Jussa: Ni Mkataba, na sio Katiba ya Muungano, ndio Sheria Kuu

6 08 2008

Haya ni mambo ya kisheria. Suala ni: zinasimama vipi kisheria Katiba zote mbili? Hapo ndipo

Ismail Jussa, Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF na Msaidizi Maalum wa Katibu Mkuu wa CUF kuhusu Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa

Ismail Jussa

penye tatizo kubwa lililojitokeza kutokana na kauli ya Waziri Mkuu Pinda. Kwa sababu, inaonekana – na wala si suala la Pinda kwa hakika – inaonekana kumekuwa na msimamo wa muda mrefu sana kwa upande wa wanasiasa na mara nyengine hata wasomi kutoka upande wa Tanganyika wanaojaribu kuleta sura kwamba vile Katiba ya Jamhuri ya Muungano iko juu ya Katiba ya Zanzibar. Na hata kauli yake, Mheshimiwa Pinda, alisema hivyo hivyo, kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano ndio Katiba Mama. Sasa hapo ndipo penye matatizo, kwa sababu katiba zote hizi mbili: Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Katiba ya Zanzibar ni katiba sawasawa. Hakuna iliyoko juu ya mwenzake.

Mahojiano kati ya Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi  na Msaidizi Maalum wa Katibu Mkuu wa CUF kuhusu Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Mhe. Ismail Jussa, na kituo cha Redio cha Zenj FM cha mjini Zanzibar kuhusiana na kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwamba Zanzibar si nchi.

Read the rest of this entry »





Muungano kama nyenzo ya kuwagawa Wazanzibari

6 08 2008

Mhe. Juma Duni Haji, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Zanzibar

Mhe. Juma Duni Haji, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Zanzibar

“Kwa hivyo suala la kuuliza ni kwa nini kila baada ya miaka mitano kunatokea mgogoro wa kisiasa Zanzibar? Mgogoro wa kisiasa unatokea kwa sababu hakuna utashi wa kufanyika uchaguzi huru na wa haki huko Zanzibar. Mimi ninaamini kwamba na huku Bara hali ni kama hiyo. Matatizo ya huku yanafichika kutokana na ukubwa wa nchi na wala si usafi wa chaguzi zenyewe. Vurugu za kuharibu uchaguzi kila baada ya miaka mitano, mara zote, husindikizwa na viongozi wa CCM na vyombo vya Serikali ya Muungano hasa vyombo vya ulinzi: jeshi la polisi, majeshi ya ndani na hata ya kuazimwa, majeshi kutoka nchi jirani, pamoja na kutumiwa Usalama wa Taifa kuendesha chaguzi hizo. Kila ikifika uchaguzi, vyombo vya Serikali ya Muungano ndivyo husindikiza na kulinda makundi haramia ya vijana wa CCM maarufu kwa jina la Janjaweed wanaosaidiwa na vikosi vya SMZ, kuhujumu utaratibu mzima wa kuendesha uchaguzi huru na wa haki.”

Hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Juma Duni Haji, katika Kongamano la Kuadhimisha Miaka 44 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tarehe 26 Aprili, 2008

Read the rest of this entry »





“Kikwete uthibitishie ulimwengu kama wewe si msanii”

6 08 2008

Baraza Kuu limesikitishwa na hatua ya Rais Jakaya Kikwete kushindwa kuonyesha ukomavu wa

Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama kweli ana nia dhati, CUF inasema, asimamie kusainiwa wa Muafaka baina ya CUF na CCM. Vyenginevyo itaendelea kuaminika kwamba anafanya usanii wa kisiasa katika mambo yanayohitaji uongozi makini wa kitaifa

Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama kweli ana nia dhati, CUF inasema, asimamie kusainiwa wa Muafaka baina ya CUF na CCM. Vyenginevyo itaendelea kuaminika kwamba anafanya usanii wa kisiasa katika mambo yanayohitaji uongozi makini wa kitaifa

uongozi kwa kusimamia utiaji saini na utekelezaji wa dhati wa makubaliano yaliyofikiwa katika Kamati ya Mazungumzo mbali na kutoa ahadi mara zote kwa Watanzania na jumuiya ya kimataifa kuwa mazungumzo hayo yamefikia ukingoni.

“Baraza Kuu linaendelea kumtaka Rais Kikwete ikiwa bado ana nia THABITI na ya DHATI katika kuumaliza mgogoro wa kisiasa Zanzibar, awakutanishe Maalim Seif Sharif Hamad na Mhe. Amani Karume kuandaa mchakato wa utiaji saini makubaliano yaliyofikiwa ikiwa ni kweli ‘CCM imeyakubali kimsingi’ kama lilivyoeleza azimio la Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho iliyokutana Butiama mwezi Machi, 2008. Vinginevyo itaendelea kuthibitisha tu kuwa Rais Kikwete ni ‘msanii wa kisiasa’ na mtaalamu aliyebobea wa kuyatelekeza hata yale mambo muhimu yanayotishia uwepo wa amani na mustakbali mwema wa Taifa letu na watu wake. Kwa kushindwa kulisimamia suala hili, Mhe Kikwete anastahili kulaumiwa na kila Mtanzania na wadau wote wa maendeleo wanaoitakia mema nchi yetu.”

Maazimio ya Kikao cha Kawaida cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kilichofanyika tarehe 29-30 Juni, 2008, Buguruni, Dares Salaam. Read the rest of this entry »