Bunge lamalizika kwa kishindo kizito cha Muungano

31 08 2008

Bendera ya Zanzibar.

Bendera ya Zanzibar.

Bunge la Bajeti la mara hii limemalizika mjini Dodoma Ijumaa iliyopita ya terehe 29 Agosti, 2008, huku likiwa limeiwacha nchi imejeruhika vibaya, hasa katika masuala ya Muungano, mahkama ya kadhi na kashafa ya EPA. Kuhusu Muungano, ambapo kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwamba Zanzibar si nchi ndiyo iliyochochea yote, hali ilikuwa ni ngumu na mbaya zaidi kwa kuwa wabunge waligawanyika baina ya Uzanzibari na Utanganyika. Wakati wa Zanzibar walipigania hadhi ya nchi yao ndani ya mipaka ya Muungano, wa Tanganyika walipigania kuidhibiti zaidi Zanzibar. Fuatilia sehemu ifuatayo ya majadiliano katika michango ya wabunge kwa Ofisi ya Makamo wa Rais (Muungano)…. Read the rest of this entry »





Serikali yaupuuza mkarafuu

29 08 2008

Karafuu za Zanzibar, zao kuu la biashara ambalo licha ya umuhimu wake, Serikali imepuuza ukuzwaji wake na inang'ang'ania udhibiti tu. Sera ya CUF kuelekea zao hili ni kuondoa mkono wa serikali na kuliingiza katika biashara huria

Karafuu za Zanzibar, zao kuu la biashara ambalo licha ya umuhimu wake, Serikali imepuuza ukuzwaji wake huku ikig'ang'ania udhibiti wake tu. Sera ya CUF kuelekea zao hili ni kuondoa mkono wa serikali na kuliingiza kwenye biashara huria

Kwa takribani karne mbili mutawaliya, historia ya imeonesha kuwa Zanzibar imeendelea kutegemea karafuu kama zao lake la kibiashara. Lakini ni bahati mbaya kwamba, licha ya kuwa tegemeo la kiuchumi kwa visiwa hivi, Serikali ya Zanzibar imeshindwa kuchukuwa hatua madhubuti na za makusudi kuliimarisha zao hili, badala yake imekuwa iking’ang’ania udhibiti wake tu. “Mkarafuu unakabiliwa na hatari ya kupotea kutokana na matatizo yanayoukabili ikiwa hatua za haraka za kuhami hazikuchukuliwa. Lakini kwa bahati mbaya Serikali bado inafanya utani juu ya kuliokoa zao la karafuu. Hivyo ni kweli kama serikali imekusudia kuuhami mkarafuu ingetenga shilingi milioni 40 kwa mradi wa kuimarisha mikarafuu? Huu ni utani na serikali haistahiki kufanya utani na maendeleo ya nchi.” Anasema Muhiddin Mohammed, mwakilishi wa CUF kutoka jimbo la Mtambile. Read the rest of this entry »





SMZ haikuwatendea haki vijana wa Jua Kali

29 08 2008

Saateni, Mjini Unguja. Hapa ndipo vijana wa Jua Kali walipokuja kutupwa na serikali ili wafanye biashara zao.

Saateni, Mjini Unguja. Hapa ndipo vijana wa Jua Kali walipokuja kutupwa na serikali ili wafanye biashara zao.

Mwezi uliopita, Julai 2008, SMZ ilitekeleza amri yake ya kuwaondosha wafanyabiashara ndogondogo katikati ya mji wa Zanzibar, Darajani, wanaojuilikana kama ‘vijana wa Jua Kali’ na kuwalazimisha kwenda katika eneo la Saateni, ambako hata hivyo hakuna na matayarisho ya kuwaweka vijana hao waliojiajiri wenyewe. Kikiwa chama kinachosimamia misingi ya haki za binaadamu na uhuru binafsi wa kujiendeleza, CUF inaiunga mkono Jua Kali kama sekta binafsi na inalaani kitendo cha kuwafukuza vijana hawa katika maeneo yao ya kazi bila ya kupewa eneo mbadala na la kibiashara. Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto katika Baraza la Wawakilishi, Bi Aziza Nabahan, anabainisha msimamo wa CUF katika hotuba hii ya kuchangia makadirio ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2008/2009. Read the rest of this entry »





Kuna harufu ya ufisadi mkubwa Zanzibar

29 08 2008

Gati ya Malindi, Zanzibar, ikiwa katika ujenzi unaondelea sasa ambao CUF inaamini kwamba una harufu ya ufisadi

Gati ya Malindi, Zanzibar, kama inavyoonekana sasa ikiwa katika ujenzi unaondelea na ambao CUF inaamini kwamba una harufu ya ufisadi

Tangu ile Orodha ya Mafisadi (List of Shame) itangazwe hadharani na vyama vya Upinzani nchini, macho na masikio yote yameelekezwa katika taasisi za Serikali ya Muungano tu, huku chochote kikiwa hakisemwi, hakiandikwi wala hakisikiki kuhusu ufisadi ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kimya hiki cha umma na hasa vyombo vya habari kimewahi kumpa juburi Amani Karume kudai kwamba serikali yake haina mafisadi. Lakini CUF imenusa harufu ya ufisadi mkubwa Zanzibar kupitia zabuni za ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, gati ya Malindi, barabara, Shirika la Meli na katika fursa za usimamizi wa Bajeti kwa visiwa viwili vya Unguja na Pemba; na sasa, kupitia msemaji wake wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi kwenye Baraza la Wawakilishi, Said Ali Mbarouk (CUF, Gando), inataka Tume huru iundwe kuchunguza zabuni hizo. Serikali ina majibu? Read the rest of this entry »





Mbona SMZ inawaangalia hadi wagonjwa kwa jicho la U-unguja na Upemba?

29 08 2008

Mhe. Rashid Seif Suleiman (CUF - Ziwani)

Mhe. Rashid Seif Suleiman (CUF - Ziwani)

Suala la mpasuko wa kisiasa Zanzibar linachangiwa kwa kiasi kikubwa na tabia ya serikali iliyopo madarakani, ambayo kwa makusudi hukitenga kisiwa cha Pemba kwa kila kitu kinachomaanisha maisha ya watu: elimu, miundombinu, uongozi na sasa hata afya. Katika hotuba hii ya Waziri Kivuli wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Rashid Seif Suleiman (Mwakilishi wa CUF, Jimbo la Ziwani), aliyoitoa kuchangia makadirio na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2008/2009 katika Baraza la Wawakilishi, Zanzibar, CUF inahoji na inataka maelezo ya kwa nini SMZ inafikia kiwango cha kuwabagua hata wagonjwa waliolazwa hospitalini kwa misingi ya U-unguja na Upemba, ambapo ingawa wagonjwa waliolazwa Pemba kwa mwaka 2008 ni asilimia 83 ya wagonjwa wote wa Zanzibar, walitengewa shilingi milioni 84 tu huku asilimia 17, ambao ni wagonjwa waliolazwa Unguja, wakipangiwa shilingi milioni 196! Read the rest of this entry »