Tarehe 21 Desemba 2005, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliapishwa kuwa Rais wa nne
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa 2005. Tarehe 30 Desemba 2005 Rais Kikwete alilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuelezea mambo muhimu ambayo atayasimamia kama Rais wa awamu ya nne. Baada ya kipindi cha mwaka mmoja huu ni wakati muafaka wa kufanya tathmini ya uongozi wa Rais Kikwete kwa kukosoa kwa lengo la kujenga na kutoa ushauri wa kusaidia kuboresha utendaji wa uongozi wake na serikali kuendeleza demokrasia, amani na utulivu wa kweli, na kujenga uchumi utakaokuwa na manufaa kwa wananchi wote na kuwahakikishia wananchi maisha bora kwa kila Mtanzania.


Maoni