askari wanakuwa na mipaka katika kutekeleza majukumu yao. Mfano, askari hatakiwi kumpekuwa raia zaidi ya saa kumi na mbili jioni.  Kwa msingi huo, napenda Mhe. Waziri alieleze Bunge hili, ni mamlaka yapi yaliyotumika kuwavamia wakazi saba wa Pemba zaidi ya saa saba za usiku waliojiita askari walifanya fujo, wakatishia hata kuvunja milango ya nyumba za hao waliowaita watuhumiwa? Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inauliza je huu si uvunjifu wa haki za raia na kwenda kinyume na matakwa ya Umoja wa Mataifa wa kuheshimu haki za binadamu….?

Hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Mhe.Muhammad Ibrahim Sanya (Mb) kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani iliyosomwa Bungeni kwa niaba yake na Mhe. Juma Khamis Shoka (Mb), pichani Read the rest of this entry »